Jukwaa la Wahariri lamfungia Mkuchika; latoa ripoti ya Tarime

Na hiyo ripoti ingeathiri vipi uchaguzi wa Tarime ? Je, ni vibaya wananchi kwa ujumla wao wakijua ukweli wa mambo ? Je, hiyo ripoti ingetolewa ina maana ingesaidia CCM na Chadema haingeshinda ? Kwa hakika nashindwa kuelewa msimamo wa hili jukwaa !!

Kuhusiana na wao kuacha kutoa ripoti mimi nilishawajaji kuwa wamegeuka kuwa wanasiasa. Sikuona sababu yoyote ya wao kuihusisha ripoti yao na kampeni za uchaguzi. Niliamini kuwa waliifanya kazi yao professsionally lakini nilipomsikia Sakina akisema kuwa wameamua kuiweka kabatini rip[oti yao kwa kuhofia kujiingiza kwenye kampeni, nikabaini kuwa it was a political move
 
Kuanzia jana kutoandika habari zozote zinazomhusu Kapt. George Mkuchika kama Waziri wa Habari kwa muda wa siku tisini. Uamuzi kama huo uliwahi pia kuchukuliwa huko nyuma dhidi ya Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Omar Ramadhani Mapuri

Hiki ni kituko, ukilaza, kichekesho, na utupu usio kipimo.

Mwandishi wa habari hutakiwi na huwezi kusema unamwadhibu kiongozi kwa kutoandika habari za kazi zake!!

Hell no!!!

Kuandika habari za kazi za Kiongozi yeyote yule ni kwa manufaa ya jamii!!!

Waandisha wa habari wana kiapo cha fani, taaluma, na kazi yao, na vile vile wana mkataba na jamii kuwapasha habari zozote na zote zile za kazi za nchi!!!

Vilaza wa crummy press ya Tanzania hawajui hicho kitu, masikini weeeeee!!!

Katika eneo la uandishi wa habari, Tanzania tuko katika cesspool la vilaza wakutupwa!!!
 
Taaluma ya habari TZ iokolewe jamani, this is kituko! ina maana siku zote huwa wanaandika habari kwa wanayemtaka tu? kwa jinsi hii sio ndio maana tunaona taarifa ya TARIME kuwa hivi? na je si ndio inathibitisha kumbe wanaweza kununuliwa? kama Mkuchika akifanya kitu cha maana kuhusu jamii mnamkomoa nani? jamii au mkuchika? Kwa namna hii je JK nna EL si ndio maana waliweza kucheza na vyombo vya habari kupata uongozi wa nchi?

Kma wamesema wazi kuwa hawataandika habari za hyu mheshimiwa, tunasuspect kuna habari nyingi huwa hawaziandiki kwa sababu ya bifu na waheshimiwa na si kwa manufaa ya jamii. Kwa staili hii unaona majina ya mawaziri fulani kila siku kwenye headlines na wengine wanakaukiwa!

Je Kubenea taarifa yake ile inakubaliwa na bodi ya wahariri kuwa ilikuwa sahihi? maana haikuwa na vithibitisho ati, au ndiyo basi waonekane kuwa wanapigania haki za mwanahalisi na huku mioyoni mwao wanafurahia?

Mkuchika je hataandikwa na UHURU, RAI NA MAGAZETI MENGINE YA CHAMA NA SERIKALI?

By the way, wametoa adhabu gani kwa wahariri wa yale magazeti yaliyoandika utumbo kuhusu TARIME?

Waberoya
 
Hiki ni kituko, ukilaza, kichekesho, na utupu usio kipimo.

Mwandishi wa habari hutakiwi na huwezi kusema unamwadhibu kiongozi kwa kutoandika habari za kazi zake!!

Hell no!!!

Kuandika habari za kazi za Kiongozi yeyote yule ni kwa manufaa ya jamii!!!

Waandisha wa habari wana kiapo cha fani, taaluma, na kazi yao, na vile vile wana mkataba na jamii kuwapasha habari zozote na zote zile za kazi za nchi!!!

Vilaza wa crummy press ya Tanzania hawajui hicho kitu, masikini weeeeee!!!

Katika eneo la uandishi wa habari, Tanzania tuko katika cesspool la vilaza wakutupwa!!!

whistling... the master of extremes.... it is either too hot to handle or too cold to paddle.. !
 
a. Kuanzia jana kutoandika habari zozote zinazomhusu Kapt. George Mkuchika kama Waziri wa Habari kwa muda wa siku tisini. Uamuzi kama huo uliwahi pia kwa nguvu kutoka nyumba zao baada ya Jeshi hilo kuzichukua kwa nguvu.

Inawezekana.Nafikiri wataendelea kuandika kwamba hawatamwandika!tubandikie hayo magazeti yaliyoandika uongo Tarime.
 
Naungana na Kuhani!.
sisi kama jamii tuna haki ya kupashwa habari,ziwe nzuri au mbaya, iwapo wanadhani Mkuchika kakosea kwa uamuzi wake wa kulifungia Mwanahalisi nadhani zipo njia za kufuata ili
kupata haki, kitendo cha kumfungia Mkuchika kutoa habari zinazoendana na kazi yake ni kuwanyima haki wananchi wa Tanzania kupata habari zinazoendelea katika wizara husika, na pia naamini kwamba kuna sheria inayovibana vyombo vya habari kutokutoa/kubania habari kwa ajili kukomoa au kupendelea watu au vyombo dhidi ya wengine/vingine.

kinachoonekana hapa ni hofu ya wenye vyombo vya habari ya siku moja kuja kufanyiwa kama walivyofanyiwa Mwanahalisi, na hivyo wanaweka Kigingi mapema, hofu yao kubwa si wananchi kupata habari za kweli, ingekuwa hiyo ndo hofu yao hoja isingekuwa kumziria mkuchika bali ingekuwa kumsumbua mkuchika na serikali mpaka vitunge sheria nzuri za kudumisha na kupanua uhuru wa habari nchini
 
Habari za wakati huu.

Hatua moja kubwa ni kwenda kupigania kufutwa kwa sheria kandamizi yenye kuminya uhuru wa habari lakini jengine ni hilo la kususia kuandika habari za waziri Mkuchika maana atakachokisema chochote kisionekane katika vyombo vya habari maana wamezowea kusikika kila wakati.

Nakumbuka aliposusiwa Mapuri alikuwa mnyonge maana alitamani aondoshwe nchini sasa hilo ni pigo kubwa sana.
 
Jukwa la wahariri ni kijiwe tuu wanamtishia nyau Mhe.Mkuchika!. Liko kama kikao cha harusi cha watu fulani kutangaza kususia kufanya sherehe yao ukumbi fulani. Hili jukwaa halina any legal status wala registration ya aina yoyote. Afadhali kidogo MOAT japo haipo kisheria imesajiliwa kama kampuni.

Chombo halali chenye nguvu ya kisheria kumuadhibu Mkuchika ni Media Council of Tanzania (MCT) na Tanzania Journalist Association(TAJA) ambacho nadhani kiko ICU.
Wahariri wa Jukwaa la wahariri hawana ubavu wa kweli kumuadhibu Mkuchika ni magazeti machache tuu ndiyo yenye uwezo wa kweli haswa yale ambayo wahariri wake ni wamiliki kama Kubenea wengine hawana jeuri hiyo kwa vile wamiliki wanajikomba serikalini hiv
yo huo ndio mwanzo wa kugeukana na kusalitiana.
Mtathibitisha kauli yangu soon. Mhe. Mkuchika ni JK type, mbabe,Jeuri, hasikilizi wala hashauriki. Kumshauri JK kumuadhibu Mkuchika ni kesi ya nyani kuipeleka kwa ngedere

Pasco. Hiki chombo "Jukwaa la Wahariri" inafaa tukichambue sasa. MCT ni chombo rasmi na halali, na kifanye shughuli yake kisiache eti Jukwaa likibwata tu. Pasco unaeleza ya kweli!!
 
Bila shaka kuandikwa kwenye magazeti ya Bongo ni issue na mara nyingine inebidi ulipie ili habari za ziara yako iandikwe kwenye magazeti husika. Lakini linapokuja suala la kususia kuandika habari za katibu mwenezi wa CCM na waziri wa Habari hapo ndipo naona kuna tatizo la msingi; kwani Oktoba 31 ndio inakaribia na Mafisadi wa EPA inabidi washitakiwe. Msimamo wa CCM katika hili sijui vyombo vya habari wataupata kwa nani. Naomba wabatilishe msimamo, kwani kwa jinsi CCM ilivyo kwenye kona kwa sasa, kususia habari za Mkuchika ni kumpa nafuu Makamba, kwani madai yoyote yale kuiba kura au ufisadi atawaelekeza waandishi kwa Mkuchika sijui wataanzia wapi.
 
