George Mason University, Virginia, USA, ada ya mwanafunzi kwa mwaka ni US $.3300. Kima cha chini cha mshahara US $ 6.50. Ikiwa mwanafunzi atafanya kazi mwaka mzima na kusave pesa zote basi anaweza kuwa na akiba ya walau US $ 10000.
Is it true kwamba kila mwanafunzi anapaswa kulipa TShs.2,000,000?? Kiwango hiki wamekipata kwa kuzingatia vigezo gani? Yaani ktk hili la kuchangia masomo, Mtanzania anashindana na mwananchi wa Marekani!!
Baada ya hapo, hebu chunguza mazingira ya elimu[academic & proffesional environment] ya GMU halafu linganisha na yale ya UDSM. Kama mwanafunzi analazimishwa kulipa Tsh 2,000,000[if that is true] halafu anasikiliza mihadhara kwa kuchungulia madirishani, au kwa kusimama kwa vile hakuna madawati, basi serikali inawaibia.
Kwa malipo ya Tshs 2,000,000[US $ 2000] wanafunzi wa UDSM walipaswa kupatiwa maktaba,lecture rooms, maabara, na karakana za kiwango cha juu zaidi ya zilizopo sasa hivi.
http://admissions.gmu.edu/common/UndergraduateTuition.asp
Si sahihi kwa watu kusema wanafunzi wamekosea. Dhana ya mgomo ni wao kushitaki kwa jamii kwa kero zao ambazo serikali haitaki kuzisikia.
Hivi hizo kazi za mtaani mnazowataka hao wanafunzi wakafanye ziko wapi?Kuna watu wamemaliza masomo na wana Qualifications zao nzuri na uwezo kikazi na KAZI KUPATA SHIDA,Wachilia kazi hata kibarua na akibahatisha malipo yake ni madogo chini ya dola mia au mia ,hiyo ni kutoka asubuhi hadi jioni ,usafiri wa taabu akirudi nyumbani ni usiku ,sasa sijui kama ni mwanafunzi atahudhuria vipindi muda gani na atasoma muda gani?Bongo Hakuna kazi za masaa au shift kwa makampuni mengi ya watu binafsi.!Hili ndilo nililosema hapo mwanzo. Huwezi kuendesha chuo cha dar es Salaama kwa kutumia mfumo wa maisha wa marekani kwa vile mazingira yake ni tofauti kabisa. Kudai kuwa mwanafunzi wa UDSM akafanye kazi mitaania ya kumsaidia kulipia gharama za chuo ni ndoto ya alinacha.
Mwajiri gani bongo atakubali akupe nafasi ya kufanya mafunzo kwa vitendo halafu bado akulipe na mshahara.Mara nyingi vyuo husika vinaomba sehemu fulani fulani na hasa ni serikalini na mara chache watu wanajitafutia wenyewe,Kwa mfumo wetu wa bongo ukisikia Field work basi ujue ina sehemu yake katika kufikia lengo la wewe kuwa mhitimu si swala la hiari ni lazima.Na watu wengi hupelekwa sehemu za mbali ukiwacha wachache wanaobahatika kubaki Dar au Morogoro kwa SUA.kichuguu,mwanasiasa,KNKCU,
nina tatizo na hizo fedha za field-work. kwanini wanafunzi wasilipwe na makampuni wanayokwenda kuyafanyia kazi? kwenye nchi za wenzetu field-work/internship huwa ni jukumu la mwanafunzi mwenyewe kutafuta. .
Wanafunzi wa udaktari,wafamasia , wahandisi na wanasheria kwa Field work kwa mfumo wetu ni lazima na inachangia towards your degree.Na si hao hata vitivo vingine.Na hulipwi.Kuhusu Internship kwa Madaktari na wafamasia na wanasheria ni lazima na kwa upande wa madaktari na wafamasia ninahakika wanalipwa na internship zao ni baada ya kuhitimu.sina uhakika kwa Madaktari na Mafamasia, lakini kwenye field nyingine fieldwork/internship huwa hai-count towards the degree..
Hapa ninakubalina nawe kuanzia kwenye kuchangia mpaka kwenye kufanyakazi kwa wanafunzi wetu ni vigumu.Hii inatokana na mfumo wetu wa elimu na kwa upande mwengine ugumu wa upatikanaji wa kazi kwani Hakuna NAFASI NYINGI ZA KAZI ZINAZOTENGENEZWA na kwa wazazi kipato ni kidogo hakikidhi na kuwawezesha kuwalipia watoto wao .Nafikiri Mikopo kwa asilimia 100 ni suluhisho zuri tu kwasasa na wale waliokopa ni vyema wakarudisha.Mimi mgogoro wangu ni huo wa kuchangia gharama za masomo ambazo nadhani ni kubwa mno kwa Mtanzania wa kawaida.
