Jukwaa la wahariri wagomea kuandika habari zote za jeshi la polisi

hoyce

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
1,117
297
TAARIFA YA JUKWAA LA WAHARIRI (TEF)
KWA VYOBO VYA HABARI
KUHUSU KUUAWA KWA MWANDISHI DAUDI MWANGOSI
UTANGULIZI:
1. Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), limepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, mkoani Iringa, Daudi Mwangosi.

2. Mwangosi ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Iringa (IPC), aliuawa akiwa kazini jana, Septemba 2, 2012, wakati polisi walipokuwa wakiwadhibiti wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

3. Tukio hili linaiingiza Tanzania katika historia mbaya ya ukiukwaji na ukandamizwaji wa uhuru wa habari, kwani ni kwa mara ya kwanza tunashuhudia mwandishi wa habari AKIUAWA WAKATI AKITEKELEZA MAJUKUMU YAKE YA KIHABARI.

4. Taarifa za awali zinaonyesha kuwa Mwangosi kabla ya kufikwa na mauti saa 9.30 alasiri katika kijiji cha Nyololo, Mufindi, alizingirwa na kushambuliwa na polisi waliokuwa katika eneo la tukio. Na hata alipopiga kelele za kuomba msaada, hakusikilizwa na matokeo yake aliuawa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu.

5. Kwa kushirikiana na Baraza la Habari Tanzania, TEF tumechukua hatua za haraka za kuunda timu ya uchunguzi wa suala hilo, ambayo itakwenda mkoani Iringa mapema kadri itakavyowezekana, ili kubaini ukweli wa tukio hilo. Lengo la uchunguzi huo ni kuweka kumbukumbu sahihi (documentation) ya tukio hilo la aina yake katika historia ya nchi yetu.

6. Matokeo ya uchunguzi huo pamoja na mwingine unaofanywa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), ndiyo yatakayotoa mwelekeo wa hatua ambazo TEF inachukua dhidi ya Jeshi la Polisi katika siku chache zijazo.

MTIZAMO NA MSIMAMO WA TEF
Kwa kuzingatia taarifa kutoka Iringa na zile za vyombo vya habari vya jana (Jumapili, Septemba 02, 2012) na leo (Jumatatu, Septemba 03, 2012), TEF ina mtizamo na msimamo kama ifuatavyo:

1. Kwanza tunalaani vikali tukio la kupigwa, kisha kuuwawa kwa mwandishi Daudi Mwangosi ambalo limeigusa tasnia ya habari kwamba sasa pengine waandishi wa habari ni malengo “target ya polisi” wanapokuwa kwenye kazi zao.

2. Ieleweke wazi kwamba matukio haya siyo yanaondoa imani ya waandishi wa habari kwa jeshi la polisi tu, bali yanaweza kuwa chanzo cha uhasama na ufa mkubwa ambao utawanyima wananchi nafasi ya kutumikiwa na pande mbili ambazo zinategemeana.

3. Kwa matukio ya aina hii, tunadhani wakati mwafaka kwa uongozi wa Jeshi la Polisi nchini kuwajibika, kuazia kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa na uongozi wa Makao Mkuu, akiwamo Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Saidi Mwema.

4. Tunasema hivi kwani kuna kila dalili kwamba polisi wanahusika kwa namna moja au nyingine na tukio au/na matukio yaliyosababisha kifo cha Mwangosi, kwani kitendo cha kumzingira tu na kumshambulia kinathibitisha kwamba hawakuwa na nia njema hata kidogo dhidi ya mwandishi huyu.

5. Taarifa ambazo TEF tunazo, pia zinadai kwamba kulikuwa na mpango wa polisi wa “kuwashughulikia waandishi wa habari watatu” (Mwangosi) akiwa mmojawapo na hilo lilionekana likitekelezwa kwa polisi kumshambulia mwandishi huyo, baadaye alipoteza maisha katika mazingira ya kutatanisha.

6. Hili linatiliwa nguvu na tukio jingine la polisi kumpiga na kumjeruhi mwandishi mwingine, Godfrey Mushi ambaye ni mwakilishi wa gazeti la Nipashe mkoani Iringa. Mwandishi wa tatu ambaye hadi tunapoandika taarifa hiyo yumo katika mpango wa ‘kushughulikiwa na polisi’ ni Francis Godwin ambaye ni mwandishi wa habari wa kujitegemea.

7. Vitendo vya aina hii havivumiliki na havipaswi kuachwa kuendelea kwani ni hatari kwa ustawi wa demokrasia na uhuru wa habari nchini. Hatuwezi kuendelea katika mazingira ambayo polisi wanageuka kuwa chombo cha mauaji ya raia badala ya kuwa walinzi wa raia.

