Kipindi Maalum Leo Mchana Saa 8: Julius Nyerere Alivyochaguliwa Kuwa President wa TAA 1953

Nyerere alimshinda Abdul Sykes kwa kura nyingi. Sykes alishauriwa asigombee akakaidi.
Laki...
Huwa napenda sana kukusoma kwani najifunza mengi kutoka kwako.
Hili mosi.

Pili unauchangamsha ubongo wangu kwa fikra.

Mathalan historia ya Abdul Sykes haikuwapo kabisa kabla sijaandika kitabu cha maisha yake.

Kitabu kiichokuwapo ambacho kilimtaja Abdul Sykes ni ''The Making of Tanganyika,'' (1965) alichoandika Judith Listowel na yeye ndiye aliyeeleza kuhusu uchaguzi huu wa mwaka wa 1953.

Sasa ninapokusoma kama hivi kwa hakika unanifurahisha.
Tupe habari zaidi tafadhali.

1702195970210.png
 
Unajua nasema kweli bila unafiki. Abdul Sykes alikuwa mkorofi sana, Alichukua madaraka kutoka mikononi kwa baba yake kwa kumfanyia vurugu na kumpindua. Nyerere hakupendezwa na mienendo ya Abdul Sykes,. Sykes hakuwa na adabu hata kidogo
 
Baba yake Abdul Sykes alifariki mwaka wa 1949.

Abdul Sykes na Vedasto Kyaruzi wameingia katika uongozi wa TAA 1950.
 
Laki...
Baba yake Abdul Sykes alifariki mwaka wa 1949.

Abdul Sykes na Vedasto Kyaruzi wameingia katika uongozi wa TAA 1950.
Wewe mwenyewe ndio ulituambia hapa, kwamba Abdul Sykes alimuondoa baba yake madarakani kwa vurugu, leo unakataa . sasa sijui tukueleweje
 
KIPINDI MAALUM LEO MCHANA SAA NANE TBC1: JULIUS NYERERE ALIVYOCHAGULIWA KUWA PRESIDENT WA TAA 1953

Katika historia ambayo haifahamiki kabisa ni vipi Julius Nyerere alichaguliwa kuwa President wa TAA mwaka wa 1953 nafasi aliyogombea na Abdulwahid Sykes katika Ukumbi wa Arnautoglo.

View: https://youtu.be/URod8wL5soQ?si=sPvqo6D_PCjWxV7F

Haya ni mambo yaliyopitwa na Wakati ambayo hayana manufaa wala faida yoyote ile kwa Watanzania wa sasa na dunia nzima kwa ujumla. Hizo ni habari mfu na hoja mufilisi.
 
Haya ni mambo yaliyopitwa na Wakati ambayo hayana manufaa wala faida yoyote ile kwa Watanzania wa sasa na dunia nzima kwa ujumla. Hizo ni habari mfu na hoja mufilisi.
John...
Ikiwa wewe unaona hivyo sawa acha kusoma lakini wako wanaoona kuwa historia waliokuwa wanasomeshwa ina makosa na hii historia niliyoandika mimi ndiyo historia ya kweli.

Kwa ajili hii kila ninapoandika wao hunisoma.

Hili ni jukwaa huru halazimishwi mtu kusoma wala kuandika.

Wala hakuna mwenye haki ya kuamrisha kipi kiandikwe kipi kisiandikwe.

Unakuja humu kwa khiyari yako.
 
Laki...
Ukiwa unapenda kujua historia ya uhuru wa Tanganyika soma kitabu cha Abdul Sykes.

Utajifunza mengi sana.
Ukijua bila shaka fedhuli itakuondoka.
Tatizo umezidisha sana mahaba kwa Abdul Sykes mpaka matatizo yake unajifanya huyajui, Abdul Sykes alikuwa mkorofi na mtu amwa vurugu vurugu, labda kwa ajili ya fani yake ya ubondia ilimfanya hivyo, Abdul Sykes alimuondoa baba yake madarakani kwa vurugu
 
Historia hii haikuwapo.

Kitabu kimetoka mwaka wa 1998 na hadi leo kimechapwa mara nne tunakwenda toleo la tano.

Mahaba sinayo mimi peke yangu na wasomaji pia.

Kila siku napokea msg watu wanadhani mimi nauza kitabu hicho.

Mimi huwaelekeza kwa wauzaji.

1702303465326.png
 
Back
Top Bottom