Joto la mapenzi

Joto la mapenzi

Hii hadithi ipo global publishers.kwa hisani yao
ILIPOISHIA

“Sasa tutafanya nini baada ya kifo cha mzee?” Ambe aliuliza.

“Kilichobakia ni kujipanga kuhakikisha tunaondoka hapa na kuhamia mjini,” Mabina alijibu.

“Lakini si unajua tunatafutwa?”

“Ni kweli, lakini bado tuna deni la uonevu juu yetu.”

ENDELEA NAYO…

“Hilo ndilo nililokuwa nalifikiria sana, kama mzee Yamungu mtu aliyeyapigania maisha yangu kwa mwaka mzima amekufa, nami nitakufa siku moja. Ambe naomba unipe ruhusa kwenda mjini nikalipe kisasi.”

“Hapana, ninafikiria tujipange kumbuka sote tuna deni la aina moja.”

‘Sasa tufanyaje?”

“Kumbuka hapa hatuwezi kuondoka kienyeji kwa vile mzee Yamungu alikuwa zaidi ya mzazi wetu hivyo basi tunatakiwa hata tukiondoka lazima turudi hapa.”

“Lakini huoni kama huku ni mbali?”

“Ni kweli mbali, lakini ni sehemu nzuri ya kujificha.”

“Mmh! Sawa, sasa tutafanyaje kazi zetu?”

“Mzee Yamungu alinieleza kutoka barabara kuu mpaka mjini ni mwendo wa saa tatu.”

“Na usafiri wake?”

“Ni wa kawaida wa masaa yote.”

“Unaonaje tukienda usiku kufanya upelelezi wetu na kabla ya kupambazuka tunarudi?”

“Hiyo itakuwa sawa, tunaanzia kufanya upelelezi kwa mzee Mtoe ili tujue habari za mpenzi wangu na mwanangu.”

“Hilo halina tatizo tujipange tuingie mjini.”

“Vipi kuhusu nywele hizi na ndevu?”

“Hizi ni nzuri kwani zimetubadili sura kwa kiasi kikubwa hakuna mtu wa kutufahamu mara moja.”

“Ni kweli kabisa, lakini lazima tujitengeneze ili kutufanya watu wasitushangae kumbuka tumekuwa kama misukule.”

“Hilo litafanyika.”

Walipunguza nywele na ndevu na kuwa katika hali ya kawaida isiyomtia hofu mtu. Walichukua dola alizokuwa nazo mzee Yamungu zilizokuwa zaidi ya elfu ishirini na kwenda nazo mjini kuchenji. Fedha za nauli zilikuwepo ambazo mzee Yamungu alikuwa nazo baada ya kuchenji dola kidogo.

Kabla ya kuondoka walikwenda porini kuangalia bunduki aliyoificha Mabina kama ipo au watu waliiona. Walijikuta wakitembea kwa zaidi ya saa nne ndipo walipofika sehemu aliyoficha bunduki. Miti ilikuwa ipo vilevile hakuna uliokatwa.

Mabina alipanda juu ya mti ule na kushangaa kuikuta bunduki ipo kama alivyoiacha, aliteremka nayo na kuanza safari ya kurudi kijijini kwao. Walifika majira ya mchana wakiwa wamechoka sana kutokana na mwendo wa saa zaidi ya nane bila kupumzika.

Walikubaliana usiku wa siku ya pili kwenda mjini kufanya upelelezi, walipumzika kwa ajili ya siku ya pili.

*-- *-- *

Siku ya pili majira ya saa moja usiku walikuwa wamesimama barabara kuu iendayo mjini. Walibahatika kupata lifti kwenye lori lililokuwa linakwenda mjini, walifika mjini majira ya saa tatu na nusu. Walichukua bodaboda kwenda nyumbani kwao na mpenzi wake Koleta.

Walionekana kama watu wa machimbo kutokana na rangi ya nguo zao zilizokuwa na vumbi nyekundu. Walipokaribia walitembea kwa miguu hadi nje ya uzio wa nyumba ya mzee Mtoe.

Walisimama pembeni ya geti kujipanga jinsi ya kufanya upelelezi, mara gari aina ya Toyota Calina ilisimama mbele ya geti na kupiga honi. Ambe alichepua mwendo kuwahi kabla mlango hujafunguliwa. Aliyemuona ndani ya gari alishtuka kidogo, alikuwa mpenzi wake Koleta.

Alijitahidi kugonga kioo cha gari ili afunguliwe lakini mlango tayari ulikuwa umefunguka na gari liliingia ndani. Alipotaka kuingia mlinzi alimuwahi kumzuia kisha alifunga geti, alijilaumu kwa kuchelewa kugonga kikoo au kusogea karibu ya geti. Aligonga mlango ili afunguliwe lakini Mabina aliwahi kumshika na kumsogeza pembeni.

“Ambe unataka kufanya nini?”

“Niache Mabina,” Ambe alikuwa mkali baada ya kumuona mpenzi wake.

“Siwezi kukuacha umeona nini?”

“Nimemuona mpenzi wangu.”

