Kabrasha chumba cha kunyongea

Hyo story ilishaletwa humu kitambo sana tena alihojiwa askari mstaafu ambae aliifanya kazi hyo kwa muda usiopungua miaka 25,alihojiwa na waandishi wa habari akaeleza kila kitu mpaka idadi ya watu walionyongwa kuanzia utawala wa nyerere mpaka........
Kila hatua alieleza,huyu kadonoa tu vitu na kuweka hapa
hivi kwanini unakuwa na mawazo kimo cha mbilikimo kiasi hiki?
 
daa kwa kweli tuishi kwa amani ndugu zanguni,ndiyo kifo hakikwepeki lakini kifo cha aina hiyo unajua kabisa kwamba kesho nitakufa (mungu aniepushe na kifo hicho)
 
umetudanganya hapo kwa bwana mnyongaji kukamatwa,anaekamatwa huwa ni bwana jela wa gereza ambalo hilo tukio la unyongaji limetokea...
 
Yule mnyongaji ilibidi amkanyage mgongoni mara 45
:D:D watu wapo siriaz na kazi ...hapo bado hakusogea huyo mwenye nyundo ...MKATA UMEME
 
Adhabu ya kunyongwa hadi kufa, ni mojawapo ya adhabu kongwe na ya kuogofya zaidi duniani... Na ndio adhabu ya juu zaidi.... Kunyongwa hadi ufe kabisa baada ya kuthibitishwa na mahakama tuhuma zako
Kuna taratibu ngumu na za muda mrefu hadi mtuhumiwa afikie kunyongwa kwakuwa kuhukumiwa kunyongwa ni jambo la kwanza lakini kutimizwa kwa adhabu ni jambo lingine... Unaweza ukahukumiwa kunyongwa na usinyongwe, ni mpaka mkuu wa nchi asaini hati yako ya kifo ndio unaweza kunyongwa!
Kabrasha la chumba cha kunyongea ni kubwa hivyo tuangalie dondoo zake wiki ya mwisho ya kutekeleza adhabu hasa masaa 72 ya mwisho...!!!! Maandalizi huwa mengi lakini haya ndio muhimu zaidi
. Viongozi wa dini huandaliwa kuja kuongea na wale wote wanaosubiri kitanzi..
. chumba cha kunyongea hufanyiwa ukarabati
Mnyongaji huandaliwa
. askari wasaidizi huandaliwa hawaambiwi kuna nini bali huambiwa wanaandaliwa kwa kazi maalum

Siku ya mwisho kuamkia kunyongwa
Ataanza Kiongozi wako wa dini kuongea nawe mara ya mwisho.. Kwa baadhi ya mazingira anaweza kuitwa hata rafiki yako ndani ya gereza
Utapewa chochote unachotaka hasa chakula na kinywaji... Baadhi hudai mpaka damu ya mnyama, sigara ama chakula chochote cha gharama.... Kwa sehemu kubwa hutimiziwa mahitaji yao haya...
Ni usiku wa kuamkia unyongaji, mnyongaji aliyeandaliwa huwekwa mahali pa pekeyake akipombeka usiku kucha
Kunapambazuka... Kiongozi wa chumba cha kunyongea hutoa amri ya wanyongwaji wote kuletwa chumba cha 'condemn' kazi hii hufanywa na wale askari wa kazi maalum
. chumba cha condemn mlangoni kina alama ya X nyekundu na fuvu kubwa...
Wanyongwaji wakiwa tayari na taarifa kuwa huo ndio mwisho wao wakishaingia tu hapa hufungwa vitambaa vyeusi usoni.. Na pingu kubadilishwa toka kufungwa kwa mbele mikononi na kufungwa kwa nyuma
Baada ya hapo huingizwa mlango wa pili kisha mlango wa tatu na wa mwisho ambako ndio kuna kitanzi
Baada ya kufika chumba cha kunyongea huvishwa kitanzi (kwa nchi nyingi za kiafrika) na mnyongaji hubonyeza kitufe kinachofungua milango ya sakafuni na mnyongwaji huning'inia na kitanzi kukaza shingoni na kunyonga....
Baada ya hapo mnyongaji anakuwa ameshaliza kazi yake, sasa kazi ya kwenda chini kufungua vitanzi na pingu na kuvuta miili juu ni ya askari wa kazi maalum... Kazi hii huwa ngumu na ya kutisha maana miili huwa na kila aina ya sura na miili mingine ikiwa bado inavuja damu.. ..
.Wakati wa kuivuta miili juu haivutwi kama unaopoa kitu majini bali hufungwa kamba miguuni na kuiweka mshazari na kuipandisha juu kama jeneza
Baada ya hapo huvuliwa nguo fasta na kuvalishwa shuka la sanda tena mwili ukiwa bado wa moto
Wafungwa walioandaliwa huchukua miili husika na kwenda kuizika fasta kwa makaburi yaliyokwisha chimbwa jana yake... Huko makaburini ni kufukiwa tu na si kuzikwa kwa heshima
Baada ya hapo wahusika wote hulipwa kulingana na majukumu yao na bwana mnyongaji hukamatwa na kupelekwa kizimabani na kusomewa mashtaka ya mauaji.... Naye hukiri kosa kwa kunukuu vifungu kadha vya Jamhuri ya nchi na hatimaye kuachiwa huru.....

Sehemu ijayo tutaendelea na vituko vya wanyongwaji
Asanteni

Kabrasha chumba cha kunyongea - JamiiForums
Kabrasha chumba cha kunyongea - JamiiForums
Duuh mnyongaji anakamatwa tena,kazi zingine
 
Mnyongaji nae anakili ameua kwa niaba ya sheria
hapa tanzania itakuja lini sheria wanyongwe wahujumu uchumi
 
Aisee
Baada ya kuhukumiwa, hupewa muda wa kukata rufaa... Rufaa ikishindikana kuna kusubiria msamaha wa rais.... (Msamaha huu si kuachiwa huru bali kupewa kifungo kirefu) kama hakuna inasubiriwa tu rais asaini hati yako na kuvunja kalamu aliyotumia(ishara ya kutotengua maamuzi) ... Hati yako ijishasainiwa kufuatana na ratiba za unyongaji hupangiwa na tarehe yako na kupewa taarifa na wahusika wa unyongaji Kiongozi wao
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom