Julius Mtatiro naye anasubiri siku tu

Julius Mtatiro naye anasubiri siku tu

Nape alimpa CCM lazima ishinde hata kwa goli la mkono
 
Julius S. Mtatiro
11 hrs ·
USHAURI WA BURE.

Msiwatukane wanaohama kwenye chama chenu ili siku wakirudi msianze kazi ya kusameheana matusi yenu na ama kununiana.

Kafulila alikulia ndani ya CHADEMA, baadaye akahamia NCCR MAGEUZI, kisha akarejea tena CHADEMA na hivi sasa amehamia CCM (amehama vyama mara 4).

Na mfano mwingine ni mwalimu wangu Prof. Kitila, amekulia ndani ya CCM (sina hakika kama aliwahi kuwa NCCR) lakini tunajua alihamia CHADEMA, akatoka CHADEMA akaanzisha ACT, na sasa ameiacha ACT amekwenda CCM.

Huo ni ushahidi thabiti kuwa wapo wanasiasa safari zao kisiasa huwa ziko namna hiyo, huhangaika sana lakini kibinadamu lazima tuwaheshimu kwa dhati. Hata binadamu anapokuwa anafariki yupo ambaye hufa kwa utulivu na yupo ambaye hufa kwa kuhangaika sana.

Msishangae kuwa baada ya mwaka mmoja au miwili Kafulila akarudi CHADEMA, Masha akaenda ACT, Patrobas akaenda CUF na Kitila akaanzisha chama kipya.

Kama mnachanganywa na hali hii ya sasa inaonekana mtakuwa wendawazimu kabisa siku mtakaposikia Kafulila ameichoka tena CCM na anahamia ACT na akitoa hoja kuwa "CCM imeshindwa kuongoza nchi!"

Msichanganywe na hali ya sasa ili msije kupumbazwa na hali ya baadaye. Nawasisitiza, waheshimuni wahamao, Songeni UGALI wenu na laleni usingizi, hakika kesho kutakucha na hali ya uchumi wa nchi itaendelea kudidimia, pambaneni na hali zenu, waacheni wahamao nao wapambane na hali zao.

Mtatiro J
waacheni wanaohama wapambane na halizao
 
Jamii Forum ina vichwa vya hatari mnoo. Kumbe kuna mdau alikuja akaliandika hili humu ndani kwa ufasaha kabisa zaidi ya miezi Tisa iliyopita kuwa Mtatiro alishafikia bei.

Kweli nimeamini wanasiasa wachumia tumbo ndio wanaonunulika vizuri kwa sasa.
 
Ijue rasmi ratiba ya rais wako.

Kwa sasa Ratiba inajulikana kabisa

~Uteuzi

~Siku ya kuapishwa

~Kutengeneza Matukio

~Kuweka mawe ya msingi

~Kuzindua miradi (kusimwangwa day)

~Ukimyaaaaaaaaaa

~Msisitizo/Matamko

~Kutenguliwa
 
Kila kitu kiko tayari punde tu naye ataungana na wenzake kusaidia taifa kupitia CCM.Alipokutana na Mh Makonda kila kitu kiiwekwa sawa.

Hata ukiingia sasa katika page zake yuko anatukanana na fans wake baada ya kuwaunga mkono waliohama.

Kila la kheri Mtatiro
a95d1d4a4418b2ce0c7da7c6a00a2ebb.jpg
mm
Mwenyekiti wa CUF Julius Mtatiro, akutana uso kwa uso na Paul Makonda
Yametimia
 
Huy utamsubiri sana hahami maana kishaanzisha chama chake kinaitwa CUF Facebook Club na ana wanachama wengi sana. Sijajua kama atamkaribisha Maalim Seif katika chama chake kipya cha Facebook
hawa jamaa hawaaminiki
 
Back
Top Bottom