“Umekuja kumchukua au kufanya upelelezi?”

“Upelelezi wa nini wakati nimemuona?” Ambe alichanganyikiwa kumuona Koleta.

“Acha ujinga kama umemuona unataka kufanya nini?”

“Si nisikie atasemaje akiniona?”

“Ambe acha kuchanganyikiwa mapema, tumekuja kufanya upelelezi ili tukirudi kwetu tujue tukija tutafanya nini.”

“Mabina upepelezi wangu ulikuwa kujua kama Koleta yupo.”

“Umemuona sasa unataka kufanya nini?”

“Nionane naye.”

“Ukishaonana naye?”

“Nitajua hapohapo.”

“Lakini unajua unatafutwa kwa kosa la mauaji na wizi wa silaha?”

“Hilo najua.”

“Sasa kwa nini unataka kujishikisha, hujui mwanamke bado ana mapenzi na wewe au vipi, anaweza kukukamatisha.”

“Bora nikamatwe nijue moja.”

“Mzee alikueleza nini?”

”Kuhusu nini?”

“Kuhusu ujinga kama huu unaotaka kuufanya?”

“Ni kweli lakini lazima nipiganie haki yangu.”

“Koleta na mama yako nani mwenye thamani kwako?”

“Mama yangu.”

“Ukikuta ameolewa?”

“Nitaua mtu.”

“Ili?”

“Nami nife.”

“Sikiliza, sipendi tutofautiane tumekuja hapa kwa kazi moja tu ya kufanya upelelezi, tuchunguze tujue Koleta baada ya kutoweka amefikaje nyumbani. Pia kujua kama mtoto wako yupo kisha tutajua tutawezaje kumpata Koleta bila mtu yeyote kujua.”

“Mmh! Kweli umezungumza jambo la msingi sana. Sasa nifanyeje?”

“Unaju…”

Mabina alinyamaza baada ya kuona gari aina ya Land Cruiser VX rangi nyeusi likisimama mbele ya geti la nyumba ile. Kabla ya kuingia aliteremka msichana mmoja kisha gari liliingia ndani. Msichana yule alielekea dukani, Ambe alimfahamu alikuwa mmoja wa wafanyakazi wa ndani lakini kwa siku ile alionekana kupendeza sana.

“Vipi unamfahamu?” Mabina aliniuliza.

“Ndiyo.”

“Msogelee akitoka tu dukani umwite.”

“Nimemsahau jina.”

“Mwite dada.”

Baada ya muda walimuona yule dada akirudi na paketi ya maziwa na mkate, alipowakaribia Ambe alimsemesha:

“Samahani dada,”

“Bila samahani,” alisema huku akisimama.

“Koleta yupo?”

“Wewe nani unayemuuliza Koleta?”

“Ambe.”

“Ambe!” alishtuka.

“Ndiyo mpenzi wa Koleta niliyefungwa kwa hila za mzee Mtoe ili nisimuoe.”

“Hata siamini, si…si…nilisikia umeua na kutoroka na silaha kwa hiyo unatafutwa?”

“Ni kweli natafutwa lakini sijaua wala kukimbia na silaha.”

© GlobalPublishers 2015 -
 
Asante sana Uduvi, yaani naipenda sana hadi nime subscribe ili niwe naisoma kila utumapo
 
ILIPOISHIA

Ester baada ya kurudi ndani kupeleka mikate aliyotumwa, alikuwa na donge zito moyoni juu ya kuficha siri ya kuonekana kwa kipenzi cha tajiri yake. Lakini alijitahidi kuificha siri ile kusubiri siku ambayo Ambe angekuja dukani kuonana na Koleta.

ENDELEA NAYO…

Siku-ya pili wakiwa dukani wakifanya biashara Koleta alimwita, baada ya kumsogelea alimweleza kitu:

“Ester eti unamuonaje Jose kweli anafaa kumkabidhi moyo wangu?”

“Mmh! Dada mbona swali gumu,” Ester aliruka mtego.

“Siyo gumu kwa vile hata wewe unamuona na bado kama siku mbili anivishe pete ya uchumba.”

“Dada mpaka mnakubaliana uliridhika naye.”

“Ni kweli, lakini ndoto ya jana ilimtoa kabisa Jose moyoni mwangu.”

“Ndoto! Umeota nini?”

“Nimeota nimekwenda shule kumuona Ambe Jr, sikuamini kumkuta yupo na baba yake kwa kweli nilipata mshtuko wa ajabu. Nilimkumbatia kwa furaha kubwa kwa mara ya kwanza kumuona mpenzi wangu aliyepotea muda mrefu.

Kilichoniumiza moyo wangu ni kauli ya ndotoni aliyoisema Ambe senior kuwa ninataka kufanya nini, eti nimemsaliti kwa kukubali kuolewa na mwingine ikiwa matatizo yote sababu ni mimi.

“Niliposhtuka usingizini nililia sana na kuamini kabisa sababu ya kufungwa gerezani kwa Ambe kunatokana na mimi. Kwa kweli imeniuma sana, si bora ningejua yupo wapi ili nijue ninayemsubiri yupo wapi, kwa kweli ndoto ile imenipa wakati mgumu sana,” Koleta alisema huku akifuta machozi.

