Kabla ya ndoa ujifunze lipi

Daah Mbu!Mi najaribu kuweka mambo yalingane na vile nataka yawe! Staki kuishi kulingana na mfalme Daudi alivotaka aisee....ndo matokeo yake mmoja kichwa mwingine miguu....Kwa nini wote tusiwe mabawa ya ndege mmoja?
Nilijaribusana kutafuta hiyo sehemu kwenye Biblia lakini sijaipata
Endelea tu kupekua hiyo Biblia mpaka uichakaze na huo mstari usiuone....kwanza sijanukuu kama nimetoa huko, shauri yako!

Luke 13:34...."Yerusalemu! We Yerusalemu! Unawaua manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako! Mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako pamoja kama kuku anavyokusanya vifaranga vyake chini ya mabawa yake, Lakini wewe umekataa"

au?

Reveletion 12:14 "
But the two wings of the great eagle were given to the woman, so that she could fly into the wilderness to her place, where she was nourished for a time and times and half a time, from the presence of the serpent."

bht chagua moja bana, usituzingue hapa....maandiko gani hayo yasopatikana?
 
Mbu, hapo sina la kuchagua, mimi namaanisha mume awe ubawa mmoja na mke ubawa mwingine (hii haipo kwenye funuo za biblia).
sasa si mambo ya mmoja kutii na mwingine kupenda.
Mbu, sijachagua hapo ila pia sikuzingui.

Walakini nimeguswa sana na umahiri wako wa kuleta mamlaka ili kuyapa nguvu unayoyazungumza.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu

...lol....bht, napenda somo la history, inanisaidia kupekua... usiku mwema nawewe.
 
Mwanzo.2:24 inasema, "Kwahiyo mwanamume atamuacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja" Ukiangalia (Zaburi.45:10-11) anasema, "Sikia binti utazame utege sikio lako, uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako na mfalme atautamani uzuri wako, maana ndiye bwana wako naye umsujudie".

Watu wengi wanataka waingie kwenye ndoa waoe au waolewe lakini uhusiano wao na wazazi wao usibadilike, haiwezekani. Biblia imeweka wazi unataka kuoa, mwanaume lazima aachane kwanza na baba yake na mama yake, maana yake kuna mabadiliko. Kuna mabadiliko mahali pa kuishi, kuna mabadiliko juu ya mtazamo wako wa kwanza wa maisha yako. Mke wako hawezi kuwa mama yako na mume wako hawezi kuwa baba yako.

Na kabla haujafikia maamuzi ya namna hiyo, ukiingia kwenye ndoa, ndoa yako itakuwa ngumu maana inawezekana unaishi vizuri na wazazi wako, kiasi kwamba maamuzi yote unayoyafanya lazima ushirikiane nao, hiyo hatua nzuri lakini ukiishaingia kwenye ndoa mtu wa kwanza kushirikiana nae ni mume wako kama umeolewa na mke wako
kama umeoa, na wazazi wengine wasingetaka kuona kwamba unakuwa mbali nao kwa jinsi hii, watataka waendeleze maamuzi yao na utawala wao waliokuwa nao juu yako mpaka kwenye ndoa yako haiwezekani.

Unapoamua kuolewa wa kwanza sio baba yako au mama yako, wa kwanza ni mume wako, ikiwa haujafikia uamuzi wa namna hii moyoni mwako basi basi bado haujafikia utayari wa kuolewa. Na ina madhara yake magumu, biblia inasema kabla haujawasahau watu wako na watu wa nyumba ya baba yako, mume wako hawezi kuutamani uzuri wako, ukitaka autamani uzuri wako lazima uwasahau kwanza watu wa nyumbani kwa wazazi wako.

Nawatakia kila la heri wale wanaotarajia kuolewa na kuoa wikiendi hii Mungu awabariki katika ndoa zenu.

TF.
Mkuu umetoa darasa la ukweli, ubarikiwe sana.
 
Hapa siswala la mwanaume alieandika maandiko, cha msingi ni kujua maandiko yameletwa kwetu na mungu kupitia watumishi wake, mboan kuna waandishi wa kike pia walihusika.
Haitokuwa vibaya, kwa kuelimishana tu, kama ukatuwekea mifano ya wanawake waliohusika, kwa kuandika au kushirikishwa katika andiko lolote takatifu: Taurat, Zaburi, Biblia, Quran....
 
Mbu, hapo sina la kuchagua, mimi namaanisha mume awe ubawa mmoja na mke ubawa mwingine (hii haipo kwenye funuo za biblia).
sasa si mambo ya mmoja kutii na mwingine kupenda.
Mbu, sijachagua hapo ila pia sikuzingui.

Walakini nimeguswa sana na umahiri wako wa kuleta mamlaka ili kuyapa nguvu unayoyazungumza.
labda kwa wazungu
 
Mwanzo.2:24 inasema, "Kwahiyo mwanamume atamuacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja" Ukiangalia (Zaburi.45:10-11) anasema, "Sikia binti utazame utege sikio lako, uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako na mfalme atautamani uzuri wako, maana ndiye bwana wako naye umsujudie".

Watu wengi wanataka waingie kwenye ndoa waoe au waolewe lakini uhusiano wao na wazazi wao usibadilike, haiwezekani. Biblia imeweka wazi unataka kuoa, mwanaume lazima aachane kwanza na baba yake na mama yake, maana yake kuna mabadiliko. Kuna mabadiliko mahali pa kuishi, kuna mabadiliko juu ya mtazamo wako wa kwanza wa maisha yako. Mke wako hawezi kuwa mama yako na mume wako hawezi kuwa baba yako.

Na kabla haujafikia maamuzi ya namna hiyo, ukiingia kwenye ndoa, ndoa yako itakuwa ngumu maana inawezekana unaishi vizuri na wazazi wako, kiasi kwamba maamuzi yote unayoyafanya lazima ushirikiane nao, hiyo hatua nzuri lakini ukiishaingia kwenye ndoa mtu wa kwanza kushirikiana nae ni mume wako kama umeolewa na mke wako
kama umeoa, na wazazi wengine wasingetaka kuona kwamba unakuwa mbali nao kwa jinsi hii, watataka waendeleze maamuzi yao na utawala wao waliokuwa nao juu yako mpaka kwenye ndoa yako haiwezekani.

Unapoamua kuolewa wa kwanza sio baba yako au mama yako, wa kwanza ni mume wako, ikiwa haujafikia uamuzi wa namna hii moyoni mwako basi basi bado haujafikia utayari wa kuolewa. Na ina madhara yake magumu, biblia inasema kabla haujawasahau watu wako na watu wa nyumba ya baba yako, mume wako hawezi kuutamani uzuri wako, ukitaka autamani uzuri wako lazima uwasahau kwanza watu wa nyumbani kwa wazazi wako.

Nawatakia kila la heri wale wanaotarajia kuolewa na kuoa wikiendi hii Mungu awabariki katika ndoa zenu.

TF.
Ujumbe mzuri sana huu nashukuru sana mkuu kwa kutukumbusha
 
Similar Discussions

15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom