Jumatano natakiwa nikapime UKIMWI, confidence zero

Jumatano natakiwa nikapime UKIMWI, confidence zero

Hope mlishspima wote na sasa mna majibu. Yawezekana hata ndoa tayari. Haitakiwi kumwamini mtu katika hili
 
Kapime bana.......sio ngumu.........unafika Angaza.......unakaa kwenye stuli.......anachukua kidude tu kidogo cha karatasi.......anakutoboa kidogo anaweka damu kwenye hicho kikaratasi na kidrop kidogo tu cha kidawa......sijui ni kidawa gani kile......basi damu inaanza kupanda.......inapanda weeeeee........mstari wa kwanza inapita inaenda wa pili.......inagomea pale........
anakwambia upo safi..........ugumu hapo upo wapi........?

...hiyo ya kupewa majibu hapohapondo staki hata kuisikia, kupima inataka moyo mama. sio kukurupuka tu aiseee
 
Wala hapatishi, ni kama vile upo sebuleni unaangalia katuni. Ukishaingia tu wanajua shida yako ni kupima. utaulizwa ni mara ya ngapi utajibu, utaulizwa umekuja na mwenzako utajibu ndiyo au hapana. Kuna kikaratasi nesi atakuandikia pale, unaweza kuwa peke yako au mkawa wengi kwenye hicho chumba ila majibu hampewi kwa pamoja ni mmoja mmoja. Utachukuliwa damu, utaambiwa subiri huku ukiwa unapewa ushauri na kuliwazwa. Yakiwa tayari utapewa majibu yako, ukiwa safi mchezo umeishia hapo utapangiwa tarehe nyingi ya kurudi kupima tena, ukiwa unao kazi inaanzia hapo utaanzishiwa klinik.
 
...hiyo ya kupewa majibu hapohapondo staki hata kuisikia, kupima inataka moyo mama. sio kukurupuka tu aiseee

Majibu hapo hapo ndio poa ujue.........kusubiri inataka moyo sana.........na mpaka ufikie stage ya kwenda kupima........si utakuwa umeshashauriana na akili yako mkuu........binafsi nikipima baada ya dk 5 uniambie nirudie lazima kiumane............
 
Wakuu salama.

Wandugu jumatano,tarehe 05.11.2014 natakiwa niende angaza kupima UKIMWI hapa nilipo confidence ni zero inaelekea negative.

Kwa kawaida mimi huwa najiamini kupita kawaida kwa kila jambo nalofanya lakini hili la ukimwi confidence imedrop significantly.

Kiukweli sijawahi kupima ukimwi toka nimezaliwa,kuna binti kaniambia hawezi kukubali kutoka nami bila kupima,alinipa interval ya miez 3 nikamshawishi hadi akakubali tufanye angalau test 1.

Sitaki kumkosa huyu binti na naogopa kupima,ebu nipeni makonfidensi wakuu

Mh kupima ukimw inataka moyo sana lkn tunapasw kujua afya zetu kaza moyo ukimwi co kufa bwana
 
Kapime wala usiogope..!
Mie hui ushauri nasaha ndio siufagilii..!
Naenda straight maabara, naacha kisusio, narudi baada ya mda naongea na dokta...nachukua mzigo...na nimemaliza..!
Ushauri nasaha ndio unaongeza presha...!

Mm naenda ushaur nasaha nibembelezwee hlf napima
 
Nilikuwaga muoga sana...ila mwezi huu sijui ujasiri ulitoka wapi!? Nilijibeba mwenyewe kwenda kupima!!
 
Ukimwi usikie kwenye vyombo vya habari.. ukimpata hata ndugu yako its very touching n painful
 
Siku naenda kupima nakumbuka siku ya nyuma yake sikupata usingizi ila baada ya kupima nilijikuta mwepesiii...toka siku ile nimekoma kuchepuka!
 
mi pia nimeambiwa bira kupima nisahau penzi lake, nimemwambia siko tayari kupima kwasasa anadai naogopa kwasababu najua ninao. but sio kweli maana sijapima bado. lakini siko tayari kupima kwasasa. na hawezi nshinikiza kupima
 
Nilipima nikasema siwezi kugonga demu tena ikapita mwezi nikapiga demu tena kavukavu mbaya zaidi nikaambiwa anangoma nikakonda bila kupima nikaamua kuliko kujitesa bora nikapime kupima nipo vizuri nikapiga na kashere kisela, juzi juzi hapa nikapiga kademu ila nilikuwa nimevaa combati na wala sijapiga denda na kutoa kondom nimevaa grooves ndo nikatoa.
 
Nilipima nikasema siwezi kugonga demu tena ikapita mwezi nikapiga demu tena kavukavu mbaya zaidi nikaambiwa anangoma nikakonda bila kupima nikaamua kuliko kujitesa bora nikapime kupima nipo vizuri nikapiga na kashere kisela, juzi juzi hapa nikapiga kademu ila nilikuwa nimevaa combati na wala sijapiga denda na kutoa kondom nimevaa grooves ndo nikatoa.

ha ha ha mpaka kasherehe duh!!
 
ha ha ha mpaka kasherehe duh!!

Jamani hii kitu tunaipenda very sweet but ikifika suala la kupima gumu sana.
Nakumbuka nilivoenda kupima mbaya zaid nikambiwa majibu kesho. Sikulala usiku mzm nawaza. Da inataka moyo sana.
 
Back
Top Bottom