Juu ya DOWANS: Mwakyembe ashangaa kutaka kulipa matapeli

Hatukatai kuilipa Dowans,lakini kabla ya kuilipa ni lazima tujue uhalali wa malipo hayo!!

Mitambo wameleta hawakuleta?
Mitambo imejaribiwa haijajaribiwa?
Mkataba ulivunjwa baada ya kuletwa mitambo au kabla?

Ukijibu hayo maswali utajuwa uhalali wa kulipwa Dowans uko wapi.
 

sitta na mwakyembe hawakuvunja mkataba wa dowans na tanesco!!!karamagi did,..
 

Haya kaseme sasa.....
 
Si uliona shida na dhiki tuliokuwa nayo wakati wa Nyerere kwa ubishi wake? Mwisho akasalimu amri, rejea LONRHO wakati wa Nyerere.

watu wanachohoji ni nani analipwa fedha hizi???obviously ni rostam na lowassa and u know it,walishinikiza from the start mkataba uvunjwe,they premeditated it,idris rashid aliridhia mkataba uvunjwe kwa sababu ana mgao wake,..they r simply partners in crime...usiniulize ushahidi sababu mazingira yanaonyesha,.u and i knw it
 
Mwakyembe huna uadilifu wowote,ulificha baadhi ya data wakati wa kamati yako kwa kisingizio cha serikali kuanguka,,,leo waendeleza unafiki ule ule kwa kushangaa,shame on you
 
Mwakyembe huna uadilifu wowote,ulificha baadhi ya data wakati wa kamati yako kwa kisingizio cha serikali kuanguka,,,leo waendeleza unafiki ule ule kwa kushangaa,shame on you

Bora kasema mengi kaficha machache....ulitaka asiseme kabisa? Wewe ukifumania utasimulia kila ulichoona au vipi?
 

hapo kwenye red, Kwa sababu DOWANS ni JK na JK ndiyo DOWANS.
 
Nyambala,

Hata Fizikia kama hiyo Law of Motion uliyoandika, inafanya kazi kwenye speed zote zilizo chini ya speed ya Mwanga. Zaidi ya hapo hiyo Law haifanyi kazi tena.

Nafikiri hawa dawa ni ndigo sana kwangu mie:

1. Wasilipwe hasa pale HUKUMU ikipelekwa mahakamanin Tanzania kusajiliwa.

2. Walipwe ndiyo ila WAHUSIKA wakamatwe na KUPIGWA RISASI uwanja wa TAIFA.
 
Akifafanua kuhusu msimamo wake wa kitaalamu, ambao alisisitiza ni tofauti na wa kisiasa, Dk. Mwakyembe alisema ana shauku ya kujua ni kwa namna gani serikali imepoteza kirahisi kesi hiyo, ambayo alisema hata mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa digrii ya sheria angeweza kuisimamia na kushinda.
HAPO NDO MJUE KWELI MWISHO WA UBAYA NI AIBU.
 
hebu acha kupotosha watu hapa hiyo redvco na rdl ni kampuni mbili tofauti na ndio maana kwenye report ya mwakyembe kulikuwa na hoja ya "trade as kwamba mojawapo ni jina la biashara na hiyo ya redvco ni kampuni ya ku-print i.e printing company nyingine iliyo tia saini na tanesco haipo kwenye usajili wowote.
 
Thank you. Hawa kina Dr. Mwakyembe na Sitta ni mavuvuzela ya CCM tu hawana lolote.

Walidandia hoja ya ufisadi na kujidai wapiganaji kumbe hamna kitu zaidi ya kuchumia tumbo tu.

Vikaragosi vya ufisadi.....mnaishia kulipwa hela ya bia na sigara , wenzenu wakiwafyonya kwa kuwapigia debe. Shame on you, Ptu! natema mate.....
 
mzee wa kariakoo hebu punguza uongo icc ina shughulika na kutatua migogoro ya kibiashara pande mbili zikikubaliana na hii ni kupunguza gharama za kesi kwenye mahakama za kawaida. hivyo tunaweza tusitekeleze hii hukumu na tukaendelea kufanya biashara na makampuni mengine. biashara za kimataifa zina kuwa regulated na unctad, na protocol zingine za kibiashara kama acp, eu, nk., hii mikataba ya icc pia hutumika zaidi kwenye nchi zenye serikali vigeu geu, ama sivyo sheria za tanzania au za nchi kakamavu zinafaa tu kutumika pale nia nzuri inapokuwepo kati ya muuzaji na mnunuzi. na si kila mkataba lazima uridhie mambo ya icc, na pia sio nchi zote zinaridhia kwenye usuluhishi wa icc. leo hii mimi ninapo nunua gari japan sio kufanya biashara? na je wakinipatia gari tofauti na nilivyo agiza nitaenda icc? ninaweza kufungua kesi huko japan, naweza nikawasiliana na afisa biashara katika ubalozi wao , naweza wasiliana na chambers of commerce yao nk nk, au naweza nikashitaki tanzania na wao wakatakiwa kuja kujitetea, wakikata mahakama inaweza wapiga marufuku kuleta bidhaa zao tanzania nk nk
 
Utachekwa kwa kusema uongo.

Inanijia picha kwamba wewe utakuwa ndio RA au wakala wake aliyejiunga JF kwa malipo toka kwa RA ili atete hoja zinazomhusu RA. Sawa bwana kazi ni kazi ilimradi mkono uende kinywani japo kuwa hii unafanya kazi haramu.
 
Maamuzi ya ICC yana maanisha serikali imeshindwa,ni aibu kwa serikali na taifa kwa ujumla,Serikali ijiuzulu,iundwe serikali ya mpito.Waliokula njama, kuliibia na kusababisha hasara kubwa kwa taifa letu wafunguliwe mashitaka ya kuhujumu uchumi,ikibidi wanyanganywe urai,wafilisiwe mali zao zote,wanyongwe kama China.Hivi ni vita kama vita vya Kagera au vita vya kuzikomboa nchi kusini mwa Afrika.Mapambano bado yanaendelea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…