Matumizi ya juisi ya bamia yameendelea kutajwa na wadau wa tiba asilia na lishe kama njia moja wapo yenye ufanisi mkubwa katika kuongeza na kuimarisha nguvu za kiume.
Bamia, inayojulikana kwa kuwa na ute na virutubisho vingi, inadaiwa kuwa na uwezo wa kuboresha afya ya uzazi na kuongeza hamu ya tendo.
Bamia, inayojulikana kwa kuwa na ute na virutubisho vingi, inadaiwa kuwa na uwezo wa kuboresha afya ya uzazi na kuongeza hamu ya tendo.
- Tunachokijua
- Bamia ni mboga inayotumiwa na watu wengi kutokana na kuwa na virutubisho mbalimbali kama vile vitamini na madini. Hata hivyo, katika siku za hivi karibuni kumekuwa na maoni tofauti na mijadala kwenye mitandao ya kijamii kuhusu matumizi ya juisi ya bamia na faida zake katika afya ya uzazi na mwili kwa ujumla.
Madai
Kunywa juisi ya bamia kunaongeza nguvu za kiume na kuboresha afya ya uzazi kwa mwanaume.
Uhalisia
Madai haya si kweli. Ukweli ni kwamba juisi ya bamia pekee haina uwezo wa moja kwa moja wa kurekebisha au kuongeza nguvu za kiume wala kutibu matatizo ya uzazi.
Kutokana na maelezo ya Dk. Ben Kimaro, Daktari Bingwa wa Uzazi na Magonjwa ya Wanawake kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, akifafanua kuhusu uhusiano uliopo kati ya matumizi ya juisi ya bamia na nguvu za kiume au afya ya uzazi.
Upungufu wa nguvu za kiume na matatizo ya uzazi ni masuala mtambuka yanayotokana na sababu mbalimbali, ikiwemo mabadiliko ya homoni, changamoto za kushindwa kufanya tendo, au ukosefu wa uzalishwaji wa mbegu za kutosha.
Kwa sababu hiyo, kutatua changamoto hizi kunahitaji uchunguzi wa kina wa kitiba na matibabu sahihi ya kihomoni au mchanganyiko wa virutubisho maalum vilivyokusanywa kitaalamu, badala ya kutegemea juisi ya bamia pekee kama tiba.