Julius Mtatiro: CHADEMA ni chama cha matapeli, wahuni

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa CUF, Julius Mtatiro amesema Chadema ni chama cha matapeli na ndiyo maana alihama upinzani.

Mtatiro ambaye chama chake cha zamani cha CUF kilikuwa katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) unaoundwa na vyama vinne vya NLD, Chadema, NCCR-Mageuzi na CUF ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Septemba 13, 2018 katika mkutano wa kampeni za CCM jimbo la Ukonga.

Katika mkutano huo, Mtatiro amesema ameshtuka na mchezo mchafu ulioko Chadema na kwamba wapo kimaslahi.
"Tupo hapa kumsapoti Mwita Waitara, ukiona kiongozi kama mimi niliyekaa miaka kumi na nimeachana na utapeli wewe kijana shtuka kapige kura kwa Waitara," amesema.

Mtariro ambaye alijiuzulu uanachama wa CUF Agosti 11, 2018 na kutangaza kujiunga na CCM amesema, “Kile chama ni chama cha wahuni ni chama kinachovuruga amani; wanashibisha matumbo yao."

MTATIRO%2BBPIC.jpg
 
Kama chama cha matapeli na wahuni na kinapokea ruzuku ya mamilioni ya Tsh kwa mwezi toka serikalini basi serikali iliyopo madarakani haina uhalali tena wa kuendelea kuwapo madarakani maana imeshindwa kuongoza nchi kwa kuacha matapeli na wahuni wakijichotea tu mamilioni ya pesa kila mwezi toka hazina
 
Tanzania ni moja ya nchi yenye wasomi wajinga sana, wasomi wa nchi hii hawana tofauti na wasio na elimu hata ya darasa la kwanza

Na mtu akihamia ccm tu uwezo wake wa kufikiri na kutenda hushuka sana
Wewe ulieko wapi uwezo wako ukoje Baba?
 
Back
Top Bottom