Mwalunenge awapa ukweli Vijana wa UVCCM, awambia waache kuharakia maisha

galimoshi

Member
Aug 5, 2023
9
6
Na Mwandishi wetu

Mwenyiki wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Mbeya Ndugu Patrick Mwalunenge amewasihi vijana wa UVCCM kuwa wavulivu, waadalifu na kutoharakia maisha kwani kwa kufanya hivyo ni kujipotezea mwelekeo.

Akizungumza na Jumuiya ya vijana wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Mbeya Mjini Alhamisi hii, Mwalunenge amesema vijana wengi wa kitanzania wamejawa na tamaa na kukosa subira jamabo ambalo baada ya muda wanapoteza mwelekeo wa maisha yao na wengine kuanza kukata tamaa.

Mwalunenge amewaeleza vijana hao kuwa, yeye kwasasa ni mkurugenzi wa kampuni ya Bens ambayo imeajiri wafanyakazi zaidi 300 na ana shughuli zingine Afrika ya Kusini ambayo ameajiri Wazungu, lakini amefikia hapo kutokana na uvumilivu, uadilifu,uaminifu na nidhamu ya kazi na fedha.

“Unakuta kijana eti anamiliki simu ya milioni tatu, halafu hana ajira, sasa unajiuliza hiyo simu kwanini asiibadili kuwa mtaji ambao, akiamua kuusimamiavizuri baada ya miaka michachache unakua mkubwa, mfano mimi Patrick Mwalunenge nilianza biashara yangu na mtaji wa shilingi kaki mbili tu, lakini sasa naitwa mwajiri” Mwalunenge.

Katika hatua nyingine mwenyekiti Mwalungenge amesema katika kipndi cha uongozi wake wa CCM mkoa wa Mbeya, matamanio yake ni kuona vijana wanabadilika na kuondokana na mitazamo ya kuwaza kuajiriwa serikalini na badala yake wawaze kujiajiri wenyewe kwa kuunganishwa na fursa mbalimbali kikiwemo kilimo.

“Matamanio yangu ni kuona ninyi vijana mnakuwa na miradi mbalimbali ya kufanya, amabayo itawapaatia ajira, kwanza itatakiwa tuwe na mashamba ya kilimo cha mazao mbalimbali kama vile, Korosho, Pareto, Viazi na mazao mengine ambayo yanasitawi huku kwetu, na niwambie tu matajiri wote wakubwa duniani ni wakulima” Mwalunenge

Akijibu ombi la vijana hao la kuwa na mradi wa kushona nguo na viatu, ndugu Mwalunenge amesema atawachangia mashine za kushonea (Cherehani) na atawaunganisha na wataalamu kutoka SIDO ili wawapatie elimu na watapatiwa mitaji ya kuanzia.

Awali mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Mbeya mjini Clemens Mwandemba amesema vinana hao wanayo mipango na mikakati mbalimbali ambayo wanaendelea kuifanyia, kama wazo hilo la kuwa na mradi wa kushona nguo na viatau, ambao wanaamini utawasaidia kujihimarisha kiuchumi.

Amesema vijana wengi wa UVCCM wilaya ya Mbeya Mjini, ni wahitimu wa elimu katika ngazi mbalimbali, lakini changamoto ni kwamba bado hawana hajira, hivyo kuwepo kwa miradi hiyo itasaidia wawo kujiajiri na kuajiri wengine.

“Viana tupo tayari kuumuunga mkono Mheshimiwa Rais wa Tanzania Dokta Samia Hassan Suluhu kwa vitendo, na endapo tutajihimarisha kiuchumi tutakuwa na kunguvu ya kusimama na kukisemea chama bila uwoga maana tutakuwa ni mfano pia kwa jamii zinazo tunzunguka” Mwandemba.[/B]

Aidha vijana hao wamemuomba Mwenyekiti wa CCM Mwalunenge kuongeza msukumo wa baadhi ya miradi mikubwa kama vile ujenzi wa barabara nne katikati ya jiji la Mbeya na mradi wa maji kutoka mto kiwira, kama serikali ya awamu ya sita ilivyoaanza utekelezaji.

Sanjali na hayo Ndugu Mwalunenge amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Samia Hassan Suluhu, kwa kuskuma maendeleo ya nchi, huku akimpongeza Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini na Spika wa Bunge la Tanzania na Rais wa Mabunge Duniani IPU Dr. Tulia Ackson kwa uwakilishi mzuri wa wananchi Bungeni.
 
Back
Top Bottom