JWTZ na Serikali waache kudanganya/Kuhadaa Vijana

Central Zone

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
243
372
Hili swala la la nafasi za kujiunga na Jeshi la ulinzi la wananchi Tanzania ni kuwadanganya na kuwahadaa watoto wa maskini Rais na watu wako chini ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga taifa Bashungwa mngeachana nalo tu hili swala, Kwa jinsi mnavyotaka kujisafisha na kujikosha kwa yanayofanyika ndani ya JWTZ na sio kusumbua watoto wa watu, kiukweli ni uhalisia unaofahamika kuwa sahili zote za Makambini Za Vijana Wa Kujitolea Ndani ya jeshi la kujenga taifa bila kuwa na mtu nyuma huwezi enda jwtz hata wenyewe Wanakwambia kwamba hakuna miujiza hiyo pale ni maelekezo tu.

Hizi zinazofanyika kudanganya watoto wa masikini kwamba ni usahili tangu wapo operation makako makuu Dodoma mpaka hawa operation samia hakuna kitu ni rollcall tu ya geresha ili mpate uhalali wa kupitisha watoto wenu wenye maelekezo kwa kisingizio usahili ulifanyika na waliopatikaa ndo hao. Hakuna kitu kama hicho ni kusumbua watoto wa watu.

Sawa kujitolea ni swala moja na kuajiriwa ni swala jingine lakini kama mtu kajitolea kwa miaka miwili na zaidi na nafasi zimetoka sifa na vigezo anavyo inakuaje anaachwa halafu anaenda kuchukuliwa mtu tu aliye nje ya mfumo huko eti kisa tu mkuu anasali nae kanisani ameona kwaya inaimba vizuri anasomba wanakwaya waende jeshini halafu tena watu hao hao wanafika kule wanatoroka au Mnajaza nafasi na kina Ibra Classic halafu tena anatoka unfit

Rais Samia ni heri ingefanyika kama kwa Hayati Magufuli kwamba kama wote wamerudi, warudi wote sio wengine walime na kujitolea si zitoke za ajira wachukuliwe ambao hawakupita kabisa kwenye haya mafunzo ya awali, miaka zaidi ya miwili halafu warudi, kisha watoto wenu na ndugu zenu waliopo uraiani hawajui lolote kuhusu kujitolea mnawapeleka na maelekezo mazito

Kwa mfano kuna hili la juzi vijana waliopo makambini oparesheni samia suluhu walifanya huo wanaoita usahili, yamekuja majina ni watu wale wale waliokwama kule oljoro meseji zilizo zuiliwa ndo yamekuja tena na wengine wamesomwa majina yao tena wakati waliisha andikishwaga(ajiriwa) ni pte sasa hivi Kama kuna kijana anaitwa Abdallah isike huyu alikua kikosi cha oljoro na wengine wengi tu waliisha andikishwaga(ajiriwa) lakini majina yao yamerudi tena hii maanaake nini?

Na sasa hivi tena mmefanya kitu ambacho hakija wahi fanywa na jeshi ili tu mjikoshe katika kuhalalisha kwamba nafasi zilitangazwa lakini sio kweli ni Mnarudisha majina ya watoto wenu tuu ambao majina ni yale yale ya pdf zilizo zuiwa oljoro kwenye ile intake ya 41 ..

Lakini ndani ya jeshi kuna watu ambao bado ni waadilifu sana lakini wanasiasa ndo wanaharibu jeshi letu lilio imara.. lakini ipo siku VIJANA WATACHOKA there is always a first time in everything.​
 
Uko sahihi mkuu Op makao walifanyishwa usaili gelesha mwaka Jana lakini dk za mwisho watu waliondoka kwa meseji hakuna mtoto wa masikini aliyepata na mwaka huu wamerudia vile vile kwa Op Samia ki ufupi hizi saili hua ni zuga tu wakubwa Wana majina yao tayari ila Mimi nawashauri vijana waombe tu huezi jua pengine ya Jana yanaeza yasiwe ya leo
 
Uko sahihi mkuu Op makao walifanyishwa usaili gelesha mwaka Jana lakini dk za mwisho watu waliondoka kwa meseji hakuna mtoto wa masikini aliyepata na mwaka huu wamerudia vile vile kwa Op Samia ki ufupi hizi saili hua ni zuga tu wakubwa Wana majina yao tayari ila Mimi nawashauri vijana waombe tu huezi jua pengine ya Jana yanaeza yasiwe ya leo
Wanaweza beba apo wawili wa kuzugia
 
Uko sahihi mkuu Op makao walifanyishwa usaili gelesha mwaka Jana lakini dk za mwisho watu waliondoka kwa meseji hakuna mtoto wa masikini aliyepata na mwaka huu wamerudia vile vile kwa Op Samia ki ufupi hizi saili hua ni zuga tu wakubwa Wana majina yao tayari ila Mimi nawashauri vijana waombe tu huezi jua pengine ya Jana yanaeza yasiwe ya leo
Hakuna muujiza huo mkuu List ipo tayar, kuingia kwingne ni kwa meseji tu
 
Daah hatariiii Sana
Hii ni hatariiii viongoz wapo ndiyo wanafanya hivi???

Nasema hii ni hatariiii mnoo
Ngoja tuone mwisho wake muda si mrefu itajibu
Haya mambo yamezoeleka tayari hata wenyewe wanasema hawawezi kupinga amri ya mkuu
 
Oljoro bogi zima likajazwa kwa meseji tu Bora hata msata kulikua na mchanganyiko wa mafundi ujenzi, vitengo pamoja na meseji
imagine et ile oljoro ilijaa kwa meseji tuu na tena wengine zilizozuiliwa ndo zinaendelea sasa hivi kwa hivi wanavyotuaminisha ni usahili eti
 
Hapo bila mmbanga maji marefu inatakiwa uwe na vigezo plus mbanga ndio uhakika
li mbuyu ndiyo kila kitu angalia mfano kwenye vigezo cha umri kwa mtu wa elimu ya juu wakiwa wamemaanisha sijui stashahada, shahada na kuendeleea hakuna mwenye umri usio zidi miaka 27 mwenye shahada na amemaliza mkataba huu ni uongo, huyo mtu hayupo
 
Back
Top Bottom