The Finest
JF-Expert Member
- Jul 14, 2010
- 21,605
- 6,071
Mwanzo.2:24 inasema, "Kwahiyo mwanamume atamuacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja" Ukiangalia (Zaburi.45:10-11) anasema, "Sikia binti utazame utege sikio lako, uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako na mfalme atautamani uzuri wako, maana ndiye bwana wako naye umsujudie".
Watu wengi wanataka waingie kwenye ndoa waoe au waolewe lakini uhusiano wao na wazazi wao usibadilike, haiwezekani. Biblia imeweka wazi unataka kuoa, mwanaume lazima aachane kwanza na baba yake na mama yake, maana yake kuna mabadiliko. Kuna mabadiliko mahali pa kuishi, kuna mabadiliko juu ya mtazamo wako wa kwanza wa maisha yako. Mke wako hawezi kuwa mama yako na mume wako hawezi kuwa baba yako.
Na kabla haujafikia maamuzi ya namna hiyo, ukiingia kwenye ndoa, ndoa yako itakuwa ngumu maana inawezekana unaishi vizuri na wazazi wako, kiasi kwamba maamuzi yote unayoyafanya lazima ushirikiane nao, hiyo hatua nzuri lakini ukiishaingia kwenye ndoa mtu wa kwanza kushirikiana nae ni mume wako kama umeolewa na mke wako kama umeoa, na wazazi wengine wasingetaka kuona kwamba unakuwa mbali nao kwa jinsi hii, watataka waendeleze maamuzi yao na utawala wao waliokuwa nao juu yako mpaka kwenye ndoa yako haiwezekani.
Unapoamua kuolewa wa kwanza sio baba yako au mama yako, wa kwanza ni mume wako, ikiwa haujafikia uamuzi wa namna hii moyoni mwako basi basi bado haujafikia utayari wa kuolewa. Na ina madhara yake magumu, biblia inasema kabla haujawasahau watu wako na watu wa nyumba ya baba yako, mume wako hawezi kuutamani uzuri wako, ukitaka autamani uzuri wako lazima uwasahau kwanza watu wa nyumbani kwa wazazi wako.
Nawatakia kila la heri wale wanaotarajia kuolewa na kuoa wikiendi hii Mungu awabariki katika ndoa zenu.
TF.