Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,400
- 465,165
JULIANA-01....Gideon alitulia kwenye kochi lililokuwa sebuleni kwake katika jumba lake la kifahari lililokuwa Masaki jijini Dar es Salaam. Alikuwa akimwangalia mke wake, Juliana Marcel jinsi alivyokuwa amekongoroka na kubaki mifupa mitupu. Alitia huruma pale alipokuwa amekaa, hakuwa mwanamke mrembo tena, uzuri wake ulipotea kabisa machoni mwa Gideon.
Mwanamke huyo aliyesifika kwa urembo kipindi cha nyuma, alichakaa, hakuwa kama Juliana yule aliyepita ambaye aliwatingisha wanaume kutokana na uzuri wake.
Gideon alikumbuka jinsi Juliana alivyokuwa kipindi cha nyuma, kipindi walichokuwa wakisoma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kipindi ambacho wanaume wote walikuwa wakivutiwa naye. Alikuwa na urembo wa ajabu, aliwavutia wanaume wengi lakini mwisho wa siku, aliwakataa wenye magari na pesa zao, akamkubalia yeye, mtoto wa mama ambaye hakuwahi hata kumiliki milioni moja mfukoni.
Leo hii, miaka kumi baada ya kumuoa na kuzaa naye mtoto mmoja aliyeitwa Jesca, Juliana hakuwa yule wa miaka ile, alichoka, uzuri wake wote ukapotea na kubaki mifupa mitupu. Kila mara Gideon alipokuwa akimwangalia, alitamani kulia, alitamani kumwambia kwamba hakumpenda tena, wakati mwingine alitamani kumpa talaka lakini kwa sababu alikuwa Mkristo, alishindwa kujua afanye nini.
“Kwenye shida na furaha, uzima na ugonjwa nitakuwa na wewe,” aliyakumbuka vilivyo maneno aliyosema mbele ya mchungaji, mbele ya kanisa zima kwamba kamwe asingeweza kumwacha mwanamke huyo.
Leo hii hakutaka kukumbuka tena, asingeweza kuendelea kuishi na mwanamke huyo, wakati mwingine alitamani kumuua, alitamani kwenda jikoni, akachukue kisu na kumchomachoma. Hakuwa na mapenzi naye tena, kisa tu alikuwa amechoka, kisa tu alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Saratani ya Damu.
“Mume wangu!” aliita Juliana huku akimwangalia Gideon.
“Unasemaje?” aliitikia Gideon kishari, kwa jinsi alivyomchoka mkewe, hakutaka hata kuisikia sauti yake.
Je, unajua nini kiliendelea?