Jukwaa la wanawake (girls/ ladies forum)

Nazjaz

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
7,684
8,833
Mods, naomba lianzishwe jukwaa maalum kwa ajili ya wanawake, ambapo tutaweza kuyajadili kiunaga ubaga mambo yetu yanayotuhusu na kutukereketa moyoni.
Kuna baadhi ya mambo hatuwezi kuyaongea hapa kwenye jukwaa la mapenzi kwani kina baba hawachelewi kutuharibia threads zetu.
Pia uhuru wa kuongea utu wetu wa ndani unakuwa ni mdogo sana kwani tumeumbwa na nyuso za aibu mbele ya kinababa.
Nawakilisha
 
kwahiyo mods wataomba passport/ids za watu ili wajue jinsia zao.....???, na Je hii itakuwa private forum kama livyo ya dini na ya wakubwa? you can never tell kwenye JF kama mtu ni mwanamke au mwanaume.. wewe mwaga hoja hapa hatuangalii mtu behind the hoja bali hoja zenyewe...
 
kwahiyo mods wataomba passport/ids za watu ili wajue jinsia zao.....???, na je hii itakuwa private forum kama livyo ya dini na ya wakubwa? You can never tell kwenye jf kama mtu ni mwanamke au mwanaume.. Wewe mwaga hoja hapa hatuangalii mtu behind the hoja bali hoja zenyewe...

mwisho wa hii thread
 
Mi naona ni vizuri wakijua tunachoongea kwasababu itawasaidia kuwaelewa wenza wao maana wanawake kujieleza majumbani ni kazi na wao mara nyingi hua wanaishia kutokutuelewa!Labda tuwaombe wajirekebishe kwenye swala la kuvuruga thread!
 
Kila siku wanawake mnalilia kujitenga, mara vyama vya madaktari wanawake, mara nini cha wanawake, mbona sie midume ya mbegu hatna complication kama za kwenu?
 
Wana jf, naja jinsi nilivyo.
Mimi si malaika kwamba nisikosee, wala si taahira nisiweze kuchangia.
Naomba nirekebishwe na kukosolewa pale ninapokosea.
Naomba nipongezwe pale ninapofanya vizuri.
Asanteni sana great thinkers
Nilivyokukaribisha ulisema tukukosoe unapokosea....., from my point of view hapa dada.... mmmhhh
 
Likianzishwa tu.... fasta babu Asprin anaibuka na ID mpya....Anti dada... afu tunakamtana huko kama kawa...how is it?.
 
Mods, naomba lianzishwe jukwaa maalum kwa ajili ya wanawake, ambapo tutaweza kuyajadili kiunaga ubaga mambo yetu yanayotuhusu na kutukereketa moyoni.
Kuna baadhi ya mambo hatuwezi kuyaongea hapa kwenye jukwaa la mapenzi kwani kina baba hawachelewi kutuharibia threads zetu.
Pia uhuru wa kuongea utu wetu wa ndani unakuwa ni mdogo sana kwani tumeumbwa na nyuso za aibu mbele ya kinababa.
Nawakilisha

Dada Nazjaz una wazo zuri sana, ila utekelezaji wake ni mgumu sana hapa JF. Hata kama itawekwa private forums za wanawake watatokea wanaume wenye ID mpya wakachungulie huko. Nakushauri kama kweli upo SERIOUS na ombi lako, basi inapaswa ianzishwe kikundi cha akina dada nje na hapa JF ambacho mtaonana physically na kuongelea mambo yenu bila woga, humu ktk mitandao lazima mtaingiliwa tu na akina baba, labda hao Mods waweke kin'gamuzi ambacho kitagundua jinsia ya kila aliye mbele ya PC/Laptop yake
 
Likianzishwa tu.... fasta babu Asprin anaibuka na ID mpya....Anti dada... afu tunakamtana huko kama kawa...how is it?.

Wajukuu zako wote na hao tunasonga huko kwa ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi
 
hakuna maisha yasiyowachanganya wanaume na wanawake kwa pamoja, hiyo aibu unayosema ni yako binafsi, siye wenzio wala hatuna aibu, kama kitu ni fact kinasemwa na macho makavuu. nakuona kama u-mgeni japo pia naona wayajua mengi ya humu JF! karibu where we dare to talk openly!
 
hii sredi haina thamani kama dola za zimbabwe. mnashauriwa kutumia pombe kwa kiasi ili kuepuka kupost sredi za ajabu ajabu kama hizi.

asanteni kwa ushirikiano.
 
Yes ni mgeni kwa kuwa sikuwa memba, but nilikuwa natembelea jf kila siku, hata nikiwa nasafiri nilikuwa natumia simu kupata uhondo
hakuna maisha yasiyowachanganya wanaume na wanawake kwa pamoja, hiyo aibu unayosema ni yako binafsi, siye wenzio wala hatuna aibu, kama kitu ni fact kinasemwa na macho makavuu. Nakuona kama u-mgeni japo pia naona wayajua mengi ya humu jf! Karibu where we dare to talk openly!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom