Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,920
- 30,261
MAKOSA KATIKA HISTORIA YA NYUMBA YA JULIUS NYERERE MAGOMENI KAMA ILIVYOANDIKWA NA DAILY NEWS
Daily News la tarehe 9 December 2023 (link hiyo hapo chini) imechapa makala yanayosema kuwa nyumba hiyo ya Mwalimu Nyerere ndipo alipoishi mara tu baada ya kuacha kazi ya ualimu St. Francis College Pugu.
Daily News linasema kuwa katika nyumba hiyo ndipo ikifanyika mikutano ya harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.
Ukweli ni kuwa Nyerere baada ya kuacha kazi alikwenda kuishi na Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu.
Nyumba hii ndipo ikifanyika mikutano yote ya siri kuanzia enzi za TAA 1950s hadi inaundwa TANU mwaka wa 1954.
Mikutano yote kuanzia vipi Nyerere ataingizwa katika uongozi hadi mipango ya safari ya UNO yote ikifanyika nyumbani kwa Abdul Sykes.
Nyerere alifikishwa nyumba hii na Joseph Kasella Bantu alipokwenda kumjulisha kwa Abdul Sykes mwaka wa 1952.
Abdul Sykes alikuwa TAA Secretary na Act. President.
Kuanzia hapo 1952 hadi Nyerere anachukua uongozi wa TAA 1953 na kuundwa kwa TANU 1954 na baadae Mwalimu Nyerere alikuwa akihudhuria vikao vyote vya harakati katika nyumba hii.
Nyumba hiyo ya Magomeni Mwalimu aliijenga na kuhamia mwaka wa 1958 na kabla ya kuhamia hapo alipohama nyumbani kwa Abdul Sykes TANU ilimtafutia nyumba Magomeni Maduka Sita.
Mwalimu aliishi nyumba hii kwa miaka mitatu na alipotoka hapo ndipo alipohamia kwenye nyumba yake aliyojenga Mtaa wa Ifunda ambako si mbali na Maduka Sita.
Nyumba hii hakuishi hata zaidi ya mwaka akahamia nyumba ya serikali Sea View.
PICHA: Nyumba ya Julius Nyerere, Majumba Sita ikimwonyesha Nyerere akiingia ndani mwake.
Nyumba ya pili ni ya Abdul Sykes alipoishi Nyerere.
Nyumba hii picha ya tatu haipo imejengwa nyumba
nyingine.

Nyerere’s house and secret of Tanzania’s independence - Daily News
WHEN you speak of the history of independence struggle in Tanzania, one cannot skip mentioning Magomeni Usalama area, in Dar es Salaam. The area became part of the history because of a small house in which Mwalimu Julius Nyerere stayed with his family during liberation struggles. This is the...
dailynews.co.tz