Jukwaa la Wahariri lamfungia Mkuchika; latoa ripoti ya Tarime

Jukwa la wahariri ni kijiwe tuu wanamtishia nyau Mhe.Mkuchika!. Liko kama kikao cha harusi cha watu fulani kutangaza kususia kufanya sherehe yao ukumbi fulani. Hili jukwaa halina any legal status wala registration ya aina yoyote. Afadhali kidogo MOAT japo haipo kisheria imesajiliwa kama kampuni.

Chombo halali chenye nguvu ya kisheria kumuadhibu Mkuchika ni Media Council of Tanzania (MCT) na Tanzania Journalist Association(TAJA) ambacho nadhani kiko ICU.
Wahariri wa Jukwaa la wahariri hawana ubavu wa kweli kumuadhibu Mkuchika ni magazeti machache tuu ndiyo yenye uwezo wa kweli haswa yale ambayo wahariri wake ni wamiliki kama Kubenea wengine hawana jeuri hiyo kwa vile wamiliki wanajikomba serikalini hiv
yo huo ndio mwanzo wa kugeukana na kusalitiana.
Mtathibitisha kauli yangu soon. Mhe. Mkuchika ni JK type, mbabe,Jeuri, hasikilizi wala hashauriki. Kumshauri JK kumuadhibu Mkuchika ni kesi ya nyani kuipeleka kwa ngedere

.....Lakini wengi wa wahariri walio na msimamo ndiyo habari zao zinauzika ati.
Unadhani nani bado anasoma Uhuru na daily news?
 
JUkwaa La Wahariri linadai kwamba taaluma yao ya uandshi habari inatakiwa kulindwa sasa inakuwaje wao wenyewe wanaidemoralize kwa kumfumgia mtu mmoja bila hata ya kumskiliza na wao wenyewe kufanyia uchunguzi taarifa ya Mwanahalisi?Hivi wao kama waandishi wabari hawaoni kama wanakuwa too biased ingawa ndio ni mwenzao kaonewa they should do some research into the issue siyo kukurupuka tuu!
 
Hiki ni kituko, ukilaza, kichekesho, na utupu usio kipimo.

Mwandishi wa habari hutakiwi na huwezi kusema unamwadhibu kiongozi kwa kutoandika habari za kazi zake!!

Hell no!!!

Kuandika habari za kazi za Kiongozi yeyote yule ni kwa manufaa ya jamii!!!

Waandisha wa habari wana kiapo cha fani, taaluma, na kazi yao, na vile vile wana mkataba na jamii kuwapasha habari zozote na zote zile za kazi za nchi!!!

Vilaza wa crummy press ya Tanzania hawajui hicho kitu, masikini weeeeee!!!

Katika eneo la uandishi wa habari, Tanzania tuko katika cesspool la vilaza wakutupwa!!!

...na wote wanaofanya migomo kwa waajili wao huwa wanakiapo na mikataba nao.
Lakini bado mgomo huwa ni fimbo ya kuwachapia waovu wote kama Mkuchika.
 
I doubt kama kumsusia huko kutamaffect in any way!By the way kwenye hilo Jukwaa la Wahariri magazeti ya Serikali nayo yamo?Kama hayapo basi habari za Mkuchika zitapeta tuu!Wakisikia amebaka mtu hawataandika?

Duh.. habari anazotoa yeye!! mweh...
 
Mnaosema hawakumpa nafasi ya kumsikiliza naona mmesahau kuwa alishawambia yeye ni mtu mkubwa hawezi kuitwa na watu wadogo kama waandishi wa habari bali yeye ndio anaweza kuwaita na ni lazima waende kwake.

huyu kufungiwa kwake na yeye nisababu tu imepatikana kwani walikuwa wanaitafuta amewadhalilisha waandishi wa habarikwa kuwaita kuwa wao ni watu wadogo sana kwake.
 
