Fred Mwakitundu
JF-Expert Member
- Dec 31, 2018
- 227
- 383
Miezi michache baada ya kuvuliwa umeya kutokana na kashifa ya kudaiwa kuhudhulia sherehe ya siku ya kuzaliwa kwa mmoja wa wanumme wanaodaiwa kuwa katika mahusiano ya mapenzi ya jinsia moja, aliyekuwa meya wa Manispaa ya Moshi, Juma Raibu ameingia katika kashifa nyingine tena, akidaiwa kumtishia kumtwanga rasasi diwani mwenzake.
Taarifa kutoka ndani ya Baraza la Madiwani wa Manispa ya Moshi zinapasha kuwa tukio hilo lilitokea hivi karibuni muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati ya Mipango Miji.
Inadaiwa kuwa kwenye kikao hicho, diwani wa Kata ya Miembeni, Mohamed Mushi, alihoji juu ya uhalali wa Juma Raibu kumilikishwa kiwanja kinachodaiwa kuwa ni eneo la wazi ambako tayari amezungushia uzio tayari kwa kuanza ujenzi wa vibanda vya maduka.
Baada ya kuhoji, inadaiwa Juma Raibu alihamaki na kuanza kumtishia diwani huyo kwamba atamteketeza yeye na familia yake huku akimtolea lugha za matusi ya nguoni ambayo kutokana na misingi ya kimaadili hatuwezi kuyaweka hapa.
Mohamed amezungumza na Jamiiforums na kukiri kutokea kwa mkasa huo na kwamba anajiandaa kupeleka barua yq malalamiko kwenye kamati ya maadili ya chama cha mapinduzi.
Amesema chanzo cha hayo ni mapema mwaka jana wkaiwa kwenye changuzi za viongozi ndani ya chama(CCM),Raibu alifika kwenye kata yake(miembeni)kwa lengo la kumnadi kiongozi mmoja.
Amesema kuwa baa ya kumuono akahoji iweje aende kwenye kata yake bila kumtaarifu kutokana na kikao hicho kuwa ni cha ndani cha kamati ya siasa ya kata.
Kutokana na hilo Mohamed anasema malalamiko hayo yote ya mwaka jana na mwaka huu ameyawasilisha kwa uongozi wa chama kwa ajili ya hatua zaidi.
Itakumbukwa kuwa mwaka jana madiwani 19 walipiga kura ya kutokuwa na imani na Raibu huku kumi wakimuunga mkono baada ya picha kusambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha akilishwa keki kwenye sherehe ya kijana mmoja anayedaiwa kuwa kwenye uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja .
Nini kinaendelea katika sakata hilo na je unajua Raibu kamtolea kashifa gani diwani huyo?,usikae mbali kesho tunakuletea picha lote.
Nawatakia Sabato njema