Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,908
- 30,249
JULIUS KAMBARAGE NYERERE ALIPOKUWA MWALIMU WA SHULE 1953
Ilikuwa wakati huu kwa mara ya pili Abdul Sykes alimshauri Nyerere kujiuzulu kufundisha ili ashughulike na kazi za TAA.
Wazo hili halikumvutia Nyerere kama vile ambavyo halikumvutia Chifu Kidaha Makwaia miaka minne iliyopita.
Lakini Nyerere alipiga hatua moja mbele kuliko Chifu David Kidaha Makwaia.
Angalau Nyerere alikuwa amekubali kuiongoza TAA.
Nyerere alikuwa anajua vyema wakati huo kwamba TAA ilikuwa ikiendeshwa kutoka mifuko ya wazalendo ambao idadi yao haikuzidi watu wanne - John Rupia, Dossa Aziz na wale ndugu wawili, Abdul na Ally Sykes.
Nyerere hakutaka kuishi kwa kutegemea msaada hata ikiwa wafadhili wake walikuwa na nia njema.
Kilichosukuma ule uongozi wa ndani wa TAA kusisitiza juu ya Nyerere kujiuzulu kazi na kuchukua uongozi wa TAA ilikuwa kwanza, ule ukweli kuwa TAA ilikuwa ikifanya kazi kama chama cha siasa na Gavana alikuwa akifahamu hivyo.
Pili, mpango ulikuwa mbioni kusajili chama cha siasa kabla ya mwisho wa mwaka wa 1954.
Wakati huo huo TAA ilikuwa ikishughulikia rasimu ya katiba ya chama kipya na mipango ilikuwa ikiendelea kwa rais wa chama cha siasa kilichokuwa kikitarajiwa kusafiri kwenda Umoja wa Mataifa, New York kutoa madai ya Tanganyika mbele ya Baraza la Udhamini kama Japhet Kirilo alivyofanya miaka miwili iliyopita.
Vilevile ilikuwa muhimu uongozi wa TAA uwe na rais aliyekuwa anafanya kazi ya chama kwa muda wote wakati chama kipo mbioni kuundwa.
(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes (1998)