TANZIA Mbunge Mkongwe wa Uganda na Jenerali Mstaafu Moses Ali Afariki Dunia akiwa na Miaka 87

TANZIA Mbunge Mkongwe wa Uganda na Jenerali Mstaafu Moses Ali Afariki Dunia akiwa na Miaka 87

Fbn

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
15,759
Reaction score
37,336
Uganda imepoteza mmoja wa wanasiasa wake wakongwe zaidi baada ya taarifa kuthibitisha kuwa Jenerali mstaafu Moses Ali, Mbunge wa Adjumani West County na aliyewahi kuwa Naibu Waziri Mkuu wa Pili wa Uganda, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 87.

Moses Ali alizaliwa tarehe 5 Aprili 1939 katika Wilaya ya Adjumani, kaskazini mwa Uganda. Kwa zaidi ya nusu karne, alihudumu katika jeshi, serikali na bunge la Uganda, jambo lililomfanya kuwa mmoja wa viongozi waliodumu kwa muda mrefu zaidi katika siasa za nchi hiyo.

Licha ya umri wake mkubwa, Moses Ali aliendelea kuonyesha nia ya kuendelea kuwatumikia wananchi. Mwaka 2024 alitangaza wazi kuwa angegombea tena kiti chake cha ubunge katika uchaguzi wa 2026, akisema bado alikuwa na kazi ambazo hajamaliza kwa wananchi wa Adjumani West.

Katika maisha yake ya kisiasa, Moses Ali aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali za juu serikalini, ikiwemo Waziri, Naibu Waziri Mkuu na Mbunge. Alijulikana kama mmoja wa wanasiasa waliokuwa na ushawishi mkubwa katika historia ya Uganda na alihudumu chini ya tawala tofauti kwa miongo mingi.

Kifo chake kinaashiria mwisho wa enzi ya mmoja wa viongozi walioshuhudia na kushiriki sehemu kubwa ya historia ya kisasa ya Uganda. Wananchi wengi wa Adjumani na Uganda kwa ujumla wanamkumbuka kwa mchango wake katika siasa, usalama na maendeleo ya taifa hilo.

FB_IMG_1784387263077.jpg

 
Screenshot 2026-07-18 at 19-10-39 Gen Moses Ali Confirmed Dead ChimpReports.png

Gen. Moses Ali, Uganda’s longest-serving Cabinet Minister and former Second Deputy Prime Minister, has died. He is remembered as both a soldier and a statesman whose career spanned decades of service in government and the military.

Beyond his national leadership, Gen. Ali was also a father figure, with his son, Ali Siraj, currently serving as the Minister of State for Works.

His long tenure in Cabinet made him a central figure in Uganda’s political landscape, contributing to governance and stability across successive administrations.

Also Read:Concern grows over Gen Moses Ali’s health as he remains hospitalised
 
Museven hafikishi huo umri walahi.
R.I.P Mbunge
 
images.webp

Aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu wa Pili wa Uganda na mwanasiasa mkongwe, Jenerali Moses Ali, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 87 wakati akipatiwa matibabu.
 
Jamaa alipata ugonjwa wa Ajabu mno.
RIP.

Japo mimi hawa Askari na Wanajeshi siwapendi sana
 
Kunahuyu rais wa sudani sijui anaitwa krrrr hivi ana seath proof maana ana 0 brain afu wasudani wanamchagua tu
 
Back
Top Bottom