Naungana na Kuhani!.
sisi kama jamii tuna haki ya kupashwa habari,ziwe nzuri au mbaya,

Kwa maelezo ya serikali ukipashwa habari mbaya na ukasikia hasira, chuki, kero au uhasama ni kosa la gazeti kufanya hivyo na linafungiwa. Hivyo huna haki ya kusikia habari mbaya zinazoweza kukuudhi. Haki yako ni ile ya kusikia habari nzuri tu.

iwapo wanadhani Mkuchika kakosea kwa uamuzi wake wa kulifungia Mwanahalisi nadhani zipo njia za kufuata ilikupata haki,

Njia nyingine hazipo ukiondoa kwenda kumpigia magoti na kumuomba chonde chonde. Uamuzi wake ni wa mwisho na hakuna mahakama inayoweza kutengua. As long as amejiridhisha kuwa habari iliyoandikwa inaangukia ibara ya 31 ya Sheria ya magazeti ya 1976, then it is done.

kitendo cha kumfungia Mkuchika kutoa habari zinazoendana na kazi yake ni kuwanyima haki wananchi wa Tanzania kupata habari zinazoendelea katika wizara husika, na pia naamini kwamba kuna sheria inayovibana vyombo vya habari kutokutoa/kubania habari kwa ajili kukomoa au kupendelea watu au vyombo dhidi ya wengine/vingine.

kinachoonekana hapa ni hofu ya wenye vyombo vya habari ya siku moja kuja kufanyiwa kama walivyofanyiwa Mwanahalisi, na hivyo wanaweka Kigingi mapema, hofu yao kubwa si wananchi kupata habari za kweli, ingekuwa hiyo ndo hofu yao hoja isingekuwa kumziria mkuchika bali ingekuwa kumsumbua mkuchika na serikali mpaka vitunge sheria nzuri za kudumisha na kupanua uhuru wa habari nchini

Kilichofanywa ni uamuzi wa kuona ni kitu gani waandishi wanaweza kusema au kufanya. Well, hawawezi kwenda mahakamani, hawawezi kulaziimisha mahakama kupitia uamuzi wa Waziri. Sasa ni kitu gani ambacho wao wanaweza kuona kuwa wanatuma ujumbe kuwa hawakuridhika na uamuzi wake. Well, waandike tu kwamba hawakuridhika na Waziri awapuuzie? Waandike habari kali halafu awaone wachochezi awafungie na pia washindwe kwenda mahakamani kupinga hata hilo?

Hii haina maana ya kwamba habarii hazitaandikwa kuhusu michezo, utamaduni au wizara ya habari. Kama wana Habari wanaweza kupitia Manaibu Waziri au Katibu na habari hiyo itaandikwa. Lakini yeye Mkuchika akitaka kuitisha waandishi wa habari kuzungumza hawaendi kumsikiliza, akiwa na jambo la kusema hakuna wa kumnukuu kwa sababu kama yeye ameweza kuzima kauli ya gazeti zima na kalamu lukuki kwa stroke of a pen, basi waandishi nao kwa kuziweka kalamu zao chini hawatoandika anayosema.

Sasa hili ni suala la Waziri wa Habari Bw. George Mkuchika. Kwa maneno mengine akienda kufungua warsha hakuna atakayeripoti na kama wao wanataka iripotiwe wamtume mtu mwingine. Lengo ni kuonesha kuwa kama vyombo vya habari vingekuwa na uwezo wa kwenda mahakamani kupinga na kutengua uamuzi huo au hata kuuzuia usitekelezwe hili lisingekuwa lazima.

Sasa unapomnyima hata haki ya kukata rufaa unataka afanye nini? Desperate times, require desperate measures. Mkuchika siyo the sum of Wizara ya Habari kiasi kwamba yeye akisusiwa basi hakuna habari itakayotoka huko. Kama wizara wana habari au jambo muhimu wanao viongozi wengine akiwemo Katibu Mkuu, Manaibu Waziri na hata Idara ya Maelezo.
 
I doubt kama kumsusia huko kutamaffect in any way!By the way kwenye hilo Jukwaa la Wahariri magazeti ya Serikali nayo yamo?Kama hayapo basi habari za Mkuchika zitapeta tuu!Wakisikia amebaka mtu hawataandika?
 