Jukwaa la Wahariri this time wamekosa shabaha kwa kweli!Badala wachukue hatua mbadala za kumshugulikia Mkuchika wao wanadai kumsusia!
Haya andikeni mnayotaka kuandika!

pendekeza hatua ya kumchukulia; kuna mambo matano yamependekezwa hapo juu mbona ni hili moja tu ambalo mnaliona baya, hayo mengine mnakubaliana nayo au nayo mnaona wamekosea? Kama yote wamekosea toeni pendekezo wafanye nini. Siyo tu kukosoa na kusubiri wafanye ili mkosoe badala ya angalau kutoa pendekezo wamshughulikiaje zaidi ya mambo hayo matano?
 
JUkwaa La Wahariri linadai kwamba taaluma yao ya uandshi habari inatakiwa kulindwa sasa inakuwaje wao wenyewe wanaidemoralize kwa kumfumgia mtu mmoja bila hata ya kumskiliza na wao wenyewe kufanyia uchunguzi taarifa ya Mwanahalisi?Hivi wao kama waandishi wabari hawaoni kama wanakuwa too biased ingawa ndio ni mwenzao kaonewa they should do some research into the issue siyo kukurupuka tuu!

Kwa mujibu wa mahojiano yao na BBC, Mkuchika hakutaka kuonana nao. Hapa nadhani wanamaanisha chombo chao cha kusimamia nidhamu ya wanahabari, yaani Baraza la Habari Tanzania (Tazama: http://www.mct.or.tz/). BBC imemnukuu mshirika wao akisema kuwa mawaziri wengine, wakiwamo mawaziri wakuu wa zamani, na hata Spika mwenyewe walipeleka malalamiko yao huko kuhusu magazeti fulani na yakafanyiwa kazi na anahoji kama Mkuchika ni mkubwa kuliko hao!

Kuhusu hilo la kumfungia Mkuchika nadhani mantiki yake ni kumweka katika hali ngumu ili ajione sio mkubwa kuliko vyombo vya habari. Mbinu hii ilifanya kazi sana kwa Mapuri maana hata mikutano yake ilisusiwa na wanahabari mpaka akaona kiti cha moto sasa sijui kama itafanya kazi kwa Mkuchika au la. Wasiwasi wangu ni hili la kumwomba Muungwana aingilie kati maana kwa kawaida maamuzi mazito kama haya hayafanyiki bila mkono wa mkuu wa wakuu. Kumbuka ya Mkapa kumuunga mkono Khatib dhidi ya HakiElimu!
 
Hiki kijiwe cha wahariri kinatupa somo moja kubwa kuwa ili habari yako iandikwe ( positively ) lazima uwe na unafuata/unaheshimu matakwa yao. Hii ni jinga la kitaifa walau wamejionyesha wenyewe jinsi walivyo.

Kosa (IF- Capital ) la Mkuchika adhabu kwa wananchi? wahandisi mnatupeleka wapi sasa? Huu ni ufisadi habari hicho kijiwe cha wahariri kimechemka big time!

Masatu hakuna fisadi wa habari kama Mkuchika ambaye katulazimisha tusipate habari kwa miezi mitatu. Haya mengine unayosema hapa hayana maana. Na huu ndio ujinga wa Mkuchika si jukwaa la wahariri.
 
JUkwaa La Wahariri linadai kwamba taaluma yao ya uandshi habari inatakiwa kulindwa sasa inakuwaje wao wenyewe wanaidemoralize kwa kumfumgia mtu mmoja bila hata ya kumskiliza na wao wenyewe kufanyia uchunguzi taarifa ya Mwanahalisi?

Hawakumfungia mtu mmoja tu kama vile ni mtu fulani toka gengeni. Walichokataa ni kuandika habari kutoka kwa mtu mwenye uwezo wa kiimla wa kulifungia gazeti lolote at will (as long as yeye ameridhika. Narudia tena hawana uwezo wa kumuita Waziri na kumtaka atoe utetezi au kujieleza. Uamuzi wa Waziri kufungia gazeti ni absolute!

