Judge Joseph Sinde Warioba ana hisa Celtel??

Kigoma asante kwa habari ulizotupa,kumbe ni member wa bodi ya TTCL pia?

so far yeye ni au alikuwa

1.Mjumbe wa Mwananchi Gold Minning
2.Mjumbe wa TTCL akiwakilisha Celtel ina maana ana hisa TTCL(kwa upeo wangu ninahisi kuna fact hapa)

Swali ambalo nitaka kujua ambalo ninahisi kumekuwa na uzugujai mkubwa sana kwa watanzania,Je ni nani alikuwa Mwenyekiti wa ile Tume ya Rushwa aliyounda Mkapa?
Ohoooo-oh! watasema unataka kufanya hewa iwe kama ya maliwatoni!
 
A man will be as honest as he is required to be. Hata mtu muadilifu mwenye nyumba Dar, ukimwambia kuna malipo mazuri ya kisheria kupanga nyumba Dar bila hata kumuuliza kama anahitaji nyumba Dar, unamkwaza.

Wewe unayempa hiyo offer unamuweka katika mtihani unaomtaka awe kama malaika wakati yeye ni mtu tu.

Tunapopiga vita rushwa, tuweke mifumo inayolazimisha watu kutochukua rushwa. Si mifumo inayolazimisha watu wachukue rushwa, halafu tutegemee watu wakatae rushwa.

Al watan upo sahihi sana lakin nadhan hukuelewa Msingi wa comment yangu!,

najaribu ku assess uadilifu wa Mtu Mmoja Mmoja sio wa Mfumo , inajulikana kabisa Mfumo wetu ni corrupt Sasa tunakuja to what extent individuals can abstain them selves from corruptions and embezzlement!
Mf. Wewe unakaa kwa Kaka yako au Ndugu yako na huna Mke wala demu lakin Kaka yako kasafiri Halafu Shemeji yako anajilengesha kwako hapo tutapima uadilifu wako wa kujizuia kwako kupiga bila ya kuhoji Kwanini Kaka yako kakuacha na Shemeji yako akijua huna Mke na Una mahitaji ya kimwili au kuhoji Kwanini Shemeji kajilengesha!

uadilifu ni pamoja na kujizuia na pato haramu bila ya kuangalia mahitaji binafsi Kwa hiyo kuchukua Malipo ya pango kwa style niliyo taja ni ukosefu wa uadilifu bila ya kujali dhamira ya mtoaji
 
Hii ilianza kama celtel, ikaja ikawa zain na sasa inayoitwa Airtel, tuamnasubiri jina lijalo litakuwa lipi hahaha
 
Ndo maana Rugemalila anataka kumtaja mwizi jaji anasema aandike barua ya maombi kupitia kwa wakili wake. Yaani maombi ya kumtaja mwizi hapo unaweza kukubaliwa au kukataliwa. Polisi wakishika jambazi wanaliminya pu,,,mb litaje majambazi wenzake sasa Ruge anaomba kutaja mwizi!
Nimwmecheka kwa sauti mpaka watu wanashangaa, yaani mtu anataka kumtaja mwizi anaambiwa aandike barua, watia majambazi wanalazimishwa
 
Halafu kwenye hotuba zao utawasikia. Naanza kwa kutanguliza shukran zangu za dhati kwa Mwenyezi Mungu mwingi rahema... Huku kea siku una lamba million 400, unalipwa Na kutunzwa Hadi kufa Na hell ya walipa Kodi. Wengine Hadi migodi wajigawia. Wengine Hadi nyumba za serikali wameonga halafu wanaona poa tu Hadi rambirambi wamepiga isitoshe bill mshipa wa aibu wanajenga international airport kijijini kwao. Tukipaza sauti kuhoji tunaitwa malofa nakusswekwa kwenye salfet cocobeach.

The problem Karma takes too long
Pole mkuu naona umeongea kwa uchungu sana.
 
Kwa jinsi watanzania tulivyo sitashangaa kabisa kusikia warioba anahusika kwenye mascandal mengi mengi tu.

Tunahangaika sana kutafuta mchawi wetu lakii mchawi Mkubwa ni matumbo yetu tu
 
Kwa jinsi watanzania tulivyo sitashangaa kabisa kusikia warioba anahusika kwenye mascandal mengi mengi tu.

Tunahangaika sana kutafuta mchawi wetu lakii mchawi Mkubwa ni matumbo yetu tu
Warioba..shujaa wa katiba mpya
 
Al watan upo sahihi sana lakin nadhan hukuelewa Msingi wa comment yangu!,

najaribu ku assess uadilifu wa Mtu Mmoja Mmoja sio wa Mfumo , inajulikana kabisa Mfumo wetu ni corrupt Sasa tunakuja to what extent individuals can abstain them selves from corruptions and embezzlement!
Mf. Wewe unakaa kwa Kaka yako au Ndugu yako na huna Mke wala demu lakin Kaka yako kasafiri Halafu Shemeji yako anajilengesha kwako hapo tutapima uadilifu wako wa kujizuia kwako kupiga bila ya kuhoji Kwanini Kaka yako kakuacha na Shemeji yako akijua huna Mke na Una mahitaji ya kimwili au kuhoji Kwanini Shemeji kajilengesha!

uadilifu ni pamoja na kujizuia na pato haramu bila ya kuangalia mahitaji binafsi Kwa hiyo kuchukua Malipo ya pango kwa style niliyo taja ni ukosefu wa uadilifu bila ya kujali dhamira ya mtoaji
Kuongelea mtu mmojani sawa. Huwezikuwana nyumba ya matofalibilakuwa na tofali moja.

Lakini pia, huwezi kuwa na nyumba ya matofali kama huna simenti ya kuyaunganisha matofali mengi tofauti yawe kuta zinazojenga nyumba.

Mtu mmoja ni kama tofali moja, mfumo mzima ni kama kuta, nondo simenti etc.

Katika somo la jurisprudence, upande wa falsafa ya sheria katika utoaji wa hukumu, ili kumhukumumtu kwa haki inabidi uangaliemazingira mazima ya jinsi kosa lilivyofanyika.

Ndiyo maana mtu anayemuua mgoni wake bila kupanga, kwa kumshtukizia tu (in the heat of the moment), anafikiriwa tofauti na mtu aliyepanga kuua kwa muda mrefu (pre-meditated murder).

Na hapo ndipo point yangu inavyokuja.

Mtu atakayeomba rushwa wazi wazi katika mfumo ambao unakataza rushwa zote na bahashishi, anakuwa amefanya kosa kubwa zaidi ya mtu aliyechukua rushwa kwa sababu mfumo umemlazimisha kuchukua rushwa kwa sababu hiyo rushwa imehalalishwa na kila mtu anaichukua na yeye asipoichukua ndiye ataonekana anafanya makosa.

Naona ni sawa kumlaumu mtu aliyeomba rushwa katika mfumo unaokataza rushwa, napata tabu sana kumlaumu mtu aliyeshindwa kukataa rushwa katika mfumo ambao umehalalisha rushwa kisheria.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom