Jukwaa la wahariri wagomea kuandika habari zote za jeshi la polisi

Mkuu Ze Marcopolo, naomba unikumbushe lini na wapi niliwahi kusema "waandishi hawaandiki kitu mpaka wapewe "bahasha"?.

Mimi ni mtetezi wa bahasha halali za waandishi ambazo ni stahili zao!, nisome HAPA - nimeeleza kwa kila kitu!.

Mkuu sana Pasco, hapo kwenye "uhalali" ndiko kunakosababisha waandishi waone kuwa wanaandika habari kwa ajili ya RPC, kwa sababu kibahasha kinawafanya waamini kuwa aliyewalipa ni mnufaika wa kwanza wa habari wanayoandika. Sasa huu mgomo lengo lake ni kutanua upana wa bahasha. By the way, link imekataa kufunguka mkuu.
 
Mkuu sana Pasco, hapo kwenye "uhalali" ndiko kunakosababisha waandishi waone kuwa wanaandika habari kwa ajili ya RPC, kwa sababu kibahasha kinawafanya waamini kuwa aliyewalipa ni mnufaika wa kwanza wa habari wanayoandika. Sasa huu mgomo lengo lake ni kutanua upana wa bahasha. By the way, link imekataa kufunguka mkuu.
Mkuu Ze Marcopolo, nimeelezea mazingira ya uhalali wa bahasha, hakuna hata RPC mmoja anayetoa bahasha kwa waandishi ili waandikwe!. Bahasha halali ni "transport", "breakfast, lunch au dinner" kwa events za saa za chakula,
"sitting" kwa mikutano, semina, warsha na makongamano ya siku nzima yenye "sitting allowance", na bahasha za DSA au "perdiem" wawapo nje ya vituo vyao!, CNN wanalipa, BBC wanalipa, na bongo kuanzia Takukuru, hadi Ikulu, wanazilipa!. Hizi ni bahasha halali, legal na zinagawiwa wazi wazi bila usiri au kificho chochote, na mpokeaji ana sign!.

Rudi kwenye link, nimeirekebisha HAPA

Pasco.
 
Propanga zao, na jinsi ya kuzideliva mnazijua vizuri, at some point mlitumika ninyi (vyombo vya habari) kusambaza hizo propaganda na kupotosha mengi.

Lengo langu hapa sio kulaumiana au kunyoosheana vidole ila ni kyuwaonesha tu waandishi ya kuwa, kwa kuwa mliwahi shiriki nao, sasa itakuwa rahisi kuwabana na mbinu zao.
Step ya kwanza vitani kumjua adui yako na strategies zake. Ninyi mna hiyo advantage, zuieni hizo propaganda na mtumie mianya hiyo hiyo kusambaza ukweli.

R.I.P Daud
 
Ivi ulinzi shirikishi nao ni kwafaida ya raia, au police; ili ikibidi tuwaache hii mijitu iuwawe na majambazi. Wao wakiambiwa "shoot" wana-shoot bila ku-reason.
 
Jukwaa la wahariri siwaelewi,,,,Mwanahalisi limefungiwa kwa kuonewa mkatoa msimamo hafifu wakati kulikuwa na kila indication ya kugomea habari za serikali.
leo mnatuambia mnagomea jeshi la polisi pekee, kwani polisi inalipwa na nani kama si serikali, GOMEENI SERIKALI! Ukipenda boga penda na ua lake
 
polisi wasipo andikwa sindio wataua zaidi ??

Unapogomea maana yake unaacha kuandika habari ambazo wao wangependa uwafikishie umma ili kufanikisha utendaji kazi wao. Kwa lugha nyingine unaacha kuandika habari zote zinazolipamba jeshi la polisi, ila habari zote mbaya zinazotendwa na jeshi la polisi zinaandikwa, kwani chanzo kinakuwa upande wa pili ambao ni ule unaobinywa na polisi.
 
Jamani wanaJF naomba mnisaidie kujua kuwa hivi hakuna namna yoyote ya kuanzisha kesi ya kuishtaki Serikali/IGP/RPC na wengineo wanaohusika na mauaji haya ya KIKATILI, Na nani wa kuianzisha? Mimi siamini katika uchunguzi wa Chagonja!
 
Inawezekana vipi kugomea kuandika taarifa toka polisi wakati kikanuni wao ndio watoa taarifa nyingi!!
 
Watu wanaongelea habari za msiba, wewe unaleta habari za dini fulani, hivi wewe kweli una akili??

wewe ndio kilaza kweli, kwani nani hajui kama msiba umetokea. Misiba hutokea sisi tunaobaki hutakiwa kujifunza kutokana na misiba hiyo.
Point yangu ni kuwa Wahariri wameweka mikwara ya kutoandika habari za polisi sawa ni wazo zuri pia mimi nikauliza ili nipate kujua kwanini hao hao wahariri huwa hawaripoti habari za waislam, ivi ni lini walikaa na kukubaliana kuwa hakuna kuripoti habari za waislam na nini waislam waliwafanyia hao waandishi wa habari mpaka wakaamua kutoandika?
Pia kuna mchangiaji hapo nimeona kachangia kuwa waripot ila wageuze wawe wanatangaza habari mbaya tu za police kitu ambacho pia haohao wahariri naona wanakifanya kwa waislam?

Tanzania inakoelekea siyo kuzuri kwa sababu ya haohao wahariri kwa kujikita zaidi kuandika habari za kuchochea na kupandisha hasira kwa wananchi. Mie kwa mtizamo wangu Police wa bongo +wahariri wote ni majanga matupu kwa taifa hili.
kwanini sioni gazeti hata moja likiripoti vitendo vinavyoendelea nchini vya police kuvunja nyumba saa8 za usiku na kuwavamia majumbani mwao eti kisa sensa, na hao wahariri siyo kwamba hawajui hizo habari wanazijua saaaaana tu ila wanaziona siyo habari na matokeo yake kushangilia hivyo vitendo. waache huo upuuzi hautotufikisha pazuri.
wao wanatakiwa waandike kwa kufuata misingi ya taaruma yao na siyo kupendelea kokote.
 
Mbona hakuna sehemu waliyosema wamesusia kuandika habari za polisi km thread ilivyoandikwa?. Ningefarijika km wangesusia.
 
Napenda kuwapa pole familia, ndugu na marafiki wa marehemu Daud Mwangosi kwa kumpoteza mpendwa wao, pia napenda kuwapa pole familia zote, ndugu wote na marafiki wote wa watu wote ambao kwa namna moja au nyingine wamepoteza maisha yao katika harakati za ukombozi au kwa njia za kiuonevu na kiukandamizaji, Mungu mwenye haki atawalipia.
Ushauri wangu kwa Jukwaa la Wahariri, Vyombo vya habari, Waandishi wa Habari nchini, Wanasheria, Taasisi za Kijamii, Taasisi za Haki za Binadamu, Wapenda haki wote, kwanza ni kuhakikisha kwamba wanafanya kila linalowezekana mapema iwezekanavyo kuhakikisha kwamba tume huru inaundwa/zinaundwa kuchunguza mauaji haya ya mwandishi wa habari na mauaji mengine yote yenye utata ili ukweli ufahamike na wahusika wafikishwe katika vyombo vya sheria ili haki itendeke, Pili ni kuhakikisha kwamba kelele za kutosha zinapigwa ili wale wote waliopewa dhamana ya kusimamia vyombo hivi wanawajibishwa, kwenye suala hili WAANDISHI WA HABARI WANA NAFASI KUBWA SANA kwani wakitumia vizuri kalamu zao serikali na chama chake dhalimu lazima watasalimu amri, kususia tu habari za jeshi la polisi haitoshi maana haiwathiri sana wale waliowatuma au kuwatumia polisi kufanya mauaji hayo au uonevu wa wananchi, WAANDISHI WANATAKIWA WASUSIE KUANDIKA HABARI ZA CCM NA SERIKALI YAKE maana ndio inayowatumia POLISI kuua na kutesa watu, WAANDISHI WANATAKIWA WAWEKE MSIMAMO WAO WA KUTORIPOTI HABARI YOYOTE INAYOHUSU CCM AU SERIKALI YAKE KWA KIPINDI CHA MIAKA MITANO na wanatakiwa wawe kitu imoja kwenye suala hili, wakiweka msimamo wa namna hiyo kilio chao kitasikika na heshima ya taaluma yao itarudi, lakini wasipokuwa na msimamo wa pamoja na wakazembea kusimamia haki yao kwa pamoja basi wajue wamekwisha, wajue kwamba huko tunakokwenda vyombo vyote vya habari vitakayopingana na matakwa ya serikali au CCM vitafungiwa na Waandishi wote watakaoripoti habari ambazo hazitawapendeza watawala na chama chao basi wataishia kuteswa au inaweza kupelekea hata kupoteza maisha, hii itahusisha na wananchi ambao watasimama kutetea haki zao. Nasisitiza sana UMOJA NA MSIMAMO kwenye suala hili kwani waandishi wana nafasi ya kujifunza kutoka kwa Madaktari ambao mpaka leo wapo baadhi yao ambao wameteswa na wengine kufukuzwa kazi baada ya kufanya mgomo wa kutofanya kazi, serikali imeweza kufanya iliyoyafanya kwa sababu madaktari walikosa UMOJA NA MSIMAMO. Tatu ni kuhakikisha kuwa chama cha waandishi wa habari kinaanzisha Taasisi au Mfuko wa Daud Mwangosi (Daud Mwangosi Foundation/Fund) ambao utakuwa na utaratibu wa kukusanya michango toka kwa waandishi wa habari na vyombo mbalimbali vya habari kila mwezi na hata kutoka kwa wapenda amani na maendeleo wote ili kiweze kuwa msaada kwa familia ya marehemu Daud Mwangosi hasa katika kuwasaidia kiuchumi na kuwasomesha watoto wake, pia mfuko/taasisi hii inaweza kuwasaidia hata familia za waandishi wa habari wowote wanachama wa mfuko huu ambao watapata matatizo na kupelekea kupata ulemavu au kupoteza maisha katika utekelezaji wa majukumu yao, ni suala linalotia uchungu sana kuona familia ile imempoteza mpendwa wao na kiongozi mkuu wa familia, najua hatuwezi kuyapunguza machungu yao yote lakini kwa yale ambayo yako kwenye uwezo wetu basi na tuyafanye. Ushauri huu vilevile sio mbaya ukatumiwa na madaktari vilevile na makundi mengine yote yaliyo katika harakati za kudai haki. Naomba kuwasilisha.
 
Wahariri wa Daily News, Habari, Leo na Uhuru nao walikuwamo kwenye hicho kikao? Walikubaliana na maazimio?
Wenzenu Polisi ndio watafurahia ili watu wauawe na kupotezwa kimya kimya! Afadhali wangegomea habari za CCM.

Serikali haiwezi kujigomea....
 
Back
Top Bottom