Kabla ya kumkosoa Rais Samia, tumuombe radhi kwanza Hayati Mkapa na familia yake na washauri wake

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,111
115,905
Sisi wengine tulikuwepo wakati Rais Mkapa (1995-2005)anatukanwa kila siku kuwa "anauza nchi Kwa makaburu".....ilifikia wakati hadi nyimbo zilitungwa zikimuimba naukumbuka wimbo mmoja .."Kama sio juhudi zako Nyerere, Mkapa angeuza nini"???..Mkapa alikuwa anatukanwa kisa ni kuleta wawekezaji wa kampuni zisizo zaidi tano kutoka Afrika Kusini..
Walikuja kuwekeza
1.TBL
2.. NBC
Zingine nimezisahau....Leo...

Uwekezaji wa NBC ulipelekea Serikali kuanzisha NMB ambayo nayo waliletwa Waholanzi kununua hisa zisizozidi asilimia 5..waka provide management baadae waholanzi wale wakashangaa jinsi soko lilivyo kubwa wakaomba kununua hisa zaidi now nasikia ni asilimia 25.

Mabadiliko ya sekta nzima ya Benki aliyoyasimamia Rais Mkapa kipindi kile Leo yamepelekea tuwe na sector ya bank kubwa inayofanya kazi Kwa ufanisi.

NMB Leo ni kubwa kuliko Zanzibar GDP..na bank zote 3 kubwa Tanzania.. NMB, NBC na Crdb ni kubwa kuliko Uchumi wa Burundi...

Haya yote yasingewekana kama Rais Mkapa angeogopa "kuitwa fisadi anaeuza nchi Kwa Makaburu"...kipindi kile usingeweza kumuelewa Mkapa ...since watu waliokuwa wanaompinga walikuwa Wana influence ya kutosha ..tukianzia na Mwl Nyerere.....Na Magazeti ya Jenerali Ulimwengu yaliyokuwa Yana influence kubwa Sana Kwa jamii ya wasomi na wakosoaji wakubwa. ungeweza fikiri nchi inauzwa kweli ukifatilia mijadala...

Leo hizo banks zote 3.. NMB na Crdb zinamilkiwa na watanzania asilimia 70 NBC pia Serikali bado ina hisa za kutosha na zote hizo serikali inapokea gawio la kutosha...wale waliokuwa wanasema Mkapa anauza nchi Kwa makaburu wamenyamaza kiimya na sasa wamehamia kwenye "Samia anauza nchi Kwa waarabu" as if nothing happened...wala hawajawi jiuliza walichokuwa wanapinga kipindi kile na Hali ikoje leo? Walikuwa sahihi??

Kama hawakuwa sahihi kwanini wasiombe hata radhi in public hapo hata waliokuwa washauri wa Mkapa ambao bado wako hai wafarijike??...kama Mkapa aliuza nchi Kwa makaburu, hii nchi wanayosema anauza Samia ni ipi tena?

Itoshe kusema TBL ilienda kuwa kampuni inayolipa Kodi kubwa kuliko kampuni zote Tanzania Kwa miaka mingi Sana kama sio mpaka Leo ninavyoandika hapa....lakini shukran pekee aliyoambulia Rais Mkapa ni kuitwa "fisadi anaeuza nchi Kwa makaburu"...

Na wale watukanaji wakubwa Hadi Leo hawajawi kusema "hatukuwa sahihi" tulikosea ...Sana Sana wamevamia basi jipya "la Samia anauza nchi Kwa waarabu" Kwa nguvu mpyaa kabisa ...wazungu wanasema "ignorance is bliss"..

Mtu mjinga ana faida ya kutojijua ujinga wake...anaweza ita hata watu werevu wajinga hadharani bila woga...'ignorance is bliss ".....ungemueleza nini Mtanzania wa kawaida kuwa Mwalimu Nyerere hayuko sahihi ..wakati CEO wa Crdb wakati ule anaenda Hadi Butiama kumuomba Nyerere anunue hata hisa kidogo za Crdb kama kushawishi jamii iamke na Ku embrace"mabadiliko ya uchumi "na Nyerere ananjibu waziwazi mbele ya Tv kuwa hakuna cha mabadiliko wala nini ..ni ubepari na wizi tu kubinafsisha mabenki"...

Kwa watanzania Wengi Nyerere ni close to God ... hawezi kuwa hayuko sahihi..huwa najiuliza kama kipindi kile mwaka 1996 kama Babu yangu angekuwa na Uwezo mdogo Tu na akanunua hisa nyingi Crdb mwaka 1996 mfano hisa zenye thamani ya hata ya milioni 2 mwaka 1996 Leo ingekuwa ni utajiri kiasi gani?but watanzania Wengi hawakuwa na uelewa na waliokuwa wanaopinga mabadiliko ndo hao kina Nyerere na Rais anaeongoza mabadiliko anatukanwa kama "anauza nchi Kwa makaburu"...miaka 17 later ... tunamtukana Rais Kwa kuleta nchini moja ya kampuni 3 kubwa duniani Kwa shughuli za Bandari... Dpworld... kampuni imewekeza kuanzia China Hadi USA Kwa mabingwa wenyewe wa uwekezaji..Hadi Kwa wajerumani mabingwa wa ubaguzi duniani......

Kampuni CEO mmarekani lakini tunaambiwa inakuja "kueneza Uislam"... kampuni imewekeza UK lakini tunaambiwa huko kote imewekeza "fair " Ila kwetu ndo "imeuziwa nchi"...hata serikali inaposema mkataba wa uwekezaji bado kusainiwa hatutaki kuelewa...

Watu unao fikiri Wana uelewa wanatokwa na mapovu kuongea with certain "hatari kubwa Sana " iliyo mbele yetu akija "huyu mwarabu"...na wimbo mpya wa Samia anauza nchi Kwa waarabu ndo unazidi kupandishwa chati Kwa nguvu kubwa... maandamano uchwara yanachochewa na Viongozi wa dini ambao unajiuliza ni Bandari tu au kuna agenda ingine?

The more things change the more they stay the same....
Walio muita Mkapa fisadi anaeuza nchi Kwa makaburu..sasa wanafanya miamala banks zile zile na pengine kununua hisa na kunywa Safari lager huku washasahau "matusi " yote waliyomtwisha Mzee Mkapa...angalau wajitokeze waombe radhi japo hata washauri wa Mzee Mkapa wafarijike...kabla hawajapanda hili basi lingine la "Samia anauza nchi Kwa waarabu"...

Pengine wanaweza wasiwe hai ikitokea haya yote yanayozungumwa Leo yakathibitika kuwa ni uzushi , upumbavu na propaganda za wanasiasa wanaotaka Mama Samia "awapishe kwenye kiti mapema".....ili waombe radhi...Bora kwanza waombe radhi hili la Mkapa ambalo limethibitika bila Shaka kuwa "kelele za Mkapa kuuza nchi Kwa makaburu" ilikuwa uwongo, upumbavu,upeo mdogo kuhusu uchumi na uwekezaji na kudandia mabasi ya propaganda ambayo hujui dereva wake nani.
 
Umeandika mengi ya msingi, lakini mkuu The Boss Kwa nini mkataba hauna ukomo?.

2. Kwa nini mkataba haujajumuisha bandari za Zanzibar?.

3. Kwa Nini apewe bandari zote mtu mmoja, mfano ataendeleza vipi bandari ya mtwara hali yakua anamiliki na bandari ya Msumbiji?.

4. Kwa Nini anaonekana kua na kesi nyingi kwenye bandari za Afrika alizowekeza?.

Hakuna ntanzania yeyote anaekataa uwekezaji, lakini watu wanakataa baadhi ya vifungu vilivyopo kwenye mkataba. Mfano wewe unaona nisahihi kubadili Sheria za nchi Kwa sababu ya muwekezaji mmoja?.

Kwa Nini apewe aridhi yeyote atakayoomba, na Serikali ndio iwajibike kulipa fidia Kwa wahanga?.

Ushawahi Kwa utashi na akili zako kuona mkataba usio na ukomo?. Nje nahuu wa Aliosaini Tz?.

Tulitunga Sheria kua masuala yote yanayohusu wawekezaji kesi zao zitatuliwe ndani ya nchi, Kwa Nini kwahuyu Serikali ikubali kua yeye kesi yake itakua S Afrika?.

Watanzania wakipindi Cha mkapa sio hawa waleo.

Kheri tubaki na Tanganyika yetu nawao wabaki na Zanzibar yao.
 
Kinachonisikitisha ni kushindwa kufahamu kwamba uendeshwaji wa benki za kibiashara (Commercial Banks) ndani ya nchi, hutegemea sana sheria na sera za uchumi (Fiscal & Monetary Policies) ambazo zinaratibiwa na benki kuu ya nchi ya Tanzania. Mabenki ni makampuni, lakini uendeshwaji wake hauko sawa na makampuni mengine. Mabenki hutumia mfumo wa FRACTIONAL RESERVE BANKING & QUANTITIVE EASING , kusema ni pesa za nje peke yake na wawekezaji ndiyo wametuinia ni kututukana watanganyika.

Hivyo unavyotoa mifano ya CRDB na NMB kufanikiwa, fahamu fika kwamba BOT imefanya kazi kubwa mno hadi hizi benki kusimama. Raisi Mkapa ataendelea kulalamikiwa kwasababu yeye aliziuza hizi benki kiholela jambo ambalo halikuwa sahihi kabisa. Halafu kama umefuatilia vizuri, kuna sababu nyingine kadhaa wa kadhaa, zinazofanya benki ya NMB kufanikiwa, mbali na mitaji ya wazungu au kuwa na wateja wengi. Hapa bado sijazungumzia uwiano mkubwa baina ya THE BANKING SECTOR in relation to other CAPITAL MARKETS.

Nashangaa wewe umeshindwa kung'amua jambo rahisi kabisa ambalo hata mtoto wa chuo angeweza kuling'amua. Mkataba wa bandari na mkataba wa ubinafsishwaji wa mashirika ya ummah kipindi cha Mkapa ni tofauti kabisa. Kwenye mikataba mingi ya Raisi Mkapa, Tanzania bado inamiliki hisa za kutosha ambazo zinaipa nchi nguvu kubwa ya maamuzi hasa kwenye upigaji wa kura. Kubwa zaidi ni kwamba maamuzi ya mwisho ya usimamiz wa hizi benki uko chini ya usimamizi wa BOT na siyo wawekezaji wa nje.

Mkataba wa DP World, unainyang'anya Tanzania haki ya kufanya chochote kile. Tena hata kufikiria walishindwa wakasaini mkataba baina ya Tanzania na DP World ambalo ni shirika binafsi linalomilikiwa na Sultan wa Dubai (Semi-Autonomous Entity). Kule Djibouti, serikali iliunda kampuni ambalo liliingia ubia na DP World na kumiliki hisa zaidi ya asilimia 60%. Sisi huku tumefanya mambo ya hovyo kupita kiasi, ambapo zaidi ya kukusanya kodi hatuna chetu. Hivyo hata wafanyakazi wa bandari wanaweza kufukuzwa na tusiseme chochote kile.

Kikubwa mkataba huu wa bandari ni LOCK-OUT AGREEMENT, ambapo imewekwa bayana kabisa kwamba mashirika mengine ya ndani au kutoka nje hayataruhusiwa kuja kuwekeza kwenye bandari za Tanzania. Hivyo DP World wamepewa EXCLUSIVE RIGHT OF OWNERSHIP WHICH CREATES A MONOPOLY OVER OUR NATIONAL RESOURCES. Mtu yoyote yule mwenye akili timamu na mwenye uzalendo na hii nchi, kamwe hawezi kushabikia huu ufedhuli.

Kule Uingereza ambako haki za binadamu zimeshika hatamu, DP World ilifukuza maelfu ya wafanyakazi wa kizungu wa shirika la P&O Ferries baada ya kulinunua. Sasa huko ni Uingereza, hapa Tanzania unadhani kitawakuta nini wale wafanyakazi wa bandari ? Mambo mengine muwe mnatumia akili nyie watu, siyo matumbo. Sasa hebu nikupashe kidogo:

Mwaka 2020, serikali ya Djibouti ilifunguliwa mashitaka na shirika la DP WORLD kwasababu lilivunja haki yake ya umiliki wa bandari za Djibouti bila kuingiliwa (Breach of Exclusive Rights), kwasababu serikali ilitaka kulipa shirika la China Merchants haki ya kuwekeza kwenye bandari ya Doraleh. Serikali ya Djibouti na China Mechants ziliburuzwa kwenye mahakama za kimataifa na kuamriwa walipe dola za Kimarekani milioni 200.

Ikumbukwe China Merchants ndiyo shirika linalotaka kuanzisha mradi wa bandari ya Bagamoyo, lakini baada ya huu mkataba kupita hiyo haki hawana tena. Unafahamu nini kinaenda kutokea hapa ? Bandari ya Bagamoyo inaweza ikaenda kujengwa nchini Kenya na tusibaki tunaamini chochote hapa. Ikumbukwe mpango wa serikali ya Uchina kipindi cha Raisi Hu Jintao ni kwamba bandari ijengwe kule Kenya lakini wakaamua kujenga Tanganyika. Sasa hapa unadhani nini kitawazuia wakenya kuwaruhusu wachina wajenge Kenya ? Subirini muone...

MWISHO KABISA:
Leo nimemsikiliza Tundu Lissu akichambua kuhusu mkataba wa DP World, ambapo amesema kwamba huu ndiyo mkataba wa ajabu kuwahi kusainiwa na serikali ya Tanganyika tokea mwaka 1920. Mimi nasema amekosea na hajafanya tafiti za kutosha. Mkataba kama huu ulishawahi kusainiwa na serikali ya Muingereza, Mbelgiji na Mfaransa juu ya matumizi ya bandari ya Dar es salaam.

Mkataba ulihusisha makoloni ya Tanganyika, Rwanda, Burundi na Congo DRC na uliitwa THE BELBASE TREATY, ambao ulisema kwamba makoloni ya Rwanda, Burundi na Congo yataruhusiwa kutumia bandari ya Dar es salaam kwa kipindi kisicho na ukomo (Infinitely/Indefinate Time), huku wakilipa kiasi cha paundi 2 za Uingereza kwa serikali ya Tanganyika. Mwalimu Nyerere kawa Waziri Mkuu akaukuta huu mkataba, yeye na Mzee Lusinde akiwa waziri mwenye dhamana waliuvunja huu mkataba bila kufikiria mara mbili kwasababu ulilenga kuiumiza Tanganyika na kuuza uhuru wake.

Hii IGA baina ya Tanzania na Dubai, ina mahadhi hayohayo ya The Belbase Treaty, kwamba waarabu wapewe bandari zetu zote za Tanganyika kwa kipindi kisicho na ukomo. Halafu wakaenda mbali zaidi kusema kwamba "Even in case of state succession, a new state shall be bound by the same treaty." Wakimaanisha kwamba hata leo hii muungano ukivunjika, serikali ya Tanganyika itakuwa imefungwa na huo mkataba ambao umesainiwa na watu watatu kutoka Zanzibar. Sasa kama huku siyo kuiuza Tanganyika ni nini ?

NB 1: Kila siku nilikuwa najiuliza nini kilipelekea wafaransa (The Jacobins) wakachanganyikiwa na kuwa na hasira kiasi cha kumuua mfalme wao Louis IV na familia yake bila huruma, kumbe mambo huwa yanaanzaga hivihivi.

Kule Yugoslavia muungano wao ulikuwa na amani kwelikweli kipindi cha mkomunisti Josep Broz Tito, lakini huwezi kuamini jinsi ambavyo wakristo wa kutoka Serbia walifanya ukatili kwa kuua maelfu wa Waislamu kutoka Bosnia na Kosovo kisa tu hawa waislamu walikuwa wanataka uhuru wao, hivyo wakaanza kushirikiana na mataifa ya kiislamu kama Uturuki ili kuhujumu nchi. Hadi leo Serbia, Bosnia na Croatia ni maadui utadhani siyo ndugu (Slavs) waliowahi kuwa nchi moja.

NB 2: Ukweli tunaufahamu kwamba mbali na kusingizio cha kufungua nchi na kuita wawekezaji kutoka nje, nyuma ya hizi siasa za Raisi Samia kuna kaharufu kakali ka UDINI. Wengi mnamtetea Samia kwasababu tu ni mwenzenu kwenye imani. Hata wengine wanaomponda na kumkosoa wanafanya hivyo kwasababu za kidini, hata kama hapa watapinga. Sasa kama mambo ndiyo yako hivi, siku siyo nyingi Tanzania itakuwa imejaa chuki kubwa mno ya DINI.

Watanzania meingizwa kwenye mtego na ninyi mmejaa mazima.....Nawapa pole!
 
Nchi iliyojaa mashimo ya migodi huku ikiendesha kampeni za kuongeza madawati mashuleni na kujenga vyoo..

Nchi iliyopo kwenye great lake region na mipaka mikubwa ya bahari lakini kupata clean water tu ni mtihani

By the way

Ulichoongelea ni sawa na wanaopinga pia wapo sawa, instead ya kuwashambulia watu, ungeshambulia hoja.
Hakuna anaekataa mkataba Ila watu wanaomba mkataba uwe na maslahi kwa nchi kwa kufanya amendments kwa vifungu baadhi,

Ungefanya la maana sana kama ungeonesha ubora wa mkataba na sio kuchukua successful story ndogo ya mkapa kwenye privatization kuhalalisha kinachoendelea sasa..

Tusigombee fito na tunajenga nyumba moja ,pinga hoja kwa hoja🙏🏽🙏🏽
 
mi sina nyongeza hapa
Umeandika mengi ya msingi, lakini mkuu The Boss Kwa nini mkataba hauna ukomo?.

2. Kwa nini mkataba haujajumuisha bandari za Zanzibar?.

3. Kwa Nini apewe bandari zote mtu mmoja, mfano ataendeleza vipi bandari ya mtwara hali yakua anamiliki na bandari ya Msumbiji?.

4. Kwa Nini anaonekana kua na kesi nyingi kwenye bandari za Afrika alizowekeza?.

Hakuna ntanzania yeyote anaekataa uwekezaji, lakini watu wanakataa baadhi ya vifungu vilivyopo kwenye mkataba. Mfano wewe unaona nisahihi kubadili Sheria za nchi Kwa sababu ya muwekezaji mmoja?.

Kwa Nini apewe aridhi yeyote atakayoomba, na Serikali ndio iwajibike kulipa fidia Kwa wahanga?.

Ushawahi Kwa utashi na akili zako kuona mkataba usio na ukomo?. Nje nahuu wa Aliosaini Tz?.

Tulitunga Sheria kua masuala yote yanayohusu wawekezaji kesi zao zitatuliwe ndani ya nchi, Kwa Nini kwahuyu Serikali ikubali kua yeye kesi yake itakua S Afrika?.

Watanzania wakipindi Cha mkapa sio hawa waleo.

Kheri tubaki na Tanganyika yetu nawao wabaki na Zanzibar yao.
 
Ni udini tu unawasumbua plus ukenya

Na burundi na rwanda wanataka kutuchafulia inchi yetu
Wengi wa hao viongozi wa dini si raia wa tz
Yaani hata kiswahili hawajui
Tuwe nao tahadhari sana hawa na familua zao na wafuasi wao wana agenda ya kuleta machafuko tz
 
Umeandika mengi ya msingi, lakini mkuu The Boss Kwa nini mkataba hauna ukomo?.

2. Kwa nini mkataba haujajumuisha bandari za Zanzibar?.

3. Kwa Nini apewe bandari zote mtu mmoja, mfano ataendeleza vipi bandari ya mtwara hali yakua anamiliki na bandari ya Msumbiji?.

4. Kwa Nini anaonekana kua na kesi nyingi kwenye bandari za Afrika alizowekeza?.

Hakuna ntanzania yeyote anaekataa uwekezaji, lakini watu wanakataa baadhi ya vifungu vilivyopo kwenye mkataba. Mfano wewe unaona nisahihi kubadili Sheria za nchi Kwa sababu ya muwekezaji mmoja?.

Kwa Nini apewe aridhi yeyote atakayoomba, na Serikali ndio iwajibike kulipa fidia Kwa wahanga?.

Ushawahi Kwa utashi na akili zako kuona mkataba usio na ukomo?. Nje nahuu wa Aliosaini Tz?.

Tulitunga Sheria kua masuala yote yanayohusu wawekezaji kesi zao zitatuliwe ndani ya nchi, Kwa Nini kwahuyu Serikali ikubali kua yeye kesi yake itakua S Afrika?.

Watanzania wakipindi Cha mkapa sio hawa waleo.

Kheri tubaki na Tanganyika yetu nawao wabaki na Zanzibar yao.
Mbona majibu yametoka..hukusikia?
Imesainiwa IGA.. intergovernmental agreement...Mkataba wa bandari lazima utakuwa na kikomo..na mda wa review utakapo sainiwa.. huelewi nini?Bunge limeridhia serikali iende kuingia mkataba.., mkataba halisi bado...
 
Sijaona relevance ya alichokifanya Hayati Mkapa na hiki anachokifanya Samia.

Mkapa alialika wawekezaji ili pamoja na serikali ziwekeze kwa pamoja katika kuboost sekta husika. Isitoshe, top management za kampuni hizo zinakuwa mikononi na Watanzania. Benki zote ulizozitaja Watendaji Wakuu (CEO) ni Watanzania wa kuzaliwa. Mkurugenzj wa NMB (Ruth Zaipuna), CRDB (Alhaji Nsekela) na NBC (Theobald Sabi) wote ni Watanzania. Serikali pia ina Mkono katika Sehemu ya benki husika.

Je, DPW Serikali itakuwa na nafasi gani katika kumoderate usimamizi? Watanzania wana nafasi katika top management?

Alafu, acheni ajenda zenu za kudai Watanzania hawataki Uwekezaji bandarini. Ila aina ya Mkataba uliongiwa ndiyo una ualakini. Vipengele vya mkataba vina vifungu vigumu na vinavyoiweka nchi katika hali isiyo nzuri.

Benki ya NBC ilikuwa ya kwanza kubinafisishwa. Lakini serikali baadae ikaunda benki nyingine ya NMB. Haikuwekewa Masharti ya kutoanzisha benki nyingine yeyote, DP kuna hiyo nafasi?

DP anapewa bandari ZOTE, huko kwenye benki Wawekezaji walipewa zote? Si wamekuja kuingia ubia mdogo mdogo huku sekta binafsi zingine zikiruhusiwa kuanzisha benki zingine?

Lakini pia, umechagua sekta moja tu ya kibenki ambayo ndiyo imefanikiwa. Umejiuliza ni Mashirika mangapi yalibinafishwa na yakashindwa kunawiri kisha kuisababisha serikali hasara kubwa na kuwa mzigo kwa Wananchi?

Kwa nini unataka kutuaminisha kuwa hili la DPW litafanikiwa? Kufeli pia ni sehemu ya biashara.

Hilo halitoshi, unadai kwa sababu DPW ipo katika nchi kubwa (USA na Uchina) basi Tanzania nayo tunapswa kuingia. Unajua vipengele vya kimkataba katika mikataba yao?

Huko kwa Wakubwa wanawaachia ports kadhaa na nyingine kuendeshwa na kampuni nyinginezo na zingine pia kuendeshwa na serikali yenyewe. Iweje kwa Tanzania waachiwe zote?

Nadhani hili swala hakuna aliyelikataa, bali lazima kama nchi tulitafakri kwa mapana yake. Lisiwe jambo la kukurupuka. Naona baadhi ya Watu mmeanza kushindwa, badala yake mnaanza kutafuta kuungwa mkono kwa kuchombeza kuwa mnapingwa kwa hofu ya kidini.

Mijadala yote inayojadiliwa huko, hakuna yeyote yule aliyeingizwa swala la udini wa Samia na Waarabu. Wote ni kwa maslahi ya nchi yetu.

Hao Pro Samia ndiyo mnatumia strategy hiyo ili kuleta picha isiyo na maana katika jamii.
 
Sisi wengine tulikuwepo wakati Rais Mkapa (1995-2005)anatukanwa kila siku kuwa "anauza nchi Kwa makaburu".....ilifikia wakati hadi nyimbo zilitungwa zikimuimba naukumbuka wimbo mmoja .."Kama sio juhudi zako Nyerere, Mkapa angeuza nini"???..Mkapa alikuwa anatukanwa kisa ni kuleta wawekezaji wa kampuni zisizo zaidi tano kutoka Afrika kusini..
Walikuja kuwekeza
1.TBL
2.. NBC
Zingine nimezisahau....Leo...

