JWTZ ina vikosi vingapi?

JWTZ ina vikosi vingapi?

Mantheman6

Senior Member
Joined
May 30, 2020
Posts
169
Reaction score
144
Habari zenu wanaJF naimani wote mkoa poa tukisheherekea sikukuu ya miaka 60 ya Uhuru

Ndugu zangu kama ilivyo kawaida kila ifikapo 9 Desemba vikosi mbalimbali vya kijeshi huenda kutoa burudani kidogo kwa wananchi na viongozi wake kwenye uwanja wa uhuru

Sasa siku ya leo kiukweli nimefurahishwa sana kuona jeshi la uhamiaji wakiongezwa kwenye gwaride kwa mara ya kwanza.

Lakini kubwa zaidi nalotamani kufahamu ni kuhusu aina mbalimbali za vikosi vya jeshi la wananchi jwtz pamoja na majukumu yao.

IMG_9985.jpg

Siku ya leo vimepita vikosi mbalimbali mbele ya rais lakini kuna baadhi ya uniform hatujazoea kuziona zikivaliwa na wanajeshi wetu lakini katika aina tofauti ya vikosi vilivyopita leo pale uwanja wa uhuru tulishuhudia gwanda nyeusi
IMG_9984.jpg

Je hiki ni kikosi gani na wanamajukumu gani?

Lakini wapo pia wanaotofautiana kwenye rangi za kofia naomba kujuzwa kuhusu wao

IMG_9982.jpg

IMG_9986.jpg

Mwisho kabisa nipongeze jeshi letu kwa uzalendo waliotuonyesha leo hakika tupo imara
 
Hao waliovaa mabaka na kofia nyekundu ni kutoka kamandi ya nchi kavu kikosi maalum(komandoo)
Hao waliovaa kama nyeusi/dark blue ni kutoka kamandi ya maji kikosi maalum ie ni makomandoo lakini wa navy
 
Uzalendo sio mavazi au kupita mbele ya jukwaa alilokaa Rais. Shule ikiwa na uniform zaidi ya moja, huwezi ukaihesabu kama ni shule zaidi ya moja.
 
Hao waliovaa mabaka na kofia nyekundu ni kutoka kamandi ya nchi kavu kikosi maalum(komandoo)
Hao waliovaa kama nyeusi/dark blue ni kutoka kamandi ya maji kikosi maalum ie ni makomandoo lakini wa navy

Pamoja sana ndugu
 
Habari zenu wanaJF naimani wote mkoa poa tukisheherekea sikukuu ya miaka 60 ya Uhuru

Ndugu zangu kama ilivyo kawaida kila ifikapo 9 Desemba vikosi mbalimbali vya kijeshi huenda kutoa burudani kidogo kwa wananchi na viongozi wake kwenye uwanja wa uhuru

Sasa siku ya leo kiukweli nimefurahishwa sana kuona jeshi la uhamiaji wakiongezwa kwenye gwaride kwa mara ya kwanza.

Lakini kubwa zaidi nalotamani kufahamu ni kuhusu aina mbalimbali za vikosi vya jeshi la wananchi jwtz pamoja na majukumu yao.

View attachment 2038369

Siku ya leo vimepita vikosi mbalimbali mbele ya rais lakini kuna baadhi ya uniform hatujazoea kuziona zikivaliwa na wanajeshi wetu lakini katika aina tofauti ya vikosi vilivyopita leo pale uwanja wa uhuru tulishuhudia gwanda nyeusi
View attachment 2038371

Je hiki ni kikosi gani na wanamajukumu gani?

Lakini wapo pia wanaotofautiana kwenye rangi za kofia naomba kujuzwa kuhusu wao

View attachment 2038373
View attachment 2038375

Mwisho kabisa nipongeze jeshi letu kwa uzalendo waliotuonyesha leo hakika tupo imara
Next time wamalizie fire brigade na wale jamaa wa porini.

Ila nadhani ujumbe iliotumwa kwa maraisi waliohudhuria umefika kikamilifu Viva jw Viva vikosi vyote
 
Back
Top Bottom