Hivi wao kama waandishi wabari hawaoni kama wanakuwa too biased ingawa ndio ni mwenzao kaonewa they should do some research into the issue siyo kukurupuka tuu!

Wameshafanya research na wakajenga hoja kuwa habari hiyo siyo ya kichochezi na katika kuthibitisha hivyo wakaonesha habari kama hiyo kutoka Raia Mwema na kutoka Rais. Guess what, Mkuchika anasema (paraphrasing) "quod scripsi, scripsi" ... niliyoyaandika, nimeyaandika. Sasa katika mazingira hayo waandishi wafanye nini? Wampigie magoti na kumuomba radhi?

Hili ni zaidi ya suala la Kubenea, it is about unfair and unjust law. It is an act of protest. It is not about Mkuchika as an invididual but what that individual represent. Hata kesho akiingia Waziri mwingine kama hatotengua uamuzi wa Mkuchika mgomo utaendelea vile vile. It is an act of protest against a dictatorial law, a law which need to be challenged, questioned and rightly discarded into the unforgiving dumpster of history.
 
Wabeloya, kevo, kuhani, mag3, Masatu na wengine mnaodhani adhabu hii haiwezi kufanya kazi nyie subirini.
Nafahamu adhabu kama hii iliwahi kufanya kazi kwa Ramadhani Mapuli na yule mkuu wa magereza Tanzania.
Nakwambia mpaka Mapuli anaondoka kwenda ubalozini ndio tulifahamu kwamba bado ana exist lakini kabla ya hapo alikuwa uvunguni na hasikiki kabisa. Ilimuathiri hata katika uchaguzi 2005.
Nyie subirini muone kama wahariri hawana power kama mnavyotaka kuwasadikisha wengine hapa.
Na kwa taarifa yenu kama yeye Mkuchika hakuona vyombo vingine vya kisheria vina haki ya kusikiliza kesi hii ila yeye mpiga propaganda za chama, then hakuwa na haki ya kuitwa mahali popote kuulizwa kuhusu uamuzi wake.
Walichofanya wahariri regardless kwamba labda kuna watakaowazunguka ndicho sahihi.
Na sisi wasomaji wa magazeti hatutanunua gazeti lenye habari ya Mkuchika. Sasa muandishi yeyote na aziandike na kuzisoma mwenyewe.
 
Hii haina maana ya kwamba habarii hazitaandikwa kuhusu michezo, utamaduni au wizara ya habari. Kama wana Habari wanaweza kupitia Manaibu Waziri au Katibu na habari hiyo itaandikwa. Lakini yeye Mkuchika akitaka kuitisha waandishi wa habari kuzungumza hawaendi kumsikiliza, akiwa na jambo la kusema hakuna wa kumnukuu kwa sababu kama yeye ameweza kuzima kauli ya gazeti zima na kalamu lukuki kwa stroke of a pen, basi waandishi nao kwa kuziweka kalamu zao chini hawatoandika anayosema.

Sasa hili ni suala la Waziri wa Habari Bw. George Mkuchika. Kwa maneno mengine akienda kufungua warsha hakuna atakayeripoti na kama wao wanataka iripotiwe wamtume mtu mwingine. Lengo ni kuonesha kuwa kama vyombo vya habari vingekuwa na uwezo wa kwenda mahakamani kupinga na kutengua uamuzi huo au hata kuuzuia usitekelezwe hili lisingekuwa lazima.

Sasa unapomnyima hata haki ya kukata rufaa unataka afanye nini? Desperate times, require desperate measures. Mkuchika siyo the sum of Wizara ya Habari kiasi kwamba yeye akisusiwa basi hakuna habari itakayotoka huko. Kama wizara wana habari au jambo muhimu wanao viongozi wengine akiwemo Katibu Mkuu, Manaibu Waziri na hata Idara ya Maelezo.

