Julius Mtatiro: CHADEMA ni chama cha matapeli, wahuni

Julius Mtatiro: CHADEMA ni chama cha matapeli, wahuni

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa CUF, Julius Mtatiro amesema Chadema ni chama cha matapeli na ndiyo maana alihama upinzani.

Mtatiro ambaye chama chake cha zamani cha CUF kilikuwa katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) unaoundwa na vyama vinne vya NLD, Chadema, NCCR-Mageuzi na CUF ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Septemba 13, 2018 katika mkutano wa kampeni za CCM jimbo la Ukonga.

Katika mkutano huo, Mtatiro amesema ameshtuka na mchezo mchafu ulioko Chadema na kwamba wapo kimaslahi.
"Tupo hapa kumsapoti Mwita Waitara, ukiona kiongozi kama mimi niliyekaa miaka kumi na nimeachana na utapeli wewe kijana shtuka kapige kura kwa Waitara," amesema.

Mtariro ambaye alijiuzulu uanachama wa CUF Agosti 11, 2018 na kutangaza kujiunga na CCM amesema, “Kile chama ni chama cha wahuni ni chama kinachovuruga amani; wanashibisha matumbo yao."

View attachment 865544
Kwani umehama kutokea chadema ama cuf??
 
Chadema imekuwa kama busta ya kisiasa ukiwa CCM, huwezi pata cheo bila kuitukana Chadema ukiwaita wa hovyo huku ukiwasifu mafisadi wa CCM hasa wale tuliombiwa wameitia nchi yetu hasara kubwa.
 
wanaCDM kazeni mikanda sna kama mtu anahama CUF na anakandia CDM kazi ipo
 
07B3A3C4-7683-47BA-8E91-70DA3780545B_w1023_r1_s.jpg

Julius Mtatiro afunguka mazito kuhusu Chadema na kusema kuwa alihama upinzani kwa sababu Chadema ni Chama cha matapeli.

Mtatiro ametoa kauli hiyo jana Alhamisi katika mkutano wa kampeni za CCM jimbo la Ukonga. Katika mkutano huo, Mtatiro amesema ameshtuka mchezo mchafu ulioko Chadema na kwamba wapo kimaslahi.

"Tupo hapa kumsapoti Mwita Waitara, ukiona kiongozi kama mimi niliyekaa miaka kumi na nimeachana na utapeli wewe kijana shtuka kapige kura kwa Waitara," amesema.

Mtatiro ambaye chama chake cha zamani cha CUF kilikuwa katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) unaoundwa na vyama vinne vya NLD, Chadema, NCCR-Mageuzi na CUF.
 
Huyu jamaa kawa kiazi kabisa sasa ivi. Afu nilimpa kura yangu[emoji37]
 
hawa wakurya sijui wamekuwaje wallah, hili kabila nilikuwa nalisifu sana kwa msimamo, lakini limekuwa la ovyo kuliko makabila yote tanzania, basi ni matapeli, jadilini sera zenu sio matusi, matusi hayajengi, nchi hii ni moja, chadema haipo rwanda, tamati yake wote ni watz, toa sera wananchi wazikubali watajua wapi kwa kwenda, lakini kukaa na kutukana chadema au upinzani haitasaidia, najua ccm itashinda , msaada wa polisi na mkurugenzi ne, lakini kwa kwenda kihalali ccm kupita ni mbinde, acheni matusi toeni sera zenu, mwingine anadai ati anamjua lowasa kuliko anavyojijua, huyo huyo aliyewekewa midomo ya bunduki 8 kichwani,
 
Chadema wanapata tabu sana! Mara hii sasa itabidi waanze kimtukana matatiro na si kumsifu tena! Dah
chadema wana akili wewe, ushasikia wapinzani wakimtukana mtu, mnawadhulumu wao na wananchi wao, na hao polisi eeh, si tupo nao mtaani, haya endeleeni kutumika, siku tukitumika na sisi msishangae
 
sasa kama alikuwa CUF kajuaje kuwa chadem Ni wajinga? au anataka kuwahisha teuzi
 
Mimi huwa naamini wanasiasa wote ni matapeli ukiacha kufanya kazi ukategemea mdomo ndiyo ukuletee riziki huna usalama mtatiro hana jinsi maana njaa inamsumbua
 
Julita, weka akiba ya maneno basi.. Usifikiri watatawala milele huko ulikoenda kama wanavyosema. Wamekutapeli nini cdm??
 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa CUF, Julius Mtatiro amesema Chadema ni chama cha matapeli na ndiyo maana alihama upinzani.

Mtatiro ambaye chama chake cha zamani cha CUF kilikuwa katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) unaoundwa na vyama vinne vya NLD, Chadema, NCCR-Mageuzi na CUF ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Septemba 13, 2018 katika mkutano wa kampeni za CCM jimbo la Ukonga.

Katika mkutano huo, Mtatiro amesema ameshtuka na mchezo mchafu ulioko Chadema na kwamba wapo kimaslahi.
"Tupo hapa kumsapoti Mwita Waitara, ukiona kiongozi kama mimi niliyekaa miaka kumi na nimeachana na utapeli wewe kijana shtuka kapige kura kwa Waitara," amesema.

Mtariro ambaye alijiuzulu uanachama wa CUF Agosti 11, 2018 na kutangaza kujiunga na CCM amesema, “Kile chama ni chama cha wahuni ni chama kinachovuruga amani; wanashibisha matumbo yao."

View attachment 865544
Njaa mbaya sana. Has kwa wasomi wa Tanzania wanayo NJAA kuliko mlalahoi wa uwanja wa fisi
 
Atueleze kwanza kipindi aliwekwa kinyumba na wasiojulikana walimfanya nini mpaka ametoka ametakata na kunawiri hadi kubadili kabisa haiba yake. Akiendelea kuchonga tutamwanika mpaka atafute kamba ajinyonge.
 
Upinzani ni muhimu kwa ajili ya checks and balance lakini TZ hakuna vyama kamili za upinzani !
 
Atuache na sisi tukifikisha miaka 10 tutahama..
Yani Kuna wahuni zaidi ya 6 million walipiga kura 2015 !! Akiwemo na yeye..
Njaa mbaya sana, Unahama CUF Matusi unaitukana Chadema duh!
Kwa kweli inasikitika sana ndugu! Tena aombe radhi sana kwa wananchi waliowapigia kura chadema! Maana hajawatukana chadema tu, Bali na wapiga kura wake! Afanya siasa za kistaarabu sio kutukana watu
 
  • Thanks
Reactions: prs
Back
Top Bottom