TANZIA Juma Jerry (almaarufu Mzee wa Mbezi) wa TOT afariki Dunia

Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
3,767
8,683
FB_IMG_1589150199652.jpg


Aliyekuwa mpiga kinanda nguli wa Kikundi cha CCM cha Tanzania One Theatre (TOT) au TOT Plus Juma Jerry au Mzee wa Mbezi ( dunia (Pichani) amefariki

Akithibitisha kifo hicho Mkurugenzi wa TOT Gasper Tumaini amesema Jerry amefariki dunia leo katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam, alikokuwa akitibiwa.

Tumaini amesema Jerry alilazwa Lugalo tangu jana akipatiwa matibabu ya presha aliyokuwa akiugua kwa mda mrefu.

Jerry pia alikuwa Mwenyekiti wa muda wa Chama cha Wanamuziki wa Taarab Tanzania.
 
Mpiga kinanda maarufu wa TOT Juma Jerry amefariki dunia muda huu.

Mkurugenzi wa TOT, Gasper Tumaini ameiambia Saluti5 kuwa Juma Jerry amefariki katika hospital ya Lugalo jijini Dar es Salaam.

Tumaini amesema Juma Jerry alikuwa anasumbuliwa na presha na alilazwa Lugalo tangu jana.View attachment 1446523

Sent using Jamii Forums mobile app

Kunakucha j3 hiyo hadi ijumaa ID ikiupiga kimya, isiwe muhani tukutane mbinguni.

Tutegemee ukimya tena jumamosi na jumapili tukijaaliwa kuwapo.

Eeh mola wetu hebu utunusuru na wabaya wetu wote waliodhamiria kututoa kafara kwa ubinafsi wao.

Mkuu tangulia twaja, tu nyuma yako.

RIP.
 
Mkuu siyo kila msiba. Hawa ni watu na majina au CV zao.

Kina kajamba nani humu hawafiki mkuu. Nani atawajua?
Hapana mkuu , nadhani kuna watu wwnataka tu kuongeza taharuki juu ya korona ,
Kuna watu wengi maarufu mwaka jana niaowajua walifariki na hawakuletwa humu,
Jf ni media kubwa sana East Africa , sijui kama Kuna forum hapa Ea amabayo ni popular zaidi ya jf tunapoitumia kwa ku feed taarifa za taharuki Ina tu expose in a wrong way. Hasa kwa majirani zetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu hawatak kulala wanaogopa watafia usingizin
Kataa hofu ya kufa
Jaman Nipo kwenye maombi Sasa hivi hapa dunian tunapita tuu jiandae muda wowote unaondoka

Eeh Mungu nipe mwisho mwema

Sent by IPhone
 
Raia hawashtuki tena kusikia mtu kafa, wamekufa wabunge, waziri, wakuu wa wilaya hawajaona mabadiliko yoyote, ndio kwanza wanapewa miili wakazike wenyewe, litakalowakuta shauri yao, wanachokifanya wanaendelea na mishe zao tu, liwalo na liwe. Tatizo coona ukijifanya kiburi anakuziba mdomo, kudadeki.
 
Acha uongo mbona huku mtaani kwetu walifariki watu wawili ndani ya siku moja sikuona habari humu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hilo la kufariki watu wawili mtaani kwa siku moja nalo ni geni mkuu? Kweli korona ipo na inaua
sana tuchukue tahadhari binafsi Mana ni kama hatuna muongozo kutoka serikalini illa pia ni wakati muafaka wa kupunguza kuleta taarifa zenye taharuki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom