Jua haki yako unapokamatwa na Polisi

Hivi muandishi wa hiki kifungu amedhamiria kuandika kilichoandikwa ama la?

Kimsingi amesema mtu asikamatwe au kupekuliwa na polisi baada ya saa 12.30 jioni na kabla ya saa 12.30 alfajiri ila tu pale kutakapokuwa na ushahidi wa kutosha kwamba kumpekua au kumkamata baada ya saa 12.30 jioni na kabla ya saa 12.30 alfajiri kunaweza kuleta madhara.

Kwa hiyo asipekuliwe wala kukamatwa katika muda huo mpaka pale kutakapokuwa na ushahidi kwamba kutakuwa na madhara, tunatafuta madhara kwa nguvu, nani kaandika utumbo huu?
Inawezekana kifungu hakina makosa, labda aliyeandika hapa kwenye jukwaa ndiye aliyekosea transcription...yale yale ya "kafa Manzese mazishi Sinza, mchicha mbichi mpishi mbishi!", unapoyatamka, ni rahisi kuchanganya ulimi kama hauko well composed.
 
Hao polisi wa marekani siyo tanzania kwanza kabla ya swali kofi
When we are talking about rights simply means the basic and necessary criterion that should be provided or considered during undertaking any legal activities. So it have to be obeyed and being obligatory the problem is, majority of Tanzania are feel inferior when aimed to proceeds for their rights .......
 
USINYANYASWE WE NDUGU FANYA HAYA UWAPO MIKONONI MWA POLISI
liftarn_Police_brutality.png

IMEANDALIWA NA MAWAKILI WETU
( 1 )Askari akikuweka chini ya ulinzi muulize kitambulisho ni haki yako.
( 2 )Askari akikukamata akuoneshe kitambulisho chenye muhuri wa mahakama kama anasema ametumwa na mahakama kukumata, ni haki yako.
( 3 )Askari akikukamata akwambie kwanini anakukamata na anakupeleka kituo gani, ni haki yako.
( 4 )Unaruhusiwa na sheria kukataa kukamatwa hata kutumia nguvu kama hukuambiwa sababu ya kukamatwa.
( 5 ) Askari anapokiuka taratibu za ukamataji anageuka na kuwa mhalifu ni haki yako kujikinga naye.
( 6 )Askari haruhusiwi kukuvuta shati, kukukaba koo, kukushika suruali kama hujakataa kutii amri halali.
( 7 )Askari haruhusiwi kuondoka na mtu mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa halisi.
( 8 ) Askari haruhusiwi kupekua nyumba ya mtu bila kibali cha kupekua.
( 9 )Askari lazima akuoneshe kibali cha kupekua na ukisome.
( 10 )Kibali kieleze jina la aliyekitoa, kituo kilipotolewa,jina la mtu au sehemu ya upekuzi, au uchanganuzi wa mtu au sehemu.
( 11 )Hairuhusiwi kupekuliwa usiku kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 12 asubuhi.
( 12 )Ni haki yako kumpekua askari kabla hajakupekua ili asipandikize kitu.
( 13 )Usipekuliwa nyumbani bila kuwapo kiongozi wa mtaa.
( 14 )Kila kitakachochukuliwa katika upekuzi lazima kiandikwe na askari aweke sahihi.
( 15 ) Mali iliyochukuliwa katika upekuzi lazima ibaki salama.
( 16 )Mwanaume haruhisiwi kumpekua mwanamke na mwamke haruhisiwi kwa mwanaume.
( 17 )Unaruhusiwa kukataa kupekuliwa iwapo taratibu hizi hazikufuatwa.
( 18 )Askari haruhusiwi kukutukana wala kukupiga.
( 19 ) Unaruhusiwa kutozungumza lolote mpaka unayemuamini afike uwapo chini ya ulinzi, ni haki yako.
( 20 )Usilazimishwe kuongea au kuandika ambacho hutaki, ni haki yako.
( 21 )Usitoe maelezo bila uhakika yatatumika mahakamani yatakuletea shida.
( 22 )Unaruhusiwa kukaa kimya na usizungumze kitu uwapo chini ya ulinzi.

HIZI ZOTE NI HAKI ZAKO, ZILAZIMISHE USIBEMBELEZE WALA USIZIOMBE.

Kutoka: Sheria Yakub Blog: USINYANYASWE NDUGU

yaani askari wa bongo kile kitendo cha kumwambia naomba kitambulisho ushakula virungu kadhaa
 
embu kwanza kamatwa na askari wetu hawa alafu ufanye hivyo unavyodai wewe uone kama utakuwa salama???
fanya hivyo alafu uone kama utaweza kushika hiyo keybody yako ulete mrejesho hapa..!!!
 
embu kwanza kamatwa na askari wetu hawa alafu ufanye hivyo unavyodai wewe uone kama utakuwa salama???
fanya hibyo alafu uone kama utaweza kushika hiyo keybody yako ulwte mrejesho hapa..!!!
yaani wakikudandia bora uwe mpole tu, hawaoni hasara kukuwekea vipisi vya bangi ukijifanya kufuata sheria
 
Hivyo ndivyo inavyotakiwa kuwa. Tatizo lipo sehemu tofauti,

1.Raia wenyewe kutokujua hizi haki zetu, na uwoga ukimwona anakuja tu hofu juu.
2. Polisi wenyewe kwa kujiona wapojuu ya sheria

3. Polisi kwa kuona kwamba raia wengi hawatambui haki zao na uwoga wao, nao wanasimamia hapo.

Mengine ongezeni wadau.......
 
Kama waliweza kuzuia msafara wa viongozi wakuu wa upinzani kwenda kumzika Mzee Kisumo...Na hakuna sheria inayosema hivyo na kwenye huo msafara palikuwa na Manguli kama Lowasa, Ndesa pesa na wengine na wote wakakubali yaishe...Sembuse wewe raia wa kawaida hakika watakuua tu na hakuna kesi....Askari wengi hufanya kazi bila weledi ama kwa kufuata order..Wacha uonekane muoga uwe salama .
 
Shukurani nyingi kwa wote mlioandaa hii elimu,
Elimu yenu imekuwa faida kwa jamii nzima. Mungu awabariki zaidi.
 
Naombeni msaada wataalam wa sheria,
Je natakiwa nifanye nini ninapokamatwa na trafiki polisi,
au yeye polisi anatakiwa afuate utaratibu gani pindi anapotaka kukagua gari / anapokuta kosa lolote kwenye gari? au chombo chochote cha moto kitumikacho barabarani.
Nami kama raia wajibu wangu ni upi pindi ninapokutwa na kosa lolote lile.
Ntashukuru kama ntaelekezwa hatua kwa hatua kama mlivyoelezea hapo kwenye kukamatwa na kukaguliwa na polisi nyumbani.
 
Shukurani nyingi kwa wote mlioandaa hii elimu,
Elimu yenu imekuwa faida kwa jamii nzima. Mungu awabariki zaidi.

Ni elimu nzuri, lakini kwa wenzetu si hapa, jeshi linaendeshwa kwa mihemko ya kisiasa, husuda ,na visasi kati ya raia na askari.
Hakuna nidhamu ya kazi.
 
n
Ni elimu nzuri, lakini kwa wenzetu si hapa, jeshi linaendeshwa kwa mihemko ya kisiasa, husuda ,na visasi kati ya raia na askari.
Hakuna nidhamu ya kazi.

Ni kweli hakuna nidhamu ya kazi kwa hao polisi , ila angalau inasaidia kuwa na ufahamu wa haki zako na nini unapashwa kufanya, tofauti na usipofahamu kabisa.
 
Kama waliweza kuzuia msafara wa viongozi wakuu wa upinzani kwenda kumzika Mzee Kisumo...Na hakuna sheria inayosema hivyo na kwenye huo msafara palikuwa na Manguli kama Lowasa, Ndesa pesa na wengine na wote wakakubali yaishe...Sembuse wewe raia wa kawaida hakika watakuua tu na hakuna kesi....Askari wengi hufanya kazi bila weledi ama kwa kufuata order..Wacha uonekane muoga uwe salama .
Mkuu hata polisi wenyewe sidhani kama wanazifahamu hizi taratibu.
 
Mkuu hata polisi wenyewe sidhani kama wanazifahamu hizi taratibu.
Mkuu naamini wanazifahamu sana ila unajua kule hufanya kazi kwa order wakiamini wako ya sheria sitaki kusema sana ila kumbuka yule mwandishi wa habari aliemiminiwa risasi akageuzwa butcher...Unadhani ni bahati mbaya tu ilitokea ile?
 
Naombeni msaada wataalam wa sheria,
Je natakiwa nifanye nini ninapokamatwa na trafiki polisi,
au yeye polisi anatakiwa afuate utaratibu gani pindi anapotaka kukagua gari / anapokuta kosa lolote kwenye gari? au chombo chochote cha moto kitumikacho barabarani.
Nami kama raia wajibu wangu ni upi pindi ninapokutwa na kosa lolote lile.
Ntashukuru kama ntaelekezwa hatua kwa hatua kama mlivyoelezea hapo kwenye kukamatwa na kukaguliwa na polisi nyumbani.
Mkuu, hata mimi nina utata na taratibu za hawa jamaa wa barabarani, naongezea swali, je ni haki yangu kutompa traffic police anapoiomba/ ihitaji leseni yangu, je nikimuonyesha tu bila kumpa aishike nitakuwa nimetenda kosa?
 
Mkuu, hata mimi nina utata na taratibu za hawa jamaa wa barabarani, naongezea swali, je ni haki yangu kutompa traffic police anapoiomba/ ihitaji, je nikimuonyesha tu bila kumpa aishike nitakuwa nimetenda kosa?

Natamani kweli kupata majibu ya haya maswali yote , ksb polisi wa barabarani ni kero mno.
Nikipata maswali ya majibu haya ntahakikisha nayaprint na kuyaweka kwenye wallet yangu. Nikikamatwa tu nayapitia ili niende sawa na hawa polisi.
 
Back
Top Bottom