Augustine Moshi
JF-Expert Member
- Apr 22, 2006
- 2,556
- 1,394
Kama zilitolewa 111.3bn/= kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi, basi mahesabu yako hivi: Ukizigawa kwa wanafunzi elfu 40, kila mmoja anapata karibu shilingi milioni 3 (2,782,555/= to be exact). Kama unazigawa kwa wanafunzi elfu 30, kila mmoja anapata karibu shilingi milioni 4 (3,710,000/= to be exact).
Hii mikopo ni kwa ajili ya wanafunzi wangapi? Kila mmoja alipata kiasi gani? Au hizi fedha zinaliwa wizarani?
Augustine Moshi
mzee kichuguu
nnaamini unahifadhi mchwa na nguchiro bila mkwaruzano
kuna hili jina la mzee mwinyi kuitwa jangala, kwangu ni jipya unaweza kunipa reason behind scene? mana nnajua anaitwa mzee rukhsa pale aliporuhusu watu waaabudu dini watakayo bila ya kuvunjas amani
kima sitokukwaza nnaomba elmu kidogo
mwalimu augustine,well said .maneno mazito haya..nilipoyasoma nimetafakari sana ,kweli kama BILLION 114 zimetolewa na wanafunzi wanolipiwa hawafiki au ni 30,000..na wengi hasa wale wa private univs wanalipiwa only part...na ukizingatia ada nyingi zinarange between 1.5 to3 million...nahisi kwamba kuna uchunguzi unahitajika...sijui kama CAG [MR UTTOUH] alipita huko ,BUT WE NEED THE ACCOUNTS AUDITED tena haraka sana,yawezekana mikopo mingi itakuja shindikana kurudishwa kwa kuwa panaweza kuwa na uwezekano wa kutoa mikopo kwa wanafunzi hewa....au mkopo ukawa zaidi ya kiwango anachostahili mwanafunzi kwa wakati huo.
nimesoma jana [guardian/nipashe] taarifa ambazo zitamsikitisha mzazi yeyote kuhusu baadhi ya wanavyuo waliokosa pesa za kujikimu au kurudi makwao kuripotiwa kuuza baadhi ya personal effect zao na vifaa vingine ,la kusikitisha mabinti zetu wanaingia viwanja [wanakula vichwa]...sasa kweli mnaweka mazingira ya kumfanya maskini huyu ajitahidi kumsomesha mwanaye aje kufa na UKIMWI mara tu baada ya kupata degree yake ,kutokana na ukata aliosababishiwa na serikali!!!!??? tuwe na hurumu...kuna baadhi ya watu kama kulikoni inanibidi nifikiri mara mbili ninaposoma tafakari zao ,ni kama vile hawajui taifa hili MASIKINI WANAFIKIA 80%.
philemon ndio maana uko hivyo kumbe migomo imo kwenye spiritual mood yako
DR KIMARO[YUKO WAPI?},,
PM: MIGOMO kipindi cha mwinyi iliandamana na dukuduku la kutaka mabadiliko ya vyama vingi ndo maana iliwazaa wanaharakati maarufu kama DR KIMARO[YUKO WAPI?},JAMES MBATIA , NAwengine wengi[kichuguu naomba tukumbushe viongozi wa ule mgomo maarufu]..huu ndio mgomo uliokomesha utaratibu wa rais wa nchi kama ilivyo kenya na uganda kuwa chancellor wa state university kwa hapa tanzania....mwiyi alishindwa kuwavumilia ...lakini kama sikosei na hawa walirudishwa kwa wazazi wao.hawakutelekezwa manzese wanye tapu tapu....
kichuguu,
Matiko Matare, na James Bazigiza, waliishia wapi? Mzee Ruksa alitia aibu sana jinsi alivyoushughulikia mgogoro ule wa UDSM.
Kama kuna mtu anaweza kunisaidia kuelewa serikali ilifikia fikia vipi uamuzi wa wanafunzi kuchangia asilimia 40 na siyo 50/50 au 15/85? kwanini 40%?