Kaa la Moto
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 7,903
- 1,053
Jukwa la wahariri ni kijiwe tuu wanamtishia nyau Mhe.Mkuchika!. Liko kama kikao cha harusi cha watu fulani kutangaza kususia kufanya sherehe yao ukumbi fulani. Hili jukwaa halina any legal status wala registration ya aina yoyote. Afadhali kidogo MOAT japo haipo kisheria imesajiliwa kama kampuni.
Chombo halali chenye nguvu ya kisheria kumuadhibu Mkuchika ni Media Council of Tanzania (MCT) na Tanzania Journalist Association(TAJA) ambacho nadhani kiko ICU.
Wahariri wa Jukwaa la wahariri hawana ubavu wa kweli kumuadhibu Mkuchika ni magazeti machache tuu ndiyo yenye uwezo wa kweli haswa yale ambayo wahariri wake ni wamiliki kama Kubenea wengine hawana jeuri hiyo kwa vile wamiliki wanajikomba serikalini hiv
yo huo ndio mwanzo wa kugeukana na kusalitiana.
Mtathibitisha kauli yangu soon. Mhe. Mkuchika ni JK type, mbabe,Jeuri, hasikilizi wala hashauriki. Kumshauri JK kumuadhibu Mkuchika ni kesi ya nyani kuipeleka kwa ngedere
Hiki ni kituko, ukilaza, kichekesho, na utupu usio kipimo.
Mwandishi wa habari hutakiwi na huwezi kusema unamwadhibu kiongozi kwa kutoandika habari za kazi zake!!
Hell no!!!
Kuandika habari za kazi za Kiongozi yeyote yule ni kwa manufaa ya jamii!!!
Waandisha wa habari wana kiapo cha fani, taaluma, na kazi yao, na vile vile wana mkataba na jamii kuwapasha habari zozote na zote zile za kazi za nchi!!!
Vilaza wa crummy press ya Tanzania hawajui hicho kitu, masikini weeeeee!!!
Katika eneo la uandishi wa habari, Tanzania tuko katika cesspool la vilaza wakutupwa!!!
I doubt kama kumsusia huko kutamaffect in any way!By the way kwenye hilo Jukwaa la Wahariri magazeti ya Serikali nayo yamo?Kama hayapo basi habari za Mkuchika zitapeta tuu!Wakisikia amebaka mtu hawataandika?
Jukwaa la Wahariri this time wamekosa shabaha kwa kweli!Badala wachukue hatua mbadala za kumshugulikia Mkuchika wao wanadai kumsusia!
Haya andikeni mnayotaka kuandika!
JUkwaa La Wahariri linadai kwamba taaluma yao ya uandshi habari inatakiwa kulindwa sasa inakuwaje wao wenyewe wanaidemoralize kwa kumfumgia mtu mmoja bila hata ya kumskiliza na wao wenyewe kufanyia uchunguzi taarifa ya Mwanahalisi?Hivi wao kama waandishi wabari hawaoni kama wanakuwa too biased ingawa ndio ni mwenzao kaonewa they should do some research into the issue siyo kukurupuka tuu!
Hiki kijiwe cha wahariri kinatupa somo moja kubwa kuwa ili habari yako iandikwe ( positively ) lazima uwe na unafuata/unaheshimu matakwa yao. Hii ni jinga la kitaifa walau wamejionyesha wenyewe jinsi walivyo.
Kosa (IF- Capital ) la Mkuchika adhabu kwa wananchi? wahandisi mnatupeleka wapi sasa? Huu ni ufisadi habari hicho kijiwe cha wahariri kimechemka big time!
JUkwaa La Wahariri linadai kwamba taaluma yao ya uandshi habari inatakiwa kulindwa sasa inakuwaje wao wenyewe wanaidemoralize kwa kumfumgia mtu mmoja bila hata ya kumskiliza na wao wenyewe kufanyia uchunguzi taarifa ya Mwanahalisi?
Hivi wao kama waandishi wabari hawaoni kama wanakuwa too biased ingawa ndio ni mwenzao kaonewa they should do some research into the issue siyo kukurupuka tuu!
Hii haina maana ya kwamba habarii hazitaandikwa kuhusu michezo, utamaduni au wizara ya habari. Kama wana Habari wanaweza kupitia Manaibu Waziri au Katibu na habari hiyo itaandikwa. Lakini yeye Mkuchika akitaka kuitisha waandishi wa habari kuzungumza hawaendi kumsikiliza, akiwa na jambo la kusema hakuna wa kumnukuu kwa sababu kama yeye ameweza kuzima kauli ya gazeti zima na kalamu lukuki kwa stroke of a pen, basi waandishi nao kwa kuziweka kalamu zao chini hawatoandika anayosema.
Sasa hili ni suala la Waziri wa Habari Bw. George Mkuchika. Kwa maneno mengine akienda kufungua warsha hakuna atakayeripoti na kama wao wanataka iripotiwe wamtume mtu mwingine. Lengo ni kuonesha kuwa kama vyombo vya habari vingekuwa na uwezo wa kwenda mahakamani kupinga na kutengua uamuzi huo au hata kuuzuia usitekelezwe hili lisingekuwa lazima.
Sasa unapomnyima hata haki ya kukata rufaa unataka afanye nini? Desperate times, require desperate measures. Mkuchika siyo the sum of Wizara ya Habari kiasi kwamba yeye akisusiwa basi hakuna habari itakayotoka huko. Kama wizara wana habari au jambo muhimu wanao viongozi wengine akiwemo Katibu Mkuu, Manaibu Waziri na hata Idara ya Maelezo.
...By the way, KLHN imepata nafasi ya kuzungumza na Mkuchika mapema leo kwa kirefu ....
Kwa hiyo unaunga mkono kitendo cha wenzio kususia kuandika habari za kiongozi. Sasa nimechoka na jinsi ulivyokuwa huna objectivity, na unavyopenda kutetea wahariri wa crummy press ya Tanzania kwa sababu tu unawaandikia. Unatufanya wajinga!
Wabeloya, kevo, kuhani, mag3, Masatu na wengine mnaodhani adhabu hii haiwezi kufanya kazi nyie subirini...............................................................................................
............................................................................................................
Na sisi wasomaji wa magazeti hatutanunua gazeti lenye habari ya Mkuchika. Sasa muandishi yeyote na aziandike na kuzisoma mwenyewe.
Basi ungeuliza nilizungumzia naye saa ngapi basi? Usishabikie tu. Kwa taarifa yako nilizungumza naye kabla ya uamuzi wa hilo baraza kutolewa mapema leo (saa moja na nusu za asubuhi za Tanzania). Na ni kutokana na hilo kwa vile ninaungana na wahariri wengine sitoweka mahojiano yangu naye kwenye KLH News kama nilivyopanga nitayaweka yala ya Marando tu.
...Hata kesho akiingia Waziri mwingine kama hatotengua uamuzi wa Mkuchika mgomo utaendelea vile vile. ....
You are missing the point!
Umetangaza kwamba Wahariri wamem boycott Mkuchika halafu baadae ndio ukatangaza kwamba umeongea na Mkuchika. Hukuweka time frame. Kwa hiyo nishukuru mimi kwa kukupa nafasi ya kuwaelewesha waandishi na wahariri waajiri wako kwamba kumbe umempa audience/sikio Mkuchika kabla ya wenzako kukubaliana kususa.
Lakini hiyo ni excuse ambayo only crummy press ya Tanzania - kwa sababu ni watupu - wataikubali.
Nitakwambia kwa nini mjanja hawezi kuikubali: Kitendo cha wewe kutangaza kwamba umeongea na Mkuchika - hata kama ilikuwa ni kabla ya makubaliano ya kususa - kwa wewe kutangaza hicho kitu baada ya kujua kwamba Mkuchika hatakiwi kuongelewa tayari umeshavunja makubaliano ya msuso. Msuso wenu hautakiwi kutamka neno Mkuchika, hata kusema "niliongea na Mkuchika lakini siwaambii alichosema..." Umeshavunja msuso.
Kususa kwenu ni kuvunja mkataba na jamii wa kuhabarisha kazi za Kiongozi. Ni kiapo cha fani yenu. Ni hallmark ethic ya taaluma ya uandishi.
Naamini ndani ya roho yangu kwamba inawezekana waandishi wa Tanzania hamjui maana ya maneno "mkataba na jamii" au "social contract."
You are missing the point!
Umetangaza kwamba Wahariri wamem boycott Mkuchika halafu baadae ndio ukatangaza kwamba umeongea na Mkuchika. Hukuweka time frame. Kwa hiyo nishukuru mimi kwa kukupa nafasi ya kuwaelewesha waandishi na wahariri waajiri wako kwamba kumbe umempa audience/sikio Mkuchika kabla ya wenzako kukubaliana kususa.
Nitakwambia kwa nini mjanja hawezi kuikubali: Kitendo cha wewe kutangaza kwamba umeongea na Mkuchika - hata kama ilikuwa ni kabla ya makubaliano ya kususa - kwa wewe kutangaza hicho kitu baada ya kujua kwamba Mkuchika hatakiwi kuongelewa tayari umeshavunja makubaliano ya msuso. Msuso wenu hautakiwi kutamka neno Mkuchika, hata kusema "niliongea na Mkuchika lakini siwaambii alichosema..." Umeshavunja msuso.
Kususa kwenu ni kuvunja mkataba na jamii wa kuhabarisha kazi za Kiongozi. Ni kiapo cha fani yenu. Ni hallmark ethic ya taaluma ya uandishi.
Naamini ndani ya roho yangu kwamba inawezekana waandishi wa Tanzania hamjui maana ya maneno "mkataba na jamii" au "social contract."