8. Kwa maana hiyo, mbali na uchunguzi ambao utafanywa na polisi, tunatoa wito kwa Serikali kuunda chombo huru, ambacho kitabaini ukweli, na matokeo yake yatangazwe kwa umma, huku wahusika wa aibu hiyo wakichukuliwa hatua za kisheria. Tunasema hivyo, tukifahamu kwamba tayari kuna jitihada za kuficha ukweli na kueneza propaganda za uongo kuhusu tukio zima.

9. Mwenendo wa aina hii wa chombo cha dola kuamua kutumia silaha kuua na baadaye kupanga mbinu chafu za kuficha ukweli ni hatari kwa Taifa, na unaiweka demokraisia ya nchi yetu njia panda, huku tukielekea katika hatari ya Taifa kutumbukia katika uovu.


IMETOLEWA NA:

NEVILLE MEENA,
KATIBU MKUU – JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA (TEF)
SEPTEMBA 3, 2012
 
Kikao azimiocha jukwaa la wahariri kilichofanyika leo kimetoa uamuzi wa kugomea kuandika habari zote zinazohusu jeshi la polisi nchini.

Source:ITV habari za saa.
Wahariri wa Daily News, Habari, Leo na Uhuru nao walikuwamo kwenye hicho kikao? Walikubaliana na maazimio?
Wenzenu Polisi ndio watafurahia ili watu wauawe na kupotezwa kimya kimya! Afadhali wangegomea habari za CCM.
 
kugomea habari za polisi haitoshi.....lazima waua wachukuliwe hatua....kuna haja ya kupeleka serikali mahakamani
 
Wapo watakaobeza, lakini kiukweli, It's a very good starting point! watakaobeza ni wale wasiojua badon umuhimu wa media!
 
Wagomee pia kuandika chochote dhidi ya hii Serikali magamba na magamba yao hadi haki itakapotendeka dhidi ya mauaji ya Mwangosi.
 
Wahariri wa Daily News, Habari, Leo na Uhuru nao walikuwamo kwenye hicho kikao? Walikubaliana na maazimio?
Wenzenu Polisi ndio watafurahia ili watu wauawe na kupotezwa kimya kimya! Afadhali wangegomea habari za CCM.

hayo magazeti hakuna anaye yanunua siku hizi sbb kila mtu siku hizi anajua habari zake ni za uongo na za kuitetea serikali iliyoshindwa! Mimi toka limefungiwa mwanahalisi nasoma makala za nyuma za mwanahalisi.
 
hiyo haitasaidia cha msingi ni waandikwe maovu yote wanayofanya na wasioneshe habari yoyote inayomhusu JK
 
Kikao cha jukwaa la wahariri nchini kilichofanyika leo mijini Iringa kimetoa uamuzi wa kususia kuandika habari zote zinazolihusu jeshi la polisi nchini ikiwa ni pamoja na shughuli za wiki ya nenda kwa usalama barabarani zitakazofanyika mkoani Iringa.

Source:ITV habari za saa.


Yaani kikao chao chote wameona hivi tu ? wasipo andika na wao si ndio wanafurahi kwa mambo yatakuwa yanaenda kimya kimya na watu hawajui, nadhani wangetafuta njia nyingine, kwa hii itazidi kuwaumiza wananchi kuliko polisi yenyewe
 
Kikao cha jukwaa la wahariri nchini kilichofanyika leo mijini Iringa kimetoa uamuzi wa kususia kuandika habari zote zinazolihusu jeshi la polisi nchini ikiwa ni pamoja na shughuli za wiki ya nenda kwa usalama barabarani zitakazofanyika mkoani Iringa.

Source:ITV habari za saa.

Ok ila ni adhabu ndogo sana. I hope kwa kuwa evidence zipo jipangeni fanyeni consultation na vyombo vyombo vya kisheria halafu muone ni namna gani mtajipanga kufungua kesi mahakamani. Ninaamini wapo wanasheria ambao wako kijamii zaaidi na watawasaidia kesi kwa gharama nafuu. Wasilianeni na Legal and Human Rights Centre watawapa ushauri.
 
Hili tamko linawahusisha hata wahariri wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo, Bahari leo na Daily News?
 
Zinazosusiwa kuandikwa ni habari ambazo polisi wanazitoa wao kwa vyombo vya habari na sio habari wanazotoa watu wengine dhidi ya polisi kama vile malalamiko, n.k.
 
Samahani sana ndugu zangu, mbona taarifa hii sijaona hapo waliposema kuwa wanagoma kuandika habari za polisi?
Nifafanulieni waungwana.
 
Back
Top Bottom