Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,781
898
MHE. JULIANA SHONZA, MBUNGE (UWT) CCM VITI MAALUM MKOA WA SONGWE AFANYA ZIARA YA KIMKAKATI

Katika ziara yake iliyoanza mnamo tarehe 18 Februari, 2023 Mhe. Juliana Daniel Shonza alifika Wilaya ya Ileje na kubisha hodi kwa Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ileje komredi Hassan Lyamba. Pia alikutana na Mkuu wa Wilaya Mpya wa Wilaya ya Ileje Mhe. Bi Farida pamoja na Mkurugenzi Mpya wa Wilaya ya Ileje Bwana Nnauye. Kwa pamoja wamejadili changamoto mbalimbali zinazosababisha wanawake kushindwa kunufaika na mikopo ya asilimia 4% ikiwepo sharti la kuwataka kuwa na kitambulisho cha NIDA. Kwa pamoja wameazimia kushirikiana kuhakikisha wanawake wananufaika na sera hii, lakini pia wanapatiwa elimu ya kutosha ya ujasiriamali.

Akiendelea na ziara yake siku ya tarehe 19 Februari 2023 ameendelea na ziara yake kwa kushiriki kikao cha Baraza a UWT Wilaya ya Ileje. Katika kikao hicho Mhe. Shonza ameshiriki kikao cha baraza la UWT Wilaya ya ileje na amewaeleza mambo yafuatayo;
  • Umuhimu wa kusema kazi nzuri alizofanya Rais wetu Mh Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi ndani ya Wilaya ya Ileje katika Sekta za Afya, Maji, Elimu n.K
  • Umuhimu wa viongozi kufanya vikao na kutembelea matawi yao pamoja na kuingiza wanachama wapya
  • Kuunda vikundi vya wanawake na kuvisaidia kupata mikopo ya halmashauri
  • Suala la malezi kwa watoto wetu
  • Mikakati ya kuwa na miradi ya jumuiya ngazi ya Kata na Wilaya
-Mpango kazi wake (Mbunge) kwa mwaka 2023 katika kuyafikia makundi yote katika jamii na kufanya mikutano ya hadhara kusikiliza kero za wananchi na kueleza utekelezaji wake ilani ya CCM.

ZIARA KATA KWA KATA - MBOZI
Mhe. Shonza ameendelea na ziara ya Kata kwa Kata. Ziara Kata kwa Kata imekuja bada ya kupokea malalamiko mengi ya vikundi vya wanawake ambao wana sifa ya kukopesheka lakini hawajapatiwa mikopo kwa muda mrefu. Mhe. Shonza amemuomba Mkurugenzi ampe Afisa maendeleo ili kwa pamoja wakavitembelee hivyo vikundi, kukagua shughuli zao za uzalishaji, na Uhai wa vikundi ili kuvisaidia kupata mkopo katika msimu ujao. Wanawake wamehamasika sana kujiunga katika vikundi, wanahitaji kusaidiwa na kuelimishwa ili wanufaike na sera hii ya Chama Cha Mapinduzi.

WhatsApp Image 2023-02-20 at 15.00.34(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-02-20 at 15.00.34(3).jpeg
WhatsApp Image 2023-02-20 at 15.00.36(3).jpeg
WhatsApp Image 2023-02-20 at 15.00.37.jpeg
WhatsApp Image 2023-02-20 at 15.00.36.jpeg
WhatsApp Image 2023-02-20 at 15.00.35(4).jpeg
WhatsApp Image 2023-02-20 at 15.00.35.jpeg
 
MHE. JULIANA SHONZA, MBUNGE (UWT) CCM VITI MAALUM MKOA WA SONGWE AFANYA ZIARA YA KIMKAKATI

Katika ziara yake iliyoanza mnamo tarehe 18 Februari, 2023 Mhe. Juliana Daniel Shonza alifika Wilaya ya Ileje na kubisha hodi kwa Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ileje komredi Hassan Lyamba. Pia alikutana na Mkuu wa Wilaya Mpya wa Wilaya ya Ileje Mhe. Bi Farida pamoja na Mkurugenzi Mpya wa Wilaya ya Ileje Bwana Nnauye. Kwa pamoja wamejadili changamoto mbalimbali zinazosababisha wanawake kushindwa kunufaika na mikopo ya asilimia 4% ikiwepo sharti la kuwataka kuwa na kitambulisho cha NIDA. Kwa pamoja wameazimia kushirikiana kuhakikisha wanawake wananufaika na sera hii, lakini pia wanapatiwa elimu ya kutosha ya ujasiriamali.

Akiendelea na ziara yake siku ya tarehe 19 Februari 2023 ameendelea na ziara yake kwa kushiriki kikao cha Baraza a UWT Wilaya ya Ileje. Katika kikao hicho Mhe. Shonza ameshiriki kikao cha baraza la UWT Wilaya ya ileje na amewaeleza mambo yafuatayo;
  • Umuhimu wa kusema kazi nzuri alizofanya Rais wetu Mh Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi ndani ya Wilaya ya Ileje katika Sekta za Afya, Maji, Elimu n.K
  • Umuhimu wa viongozi kufanya vikao na kutembelea matawi yao pamoja na kuingiza wanachama wapya
  • Kuunda vikundi vya wanawake na kuvisaidia kupata mikopo ya halmashauri
  • Suala la malezi kwa watoto wetu
  • Mikakati ya kuwa na miradi ya jumuiya ngazi ya Kata na Wilaya
-Mpango kazi wake (Mbunge) kwa mwaka 2023 katika kuyafikia makundi yote katika jamii na kufanya mikutano ya hadhara kusikiliza kero za wananchi na kueleza utekelezaji wake ilani ya CCM.

ZIARA KATA KWA KATA - MBOZI
Mhe. Shonza ameendelea na ziara ya Kata kwa Kata. Ziara Kata kwa Kata imekuja bada ya kupokea malalamiko mengi ya vikundi vya wanawake ambao wana sifa ya kukopesheka lakini hawajapatiwa mikopo kwa muda mrefu. Mhe. Shonza amemuomba Mkurugenzi ampe Afisa maendeleo ili kwa pamoja wakavitembelee hivyo vikundi, kukagua shughuli zao za uzalishaji, na Uhai wa vikundi ili kuvisaidia kupata mkopo katika msimu ujao. Wanawake wamehamasika sana kujiunga katika vikundi, wanahitaji kusaidiwa na kuelimishwa ili wanufaike na sera hii ya Chama Cha Mapinduzi.

View attachment 2524061View attachment 2524062View attachment 2524064View attachment 2524065View attachment 2524066View attachment 2524067View attachment 2524068
Cc Wakudadavuwa
 
😐🤨🤨😶😶🤨🤨🤨😐😐🤨🤨😶🤨🤨😐😐🤨🤨😶😶
 
Waendelee kujipanga moto wa chadema hauzimwi kwa iyena iyena.yule mwizi wa uchaguzi hayupo tena
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom