Kuna tatizo moja nimeligundua. Watu wanaamini kwamba ukishakuwa mtaalamu wa kitu fulani , basi hakuna la kujifunza kutoka kwa yule asiye mtaalamu. HII NI FIKRA POTOFU. Mtu anaona kwakuwa yeye ni mkali wa hiki, basi akiwa na swali au shida au changamoto anaona hawezi kuileta humu jf kwa sababu anaamini kama yeye imemshinda basi humu hakuna msaada.
MFUPA ALIOUSHINDWA FISI, MBWA HATAUWEZA.
HII NI FIKRA POTOFU PIA.
Anyone can be a hero, anyone can be a star and anyone can be a professional.
Sasa basi. Tusife na matatizo yetu! Tuyalete huku.
Na pia wale mnaoangalia post mnazipita kisa hazihusiani na simu- android,ios,bb,wp. Sasa mbadilike . TECHNOLOGY SIO SIMU PEKEE, hata blender lako la nyumbani ni tech.....