Watu waliobadili jinsia wanaweza kuwa wazazi wa ubatizo katika Kanisa Katoliki, mashahidi katika harusi za kidini na kubatizwa

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,992
17,892
Watu waliobadili jinsia wanaweza kuwa wazazi wa ubatizo katika Kanisa Katoliki, mashahidi katika harusi za kidini na kubatizwa , ofisi ya mafundisho ya Vatikani ilisema Jumatano, ikijibu maswali kutoka kwa askofu.

Idara hiyo, inayojulikana kama Dicastery of the Doctrine of the Faith, haikuwa wazi hata hivyo, katika kujibu swali la ikiwa wenzi wa jinsia moja wanaweza kuruhusiwa kupata ubatizo wa Kanisa kwa ajili ya mtoto aliyeasiliwa au ule uliopatikana kupitia mama mlezi.

Askofu Jose Negri wa Santo Amaro nchini Brazili alituma kwa ofisi ya mafundisho maswali sita mnamo Julai kuhusu watu wapenzi wa jinsia moja na waliobadili jinsia (LGBT ) na ushiriki wao katika sakramenti za ubatizo na ndoa.

Kurasa hizo tatu za maswali na majibu zilitiwa saini na mkuu wa idara hiyo, Kadinali wa Argentina Víctor Manuel Fernández, na kuidhinishwa na Papa Francis mnamo Oktoba 31.

Ziliwekwa kwenye tovuti ya idara hiyo Jumatano kwa kutumia neno la Kiitaliano "transsexuals".

Francis, mwenye umri wa miaka 86, amejaribu kulifanya Kanisa liwe na ukarimu zaidi kwa watu wa jumuiya ya LGBT bila kubadili mafundisho ya Kanisa, ikiwa ni pamoja na msemo mmoja kwamba kuvutia watu wa jinsia moja si dhambi bali ni dhambi ni kitendo chenyewe cha kushiriki mapenzi ya jinsi moja.

Katika kujibu swali la kama watu waliobadili jinsia wanaweza kubatizwa, ofisi ya mafundisho ilisema wanaweza kwa masharti fulani na mradi tu "hakuna hatari ya kusababisha kashfa ya umma au kuchanganyikiwa miongoni mwa waumini".

BBC

1699552280788.jpg
 
Kanisa takatifu la mitume.....Pia tunalo taifa takatifu teule la Israel...Sauti ya Papa na Kanisa ni sauti ya Mungu" kwa mujibu wa wenye dini yao

Watu waliobadili jinsia wanaweza kuwa wazazi wa ubatizo katika Kanisa Katoliki, mashahidi katika harusi za kidini na kubatizwa, ofisi ya mafundisho ya Vatican imesema Jumatano, ikijibu maswali kutoka kwa askofu.

Kusoma zaidi taarifa hii https://bbc.in/3QP7cje

#bbcswahili #vatcan #papafrancis #catholic #katoliki #dini
1699552280788.jpg
Screenshot_20231109-204058.jpg
 
Kanisa takatifu la mitume.....Pia tunalo taifa takatifu teule la Israel...Sauti ya Papa na Kanisa ni sauti ya Mungu" kwa mujibu wa wenye dini yao

Watu waliobadili jinsia wanaweza kuwa wazazi wa ubatizo katika Kanisa Katoliki, mashahidi katika harusi za kidini na kubatizwa, ofisi ya mafundisho ya Vatican imesema Jumatano, ikijibu maswali kutoka kwa askofu.

Kusoma zaidi taarifa hii https://bbc.in/3QP7cje

#bbcswahili #vatcan #papafrancis #catholic #katoliki #diniView attachment 2809069View attachment 2809070
Umehamia huku? Vipi kule Gaza kipigo kinaendeleaje?
 
Nilijua unawasingizia wafuasi wa Brian Deacon.

Hao ndiyo mazezeta namba moja.

Unamuuliza swali biblia mbona inasema hivi na nyie mnafanya vile wanadai hauwezi kuelewa hadi roho mtakatifu.

Wewe mwenye roho mtakatifu fafanua anavuruga mambo.
 
Yesu alikuja duniani kutafuta watu waliopotea katika dhambi ili wamjue,kumpenda na kumtumikia Mungu na kuacha dhambi.
Sioni tatizo unataka watengwe?
Ndo hapo sasa, nani kaumba hayo mashoga? Na kama anachukizwa nayo kwanini anaruhusu yawepo?

Na kama anaruhusu yawepo ana sababu gani ya kufanya hivyo?

Dini badala iwe chombo cha kuunganisha watu inatenganisha

Ushoga ni swala mtambuka hautokaa uishe
 
Kwani Yesu Kristo alikuja Duniani kwaajili ya wenye afya na watakatifu au wadhambi na wahitaji?

Hivi mwenye afya anahitaji tabibu kweli? Na mgonjwa atamuhitaji nani sasa?

Ni Vizuri kujua lengo la kanisa hilo kama limeanzishwa kwajili ya wenye afya na watakatifu basi it's wrong kuwapokea wadhambi, wenye shida na wahitaji.

Lakini kama lilianzishwa kwaajili ya wenye dhambi,shida na wahitaji,then hapo ndipo penyewe, hao ni miongoni mwa wanaostahi huduma za kanisa hilio baraa baraaa...
 
Kanisa ni kwa ajili ya wenye dhambi. Waitwe kwa wingi na waende zaidi mataifa yaliyoruhusu ushoga, waende kuwabatiza kwa jina la Baba na la Mwana na Roho Mtakatifu.

Ndio maana siku hizi makanisa hayakemei dhambi, wenye dhambi (walevi, malaya, wachawi nk) wanatengwa na kusimangwa badala ya kuwekwa pamoja.

Kanisa Takatifu la Mitume limefanya kitu sahihi, bila shaka hao mashoga watapata mafunzo kabla ya ubatizo na kumkiri Kristo na kuachana na ushoga.
 
Kwani Yesu Kristo alikuja Duniani kwaajili ya wenye afya na watakatifu au wadhambi na wahitaji?...

Sasa basi tabia za kuwaexcommunicate watu kwa sababu yoyote ile ziishe!

Unabariki mtu aliyebadili jinsia kuwa mzazi wa ubatizo, what do you expect?

Mdogo mdogo, hatua kwa hatua, mnasogezwa kwenye kukubali Usenge kama ni kitu cha kawaida kisicho na shida yoyote
 
Back
Top Bottom