Tatizo letu Tanzania ni kwamba viwango vya malipo ya kazi haviendani kabisa na gharama za huduma/maisha. Kama nilivyoonyesha in my previous posting, katika nchi za wenzetu, mwanafunzi anaweza kujilipia Chuo Kikuu kwa ku-serve malipo ya kazi ya kima cha chini.
Kuhusu suala la kuiga, naomba ieleweke kwamba: mwanafunzi anayesoma FULL-TIME hawezi kufanya kazi hata part-time. Ulaya na Marekani, ukiona mwanafunzi anasoma na kufanya kazi ujue huyu ni PART-TIME STUDENT. Hapa ninazungumzia Universities zinazotambulika na kuheshimika.
Kitu kingine kinachowasaidia wenzetu hasa Marekani ni mfumo wa semester system. Vilevile mwanafunzi anaruhusa ya kuchagua masomo anayoona atayamudu kulingana na mazingira yake in a particular semester.
In case mwanafunzi analazimika kufanya kazi na hatukuwa na muda mwingi wa kujisomea basi huchagua masomo rahisi kidogo. Kwenye semester ambayo anaona ana masomo magumu basi huacha kazi na ku-concentrate kwenye masomo. Hilo haliwezekani kwa mfumo wetu wa masomo UDSM.
kichuguu,mwanasiasa,KNKCU,
nina tatizo na hizo fedha za field-work. kwanini wanafunzi wasilipwe na makampuni wanayokwenda kuyafanyia kazi? kwenye nchi za wenzetu field-work/internship huwa ni jukumu la mwanafunzi mwenyewe kutafuta.
sina uhakika kwa Madaktari na Mafamasia, lakini kwenye field nyingine fieldwork/internship huwa hai-count towards the degree.
Mimi mgogoro wangu ni huo wa kuchangia gharama za masomo ambazo nadhani ni kubwa mno kwa Mtanzania wa kawaida.
Tatizo letu Tanzania ni kwamba viwango vya malipo ya kazi haviendani kabisa na gharama za huduma/maisha. Kama nilivyoonyesha in my previous posting, katika nchi za wenzetu, mwanafunzi anaweza kujilipia Chuo Kikuu kwa ku-serve malipo ya kazi ya kima cha chini.
Kuhusu suala la kuiga, naomba ieleweke kwamba: mwanafunzi anayesoma FULL-TIME hawezi kufanya kazi hata part-time. Ulaya na Marekani, ukiona mwanafunzi anasoma na kufanya kazi ujue huyu ni PART-TIME STUDENT. Hapa ninazungumzia Universities zinazotambulika na kuheshimika.
Kitu kingine kinachowasaidia wenzetu hasa Marekani ni mfumo wa semester system. Vilevile mwanafunzi anaruhusa ya kuchagua masomo anayoona atayamudu kulingana na mazingira yake in a particular semester.
In case mwanafunzi analazimika kufanya kazi na hatukuwa na muda mwingi wa kujisomea basi huchagua masomo rahisi kidogo. Kwenye semester ambayo anaona ana masomo magumu basi huacha kazi na ku-concentrate kwenye masomo. Hilo haliwezekani kwa mfumo wetu wa masomo UDSM.
Inategemea unasomea nini? Na vyuo vingi kwa mwaka wa kwanza kwa marekani huruhusiwi kufanyakazi kama ni mwanafunzi wa kigeni lakini kama ni Muhamiaji ni kivyakovyako utakavyoweza kujipanga.Kwa uingereza ukishapata ukipata namba tu mwendo mdundo kivyakovyako!Ndugu yangu JokaKuu, labda nikupe taarifa ya kusikitisha kuwa hata bila malipo, makampuni hukataa kuwachukua vijana wetu kwa ajili ya fieldwork! Sasa kama utataka walipe na kulipa sijui nani atawachukua hao vijana. Sitaki kuongelea hapa uwezo wenyewe wa vijana wetu, hiyo ni mada ya aina yake.
Naomba pia nitifautiane nawe kuwa wanafunzi wanaofanya kazi marekani ni wale tu wanaosoma part-time. Hii sio kweli hata kidogo, labda ni experience uliyo nayo katika vyuo ulivyopita wewe. Lakini ukweli ni kuwa katika vyuo vingi wanafunzi wawe parttime au full time wanachapa mzigo. Isipokuwa kuna limitation ya masaa ya kufanya kazi. Tena wabongo waliosoma fulltime ulaya na marekani wakikusimulia walivyokuwa wanachapa mzigo, acha kabisa! Hivi niandikapo hapa kuna wanafunzi fulltime wanaosha masufuria, wanasafisha vyoo, n.k.