“Mmh! Pole sana dada.”

“Ndiyo maana nikakuuliza unamuonaje shemeji yako mpya.”

“Kabla ya kukujibu ukisikia Ambe yupo utafanya nini?”

“Sina budi kubadili msimamo wangu, nampenda sana Ambe pamoja na maneno ya baba ya kunikatisha tamaa ili nimchukie, lakini najua sababu yote ni yeye aliyetengeneza mazingira yale ili tu nisioane na mpenzi wangu.”

“Mmh! Lakini… tuache,” Ester alitaka kutoboa siri ya kumuona Ambe na waliyozungumza.

“Tuache nini Ester kumbuka kipindi hiki nahitaji msaada wako kuliko kitu kingine, najiuliza huenda ndoto ina ukweli naolewa Ambe anatokea nitauweka wapi uso wangu?” Koleta alisema kwa sauti iliyokosa majibu ya maswali ambayo yalitegemea sana uwezo wa Ester.

Ester pamoja na kukatazwa na Ambe aliona ni ujinga kukaa kimya- kwa kuamini huenda akachelewa kutokea na kukuta Koleta kaolewa.

“Dada nilikuwa nakuomba umsubiri Ambe.”

“Sawa nitamsubiri mpaka lini, hajulikani amekufa au yupo hai au amekamatwa tena na kunyongwa.”

“Ambe ni mzima wa afya.”

“Mzima! Umemuona wapi?”

“Tena hukujua, jana usiku kuna mtu aligonga mlango wa gari pale getini ili ufungue lakini hukusimama uliliingiza mpaka ndani na wala hukutoka tena nje.”

“Eeh! Nimekumbuka kuna mtu aligonga mlango wa gari yangu.”

“Basi yule alikuwa Ambe.”

“Muongo! Umejuaje?”

Ester aliamua kuifungua siri aliyokatazwa na Ambe, Koleta hakuamini alijilaumu kwa kitendo cha kutomsikiliza.

“Ester unayosema ni kweli au uongo ili kunirusha roho.”

“Mimi nimejuaje hayo, kuna mtu aligonga gari lako hata alipotaka kuingia ndani alizuiwa na mlinzi. Tena kama ungewahi kutoka ndani ya gari ungemsikia akikuita kwa sauti ya juu.”

“Mungu wangu! Ambe atanielewaje?”

“Hawezi kukuelewa vibaya kwa vile hamkuwa na miadi ya kuonana.”

“Kwa nini hukunifuata kuja kumuona.”

“Alikataa.”

“Alimuulizia mwanaye.”

“Alimuulizia.”

“Ulimjibu nini?”

“Nilimwambia yupo katika hali nzuri.”

“Afya yake ipo vipi, amekonda sana?”

“Wala tena ana afya nzuri huwezi kuamini utadhania kama hakuwa gerezani.”

“Kwa nini alikataa kuonana na mimi, au amenichukia kwa ajili ya baba kusababisha kufungwa.”

“Bado Ambe anakupenda tena anakupenda sana, tena kanihakikishia kuna siku atarudi mjini na kufunga ndoa na wewe.”

“Eti?” kauli ile ilimshtua Koleta.

“Amesema atarudi mjini na kufunga ndoa na wewe.”

“Ester unayosema ni kunifurahisha au kweli?”

“Sijawahi kukutania pia siwezi kuleta utani katika jambo zito kama hili.”

“Amesema anakaa wapi?”

“Hakusema, lakini inaonesha yupo nje ya mji, hata mavazi yao kama watu wa machimbo, pia wamefuga nywele na ndevu nyingi.”

“Alikuwa na nani?”

“Na rafiki yake mmoja.”

“Mmh! Sasa huu mtihani mwingine.”

“Mtihani gani tena?”

“Si kuhusu mchumba na Ambe.”

“Mwenye mali karudi hapo kuna mtihani gani?”

“Na kweli, sasa sijui atakuja lini?”

“Kwa vile nimemuelekeza huenda anataka kukufanyia suprise.”

“Yaani siamini, nitaamini baada ya kumuona, kwa nini hakutaka kuniona au alijua simpendi tena, nisipompenda yeye nimpende nani.”

Wakati huo mwanaye Ambe Jr alikuwa akiingia na bibi yake, alimuangalia kwa muda na kukumbuka taarifa za kuonekana kwa baba yake. Aliomba kimoyomoyo mwanaye amuone baba yake hata mara moja kwani alishakata tamaa ya mwanaye kumuona baba yake.

******

Usiku wa siku ile kama kawaida- Ambe na Mabina walifika mji aliokuwa akiishi mzee Samjo mtu aliyesababisha kifo cha baba yake Mabina na kufungwa kwake ili kujua nini kinaendelea baada ya muda mrefu kupita bila taarifa ya nini kinaendelea.

Baada ya kufika nje ya geti la nyumba ya mzee Samjo lililokuwa linalindwa na walinzi wa kampuni za ulinzi.

“Sasa tutafanyaje?” Ambe alimuuliza Mabina aliyekuwa ametulia akijaribu cha kufanya.

“Cha muhimu kujua kama bado yupo na anapatikanaje?”

“Hilo wazo zuri.”

“Hapa ni kumfuata mlinzi atatusaidia tu.”

Walisogea hadi getini na kugonga geti, baada ya muda alitoka mlinzi.

“Niwasaidie nini?”

“Mzee Samjo yupo?”

“Ninyi kina nani?”

“Kaka badala ya kutujibu unatuuliza swali.”

“Lazima niwajue kabla ya kuwajibu.”

“Mpaka tunafika hapa tuna shida naye tumevuka nyumba ngapi?”

“Yupo, mnasemaje?”

“Tulitaka kujua hilo, mengine tutazungumza naye kwenye simu, asante kwa msaada wako.”

Waliagana na yule mlinzi na kurudi pembeni kupanga jinsi ya kuingia ndani ya nyumba ya mzee Samjo.

“Sasa tufanye nini?” Ambe aliuliza.

“Nilikuwa na wazo moja la kuja kufanya mauaji akiwa mlangoni kwake.”

“Sasa si utakuwa umefanya kazi bure.”

“Kivipi?”

“Ukimuua bila kupata vyako utapoteza vitu vyako vingi.”

“Ambe, nikimuua kila kitu kitarudi kimoja baada ya kingine.”

“Kivipi?”

“Nitaua mmoja baada ya mwingine mpaka mali zangu zipatikane.”

“Sasa utamuua nani?”

“Ukoo mzima.”

“Huoni utakuwa unaingia katika vita nyingine na serikali?”

-

“Ambe kwanza nikifanikiwa kumuua mzee Samjo moyo wangu utakuwa kwatu hata nikikosa vitu vyangu.”

“Unajua unachotaka kufanya ni kitu cha kubahatisha unaweza kumkosa mzee Samjo na wewe kufa kibudu.”

“Una maana gani?”

“Kwa nini tusifanye jambo kisomi zaidi.”

“Tufanyeje?”

“Inatakiwa tukiweza kupenya tuingie mpaka ndani kwa mzee Samjo kisha akuone upo hai na kumweleza akulipe haki yako kwa hiyali yake, kama atakataa tutaanza kuiteka familia yake na kumuomba atulipe haki yako na akikaidi basi tutarudisha mwili bila uhai.”

“Mmh! Mbona hayo mawazo hukuwa nayo siku tulipokwenda ukweni?”

“Hiyo ndiyo faida ya kuwa wawili mawazo yangu mwenyewe ningeweza kupotea.”

“Lakini huoni mpango wako ni njia ndefu inayohitaji mtaji mkubwa pia tuwe na vyombo vya kufanyia kazi japo ni mzuri sana.”

“Kama huo ni wa njia ndefu tena wa gharama basi tunangalie mwingine ambao utafanikiwa kulipa kisasi- pia kupata haki yako, unajua nini?”

“Nitajuaje bila kuniambia.”

“Mpaka sasa hivi kila mtu anajua wewe ni marehemu.”

“Kama wanajua- mimi marehemu inasaidia nini?”

“Ni wewe kuvaa vizuri na kwenda nyumbani kwa mzee Samjo nina imani akikuona atachanginyikiwa na hapo kumweleza ukweli kuwa amefufuka kudai haki yako na kumweleza huta kufa mara mbili tena kwa kujiamini mweleza unaitaka siku gani akikupa kinafuata kifo chake.”

“Na asipokubali kutoa?”

“Tunamuua popote.”

“Unaweza kufanya mauaji wewe?”

“Hilo jibu, hivi nimepanga kumuulia mbali mzee Mtoe.”

“Unajua sikuelewi unasema bado unamtaka mpenzi wako, atakukubali ukimuua baba yake?”

“Kuua kuko pale pale hata kwa siri lakini lazima nimtie adabu.”

“Mfano mpenzi wako akiwa tayari kuwa na wewe na kukuomba usimuue baba yake utafanya nini?”

“Hebu kwanza kujadili hili la kwako tulipatie ufumbuzi tulichanganya mada mbili kwa mara moja.”

“Najua jibu lake ni gumu, haya tuendelee na mipango yetu.”

“Tuliishia wapi vile unajue ulivuruga mipango yangu.”

“Kama atakataa kutoa mali tumuue popote, nimekuuliza ukasema kuua kwako si tatizo.”

“Nataka tufanye mambo kitaalamu, tumeona kwenye sinema watu wanavyodai fedha zao na polisi hawawakamati na mwisho wa siku wanapata vitu vyao.”

“Ambe kuigiza kuna tofauti na tukio la kweli.”

“Mabina kuna matukio mangapi ya kweli- yametokea na watu kusikia wakisema tukio lilikuwa kama muvi.”

“Sisi tumejiandaa kufanya hayo?”

“Kwani hao wana miguu na mikono- mingapi?”

“Unajua kutumia siraha?”

“Mimi ni mtaalamu wa mapigano ya mikono nikichanganya na uwezo wako wa siraha litakuwa jeshi kamili.”

“Unaweza kuwa na uwezo wa mapigano ya mikono lakini huna moyo wa ujasiri.”

“Maisha niliyoishi porini nina roho kama shetani.”

“Kama una roho kama shetani mbona mapenzi yanakuendesha.”

“Kaka mapenzi kitu kingine, huyo Samson kwenye mapenzi alitepeta kwa Delilah, huyu simba mkali lakini kwenye mapenzi huwa mpole. Samson si kitu kwa Delilah lakini katika suala la kujitetea Samson aliua simba kwa mkono.”

“Nimekuelewa, kwani ulivyokuwa gerezani na ulivyotoka ilikuwa tofauti kabisa nimekukuta unafanya kazi kama katapira.”

“Nimeamini mwanadamu huweza kuishi maisha ya aina yoyote sikuwaza kuna siku nitaishi kama mnyama na kuyazoea maisha na kuyaona ya kawaida.”

“Kwa hiyo?”

“Nataka tujipanga wiki ijayo baada ya kuonana na Koleta tunavamia kwa mzee Samjo.”

“Unajua tuna bunduki na kazi yetu inataka inataka siraha ndogo.”

“Mmh! Nimepata wazo acha nionane na Koleta nitakupa jibu la uhakika.”

“Hiyo siraha ataitoa Koleta?”

“Nimekwambia ngoja nionane naye nijue kwanza msimamo wake kwangu kisha tutamalizia na la kwako.”

“Hakuna tatizo.”

Walitafuta usafiri na kurudi kijijini kwao kujipanga kwa ajili ya siku ya pili ya kwenda kuonana na Koleta.
 
Kwenye gazeti la risasi la kila jumamosi ndo mimi naendelea nayo iko poa nunueni magazeti acheni ubahili
 
ILIPOISHIA
"Ukimuua bila kupata vyako utapoteza vitu vyako vingi."
"Ambe, nikimuua kila kitu kitarudi kimoja baada ya kingine."
"Kivipi?"
"Nitaua mmoja baada ya mwingine mpaka mali zangu zipatikane."
"Sasa utamuua nani?"
"Ukoo mzima."
ENDELEA NAYO...


"Huoni utakuwa unaingia katika vita nyingine na serikali?"
"Ambe kwanza nikifanikiwa kumuua mzee Samjo moyo wangu utakuwa kwatu hata nikikosa vitu vyangu."
"Unajua unachotaka kufanya ni kitu cha kubahatisha unaweza kumkosa mzee Samjo na wewe kufa kibudu."
"Una maana gani?"
"Kwa nini tusifanye jambo kisomi zaidi."
"Tufanyeje?"

"Inatakiwa tukiweza kupenya tuingie mpaka ndani kwa mzee Samjo kisha akuone upo hai na kumweleza akulipe haki yako kwa hiyari yake, kama atakataa tutaanza kuiteka familia yake na kumuomba atulipe haki yako na akikaidi basi tutarudisha mwili bila uhai."

"Mmh! Mbona hayo mawazo hukuwa nayo siku tulipokwenda ukweni?"
"Hiyo ndiyo faida ya kuwa wawili mawazo yangu mwenyewe ningeweza kupotea."
"Lakini huoni mpango wako ni njia ndefu inayohitaji mtaji mkubwa pia tuwe na vyombo vya kufanyia kazi japo ni mzuri sana."

"Kama huo ni wa njia ndefu tena wa gharama basi tuangalie mwingine ambao utafanikiwa kulipa kisasi pia kupata haki yako, unajua nini?"
"Nitajuaje bila kuniambia."
"Mpaka sasa hivi kila mtu anajua wewe ni marehemu."

"Kama wanajua mimi marehemu inasaidia nini?"
"Ni wewe kuvaa vizuri na kwenda nyumbani kwa mzee Samjo nina imani akikuona atachanganyikiwa na hapo kumweleza ukweli kuwa umefufuka kudai haki yako na kumweleza hutakufa mara mbili tena kwa kujiamini mweleze unaitaka siku gani akikupa kinafuata kifo chake."

"Na asipokubali kutoa?"
"Tunamuua popote."
"Unaweza kufanya mauaji wewe?"
"Hilo jibu, hivi nimepanga kumuulia mbali mzee Mtoe."

"Unajua sikuelewi unasema bado unamtaka mpenzi wako, atakukubali ukimuua baba yake?"
"Kuua kuko palepale hata kwa siri lakini lazima nimtie adabu."
"Mfano mpenzi wako akiwa tayari kuwa na wewe na kukuomba usimuue baba yake utafanya nini?"
"Hebu kwanza tujadili hili la kwako tulipatie ufumbuzi tulichanganya mada mbili kwa mara moja."
"Najua jibu lake ni gumu, haya tuendelee na mipango yetu."

