Jua haki yako unapokamatwa na Polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jua haki yako unapokamatwa na Polisi

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Bikra, Jun 2, 2009.

 1. Bikra

  Bikra Senior Member

  #1
  Jun 2, 2009
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 103
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  • Raia ana haki ya kumwomba askari ajitambulishe kwako.
   • Mwulize jina lake
   • Mwulize namba yake ya uaskari
  • Raia ana haki ya kujulishwa kwanini anatiliwa mashaka ama kukamatwa.
  • Raia ana haki ya kuwajulisha ndugu, jamaa ama sehemu anakofanyia kazi kwamba ama amekamatwa na polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
  • Raia ana haki ya kuomba na kupewa dhamana wakati akiwa kituo cha polisi ama Taasisi ya kuzuia rushwa.
   • Hutakiwi kutoa fedha kama dhamana uwapo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa, isipokuwa maelezo utakayoandika.
  • Raia ana haki ya kuwaeleza polisi ama Maafisa wa Kuzuia Rushwa kwamba lolote atakalosema linaweza kutumiwa kama ushahidi mahakamani, na asiburuzwe kuandika tu.
  • Raia ana haki ya kuomba Wakili wake awepo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa wakati anatoa maelezo yake.
  • Raia ana haki ya kuyasoma kabla ya kutia sahihi yake.
  • Raia ana haki ya kudai risiti ya orodha ya vitu vyake/fedha zake alizozitoa ama kukabidhi kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
  • Raia kama ni mwanamke ana haki ya kupekuliwa na polisi wa kike, na iwapo hakuna polisi mwanamke, basi mwanamke yeyote na vile vile kwa mwanamume.
  • Raia ana haki ya kufikishwa mahakamani katika muda usiozidi saa 24 tangu alipokamatwa na kufikishwa kituo cha polisi.
   
  Last edited by a moderator: Jul 13, 2009
 2. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #2
  Jun 2, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Thank you sweet heart
   
 3. K

  Kamuna JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 297
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Asante,wabheja, sancho mukwai,tuhongise,sante kalesa,dankie,aika, mwalemi,enaa, wasalipa!
   
 4. Maarifa

  Maarifa JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2009
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 2,880
  Likes Received: 1,050
  Trophy Points: 280
  Hizo haki na nyingine nyingi tu Zinavunjwa kila leo na polisi. Ama kwa makusudi ama kwa wao polisi kudhani wako juu ya sheria. Kwa nchi kama Tanzania Polisi hujifanya mahakimu. nitajie aliywahi kulalmikia kuhusu unyanyasaji wa polisi na akashinda! sana sana polisi wakibaini mwenzao kacheza Faul basi ni quick transfer! Hayo labda ughaibuni. Maana Polisi waweza kuwakoromea mpaka wakaingia mitini!! as afar as wakigundua kuwa kuwa wajua haki zako. Jifanye kujua hakia zako katika vituo vya Polisi Tanzania uone vijana wa Said Mwema watakavyokurarua na virungu!!
   
 5. m

  mamah Member

  #5
  Jun 3, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 31
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Polisi na haki za raia...mh. Hivi wale jamaa waliovamiwa na kushambuliwa na polisi pale Kinondoni kwa madai kuwa majambazi sugu issue yao illishia wapi? Sidhani kama kuna chochote kilichofanyika. Mwenye fununu atudokeze tafadhali.
   
 6. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #6
  Jul 13, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Umesahau hizi:

  • Iwapo askari polisi ataamua kumpekua mtuhumiwa, mtuhumiwa ana haki ya kumpekua askari polisi KABLA ya kupekuliwa yeye mwenyewe
  • Pia, askari polisi hawana haki ya kuingia kwenye gari, nyumba au ofisi ya mtu wanayemtuhumu, kwa madhumuni ya kufanya upekuzi, pasi na kuwapo kwa (a) hati ya upekuzi ambayo hutolewa mahakamani, (b) mashahidi wanaotambulika rasmi kisheria, kama vile, mwenyekiti/mjumbe wa serikali ya mtaa au mwenyekiti wa nyumba kumi kumi (iwapo mfumo huo unatumika), au (c) jirani wa myu anayetuhumiwa
  • Aidha, mtuhumiwa hatakamatwa au kupekuliwa na askari polisi baada ya saa 12.30 jioni au kabla ya saa 12.30 alfajiri, kwa mujibu wa Mwendendo wa Makosa ya Jinai (Penal Code Act), isipokuwa tu, kama kutakuwa na ushahidi wa kutosha kwamba, kumpekua mtuhumiwa kabla ya saa 12.30 alfajiri au baada ya saa 12.30 jioni kunaweza kuleta madhara kwa askari polisi, mashahidi au watu wengine wowote wale
  Nikikumbuka mengine nitawapa mkanda.

  ./Mwana wa Haki
   
 7. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #7
  Jul 13, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo jizi likivamia usiku wa manane inabidi kisheria tusubiri kuche ndio tiulikimbize kulikamata na kulisachi?
   
 8. Kyakya

  Kyakya JF-Expert Member

  #8
  Jul 13, 2009
  Joined: Apr 24, 2009
  Messages: 397
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35


  Ndo hapo sheria inapokanganya
   
 9. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #9
  Jul 13, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Hivi muandishi wa hiki kifungu amedhamiria kuandika kilichoandikwa ama la?

  Kimsingi amesema mtu asikamatwe au kupekuliwa na polisi baada ya saa 12.30 jioni na kabla ya saa 12.30 alfajiri ila tu pale kutakapokuwa na ushahidi wa kutosha kwamba kumpekua au kumkamata baada ya saa 12.30 jioni na kabla ya saa 12.30 alfajiri kunaweza kuleta madhara.

  Kwa hiyo asipekuliwe wala kukamatwa katika muda huo mpaka pale kutakapokuwa na ushahidi kwamba kutakuwa na madhara, tunatafuta madhara kwa nguvu, nani kaandika utumbo huu?
   
 10. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #10
  Jul 14, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135

  Acha kulalamika, chukua hatua sasa.

  Umekwishajulishwa HAKI zako sasa ni WAJIBU wako wewe kuhakikisha unatumia haki hizo.

  Mimi binafsi ninazifahamu haki hizo na huzitumia wakati wote inapobidi. Ukijiamini na kuonesha kuwa unatambua haki zako wale Polisi wasiokuwa waaminifu hawezi kukutendea kinyume na taratibu za kazi yao.

  Hili bandiko ni zuri sana kwani ni moja katika mambo mengi ambayo raia hawayafamu au hawataki kuyafahamu.
   
 11. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #11
  Jul 14, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135

  Kuna sheria au sababu zinazoweza kuondoa haki au ku-overrule sheria moja kwa nyingine. Ningependa kujua ni katika mazingira gapi hilo linaweza kutokea.
   
 12. MwanaCBE

  MwanaCBE JF-Expert Member

  #12
  Oct 7, 2009
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,773
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Mbona vihaki vyenyewe vichache hivi(si haba hata hivyo)!! Vitakidhi haja dhidi ya uonevu na manyanyaso tunayopata kutoka kwa polisi na wenye mamlaka? Na kama polisi akivunja haki hizi nichukue hatua gani. UELEWA WA SHERIA KWETU WA TZ NI TATIZO KUBWA SAAANA.
   
 13. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #13
  Oct 7, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Binafsi nashukuru kwa elimu hii muhimu
  ingawa inabidi kuipeleka na vijijini kwa sababu nako uko wako gizani kabisa polisi wanakula pesa za wananchi kama nini kwa wananchi kutokujua wajibu wao
   
 14. Absolute

  Absolute JF-Expert Member

  #14
  Dec 5, 2009
  Joined: Jan 19, 2007
  Messages: 335
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Uko sawa kabisa mkuu;
  Lakini tatizo ni kwamba je huyo(hao) maaskari wa kibongo watakupa mda wa ww kumuuliza hayo maswali? na ni wangapi wanasota kwenye vituo vya polisi zaidi ya wiki bila kwenda mahakamani mpaka wengine wanapewa cheo cha ubalozi?

  Nadhani muda umewadia kwa askari wetu kupata lessons freequently kuhusu haki za raia na limitation za haki zao maana raia wengi wasokuwa na hatia huishia kupata adha ya kipondo heavy tena ukijidai unajua sheria au una confident ndo kabisa wanakutoa wenge.

  Lakini pia swala la mahabusi kusota bila sheria kufata mkondo wake inavyostahili ni jipu jingine lililosahaulika, nadhani mlisikia last time kule Arusha mahabusu walivyolalama mpaka wakakataa kushuka kwenye karandinga.

  Anyway, ni maoni yangu tuu...
   
 15. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #15
  Dec 11, 2009
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  nashukuru kwa mwanga wa kisheria niloupata kupitia JF kwa kweli tuliowengi atujui haki zetu na ata police wengi awajui sheria kwann nasema hivyo police waliwaikuja kunikamata ofisini kwangu kinguvu bila ya rb wala restwarant nilipouliza nimefanya kosa gani naambiwa utajua ukokituoni ukifika nilopojaribu kuwambiaa wanitajie kituo gani niende mwenyewe kabla sijamaliza nimevutwa kinguvu nje wakanipeleka kituoni nilijisikia vbaya kweli. ila leo nimepata mwanga zaidi itumu JF yetu
   
 16. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #16
  Jan 5, 2010
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,753
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  hapana haimaanishi hata kidogo kwamba mtuhumiwa akifanya kosa baada ya sdas kumi na mbili na nusu ina maana kwamba ni absolute,that is the general rule which bears some exception,ndo maana kifungu hicho kina proviso(exception) kwamba katika mazingira fulani fulani,that kind of rule can be waived to pave the way to justice.
   
 17. consigliori

  consigliori JF-Expert Member

  #17
  Apr 15, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 390
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Bikra na Mwanahaki, nawapa big up. Yaani mmetupa vitu vitu vya maana sana. Binafsi mmeninielimisha sana katika hili, thanks again.
   
 18. N

  Ngala Senior Member

  #18
  Apr 15, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Umeeleza hali halisi ya ukamataji wao na hata baada ya kujua haki zako hizo bado wanaweza wakatenda kama kawaida yao na ubishi wwt wa kujua haki zako ujue virungu vitautenda mwili wako bila simile kwa kisingizio cha TUMIA NGUVU KIASI KUFANIKISHA UKAMATAJI ENDAPO MTUHUMIWA ANAGOMA KUKAMATWA. Hicho ni kifungu ndani POLICE GEN. ORDER Kinachowapa jeuri ya kututenda. Kumbuka ukamatwaji wa MURO silaha nzito za kivita utadhani jambazi MAFISADI ah ah kwa raha zao haki itoke wapi bwana kwa kapuku
   
 19. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #19
  May 15, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  kama hivyo ndivyo kwanini waweke sheria ambazo awazitekelezi jamani so tutaendelea kuburuzwa tu au ila mm nakataa kuburuzwa tena wataniforce na ukweli nitawaeleza tu
   
 20. b

  blackpepper JF-Expert Member

  #20
  May 15, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 382
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Raia ana haki ya kujua elimu ya anayemkamata
   
Loading...