Uwekezaji wa NBC ulipelekea Serikali kuanzisha NMB ambayo nayo waliletwa Waholanzi kununua hisa zisizozidi asilimia 5..waka provide management baadae waholanzi wale wakashangaa jinsi soko lilivyo kubwa wakaomba kununua hisa zaidi now nasikia ni asilimia 25..

Mabadiliko ya sekta nzima ya Benki aliyoyasimamia Rais Mkapa kipindi kile Leo yamepelekea tuwe na sector ya bank kubwa inayofanya kazi Kwa ufanisi...

NMB Leo ni kubwa kuliko Zanzibar GDP..na bank zote 3 kubwa Tanzania.. NMB, NBC na Crdb ni kubwa kuliko Uchumi wa Burundi...

Haya yote yasingewekana kama Rais Mkapa angeogopa "kuitwa fisadi anaeuza nchi Kwa Makaburu"...kipindi kile usingeweza kumuelewa Mkapa ...since watu waliokuwa wanaompinga walikuwa Wana influence ya kutosha ..tukianzia na Mwl Nyerere.....Na Magazeti ya Jenerali Ulimwengu yaliyokuwa Yana influence kubwa Sana Kwa jamii ya wasomi na wakosoaji wakubwa..... ungeweza fikiri nchi inauzwa kweli ukifatilia mijadala...

Leo hizo banks zote 3.. NMB na Crdb zinamilkiwa na watanzania asilimia 70 NBC pia Serikali bado ina hisa za kutosha na zote hizo serikali inapokea gawio la kutosha...wale waliokuwa wanasema Mkapa anauza nchi Kwa makaburu wamenyamaza kiimya na sasa wamehamia kwenye "Samia anauza nchi Kwa waarabu" as if nothing happened...wala hawajawi jiuliza walichokuwa wanapinga kipindi kile na Hali ikoje leo? Walikuwa sahihi??

Kama hawakuwa sahihi kwanini wasiombe hata radhi in public hapo hata waliokuwa washauri wa Mkapa ambao bado wako hai wafarijike??...kama Mkapa aliuza nchi Kwa makaburu, hii nchi wanayosema anauza Samia ni ipi tena??

Itoshe kusema TBL ilienda kuwa kampuni inayolipa Kodi kubwa kuliko kampuni zote Tanzania Kwa miaka mingi Sana kama sio mpaka Leo ninavyoandika hapa....lakini shukran pekee aliyoambulia Rais Mkapa ni kuitwa "fisadi anaeuza nchi Kwa makaburu"...

Na wale watukanaji wakubwa Hadi Leo hawajawi kusema "hatukuwa sahihi" tulikosea ...Sana Sana wamevamia basi jipya "la Samia anauza nchi Kwa waarabu" Kwa nguvu mpyaa kabisa ...wazungu wanasema "ignorance is bliss"..

Mtu mjinga ana faida ya kutojijua ujinga wake...anaweza ita hata watu werevu wajinga hadharani bila woga...'ignorance is bliss ".....ungemueleza nini Mtanzania wa kawaida kuwa Mwalimu Nyerere hayuko sahihi ..wakati CEO wa Crdb wakati ule anaenda Hadi Butiama kumuomba Nyerere anunue hata hisa kidogo za Crdb kama kushawishi jamii iamke na Ku embrace"mabadiliko ya uchumi "na Nyerere ananjibu waziwazi mbele ya Tv kuwa hakuna cha mabadiliko wala nini ..ni ubepari na wizi tu kubinafsisha mabenki"...

Kwa watanzania Wengi Nyerere ni close to God ... hawezi kuwa hayuko sahihi..huwa najiuliza kama kipindi kile mwaka 1996 kama Babu yangu angekuwa na Uwezo mdogo Tu na akanunua hisa nyingi Crdb mwaka 1996 mfano hisa zenye thamani ya hata ya milioni 2 mwaka 1996 Leo ingekuwa ni utajiri kiasi gani?but watanzania Wengi hawakuwa na uelewa na waliokuwa wanaopinga mabadiliko ndo hao kina Nyerere na Rais anaeongoza mabadiliko anatukanwa kama "anauza nchi Kwa makaburu"...miaka 17 later ... tunamtukana Rais Kwa kuleta nchini moja ya kampuni 3 kubwa duniani Kwa shughuli za Bandari... Dpworld... kampuni imewekeza kuanzia China Hadi USA Kwa mabingwa wenyewe wa uwekezaji..Hadi Kwa wajerumani mabingwa wa ubaguzi duniani......

Kampuni CEO mmarekani lakini tunaambiwa inakuja "kueneza Uislam"... kampuni imewekeza UK lakini tunaambiwa huko kote imewekeza "fair " Ila kwetu ndo "imeuziwa nchi"...hata serikali inaposema mkataba wa uwekezaji bado kusainiwa hatutaki kuelewa...