"Tuliishia wapi vile unajua ulivuruga mipango yangu."
"Kama atakataa kutoa mali tumuue popote, nimekuuliza ukasema kuua kwako si tatizo."
"Nataka tufanye mambo kitaalamu, tumeona kwenye sinema watu wanavyodai fedha zao na polisi hawawakamati na mwisho wa siku wanapata vitu vyao."
"Ambe kuigiza kuna tofauti na tukio la kweli."

"Mabina kuna matukio mangapi ya kweli yametokea na watu kusikia wakisema tukio lilikuwa kama muvi."
"Sisi tumejiandaa kufanya hayo?"
"Kwani hao wana miguu na mikono mingapi?"
"Unajua kutumia silaha?"
"Mimi ni mtaalamu wa mapigano ya mikono nikichanganya na uwezo wako wa silaha litakuwa jeshi kamili."
"Unaweza kuwa na uwezo wa mapigano ya mikono lakini huna moyo wa ujasiri."
"Maisha niliyoishi porini nina roho kama shetani."

"Kama una roho kama shetani mbona mapenzi yanakuendesha."
"Kaka mapenzi kitu kingine, huyo Samson kwenye mapenzi alitepeta kwa Delilah, huyu simba mkali lakini kwenye mapenzi huwa mpole. Samson si kitu kwa Delilah lakini katika suala la kujitetea Samson aliua simba kwa mkono."
"Nimekuelewa, kwani ulivyokuwa gerezani na ulivyotoka ilikuwa tofauti kabisa nimekukuta unafanya kazi kama katapila."
"Nimeamini mwanadamu huweza kuishi maisha ya aina yoyote sikuwaza kuna siku nitaishi kama mnyama na kuyazoea maisha na kuyaona ya kawaida."

"Kwa hiyo?"
"Nataka tujipange wiki ijayo baada ya kuonana na Koleta tunavamia kwa mzee Samjo."
"Unajua tuna bunduki na kazi yetu inataka silaha ndogo."
"Mmh! Nimepata wazo acha nionane na Koleta nitakupa jibu la uhakika."
"Hiyo silaha ataitoa Koleta?"

"Nimekwambia ngoja nionane naye nijue kwanza msimamo wake kwangu kisha tutamalizia na la kwako."
"Hakuna tatizo."
Walitafuta usafiri na kurudi kijijini kwao kujipanga kwa ajili ya siku ya pili ya kwenda kuonana na Koleta.
***
Baada ya taarifa ya kuonekana Ambe na kusema atafika dukani kuonana na Koleta, taarifa zile zilimkosesha raha kabisa Koleta, akiwa dukani kwake kila mteja aliyeingia alimtazama na kufikiria huenda ni mpenzi wake. Mpaka jioni inaingia hakumuona mtu yeyote ilibidi amuulize Ester.
"Ester, alisema anakuja lini?"

"Hakusema lini lakini niliamini leo angeweza kuja tusubiri muda bado."
"Au ulimuelekeza vibaya."
"Vizuri kabisa na kusema sehemu hii anaijua."
"Sasa mbona haji?"

"Labda anaogopa kuja mchana kuhofia kukamatwa."
"Mmh! Itabidi leo nisubiri muda wote mpaka nimuone."
"Mmh! Mpaka muda huu huenda haji labda kesho."
"La..lakini Ester mbona kama sikuamini."
"Kuhusu nini?"
"Kuhusu Ambe."

"Dada haki ya nani nimeonana naye uso kwa uso labda ningekuwa nimeelezwa na mtu ningekuwa na wasiwasi."
"Sasa mbona haji?"
"Sijajua."
"Hakukupa namba ya simu?"
"Kwake kutokana na kuchanganyikiwa baada ya kumuona sikukumbuka kitu hicho ambacho kwa kweli ni muhimu sana ungeweza kuwasiliana naye moja kwa moja hata kupanga sehemu ya kuonana bila wasiwasi."
"Mmh! Sasa atakuwa wapi?"

Wakati wakijadiliana simu ya Koleta iliita, alipoitazama aliikata.
"Vipi mbona umeikata?"
"Si huyu mshenzi."
"Mshenzi gani tena dada?" Ester alimshangaa Koleta.
"Si Jose."

"Jose kafanya nini tena?"
"Tunazungumza nini sasa hivi?"
"Kuhusu Ambe."
"Unafikiri nitazungumza naye nini?"
"Msikilize tu."

"Siwezi, hapa namsubiri mtu mmoja si mwingine ni Ambe baba Ambe Jr."
Mara simu iliita tena, aliikata na kuizima kabisa.
"Dada ungemsikiliza tu na kumdanganya ili tu aridhike."
"Siwezi kumdanganya, lazima nionane na Ambe kabla ya hiyo kesho kutwa."
"Asipoonekana?"

"Kama yupo hai bado sitakuwa na chaguo lingine zaidi yake, Ester hujui tu kila siku ya Mungu kabla ya kulala humuomba Mungu mwanangu siku moja aonane na baba yake. Muone Ambe alivyochoka kumsubiri baba yake."
Simu ya Ester iliita alipoangalia alikuta ni Jose, kabla ya kuipokea alimwambia Koleta.
"Dada, Jose kapiga kwangu."
"Pokea lakini mwambie nina kikao na wazazi."
Ester aliipokea na kumueleza Jose mchumba mtalajiwa wa Koleta kuwa mwenzake yupo kwenye mazungumzo na wazazi wake.

"Basi akimaliza mwambie anipigie siwezi kulala bila kusikia sauti yake, mwambie nampenda sana Koleta."
"Sawa shemu akimaliza nitamweleza."
Baada ya kukata simu alimgeukia Koleta aliyekuwa akimsikiliza kwa sauti ya nje ya simu.
"Umemsikia mzee?"
"Achana naye."

"Sasa dada muda unakwenda japo bado kuna wateja lakini tumevuka saa tatu sasa, muonee huruma Junior muone mtoto anasinzia."
"Mmh! Naona leo haji, sasa atakuja lini jamani?" Koleta aliuliza kwa sauti ya huzuni.
"Kama nilivyokueleza lazima aje na kama alivyosema kwa kauli yake kuwa lazima atarudi na kukuoa."

"Sasa atanioa lini, nitaendelea kuteseka mpaka lini?"
"Tusubiri basi nusu saa ikivuta tuamini leo haji."
Muda nao ulikatika mpaka saa nne kasoro usiku hakuonekana, Koleta alikubali kufunga duka na kuondoka shingo upande.
 
ILIPOISHIA:
"Kama yupo hai bado sitakuwa na chaguo lingine zaidi yake, Ester hujui tu kila siku ya Mungu kabla ya kulala humuomba Mungu mwanangu siku moja aonane na baba yake. Muone Ambe alivyochoka kumsubiri baba yake."
Simu ya Ester iliita alipoangalia alikuta ni Jose, kabla ya kuipokea alimwambia Koleta.
"Dada, Jose kapiga kwangu."
"Pokea lakini mwambie nina kikao na wazazi."
SASA ENDELEA…

Ester aliipokea na kumueleza Jose mchumba mtarajiwa wa Koleta kuwa mwenzake yupo kwenye mazungumzo na wazazi wake.
"Basi akimaliza mwambie anipigie siwezi kulala bila kusikia sauti yake, mwambie nampenda sana Koleta."
"Sawa shemu akimaliza nitamweleza."
Baada ya kukata simu alimgeukia Koleta aliyekuwa akimsikiliza kwa sauti ya nje ya simu.
"Umemsikia mzee?"
"Achana naye."
"Sasa dada muda unakwenda japo bado kuna wateja lakini tumevuka saa tatu sasa, muonee huruma Junior muone mtoto anasinzia."
"Mmh! Naona leo haji, sasa atakuja lini jamani?" Koleta aliuliza kwa sauti ya huzuni.
"Kama nilivyokueleza lazima aje na kama alivyosema kwa kauli yake kuwa lazima atarudi na kukuoa."
"Sasa atanioa lini, nitaendelea kuteseka mpaka lini?"
"Tusubiri basi nusu saa ikivuka tuamini leo haji."
Muda nao ulikatika mpaka saa nne kasoro usiku hakuonekana, Koleta alikubali kufunga duka na kuondoka shingo upande.
****
Ambe na Mabina waliwasili mjini wakiwa katika muonekano tofauti kila mmoja alikuwa mtanashati. Hawakuwa na wasiwasi kutokana na mabadiliko ya mwili pia kupotea mjini kwa muda mrefu. Hata picha za Ambe kutafutwa zilikuwa zimeshabanduka na nyingine kuchanika.

Mabina yeye ndiye ambaye hakuwa na wasiwasi kwa kuamini kila mmoja anajua ameshakufa hata usoni kwake hakuvaa kitu chochote tofauti na Ambe aliyekuwa amevaa miwani usoni. Waliwasili kwenye duka la Koleta Super Market na kuingia ndani kama wateja wa kawaida. Ambe alikwenda mpaka alipokuwa amekaa Koleta aliyeonekana akitazama kitu kwenye kompyuta mara simu yake iliita.

"Haloo Rich… Nimekueleza subiri….Kuwa muelewa jibu la ndiyo au hapana nitakupa leo jioni….Kuna tatizo nimekueleza hebu kuwa muelewa….Nasikia baba watoto wangu amerudi….Inawezekana nitakuwa na uamuzi mwingine tofauti na huo….Naomba usubiri, nipo kazini tutazungumza jioni….Rich nimesema tutazungumza jioni kuwa muelewa," baada ya kusema yale kwa sauti ya ukali alikata simu.

"Vipi dada?" Ester alimsogelea Koleta."Si Rich nimemweleza jibu la ndiyo au hapana nitampa jioni lakini anakuwa king'ang'anizi, baba Junior akitokea nitafanya nini?"

"Kweli, shemu heri angetokea ukajua moja."

"Ester unajua sikuamini." "Kuhusu nini?" "Kuhusu kuonana na baba Junior."

"Koleta, Ambe yupo nina imani siku yoyote atakuja."

"Mbona haji, hebu ona ninavyoteseka, jana sijalala kwa ajili ya kumuwaza nampenda sana mpenzi wangu sijui akitokea itakuwaje?"

"Ha..ha..lafu itakuwaje?"

"Kuhusu kuwa pamoja, yeye anatafutwa na baba yako hataki?"

"Tutapanga tukionana."

Ester aligundua kitu kwa mtu aliyekuwa amesimama karibu na wao walipokuwa wakizungumza, kwa chati alishangaa kumuona ameshika bidhaa moja muda mrefu huku akifuatilia mazungumzo yao.

Alipomuangalia vizuri yule mwanaume aliondoka eneo lile na kuelekea kwenye shefu za bidhaa zingine. Koleta alimshangaa Ester kuonekana anashtuka kitu.

"Vipi mbona hivyo?"

"Mmh! Kuna kitu hebu subiri." "

Kitu gani?"

"Nitakupa jibu si muda mrefu."

Ester alinyanyuka na kujifanya akiendelea na shughuli zake, alimfuatilia Ambe aliyejifanya yupo bize. Alipomsogelea alijifanya hana habari naye lakini alipata uhakika kwa kumuona rafiki yake aliyekuwa naye siku ile usiku. Baada ya kupata uhakika alijifanya akipanga vitu na kuelekea kwa Koleta aliyekuwa akiendelea na mahesabu yake."Dada nikuambie kitu?"

"Niambie mdogo wangu."

"Unajua shemu alikuwa amesimama hapa muda mrefu bila sisi kumjua."

"Shemejii yupi Rich?" "Hapana Ambe." "Muongo!" "Kweli dada."

"Usiniambie, kwa hiyo ameondoka?"

Koleta aliuliza kwa sauti ya hamaki kidogo.

"Usipige kelele bado yumo ndani."

"Yupo wapi?" "Nenda hivi… kuna mwanaume amevaa jinzi na tisheti ya machungwa na rafiki yake amevaa shati la drafti na jinzi wote wana raba nyeupe."

Kabla mazungumzo hayajaisha Koleta alikuwa ameshanyanyuka na kuelekea alipokuwa Ambe. Alitembea taratibu kuwafuata baada ya kuwaona kwa mbali. Alikwenda moja kwa moja hadi alipokuwa amesimama Ambe aliyejifanya yupo bize.Alipomfikia bado Ambe hakushtuka aliamini hakuna mtu aliyemfahamu aliendelea kuoneshana bidhaa na Mabina. Alipofika alisimama mbele ya Ambe ambaye alikuwa ni yeye kabisa. Koleta alimtazama Ambe na kuanza kutokwa machozi kila alipotaka kusema midomo ilimcheza maneno yaligoma kutoka mdomoni, hakuamini katika maisha yake angeweza kuonana na mpenzi wake baba wa mtoto wake Ambe Junior.Ambe hakuwa na jinsi zaidi ya kutoa kitambaa na kumfuta machozi Koleta."Pole mpenzi," Ambe alisema kwa sauti ya chini.

Koleta hakusema kitu zaidi ya kujitupa kifuani kwa Ambe na kuendelea kulia."Koleta unalia nini?" "Inauma Ambe siamini…siamini naona kama ndoto kwa nini hukutaka kuonana na mimi siku ya kwanza ulipokuja nyumbani?"
"Nilitaka kujua kama upo na kujipanga, hata leo sikutaka unione nilitaka kukuona tena mpenzi wangu kabla ya kujipanga kukunyakua." "Ambe nipo tayari hata sasa hivi tuondoke wote." "Maisha yangu ni kama mnyama huyawezi lazima nijipange."
"Nitayaweza tu, nimeishi jalalani zaidi ya miezi minne sitashindwa kukaa popote." "Mtoto yupo wapi?" "Yupo shule muda si mrefu atakuja…" "Dada, babu na Junior wanakuja!" Ester alimshtua Koleta aliyekuwa bado amelala kifuani kwa Ambe."Mwache aje atanifanya nini?" Koleta alijibu kwa kiburi."Hapana Koleta bado sijajipanga, rudi sehemu yako ya kazi mimi nipo," Ambe alimwambia Koleta kwa sauti ya upole naye alimwelewa.

Koleta alirudi ofisini kwake lakini alijisahau kufuta machozi, baba yake mzee Mtoe alipofika alishtuka kumkuta mwanaye akitokwa na machozi."Babu, mama analia?" Ambe Junior alimwambia babu yake aliyekuwa amejiandaa kumuuliza mwanaye. "Koleta vipi?" "Safi baba," alijibu huku akifuta machozi, pembeni ya mzee Mtoe alikuwa amesimama Ambe na Mabina ambao hakuwajua."Safi vipi?""Basi tu nipo sawa.""Hapana kuna kitu usinifiche naomba uwe mkweli?""Nimemkumbuka baba Junior.""Wewe kweli una matatizo unamkumbuka muuaji?""Ndiyo baba yote umesababisha wewe.""Acha akili za kipuuzi, unakosa nini si nimesikia una mchumba mlete mfunge ndoa uache kumfikiria muuaji, kama kaua huko angeshindwa nini kukuua wewe."
 
Back
Top Bottom