Kufungwa kwa chuo kikuu, ni ishara nyingine inayotuonyesha ni jinsi gani serikali yetu ilivyodhaifu, kwa kutumia nguvu nyingi kwa wanyonge na kuwakumbatia wenye mali.
Mahojiano ya Prof Mkandara, wakati akiongea na waandishi wa habari inadhiirisha yao.
-Prof Mkandara alikiri kuwa kuondesha chuo kwa siku inagharimu kiasi cha Tzs 100 million.
-Amezungumzia pia misaada inayotolewa na wafadhili wa nje kuendesha chuo inatokana na stability ya chuo, kama chuo kitafungwa kila mara kuna hatari ya kuwapoteza hawa fadhili.
-Elimu ni biashara, amekiri pia kuna hatari ya kuwapoteza wanafunzi wanaotoka nchi za nje ambao wao huchangia kwa kiasi kikubwa, kwani wanalipa kwa fedha za kigeni.
Kwa kukubaliana na serikali kufunga chuo, prof mkandara ameonyesha udhaifu mkubwa, huyu si yule mkandara wa miaka ya 1998 nilipokuwa UD.
Prof mkandara, anatamka mbele ya waandishi wa habari, kuwa hakuna mwananfunzi atakayeruhusiwa kurejea chuo, ila kwa kuja na cash au bank deposit slip ya 40%, hii ni dhihaka ya mwaka.
Kwanini wauza madawa ya kulevya, walarushwa, na wakwepa kodi anakumbatiwa ili hali nguvu nyingi inatumika kuwakandamiza wanyonge wasio na sauti.
heshima itakuja pale damu itakapo mwagika.