Watu unao fikiri Wana uelewa wanatokwa na mapovu kuongea with certain "hatari kubwa Sana " iliyo mbele yetu akija "huyu mwarabu"...na wimbo mpya wa Samia anauza nchi Kwa waarabu ndo unazidi kupandishwa chati Kwa nguvu kubwa... maandamano uchwara yanachochewa na Viongozi wa dini ambao unajiuliza ni Bandari tu au kuna agenda ingine??

The more things change the more they stay the same....
Walio muita Mkapa fisadi anaeuza nchi Kwa makaburu..sasa wanafanya miamala banks zile zile na pengine kununua hisa na kunywa Safari lager huku washasahau "matusi " yote waliyomtwisha Mzee Mkapa...angalau wajitokeze waombe radhi japo hata washauri wa Mzee Mkapa wafarijike...kabla hawajapanda hili basi lingine la "Samia anauza nchi Kwa waarabu"...

Pengine wanaweza wasiwe hai ikitokea haya yote yanayozungumwa Leo yakathibitika kuwa ni uzushi , upumbavu na propaganda za wanasiasa wanaotaka Mama Samia "awapishe kwenye kiti mapema".....ili waombe radhi...Bora kwanza waombe radhi hili la Mkapa ambalo limethibitika bila Shaka kuwa "kelele za Mkapa kuuza nchi Kwa makaburu" ilikuwa uwongo, upumbavu,upeo mdogo kuhusu uchumi na uwekezaji na kudandia mabasi ya propaganda ambayo hujui dereva wake nani.....
Saga la NBC in the long run limeiyumbisha sana Tanzania kuliko tunavyoweza kufikiri hasa kiuchumi.
Ilikua ni matakwa ya IMF kuiua NBC ili sekta binafsi ya kibenki iweze furukuta lakini kilichoipata NBC leo hamna mpambe anataka kizungumzia. Sekta ya benki imekua Yes... je implication yake kwa uchumi wa nchi ikoje ukilinganisha na nguvu ya NBC ya wakati ule? Je why benki nyingine zisingekuja kupambana na NBC?

Mkapa amekiri mara nyingi hadharani na kwenye kitabu chake kuwa ubinafsishaji kwa sehemu kubwa alikosea maana 80% ya mashirika ya umma yaliingia mifukoni mwa matapeli!

Hoja zile sile waliosimamia watu juu ya uwezo na aina ya mikataba ya hovyo ya ubinafsishaji ndizo zilikuja kuonekana wazi kweli waliopinga walikua na hoja tena kubwa sana.

Vipi NET group Solutions? ATCL? TRL?
Meremeta? Na mengine?

Shida yetu kubwa tunakimbilia sana kwenye petty issues when it comes to analysis

Mfano huu mkataba wa Tanzania na DP World ni wa hovyo usioelezeka! Hoja si kubinafsisha bandari Hoja ni mkataba wa hovyo!

Madini hadi leo yametufikisha wapi ukitulinganisha na Botswana na SA? Mbona kwao pia kuna sector binafsi?
HOJA sio ubinafsishaji hoja aina ya mikataba ya kishenzi ambayo nchi zetu zinaingia.
 
Sisi wengine tulikuwepo wakati Rais Mkapa (1995-2005)anatukanwa kila siku kuwa "anauza nchi Kwa makaburu".....ilifikia wakati hadi nyimbo zilitungwa zikimuimba naukumbuka wimbo mmoja .."Kama sio juhudi zako Nyerere, Mkapa angeuza nini"???..Mkapa alikuwa anatukanwa kisa ni kuleta wawekezaji wa kampuni zisizo zaidi tano kutoka Afrika kusini..
Walikuja kuwekeza
1.TBL
2.. NBC
Zingine nimezisahau....Leo...

Uwekezaji wa NBC ulipelekea Serikali kuanzisha NMB ambayo nayo waliletwa Waholanzi kununua hisa zisizozidi asilimia 5..waka provide management baadae waholanzi wale wakashangaa jinsi soko lilivyo kubwa wakaomba kununua hisa zaidi now nasikia ni asilimia 25..

Mabadiliko ya sekta nzima ya Benki aliyoyasimamia Rais Mkapa kipindi kile Leo yamepelekea tuwe na sector ya bank kubwa inayofanya kazi Kwa ufanisi...

NMB Leo ni kubwa kuliko Zanzibar GDP..na bank zote 3 kubwa Tanzania.. NMB, NBC na Crdb ni kubwa kuliko Uchumi wa Burundi...

Haya yote yasingewekana kama Rais Mkapa angeogopa "kuitwa fisadi anaeuza nchi Kwa Makaburu"...kipindi kile usingeweza kumuelewa Mkapa ...since watu waliokuwa wanaompinga walikuwa Wana influence ya kutosha ..tukianzia na Mwl Nyerere.....Na Magazeti ya Jenerali Ulimwengu yaliyokuwa Yana influence kubwa Sana Kwa jamii ya wasomi na wakosoaji wakubwa..... ungeweza fikiri nchi inauzwa kweli ukifatilia mijadala...

Leo hizo banks zote 3.. NMB na Crdb zinamilkiwa na watanzania asilimia 70 NBC pia Serikali bado ina hisa za kutosha na zote hizo serikali inapokea gawio la kutosha...wale waliokuwa wanasema Mkapa anauza nchi Kwa makaburu wamenyamaza kiimya na sasa wamehamia kwenye "Samia anauza nchi Kwa waarabu" as if nothing happened...wala hawajawi jiuliza walichokuwa wanapinga kipindi kile na Hali ikoje leo? Walikuwa sahihi??

Kama hawakuwa sahihi kwanini wasiombe hata radhi in public hapo hata waliokuwa washauri wa Mkapa ambao bado wako hai wafarijike??...kama Mkapa aliuza nchi Kwa makaburu, hii nchi wanayosema anauza Samia ni ipi tena??

Itoshe kusema TBL ilienda kuwa kampuni inayolipa Kodi kubwa kuliko kampuni zote Tanzania Kwa miaka mingi Sana kama sio mpaka Leo ninavyoandika hapa....lakini shukran pekee aliyoambulia Rais Mkapa ni kuitwa "fisadi anaeuza nchi Kwa makaburu"...

Na wale watukanaji wakubwa Hadi Leo hawajawi kusema "hatukuwa sahihi" tulikosea ...Sana Sana wamevamia basi jipya "la Samia anauza nchi Kwa waarabu" Kwa nguvu mpyaa kabisa ...wazungu wanasema "ignorance is bliss"..

Mtu mjinga ana faida ya kutojijua ujinga wake...anaweza ita hata watu werevu wajinga hadharani bila woga...'ignorance is bliss ".....ungemueleza nini Mtanzania wa kawaida kuwa Mwalimu Nyerere hayuko sahihi ..wakati CEO wa Crdb wakati ule anaenda Hadi Butiama kumuomba Nyerere anunue hata hisa kidogo za Crdb kama kushawishi jamii iamke na Ku embrace"mabadiliko ya uchumi "na Nyerere ananjibu waziwazi mbele ya Tv kuwa hakuna cha mabadiliko wala nini ..ni ubepari na wizi tu kubinafsisha mabenki"...

Kwa watanzania Wengi Nyerere ni close to God ... hawezi kuwa hayuko sahihi..huwa najiuliza kama kipindi kile mwaka 1996 kama Babu yangu angekuwa na Uwezo mdogo Tu na akanunua hisa nyingi Crdb mwaka 1996 mfano hisa zenye thamani ya hata ya milioni 2 mwaka 1996 Leo ingekuwa ni utajiri kiasi gani?but watanzania Wengi hawakuwa na uelewa na waliokuwa wanaopinga mabadiliko ndo hao kina Nyerere na Rais anaeongoza mabadiliko anatukanwa kama "anauza nchi Kwa makaburu"...miaka 17 later ... tunamtukana Rais Kwa kuleta nchini moja ya kampuni 3 kubwa duniani Kwa shughuli za Bandari... Dpworld... kampuni imewekeza kuanzia China Hadi USA Kwa mabingwa wenyewe wa uwekezaji..Hadi Kwa wajerumani mabingwa wa ubaguzi duniani......

Kampuni CEO mmarekani lakini tunaambiwa inakuja "kueneza Uislam"... kampuni imewekeza UK lakini tunaambiwa huko kote imewekeza "fair " Ila kwetu ndo "imeuziwa nchi"...hata serikali inaposema mkataba wa uwekezaji bado kusainiwa hatutaki kuelewa...

Watu unao fikiri Wana uelewa wanatokwa na mapovu kuongea with certain "hatari kubwa Sana " iliyo mbele yetu akija "huyu mwarabu"...na wimbo mpya wa Samia anauza nchi Kwa waarabu ndo unazidi kupandishwa chati Kwa nguvu kubwa... maandamano uchwara yanachochewa na Viongozi wa dini ambao unajiuliza ni Bandari tu au kuna agenda ingine??

The more things change the more they stay the same....
Walio muita Mkapa fisadi anaeuza nchi Kwa makaburu..sasa wanafanya miamala banks zile zile na pengine kununua hisa na kunywa Safari lager huku washasahau "matusi " yote waliyomtwisha Mzee Mkapa...angalau wajitokeze waombe radhi japo hata washauri wa Mzee Mkapa wafarijike...kabla hawajapanda hili basi lingine la "Samia anauza nchi Kwa waarabu"...

Pengine wanaweza wasiwe hai ikitokea haya yote yanayozungumwa Leo yakathibitika kuwa ni uzushi , upumbavu na propaganda za wanasiasa wanaotaka Mama Samia "awapishe kwenye kiti mapema".....ili waombe radhi...Bora kwanza waombe radhi hili la Mkapa ambalo limethibitika bila Shaka kuwa "kelele za Mkapa kuuza nchi Kwa makaburu" ilikuwa uwongo, upumbavu,upeo mdogo kuhusu uchumi na uwekezaji na kudandia mabasi ya propaganda ambayo hujui dereva wake nani.....
NET GROUP umeisahau au unaleta ujanja tu ?
 
Back
Top Bottom