Kwa hiyo unaunga mkono kitendo cha wenzio kususia kuandika habari za kiongozi. Sasa nimechoka na jinsi ulivyokuwa huna objectivity, na unavyopenda kutetea wahariri wa crummy press ya Tanzania kwa sababu tu unawaandikia. Unatufanya wajinga!

...By the way, KLHN imepata nafasi ya kuzungumza na Mkuchika mapema leo kwa kirefu ....

Wahariri wa crummy press ya Tanzania eeeeeeeh!

Mwandishi mwenzenu, M.M. Mwanakijiji wa KLH News, yuko pembeni huku anampa audience Mkuchika!!
 
Hivi wajameni, UHURU na MZALENDO nao wana msimamo huo?????

Kazi ipo!!!!!!!
 
Kwa hiyo unaunga mkono kitendo cha wenzio kususia kuandika habari za kiongozi. Sasa nimechoka na jinsi ulivyokuwa huna objectivity, na unavyopenda kutetea wahariri wa crummy press ya Tanzania kwa sababu tu unawaandikia. Unatufanya wajinga!

Nope, siyo kukususia habari za "kiongozi" tu bali kiongozi ambaye ana uwezo wa kufuta ajira za watu 15 kwa nguvu ya kalamu yake. Anayetufanya wajinga ni yule ambaye anafikiri anaweza kuwaamulia Watanzania nini cha kusoma au kuandika na wewe huyo hakupi tatizo. Magazeti haya ni vyombo huru vya watu binafsi au taasisi na vina haki ya kufanya wanachotaka kufanya wakiongozwa na dhamira zao.

Huwezi kumlazimisha mganga ambaye dhamira yake haimuongozi kukubali utoaji mimba atoe mimba kwa sababu tu yeye ni mganga. Dhamira ya mtu ni juu ya uamuzi wa mtu mwingine. Wahariri kwa dhamira zao wameona kuwa hawawezi kupokea habari kutoka kwa mtu mwenye uwezo wa kufuta na kusimamisha ajira zao kwa nguvu ya mkono wake. Dhamira zao zimeinuka juu kuliko kitu kingine na hapo ninawaunga mkono.

Kama wewe dhamira yako inakutuma kuamini kuwa ni sawa kwa Mkuchika kuwa na nguvu hiyo na mtu yeyote asioneshe njia ya kupinga nguvu hiyo kwa civil disobedience hiyo ni haki yako kwani unafuata dhamira yako.

Wahariri wa crummy press ya Tanzania eeeeeeeh!

Mwandishi mwenzenu, M.M. Mwanakijiji, yuko pembeni huku anampa audience Mkuchika!!
[/QUOTE]

Basi ungeuliza nilizungumzia naye saa ngapi basi? Usishabikie tu. Kwa taarifa yako nilizungumza naye kabla ya uamuzi wa hilo baraza kutolewa mapema leo (saa moja na nusu za asubuhi za Tanzania). Na ni kutokana na hilo kwa vile ninaungana na wahariri wengine sitoweka mahojiano yangu naye kwenye KLH News kama nilivyopanga nitayaweka yala ya Marando tu.
 
Wajameni!!
Hebu tunaohoji kama magazeti ya Uhuru na Mzalendo nayo yamo ktk mgomo huu mjiulize kwa mara ya mwisho ninyi kuyanunua ilikuwa lini.Haya magazeti yapo kinadharia tu lakini majority ya watanzania/jamii hawayasomi.mniamini kwa hili.

Kuhusu adhabu aliyopewa huyu bwn mwanajeshi inatosha kabisa.Mimi naungana nao kwa kichwa na miguu.Na kwa kuanza hapa mtandaoni nikiona tu neno mkuchika nitakavyokimbiza kasa yangu ku-scroll mbali wewe acha tu.

Hawa wahariri wana akili SANA.Wao walichokifanya ni kumpa adhabu ya kisaikolojia.Hebu wewe fikiria kwa muda huu akiwa na jambo la kiserikali au kichama lisipoandikwa au kutekelezwa kama litakavyotakiwa kuwa,mwajiri wake atajisikiaje????Naamini hata Rais akisikia wahariri wamemgomea KAMWE hatompa issue serious azishughulikie ili ilhali nia ni kuzifikisha kwa wananchi.Kwa suala hilo la kutumia c/o limamuumiza sana mwanajeshi mkuchika.Halafu zingatia hapo hapo ccm kuna watu wanapiga jalamba kufukuzia nafasi ya uwaziri,utafikiri wanamnong'onezaje muungwana???
Mimi nawapa 5 JUKWAA LA WAHARIRI.Pia nimependa mchakato wa tamko la adhabu hiyo ulivyo.Yeye si amemwaga mboga,wahariri wamemwaga ugali.
 
Wabeloya, kevo, kuhani, mag3, Masatu na wengine mnaodhani adhabu hii haiwezi kufanya kazi nyie subirini...............................................................................................
............................................................................................................
Na sisi wasomaji wa magazeti hatutanunua gazeti lenye habari ya Mkuchika. Sasa muandishi yeyote na aziandike na kuzisoma mwenyewe.

mchukia fisadi,

Umekosea kuniweka kwenye kundi hili na nakuomba tena usome post yangu uielewe vizuri na nilichoongelea ni uamuzi wao wa kutokuitoa hiyo ripoti mapema. Nilisema hivi;

Na hiyo ripoti ingeathiri vipi uchaguzi wa Tarime ? Je, ni vibaya wananchi kwa ujumla wao wakijua ukweli wa mambo ? Je, hiyo ripoti ingetolewa ina maana ingesaidia CCM na Chadema haingeshinda ? Kwa hakika nashindwa kuelewa msimamo wa hili jukwaa !!
 
Basi ungeuliza nilizungumzia naye saa ngapi basi? Usishabikie tu. Kwa taarifa yako nilizungumza naye kabla ya uamuzi wa hilo baraza kutolewa mapema leo (saa moja na nusu za asubuhi za Tanzania). Na ni kutokana na hilo kwa vile ninaungana na wahariri wengine sitoweka mahojiano yangu naye kwenye KLH News kama nilivyopanga nitayaweka yala ya Marando tu.

You are missing the point!

Umetangaza kwamba Wahariri wamem boycott Mkuchika halafu baadae ndio ukatangaza kwamba umeongea na Mkuchika. Hukuweka time frame. Kwa hiyo nishukuru mimi kwa kukupa nafasi ya kuwaelewesha waandishi na wahariri waajiri wako kwamba kumbe umempa audience/sikio Mkuchika kabla ya wenzako kukubaliana kususa.

Lakini hiyo ni excuse ambayo only crummy press ya Tanzania - kwa sababu ni watupu - wataikubali.

Nitakwambia kwa nini mjanja hawezi kuikubali: Kitendo cha wewe kutangaza kwamba umeongea na Mkuchika - hata kama ilikuwa ni kabla ya makubaliano ya kususa - kwa wewe kutangaza hicho kitu baada ya kujua kwamba Mkuchika hatakiwi kuongelewa tayari umeshavunja makubaliano ya msuso. Msuso wenu hautakiwi kutamka neno Mkuchika, hata kusema "niliongea na Mkuchika lakini siwaambii alichosema..." Umeshavunja msuso.

Kususa kwenu ni kuvunja mkataba na jamii wa kuhabarisha kazi za Kiongozi. Ni kiapo cha fani yenu. Ni hallmark ethic ya taaluma ya uandishi.

Inawezekana waandishi wa Tanzania hamjui maana ya maneno "mkataba na jamii" au "social contract."
 
Naamini ndani ya roho yangu kwamba inawezekana waandishi wa Tanzania hamjui maana ya maneno "mkataba na jamii" au "social contract."

Kuhani,

Naona wewe objectivity yako ni kujibizana na Mwanakijiji tu! Hasa kwa siku za karibuni! It is always healthy to have different ways of looking at 'a thing' but it looks to me like 'the thing' to you is nothing but hoja za Mwanakijij! Of late, your posts are becoming NOISY!
 
You are missing the point!

Umetangaza kwamba Wahariri wamem boycott Mkuchika halafu baadae ndio ukatangaza kwamba umeongea na Mkuchika. Hukuweka time frame. Kwa hiyo nishukuru mimi kwa kukupa nafasi ya kuwaelewesha waandishi na wahariri waajiri wako kwamba kumbe umempa audience/sikio Mkuchika kabla ya wenzako kukubaliana kususa.

Asante sana. Lakini mimi hao wahariri hawajaniajiri unless unaushahidi kuwa mimi ni mwajiriwa wa hao "wahariri".

Lakini hiyo ni excuse ambayo only crummy press ya Tanzania - kwa sababu ni watupu - wataikubali.
Nitakwambia kwa nini mjanja hawezi kuikubali: Kitendo cha wewe kutangaza kwamba umeongea na Mkuchika - hata kama ilikuwa ni kabla ya makubaliano ya kususa - kwa wewe kutangaza hicho kitu baada ya kujua kwamba Mkuchika hatakiwi kuongelewa tayari umeshavunja makubaliano ya msuso. Msuso wenu hautakiwi kutamka neno Mkuchika, hata kusema "niliongea na Mkuchika lakini siwaambii alichosema..." Umeshavunja msuso.

Mimi kuwaunga mkono siyo kwa sababu ni sehemu ya wahariri hao, mimi si mmoja wao. Ninawaunga mkono kutokana na uamuzi wangu mimi mwenyewe na wa KLHN na as a matter of fact nilipendekeza msimamo huo kabla ya wao kuzungumza (utaona pendekezo hilo kwenye makala yangu ya kesho ambayo iliandikwa jana (jumatatu).

Na hata nikiamua kuweka matangazo hayo ni uamuzi wangu wetu sisi kuwapa wananchi nafasi ya kusikia majadiliano (yaliyogeuka kuwa mabishano) na Mkuchika kwani mimi siyo sehemu ya Jukwaa la Wahariri. Tunawaunga mkono on principle.
Kususa kwenu ni kuvunja mkataba na jamii wa kuhabarisha kazi za Kiongozi. Ni kiapo cha fani yenu. Ni hallmark ethic ya taaluma ya uandishi.

Hakuna kiapo cha uandishi wa habari na ni hakuna mkataba wa aina hiyo isipokuwa ni suala pia la biashara na uhuru wa kufanya kazi ya uandishi. Maadili ya habari hatulazimishi kuandika habari kama dikteta anavyotaka. Kufanya hivyo kuvunja msingi wa kwanza kabisa wa hiyo fani.

Kutoandika habari za dikteta au kiongozi anayetumia madaraka yake vibaya kufungia vyombo vya habari ni uamuzi wa dhamira na ni suala la survival. How can we sing songs of redemption in the land of captivity?

Naamini ndani ya roho yangu kwamba inawezekana waandishi wa Tanzania hamjui maana ya maneno "mkataba na jamii" au "social contract."

Mkataba wa jamii hauko juu ya dhamira ya mtu. Mkataba wa jamii unahitaji pia kuoensha kuwa jamii hailazimishwi kupewa habari za uongo, za kuburuzwa au zinazoandikwa kwa woga. Na unafanya jambo hili liwe kubwa zaidi kuliko lilivyo kwani hakuna aliyekataa kuandika habari za Wizara husika bali zinasusia habari hizo kupitia Mkuchika.

Ina MAANA, kama Wizara wana habari ambazo wanataka wananchi wajue, basi wanaweza kutoa kupitia Katibu Mkuu, au Manaibu msemaji mwingine as long as siyo Mkuchika. Na kwa kufanya hiyo huo mkataba wa jamii unaendelea kuwepo na kuheshimiwa na waandishi wanaendelea kumsusia Mkuchika.

Au unataka kusema lazima habari zote za hiyo wizara zitolewe na Mkuchika ndio ziandikwe?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom