Julius Kambarage Nyerere alipokuwa mwalimu wa shile 1953

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
17,602
24,709
JULIUS KAMBARAGE NYERERE ALIPOKUWA MWALIMU WA SHULE 1953

Ilikuwa wakati huu kwa mara ya pili Abdul Sykes alimshauri Nyerere kujiuzulu kufundisha ili ashughulike na kazi za TAA.

Wazo hili halikumvutia Nyerere kama vile ambavyo halikumvutia Chifu Kidaha Makwaia miaka minne iliyopita.

Lakini Nyerere alipiga hatua moja mbele kuliko Chifu David Kidaha Makwaia.

Angalau Nyerere alikuwa amekubali kuiongoza TAA.

Nyerere alikuwa anajua vyema wakati huo kwamba TAA ilikuwa ikiendeshwa kutoka mifuko ya wazalendo ambao idadi yao haikuzidi watu wanne - John Rupia, Dossa Aziz na wale ndugu wawili, Abdul na Ally Sykes.

Nyerere hakutaka kuishi kwa kutegemea msaada hata ikiwa wafadhili wake walikuwa na nia njema.

Kilichosukuma ule uongozi wa ndani wa TAA kusisitiza juu ya Nyerere kujiuzulu kazi na kuchukua uongozi wa TAA ilikuwa kwanza, ule ukweli kuwa TAA ilikuwa ikifanya kazi kama chama cha siasa na Gavana alikuwa akifahamu hivyo.

Pili, mpango ulikuwa mbioni kusajili chama cha siasa kabla ya mwisho wa mwaka wa 1954.

Wakati huo huo TAA ilikuwa ikishughulikia rasimu ya katiba ya chama kipya na mipango ilikuwa ikiendelea kwa rais wa chama cha siasa kilichokuwa kikitarajiwa kusafiri kwenda Umoja wa Mataifa, New York kutoa madai ya Tanganyika mbele ya Baraza la Udhamini kama Japhet Kirilo alivyofanya miaka miwili iliyopita.

Vilevile ilikuwa muhimu uongozi wa TAA uwe na rais aliyekuwa anafanya kazi ya chama kwa muda wote wakati chama kipo mbioni kuundwa.

(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes (1998)

1658690323065.png
 
Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
17,602
24,709
... hao akina Sykes kuna kitu cha kipekee walikiona kwa Nyerere wao hawakuwa nacho au sielewi? Walimshobokea sana.
Dudus,
Nakuomba tumia lugha safi ili huu mjadala uwe wenye hadhi.

Acha hizi lugha za, "shoboka."
Hakika Nyerere alikuwa si wa kawaida.

Katika Nyaraka za Sykes kuna barua Nyerere akiwa Rais wa TAA anamwandikia Gavana Twining mwaka wa 1953.

Barua hii mimi nimeipenda sana na nimeipa jina, "Bread and Butter," sababu ni kuwa Mwalimu alitumia maneno hayo katika barua ile.

Mtu wa kwanza kujua uwezo wa Nyerere alikuwa Hamza Mwapachu.
 
Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
8,040
5,081
... hao akina Sykes kuna kitu cha kipekee walikiona kwa Nyerere wao hawakuwa nacho au sielewi? Walimshobokea sana.
Shule combined na exposure vya Nyerere vilikuwa "a unique feature" kwa Nyerere. Nyerere amelelewa na kukulia Ikulu, tofauti na watu walio wengi. Ni kama alivyokuwa Rais Mkapa; alikulia Ikulu and so was a trained President; sawa tu tuseme kama alivyokuwa Geoge Bush Jr wa Marekani!

Katika historia ya Taifa letu, ni vigumu sana kuja kupata tena a trained President kama tulivyowahi kumpata Mkapa, labda kama itakuja kutokea Hussein Mwinyi akawa Rais wa JMT
 
Ujamaamf

Senior Member
Jul 28, 2021
156
238
Uandishi wako ungekua katika mtindo huu wengi tungenunua vitabu yako kwa idadi kubwa kuliko namba uliyouza. huu ndio uandishi wako bora kuwahi kuusoma sijaskia hapa Habari za waislam katika kupigania uhuru kama harakati za mugawama wa kiislam kule palestine.

Uandishi huu umekua wa umoja sana hata madai yako ya watu wengi kutokutambulishwa kwene vitabu ungeandika kama watu wazalendo walio watanzania au watanganyika kuna kitu watu wangekiona hata sisi tungehoji kwanini hawa wawepo hawa wasiwepo ila hizi Habari za waislam sijui nini mala waislam vile mala harakati za waislam hapo unagawa waandishi. Umoja mshikamano na amani ndio jadi yetu kama alivyofanya baba wa taifa hayati JULIUS KAMBARAGE NYERERE.
 
Ujamaa...
Hupendi kusikia historia ya Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Sasa tufanye kitu gani na huu ndiyo ukweli wenyewe?

Unadhani nisingemwandika Abdul Sykes, Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Suleiman Takadir, Sheikh Abdallah Sembe, Sheikh Mohamed Ramia, Ali Migeyo, Bi. Tatu bint Mzee, Bi. Hawa bint Maftah, Mama bint Maalim, Amina Kinabo, Zarula bint Abdulrahman na wengine na wengine kitabu changu kingeuzika zaidi.

Huwezi kuwa na historia ya kweli ya TANU bila hawa.

Iweje kama hivyo ni kweli kitabu, ''Historia ya TANU,'' kilichoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni kimekufa toka siku ya kwanza kilipochapwa na wao kitabu kizima hakuna popote Abdul Sykes na hao wenzake hapo juu wametajwa?

Ikiwa hujui nakufahamisha sasa.

Kitabu changu kimependwa sana na kinauzwa hadi leo toka kichapwe mwaka wa 1998.

Kinakwenda sasa chapa ya tano.
Hakuna kitabu nlichandika ambacho hakijapendwa.

Ryzen

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
6,944
7,921
Mzee Said,

Umejaa madini mengi sana, tatizo umekaa Kidini sana, Historia zako ni Njema na nzuri sana zisingelalia Upande Mmoja.
 
Jabari XVI

JF-Expert Member
May 31, 2018
865
1,081
Shule combined na exposure vya Nyerere vilikuwa "a unique feature" kwa Nyerere. Nyerere amelelewa na kukulia Ikulu, tofauti na watu walio wengi. Ni kama alivyokuwa Rais Mkapa; alikulia Ikulu and so was a trained President; sawa tu tuseme kama alivyokuwa Geoge Bush Jr wa Marekani!
Katika historia ya Taifa letu, ni vigumu sana kuja kupata tena a trained President kama tulivyowahi kumpata Mkapa, labda kama itakuja kutokea Hussein Mwinyi akawa Rais wa JMT
Nilitamani sana siku moja daktari Hussein Ali Hassan Mwinyi awe rais wa JMT
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Top Bottom