Hiki kijiwe cha wahariri kinatupa somo moja kubwa kuwa ili habari yako iandikwe ( positively ) lazima uwe na unafuata/unaheshimu matakwa yao. Hii ni jinga la kitaifa walau wamejionyesha wenyewe jinsi walivyo.

Kosa (IF- Capital ) la Mkuchika adhabu kwa wananchi? wahandisi mnatupeleka wapi sasa? Huu ni ufisadi habari hicho kijiwe cha wahariri kimechemka big time!
 
I doubt kama kumsusia huko kutamaffect in any way!By the way kwenye hilo Jukwaa la Wahariri magazeti ya Serikali nayo yamo?Kama hayapo basi habari za Mkuchika zitapeta tuu!Wakisikia amebaka mtu hawataandika?

Itakuwa front page!
 
Itakuwa front page!

Jukwaa la Wahariri this time wamekosa shabaha kwa kweli!Badala wachukue hatua mbadala za kumshugulikia Mkuchika wao wanadai kumsusia!
Haya andikeni mnayotaka kuandika!
 
Jukwaa la Wahariri this time wamekosa shabaha kwa kweli!Badala wachukue hatua mbadala za kumshugulikia Mkuchika wao wanadai kumsusia!
Haya andikeni mnayotaka kuandika!

Waswahili wanasema "ukisusa wenzio wala!"
 
Jukwaa la Wahariri latoa ripoti ya Tarime

c. Habari zote zilikuwa zimeandikwa na mwandishi mmoja.

(to be updated)

MKJJ, some updating:

Kwa mujibu wa Taarifa ya Habari ya ITV, leo (14 Oktoba 2008) saa mbili usiku, Tume ya Wahariri imemtaja George Maratu, mwandishi wa kujitegemea aliyeko Tarime amabye ITV humtumia kupata habari kuwa ndiye chanzo cha hiyo habari tata, iliyoshabikiwa na kusambazwa na hayo magazeti kadhaa. Tume imeendelea kuripoti kwamba iliwahoji mashahidi kadhaa (18, au 20?) akiwemo bwana Maratu, wote kwa pamoja wamethibitisha kutokuona ushahidi wowote (silaha: mapanga nk) kama ilivyotuhumiwa. Ni Maratu pekee ndiye kariri kwamba aliona hilo.

Kamishna wa Polisi Mara naye amekana kuona ushahidi wowote ulioashiria maandalizii ya silaha na tafrani dhidi ya viongozi wa Chadema, hususan mwenyekiti wake, Freeman Mbowe.

Kuanzia sasa, ITV imesitisha kufanya kazi na George Maratu na haitamtumia tena kuipatia habari.
 
Mzee Mwanakijiji,

Mbona na wao wanamfungia bila kumpa nafasi ya kujitetea? Inaelekea hata wao hawana tofauti na huyo Mkuchika

Kila mbuzi anakula kwa urefu wa kamba yake ati.
Yeye alidhani nchi hii ni yake pekee sio? kwani kunatakiwa kujitetea gani kwenye udictator?
Wakitumia kwa uaminifu adhabu yao, nakwambia haya mambo ya kujifanya wanatamba kwa madaraka waliyonayo, yatawamaliza maana hatutawasikia tena!
 
MKJJ, some updating:

Kwa mujibu wa Taarifa ya Habari ya ITV, leo (14 Oktoba 2008) saa mbili usiku, Tume ya Wahariri imemtaja George Maratu, mwandishi wa kujitegemea aliyeko Tarime amabye ITV humtumia kupata habari kuwa ndiye chanzo cha hiyo habari tata, iliyoshabikiwa na kusambazwa na hayo magazeti kadhaa. Tume imeendelea kuripoti kwamba iliwahoji mashahidi kadhaa (18, au 20?) akiwemo bwana Maratu, wote kwa pamoja wamethibitisha kutokuona ushahidi wowote (silaha: mapanga nk) kama ilivyotuhumiwa. Ni Maratu pekee ndiye kariri kwamba aliona hilo.

Kamishna wa Polisi Mara naye amekana kuona ushahidi wowote ulioashiria maandalizii ya silaha na tafrani dhidi ya viongozi wa Chadema, hususan mwenyekiti wake, Freeman Mbowe.

Kuanzia sasa, ITV imesitisha kufanya kazi na George Maratu na haitamtumia tena kuipatia habari.

Na aliyewapa ITV ya Mtikila ni nani? Naamini hatokuwa huyu Maratu .
 
Back
Top Bottom