Kabrasha chumba cha kunyongea

Haya asante. Mnyongwaji huambiwa lini kwa mara ya kwanza kuwa utanyongwa siku fulani na huambiwa na nani?
Baada ya kuhukumiwa, hupewa muda wa kukata rufaa... Rufaa ikishindikana kuna kusubiria msamaha wa rais.... (Msamaha huu si kuachiwa huru bali kupewa kifungo kirefu) kama hakuna inasubiriwa tu rais asaini hati yako na kuvunja kalamu aliyotumia(ishara ya kutotengua maamuzi) ... Hati yako ijishasainiwa kufuatana na ratiba za unyongaji hupangiwa na tarehe yako na kupewa taarifa na wahusika wa unyongaji Kiongozi wao
 
Adhabu ya kunyongwa hadi kufa, ni mojawapo ya adhabu kongwe na ya kuogofya zaidi duniani... Na ndio adhabu ya juu zaidi.... Kunyongwa hadi ufe kabisa baada ya kuthibitishwa na mahakama tuhuma zako
Kuna taratibu ngumu na za muda mrefu hadi mtuhumiwa afikie kunyongwa kwakuwa kuhukumiwa kunyongwa ni jambo la kwanza lakini kutimizwa kwa adhabu ni jambo lingine... Unaweza ukahukumiwa kunyongwa na usinyongwe, ni mpaka mkuu wa nchi asaini hati yako ya kifo ndio unaweza kunyongwa!
Kabrasha la chumba cha kunyongea ni kubwa hivyo tuangalie dondoo zake wiki ya mwisho ya kutekeleza adhabu hasa masaa 72 ya mwisho...!!!! Maandalizi huwa mengi lakini haya ndio muhimu zaidi
. Viongozi wa dini huandaliwa kuja kuongea na wale wote wanaosubiri kitanzi..
. chumba cha kunyongea hufanyiwa ukarabati
Mnyongaji huandaliwa
. askari wasaidizi huandaliwa hawaambiwi kuna nini bali huambiwa wanaandaliwa kwa kazi maalum

Siku ya mwisho kuamkia kunyongwa
Ataanza Kiongozi wako wa dini kuongea nawe mara ya mwisho.. Kwa baadhi ya mazingira anaweza kuitwa hata rafiki yako ndani ya gereza
Utapewa chochote unachotaka hasa chakula na kinywaji... Baadhi hudai mpaka damu ya mnyama, sigara ama chakula chochote cha gharama.... Kwa sehemu kubwa hutimiziwa mahitaji yao haya...
Ni usiku wa kuamkia unyongaji, mnyongaji aliyeandaliwa huwekwa mahali pa pekeyake akipombeka usiku kucha
Kunapambazuka... Kiongozi wa chumba cha kunyongea hutoa amri ya wanyongwaji wote kuletwa chumba cha 'condemn' kazi hii hufanywa na wale askari wa kazi maalum
. chumba cha condemn mlangoni kina alama ya X nyekundu na fuvu kubwa...
Wanyongwaji wakiwa tayari na taarifa kuwa huo ndio mwisho wao wakishaingia tu hapa hufungwa vitambaa vyeusi usoni.. Na pingu kubadilishwa toka kufungwa kwa mbele mikononi na kufungwa kwa nyuma
Baada ya hapo huingizwa mlango wa pili kisha mlango wa tatu na wa mwisho ambako ndio kuna kitanzi
Baada ya kufika chumba cha kunyongea huvishwa kitanzi (kwa nchi nyingi za kiafrika) na mnyongaji hubonyeza kitufe kinachofungua milango ya sakafuni na mnyongwaji huning'inia na kitanzi kukaza shingoni na kunyonga....
Baada ya hapo mnyongaji anakuwa ameshaliza kazi yake, sasa kazi ya kwenda chini kufungua vitanzi na pingu na kuvuta miili juu ni ya askari wa kazi maalum... Kazi hii huwa ngumu na ya kutisha maana miili huwa na kila aina ya sura na miili mingine ikiwa bado inavuja damu.. ..
.Wakati wa kuivuta miili juu haivutwi kama unaopoa kitu majini bali hufungwa kamba miguuni na kuiweka mshazari na kuipandisha juu kama jeneza
Baada ya hapo huvuliwa nguo fasta na kuvalishwa shuka la sanda tena mwili ukiwa bado wa moto
Wafungwa walioandaliwa huchukua miili husika na kwenda kuizika fasta kwa makaburi yaliyokwisha chimbwa jana yake... Huko makaburini ni kufukiwa tu na si kuzikwa kwa heshima
Baada ya hapo wahusika wote hulipwa kulingana na majukumu yao na bwana mnyongaji hukamatwa na kupelekwa kizimabani na kusomewa mashtaka ya mauaji.... Naye hukiri kosa kwa kunukuu vifungu kadha vya Jamhuri ya nchi na hatimaye kuachiwa huru.....

Sehemu ijayo tutaendelea na vituko vya wanyongwaji
Asanteni
Big bro kwanini hukusubiri huu msimu wa sikukuu uishe maana dah kwa stimu ulizonikata itabidi ulipie tu hakuna namna.
 
Hapo mnyongaji anapokamatwa ndo halafu kusomewa mashtaka wakati alikuwa anatekeleza majukumu yake?
 
Hapo mnyongaji anapokamatwa ndo halafu kusomewa mashtaka wakati alikuwa anatekeleza majukumu yake?
 
Ooh habari nzuri sana hii. Vipi hakuna aina nyingine ya adhabu ya kifo anaweza kuchagua mnyongwaji?
Mnyongwaji hana uamuzi wa
. gereza
. adhabu
. mnyongaji
Bali siku ya mwisho hupewa uchaguzi wa kula apendacho, kunywa apendacho, hata sigara (sio kubwa) hupewa kwa idadi ya kutosha.. Na hata nyimbo anaweza kupigiwa hata Nyegezi
 
Mnyongwaji hana uamuzi wa
. gereza
. adhabu
. mnyongaji
Bali siku ya mwisho hupewa uchaguzi wa kula apendacho, kunywa apendacho, hata sigara (sio kubwa) hupewa kwa idadi ya kutosha.. Na hata nyimbo anaweza kupigiwa hata Nyegezi
Anaweza kuosha rungu mara moja au hiyo haki hana?

Na vipi huwa mara nyingi wananyongwa nyakati gani? Usiku, asubuhi au mchana.
 
najua uzi umespecify kunyongwa ila kuuliza sio ujinga ...je kuna style ya kuua ambayo haina maumivu ya aina yeyote? na je kwenye ķuuliwa nani anae amua atanyongwa au sumu au shoti jaji au mtumiwa
 
Hapo mnyongaji anapokamatwa ndo halafu kusomewa mashtaka wakati alikuwa anatekeleza majukumu yake?
Kuua ni kuua tuu lakini kila mtuhumiwa wa mauaji hupewa nafasi ya kujitetea naye hujitetea kwa kusema hivyo kuwa kulingana na katiba ya nchi hayo ndio majukumu yake kisheria hivyo hana hatia
 
Mkuu hiyo ya mnyongaji kupombeka usiku kucha sijui kama nimekuelewa..
Maana kuna mnyongaji (mtaani ni maarufu kama nyonganyonga) mstaafu tuko nae kitaa,

Kunyonga kwake mbona haihitaji mbwembwe zozote (kulingana na maelezo yake) kama hizo za kupombeka usiku kucha..
 
Inaonesha mnyongaji ula fedha ndefu kuzidi wote kwa kazi ya kubonyeza kitufe tuu cha kufungua mlango wa kunyongea, bora na mm niombe nafasi hiyo zikitokea
 
najua uzi umespecify kunyongwa ila kuuliza sio ujinga ...je kuna style ya kuua ambayo haina maumivu ya aina yeyote? na je kwenye ķuuliwa nani anae amua atanyongwa au sumu au shoti jaji au mtumiwa
Kwa wenzetu walioendelea bado wanazidi kuboresha adhabu ya kifo kwa
Kukuwekea chumba kizuri chenye AC na manukato
Taa nzuri
Kitanda cha stainless steel
Godoro la gharama
Mikanda laini ya pure leather
Sindano ya usingizi
Sindano ya kuondoa maumivu
Sindano ya sumu
Mchomaji expert nknk
 
Anaweza kuosha rungu mara moja au hiyo haki hana?

Na vipi huwa mara nyingi wananyongwa nyakati gani? Usiku, asubuhi au mchana.
Hapana hiyo haipo.... Maranyingi kama si zote unyongaji hufanyika asubuhi kabla ya saa tatu
 
Mkuu hiyo ya mnyongaji kupombeka usiku kucha sijui kama nimekuelewa..
Maana kuna mnyongaji (mtaani ni maarufu kama nyonganyonga) mstaafu tuko nae kitaa,

Kunyonga kwake mbona haihitaji mbwembwe zozote (kulingana na maelezo yake) kama hizo za kupombeka usiku kucha..
Wanapewa lakini si kila mtu anapendelea kilevi cha pombe, vingine havitajwi na wengine hunywa lakini hawalewi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom