Jua lile literemke mama! Maisha ni mapambano hakuna budi kuingia vitani.

Status
Not open for further replies.

passion_amo1

JF-Expert Member
Dec 3, 2023
1,578
3,148
Wakuu habari za uzima?

Jua lile literemke mama ni moja ya nyimbo wengi wetu tuliokuwa tukiimba pindi tupo mchakamchaka shule. Hii nyimbo ilikuwa inatupa nguvu na hali mpya siku nyingine inapoanza.

Leo nita share na nyinyi stori ya kaka yangu ni mtoto wa baba mkubwa Na kanizidi umri.
Stori hii ni kwa ajili ya kujifunza na kuongeza hali baina yetu vijana tuendelee kupambana.

Stori yake nataka nianzie akiwa form six.bro alichukua masomo ya economics, sasa kipindi yupo advance ni type ya wale wanafunzi ambao hawaogopi ku question walimu na hata viongozi.
sasa baada ya kupishana na mwalimu wake sababu ya kuhoji kwake akapewa suspension na uongozi wa shule na kipindi hicho walikuwa wanakaribia maandalizi ya mitihani ya form six.


Baada ya kurudi akaanza kutafuta tution na kujisomea, sasa kipindi anaenda tution huko akiwa yupo nje ya shule akakutana na manzi(msichana) wa kinyaturu yeye alikuwa yupo shule za kwenda na kurudi. basi siku zikaenda wakazoeana wakaingia kwenye mahusiano.

suspension aliyopewa ikaisha ikabidi arudi ila akiwa na mzazi, hakumwambia mtu yoyote akarudi shule peke yake, mwalimu mkuu na mwalimu wa nidhamu wakamwambia mbona upo peke yako?akawajibu mama yangu ni mgonjwa baba kasema hawezi kuja.mkuu akasema hii ni kwa ajili ya maisha yako rudi kamlete mzazi.


Bro akarudi lakini alivyorudi hakurudi nyumbani tena akaenda kwa uncle yake. Basi akamwambia uncle wamenirudisha ila mimi nataka sasahiv nirudi three weeks kabla ya pepa. Uncle akaongea pale lakini hakumsikia . Ikabidi atafute mtu apge simu shule awaambie kwamba yeye kalazwa na anaumwa.basi jamaa alijitambulisha kama mjomba ikabidi walimu waitike sababu bro walishamchoka kwa tabia.



Siku zikaenda akiwa anaendelea mahusiano na mtoto wa kinyaturu (ni pisi haswa). Basi wiki tatu kabla ya mtihani alirudi shule akiwa na uncle akiwa na document za hosptal kwamba alikuwa anaumwa ila zilitengenezwa tu. sasa kuna mwalimu wake wa jiografia alikuwa anapingana nae sana. Wapo siku za mwisho wanafanya review ticha akaingia akamwambia Ricky(code sababu anampenda Ricky gervais (american comedian), ticha akasema wewe kama ukifaulu sijui😂. Ricky akasema ticha ikitokea mtihani huu watafaulu watu watatu tanzania mimi nitakuwa kwenye hio tatu bora na nitarudi hapa nikuletee zawadi ya mkanda( walikuwa wanamtania ticha huyo sababu hajawahi badilisha mkanda)

inaendelea hapa chini👇.
 
Basi bro baada ya kumwambia vile ticha, darasa zima likacheka ikabidi ticha amuite atoke nae akampeleka ofisini akamchapa sababu amemzalilisha mbele ya darasa. Baada ya hapo akarudi zake, siku zikasogea asubuhi ikawa mchana, mchana ikawa usiku hatimaye mtihani ukafika.

Wakafanya pepa, akamaliza salama akarudi mtaani. kipindi hicho yule mchumba aliyekuwa naye wakawa wamepoteza mawasiliano, picha linaanza akagoma kwenda jeshi akaanza kutafuta connection akawa yupo kwa wachina kariakoo anahesabu mizigo inayotoka na kuingia kwenye mastore, na kusambaza mizigo.
Basi siku zikaenda akakaribia kwenda chuo maana alifaulu kwa division 2 kitu ambacho hata walimu hawakutegeme. Anarudi home hiyo siku anamkuta mchumba akiwa na wazazi wake nyumbani😂. Akapiga jicho akamuona mchumba ana kitumbo ni ya wiki kadhaa tu kujifungua. Basi ikabidi aitwe akae pale chini wazazi waongee. Akaulizwa unamfahamu binti huyu? Akajibu ndio, unamfahamu vipi? Mpenzi wangu , baba yake akainuka akampga bonge la ngumi😂(baba mkubwa). A long story short wazazi wakasema basi ngoja tujadiliane na kijana wetu halafu sisi kama wazazi tuone tunamaliza vipi hili suala.

Wale wazazi wakaondoka mzee alikuwa amekasirika sana sababu process zote za chuo alikamilisha, akamwambia ushakua baba sasa haya hongera. Ni wale wazee ambao wanamini sana katika elimu kwahyo alikuwa disappointed sana.
Basi vyuo vilivyofunguliwa tu akakata mawasiliano kabisa kwenda home akihofia msala wa mchumba anaweza kuja. Wazazi wakawa wanaulizia lakini upande wa mwanaume wazazi wakawa wanasema mtoto wao kabadilisha laini na chuo hajaenda. Kumbe mama kaamua kumficha mwanae. Jamaa alivyoanza chuo mzee akawa anamtumia vipesa lakini mahitaji yakawa makubwa ikabidi amtafute mshkaji wake maana kipindi anatoka kwa wachina kule alimuunganisha mshkaji wake. Baada ya kumtafuta jamaa akasema kwamba sasahiv kashaama pale yupo sehemu nyingine akiwa katika kufikkri atafanya nini. Ikabidi bro arudi ghetto alipopanga. sasa kipindi anarudi mbaya zaidi akamkuta mchumba akiwa na jamaa yake wa mtaani wapo pale nje.
Huku jamaa kamwambia pale kwa mchina hayupo huku anarudi anamkuta mchumba yupo nje ya ghetto lake na mshkaji wake wa mtaani.


Inaendelea hapa chini👇
 
Bro baada ya kufika pale kwanza ikabidi amuangalie mshkaji wake( yale macho unamwambia mtu umefanya nini?) mshkaji alijua tu kinachofata hapa ni lawana za kutosha. Ikabidi afungue ghetto akamwambia demu aingie ndani, demu akanyanyuka akaingia akatoka nje aongee na mshkaji. Wakatoka mbali kidogo na pale.

Mshkaji ikabidi aanze kumuelezea demu kwao kabanwa kaambiwa aje kukutafuta, mimi demu huyu sijaongozana nae alikuja rafiki yake akasema anashida na wewe na mimi kuangalia nikaona pisi nikajua yako. Lakini nafika hapa kwako baada ya kumuonyesha nikamuona anaongea na simu ndo akaja demu wako huyo.
Akasema nishaumia umekosea sana.


Maana huyu mshkaji alikuwa anpafahamu kwa bro. Basi ikabidi akubaliane na hali akaongea na mshkaji wake ikabidi amuache. Akarudi kwa demu ndani, demu akaanza kujieleza home sasahiv hapakaliki baba kawa mkali sana na sijui nifanye nini. Bro akauliza mtoto? akamwambia yupo home akazidi kupagawa.

Akamwambia hali yake halisi pale, demu akasema basi twende hata nyumbani ujitambulishe na uwaambie upo tayari kumlea mtoto. Ikabidi aumize kichwa anafanya nini. Akamtafuta uncle wake yule aliyekaa kwake kipindi yupo form six. Uncle akawa yupo busy na haeleweki.nyumbani mzee aeleweki demu kashaletwa mpaka ghetto.


Ikabidi amatafute rafiki yake wa chuo amuazime pesa. Akamwambia demu wewe nenda mimi nitakuja. Mchumba akamuelewa kishingo upande, ile pesa aliyomuazima rafiki yake ilikua 150,000 akamshirikisha mshkaji wake anataka a stop nakumbuka hapo ndio mwaka wa kwanza. Anataka kuandika barua. Ikabidi aandike barua akarudi mtaani kuanza kuhangaika na wazazi hawafahamu chochote hapo.

Baada ya kurudi kariakoo kupambana sanA, akaanza kupata connection anawauzia wateja wa mikoani magwanji anayopiga basi akawa anasogeza siku hivyo hivyo.

Akampgia mama yake mzazi simu akamwambia mama naomba nije tuongee. Akaenda home mama anamshangaa kapungua sana ikabidi amfiche tu kwamba masomo magumu.
Akamueleza mama anashida kama ya milion2 tu nahitaji kufanya biashara. Akasema utaweza na chuo na baba yako ashakua mkali sana sikuhizi.

Akasema nitaweza mama wewe nisaidie hiyo pesa. Ikabidi mama yake ampe milion1 ya kukopa baada ya milion2 aliyoomba.

Akarudi chuo, alipopanga akamtafuta uncle wake tena ili aende kule ukweni akaweke mambo sawa, uncle akapatikana akampanga wakaenda mpaka kwa wazazi pale uncle akaongea wakasema yupo tayari kulea mtoto na Akikaa sawa atakuja na kuoa.

Akaacha laki3 pale ukweni. Akarudi kariakoo kupambana kwenye mastore ya wachina,baada ya Kama mwezi akampgia mchumba akamwambia njoo ghetto na mtoto wangu, aksasema kuhusu wazazi akasema wewe njoo.
Mchumba akaaga akasema anampeleka mtoto kwa baba yake maana alikuwa ashajitambulisha na anatoa matumizi wazazi wakamruhusu.

inaendelea chini👇
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom