Judge Joseph Sinde Warioba ana hisa Celtel??

Yale yale tu, wa-Tanzania tunampa marupu rupu makubwa sana WArioba ya u-former PM, at this time tungetegemea awe anafanya kazi za kujitolea kwa taifa kwa sababu bado tunamlipia mpaka kufa kwake kila kitu katika maisha yake,

Lakini hiii tamaa isiyokwisha wala kuwa na mipaka, alyways wanting more, wanaishia mpaka kujiabisha kwa kujiepndekeza pendeka kwa mtandao na muungwana, hivi unakumbuka hotuba ya warioba kwenye TV zetu bongo baada ya uchaguzi wa rais uliopita?

Warioba alitakiwa saa hizi atoe huduma bure kama ni za sheria, au za siasa kwa taifa na hasa wananchi, hawa viongozi wetu wapunguze tamaa, kwenye hizo hisa Warioba anatafuta nini hasa kama sio greedy?
 
Mkuu FMES!

Warioba kuwa kwenye board of directors ya TTCL ni greedy kivipi? Kwani hizo kazi nyingine anazofanya kwa kujitolea...kusimamia uchaguzi wa nchi mbalimbali...Mwenyekiti wa wadhamini UWT nk.....hazionekani??
 
Quote:- Mtanzania

What about Mwananchi Gold? Warioba naye ni mjumbe kwenye projects tata nyingi tu.
 
Hili la kumsema Warioba kuwa mwakilishi wa Celtel, TTCL kwa kweli halina maana yoyote. Celtel wanamlipa Warioba ili aweze kuwawakilisha kutokana na uwezo wake kisheria na busara.

Ina maana ukichaguliwa kuwa MD wa Celtel lazima uwe na shares?? MD naye ni board member.
 
Kigoma,

Utakuwaje board director wa kampuni binafsi bila wewe kuwa na shares? Hapo corporate governance inaelekea hakuna kabisa.

Ningelewa kama angelikuwa board member akiwakilisha serikali, hapo angelikuwa analinda maslahi ya sisi sote.

Nitashangaa kweli kweli kama mtu atakuwa board member wa Celtel huku yeye mwenyewe hana kitu. Unaweza ukawa CEO au Executives wengine bila kuwa na shares lakini sio hao part time board members maana kikawaida hao wapo kulinda maslahi ya wana shares wakiwemo wao wenyewe.

MTZ!

Unaweza kuwa board member wa kampuni yeyote bila kuwa na hisa. Mara nyingi board members huwa ni eminent persons. Kama vile Dr. Salim alivyo board member wa Celtel International (Sasa Zein...kuanzia 08/01). Pia ukiangalia makampuni makubwa mengi (ya ndani na nje ya TZ) utaona board members wao ni kutoka nyanja mbalimbali na wengi ni independent wasio na hisa!
 
Wakuu hapa nadhani mnachanganya, nijuavyo ni kwamba Director kwenye kampuni yeyote lazima awe na share na lazima awe board member vilevile, lakini board member anaweza asiwe na share. Kimsingi Director anahusika na maamuzi fulani fulani katika utekelezaji na hawezi kupewa hiyo nafasi ya kuamua juu ya faranga za waliowekeza bila ya yeye kuwa amewekeza pia. Tena kutia msisitizo ni kwamba ma-Directors wanakuwa ni wale wenye share nene, yaani faranga mingi. Hayo ni yale niyajuayo mimi.
 
Akilimtindi,

Sio kweli, ni kwamba kwenye board kuna members wa aina mbili, executive directors na non-executive directors. Inategemea na kampuni husika inafuta vipi corporate governance rules za sehemu husika. Lakini ukifuata Anglo-American model basi inatakiwa non-executive directors wawe wengi kuliko hao wengine.

Executive directors ndio wanaongoza kampuni na ni kama CEO, CFO nk. Kwa kufuata Anglo-Americal model ni kawaida kwenye remuneration package yao kuwa pamoja na shares. Lengo hapa ni kuhakikisha kwamba hawafanyi maamuzi ya muda mfupi ambayo yatawapata wapate kwa mfano bonuses lakini mbele shares zikanguka.

Non-directors hawa wanaohudhuria vikao tu na kwa mfano wa hapa ni kama Warioba au Salim. Hili kundi huwakilisha maslahi ya shareholders, mara nyingi wanakuwa na shares au wanatumwa na tajiri mwenye shares.

Nitashangaa sana kama Warioba hana shares Celtel, inawezekana lakini nasema nitashangaa sana. Lengo la kuhakikisha board members wana shares ni kuhakikisha hawachukui maamuzi ambayo yanaweza kuwaletea faida wao na kuleta hasara kwa share holders wengi.

Kuna pia Non Anglo-American Model ambayo ni maarufu Ufaransa, Germany na Japan. Hii inaweka nguvu kwenye makundi ya wafanyakazi, vyama vya kitaaluma nk. Hapa mara nyingi board member anaweza asiwe na interest kwenye kampuni. Hii model inakufa sasa taratibu shauri ya globalisation. Wamarekani na mabepari wengine wameanza kuwa na shares kubwa kwenye mashirika mbalimbali ya dunia na kitu cha kwanza wanachotaka ni kulinda maslahi ya shareholders zaidi, hivyo kufuata Anglo-American model.

Narudia nitashangaa sana kama Warioba hana shares Celtel.
 
Wakuu,

Nina swali,Je Jaji warioba ana hisa katika Kampuni ya Celtel?there is a story i have here mpaka naoanza kuogopa.Inasemekana alikuwa ni mmoja wa watu wa kwanza kuwa wajumbe wa bodi wa kampuni ya celtel na ninajaribu kujua alikuwa akiwakilisha serikali au na yeye ni mwana hisa.

Ukikumbuka kampuni ya Celtel haikuwahi kutumia pesa yake kwaunzisha kampuni hiyo ambayo hivi karibuni itabadili jina na kuitwa zein.Mie nataka kujua kuhusu hili.

conecting to the dot...

Mimi nina majibu uyatakayo lakini siwezi kukupa. Tafadhali nakuomba badilisha picha yako kwani nikimuona Mkapa ninasikia kutapika na kizunguzungu.
 
Yale yale tu, wa-Tanzania tunampa marupu rupu makubwa sana WArioba ya u-former PM, at this time tungetegemea awe anafanya kazi za kujitolea kwa taifa kwa sababu bado tunamlipia mpaka kufa kwake kila kitu katika maisha yake,

Lakini hiii tamaa isiyokwisha wala kuwa na mipaka, alyways wanting more, wanaishia mpaka kujiabisha kwa kujiepndekeza pendeka kwa mtandao na muungwana, hivi unakumbuka hotuba ya warioba kwenye TV zetu bongo baada ya uchaguzi wa rais uliopita?

Warioba alitakiwa saa hizi atoe huduma bure kama ni za sheria, au za siasa kwa taifa na hasa wananchi, hawa viongozi wetu wapunguze tamaa, kwenye hizo hisa Warioba anatafuta nini hasa kama sio greedy?

Umemsahau Mzee Malecela ambaye bado ni MBUNGE pamoja na kuwahi kuwa PM na VP?
 
Mimi nina majibu uyatakayo lakini siwezi kukupa. Tafadhali nakuomba badilisha picha yako kwani nikimuona Mkapa ninasikia kutapika na kizunguzungu.
Mkuu kidatu,

Hiyo ni Picha Ya Mzee Mkapa kabla ya kuwa Rais,Ndiyo Sura ambayo MWalimu alizoea,ndoyo ya yule Mkapa Muadilifu.

Majibu uliyonayo ni mzuri na kwanini unawaficha watanzania Wenzako?Mie nafahamu kidogo ila nakusanya ili yaweze kujaa na kutimia kabla ya kumshauri huyu Mzee.Kama alivyomsema Mzee FMES ni kuwa hawa wanatakiwa wafanye kazi za kushauri tu
 
Hivi kweli anaweza kuwa BOD member bila kuwa na hisa huku akijua kuwa tangu kuzaliwa kwa celtel ni kashfa tupu? Sielewi hapa!
 
Hivi kweli anaweza kuwa BOD member bila kuwa na hisa huku akijua kuwa tangu kuzaliwa kwa celtel ni kashfa tupu? Sielewi hapa!

Hilo tutalijua baadaye,

ila kama kweli alihusika wakati TTCL inapewa watu wachache na yeye alikuwa mmoja ya waliotoa maamuzi ya mkataba huo,unategemea kweli uwezo wake wa kisheria ulisaidia?

Au ni kusema kwamba hakushirikishwa jambo lolote?Au Alilinda maslahi ya mtu flani?Je ni kwanini aliamua kulinda maslahi hayo..?

Hapa ukiendelea kuzunguka utagundua kwamba hakuna mtu mwadilifu katika serikali yetu na hata wale waliokuwa wastaafu..Ibara ya 13 ndiyo imekuwa msingi wa kutusababisha siye tuwe hapa.
 
Finca...kuna kiongozi mzito ana hisa pale
Baypot....Mama ana Mkapa..

kwanini kila sehemu viongozi wetu wapo??

ukiona kitu chochote kizuri hapa nchini ujue hawa watu wamecover up.. gorofa nzuri, hotel nzuri, kilakitu wapo mpaka wenye mabendi ya dansi hawa watu ni walafi wasioridhika na nihatari wameshika kila kona
 
Jamani lakini tukumbuke kuwa hatutaki kurudi kwenye ujamaa. Tatizo lilipo hapa ni kuwa huria iswe holelana viongozi wetu waache ufisadi wakiwa na hisa kwa njjia halali kuna ubaya gani?
 
Quote:- Mtanzania

What about Mwananchi Gold? Warioba naye ni mjumbe kwenye projects tata nyingi tu.

Mkuu sasa naona unataka kututega najua kama unafahamu kuwa hili ni tatizo la kisera, Watendaji serikalini wanakuwa wakiritimba sana na wanaweka sera comparable to Developed World wakati infact ni second poorest in the World
bila sababu yeyote
The only way out is to use political or executive influence to avoid those imoral obstacles.
Nikikukumbusha madaladala yote wanaseme ni ya viongozi wakubwa na mapolisi hilo lengo lake ni kuavoid kukumatwa kirejareja na askari wadogo
Hata wewe leo ukiwa na issue kubwa mshike Ridhiwani uone nani atakae zuia
au fanya mwenyewe uone watakukwamisha na upoteze pesa yako yote.
Ikiwezekana wakutie na kashfa
 
Kuwa na hisa si kitu kibaya lakini ni kiasi gani? unaweza kuwa na hisa za laki moja au hisa za milioni mia mbili hivyo bila kuwa na kiwango inapotosha ukweli!!
 
Hivi Celtel ilianza lini? najua ya kwanza ilikuwa MOBITEL: Je Celtel ndiyo ile iliyoletwa na wamalasyia? Niliwahi kusikia kuwa ilifungwa.
 
Hivi Celtel ilianza lini? najua ya kwanza ilikuwa MOBITEL: Je Celtel ndiyo ile iliyoletwa na wamalasyia? Niliwahi kusikia kuwa ilifungwa.

Ndugu inaonekana uliondoka zamani sana Tanzania. To my knowledge Celtel haina uhusiano wowote na Mobitel, ni ya waarabu ambao wanasadikiwa kuwa na uhusiano na al qaeda lakini wanafanya kazi nzuri ya kuboresha cellphone communication hapa TZ. JF members wengine wanafahamu mengi zaidi kuhusu Celtel
 
Wakuu,

Nina swali,Je Jaji warioba ana hisa katika Kampuni ya Celtel?there is a story i have here mpaka naoanza kuogopa.Inasemekana alikuwa ni mmoja wa watu wa kwanza kuwa wajumbe wa bodi wa kampuni ya celtel na ninajaribu kujua alikuwa akiwakilisha serikali au na yeye ni mwana hisa.

Ukikumbuka kampuni ya Celtel haikuwahi kutumia pesa yake kwaunzisha kampuni hiyo ambayo hivi karibuni itabadili jina na kuitwa zein.Mie nataka kujua kuhusu hili.

conecting to the dot...
 
Ndo maana Rugemalila anataka kumtaja mwizi jaji anasema aandike barua ya maombi kupitia kwa wakili wake. Yaani maombi ya kumtaja mwizi hapo unaweza kukubaliwa au kukataliwa. Polisi wakishika jambazi wanaliminya pu,,,mb litaje majambazi wenzake sasa Ruge anaomba kutaja mwizi!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom