TANZIA Juma Jerry (almaarufu Mzee wa Mbezi) wa TOT afariki Dunia

1589196512823.png


Aliyekuwa mpiga kinanda nguli wa Kikundi cha CCM cha Tanzania One Theatre (TOT) au TOT Plus Juma Jerry au Mzee wa Mbezi ( dunia (Pichani) amefariki

Akithibitisha kifo hicho Mkurugenzi wa TOT Gasper Tumaini amesema Jerry amefariki dunia leo katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam, alikokuwa akitibiwa.

Tumaini amesema Jerry alilazwa Lugalo tangu jana akipatiwa matibabu ya presha aliyokuwa akiugua kwa mda mrefu.

Jerry pia alikuwa Mwenyekiti wa muda wa Chama cha Wanamuziki wa Taarab Tanzania.
 
J J eeeh!
Sema Banza!
Ya kwake ndogooo!
Ya mwenzie!?
Kubwaaaaaaaa........!
Nini hiyo!?
Aaah!.....simu ya mkononi!

R.I.P JJ mzee wa mbezi!
 
View attachment 1447041


Mpiga kinanda maarufu wa Bendi ya Tanzania One Theatre (TOT), Juma Jerry 'JJ Mzee wa Mbezi' amefariki dunia leo Mei 10, 2020.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa TOT Gasper Tumaini, marehemu amefariki leo jioni katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa tangu jana Mei 9, 2020 ambapo alikuwa anasumbuliwa na shinikizo la damu.
Ni Abdallah Kitia au Juma Jerry ama ndio huyo huyo?!
 
Back
Top Bottom