Jumatano natakiwa nikapime UKIMWI, confidence zero

Jumatano natakiwa nikapime UKIMWI, confidence zero

Pole kwanza lakini wacha kukwambie kweli kupima sio jambo rahisi ,mimi nipime jana na leo unambie tupime tena basi tumbo
lakuharisha litazuka hata lilipo tokea silijui hiyo ni kawaida lakini ukisha maliza kupima sikufichi utafurahia maisha japo huna hela mfukoni sababu afya ndio mpango mzima na utapenda umwambie mwenzio aende.. sikuizi mwenzio nna vile vipimo najipima mwenyewe manake uko kwenye majibu hayo maneno yao ndio full Bp............
Umenikumbusha sister wangu alitoka jasho mpaka la nyayo, akiangalia mume anamtaka issue ni kupima aliharusha usiku kucha... ...
 
Wakuu salama.

Wandugu jumatano,tarehe 05.11.2014 natakiwa niende angaza kupima ukimwi,hapa nilipo confidence ni zero inaelekea negative.

Kwa kawaida mimi huwa najiamini kupita kawaida kwa kila jambo nalofanya lakini hili la ukimwi confidence imedrop significantl.

Kiukweli sijawahi kupima ukimwi toka nimezaliwa,kuna binti kaniambia hawezi kukubali kutoka nami bila kupima,alinipa interval ya miez 3 nikamshawishi hadi akakubali tufanye angalau test 1.

Sitaki kumkosa huyu binti na naogopa kupima,ebu nipeni makonfidensi wakuu

Mkuu ni vema wewe na huyo binti muende wote kupima Angaza. Mtapewa majibu na ushauri kwa pamoja.

Kwa wanaume wenzangu, kucheza mechi bila viatu ni ujinga wa hali ya juu. Tuwe makini sana na uraka (pombe) kwa sababu maamuzi yote ya maana yana sepa geji ikiwa juu.
 
Kapime tu mkuu, kwa msoso wetu ingelikua unao ungeshatoa symptom
 
Nenda kapime kwanza ukishajijua uko fiti, unaenda nae ila kama umekanyaga miwaya unamzingua kwa kupiga kimya.

nakubaliana na wewe. jamaa inabidi akapime akiwa peke yake kwanza, mambo yakiwa poa ndio aongozane na huyo binti kwenda kupima tena
 
kupima ukimwi sio shida,sheeeda ni kupokea majibu, maana majibu huwa ni kama ya msiba na majibu yakiwa mabaya malengo yote uliojipangia yanavurugika
 
The best way to stay negative is not to test at all

Kupima ukimwi sio mchezo,unaweza kujikuta umepatwa na cardiopulmonary arrest hivi hivi kijinga jinga.

Hapa nawaza sana kuhusu huo mtihani,leo nimeonana nae,nikaonyesha hamu sana ya kwenda kupima nae,akaniambia wanaume wengi waliomtaka walikimbia hiyo hatua ingawa kiukweli deep inside nina wasiwasi kinoma.

Naona kwa makonfidensi ninayomuonyesha kama anaelekea kulegeza msimamo,ngoja tuone hiyo jumatano itakuwaje.
 
Mkuu ni vema wewe na huyo binti muende wote kupima Angaza. Mtapewa majibu na ushauri kwa pamoja.

Kwa wanaume wenzangu, kucheza mechi bila viatu ni ujinga wa hali ya juu. Tuwe makini sana na uraka (pombe) kwa sababu maamuzi yote ya maana yana sepa geji ikiwa juu.

Mkuu unachokisema kina ukweli ndani yake ingawa mimi situmii kilevi chochote.

Muda mwingine inatokea tu unajikuta umeuza mechi. Kuna viwanja vingine sio mchezo mkuu.

Tunatakiwa kuchukua tahadhari sana ingawa pia kondom haitoi guarantee ya usalama wako,the best way ni kuacha ngono vinginevyo hatutapona.
 
Pole kwanza lakini wacha kukwambie kweli kupima sio jambo rahisi ,mimi nipime jana na leo unambie tupime tena basi tumbo
lakuharisha litazuka hata lilipo tokea silijui hiyo ni kawaida lakini ukisha maliza kupima sikufichi utafurahia maisha japo huna hela mfukoni sababu afya ndio mpango mzima na utapenda umwambie mwenzio aende.. sikuizi mwenzio nna vile vipimo najipima mwenyewe manake uko kwenye majibu hayo maneno yao ndio full Bp............

Yani mimi nikiwaza kuhusu jumatano kupima gafla hata kama nimeshiba nahisi njaa ya hatari kama sijala siku 3,jasho hadi sehem za siri.
 
Hapana usijal, inawezekan, mi kwa miaka ming mwaka huu ndio nimepata nguv na nimepima zaid ya mara mbil na kufuata majibu. Ila nenda hospital za kulipia kwan ki ukwel wale wa kuanza kuulizana kwann, umefikiria nn, yakiwa mabay utafanyaje!? Wale mi cwapend na wanazingua!?
 
Mwambie huyo Mwanamke akitaka mjuwe afya zenu mkapime full medical examinatin, wajinga wengi wanadhani ukimwi ndio wa kupimwa kumbe wana ngwengwe zao na hawajijui.
 
Fasta kapime. Hiv siku hizi ni jambo la kawaida. Wenye cancer watakufa wataluacha unaishi.
 
Back
Top Bottom