Judith Kapinga (Mbunge CCM): Kosa la Uhujumu Uchumi limerahisishwa sana nchini ili kuwezesha kuumiza watu kisha kuwashinikiza kukubali makosa

Kwani ndicho walichopitisha? Acha kutukana wanzako; na utakufa bila kufika bungeni hata kwa ziara binafsi wacha utalii wa ndani
Watu wengine wao wako programmed kutukana tu, huyo dada ndio kwanza anaingia Bungeni kwa muhula wa kwanza.

Kwa mchango wa aina hiyo anaipa hadhi nafasi ya viti maalum, if only wote wangekuwa wanaingia kwa uwezo huo.
 
Watu wengine wao wako programmed kutukana tu, huyo dada ndio kwanza anaingia bungeni kwa muhula wa kwanza.

Kwa mchango wa aina hiyo anaipa hadhi nafasi ya vitu maalum, if only wote wangekuwa wanaingia kwa uwezo huo.
Mkuu sijui kama watakuelewa na umesema vizuri kabisa wako PROGRAMMED kiasi kwamba hata ukiwambia karibu chakula watakutukana.
 
Tulipata mapokeo ya Sheria ya uhujumu uchumi bila kuangalia mazingira yetu, sasa inatumika kupora wala mali na Uhuru wao kwa kuondoa dhamana.

Kosa la uhujumu uchumi limerahisishwa sana na nchini ili kuwezesha kuumiza watu kisha tunawashinikiza kukubali makosa.

Huyu Mbunge wenda ni akili kubwa kati ya Wabunge walio Bungeni, achana na wale kanisa la kukufua WATU, kiroho namuona ni mtu makini Sana
 
Eneo la haraka sana la Mama Samia kuliangalia ni hili la (sheria ya) uhujumu uchumi! Kati ya sheria mbovu kabisa kuwahi kutungwa ni hii!
Usisahahau na MEDIA SERVICES LAW, ile inayohusu blogs, youtube, websites na mengine ya kimtandao. Adhabu yake haipishani sana na ya uhujumu uchumi. Ndio hio ilitaka kuiondoa JF hewani, Maxence Melo kapigana nayo sana hiyo kesi. Hii sheria ni mbovu sana
 
Hata kama angekuwepo asingeweza kuyasema hayo mbele ya utawala wa Mwendazake.Na hilo umeshindwa kulitambua?
Aaah hapana mkuu ila wanasiasa wanashangaza sana, ila tusiwalaumu sana maana huenda ukiwa kwenye nafasi alonayo ukafanya afanyayo.
 
Back
Top Bottom