Joto la mapenzi

Joto la mapenzi

JOTO LA MAPENZI-16

ILIPOISHIA

Siku moja ambayo ilikuwa chanzo cha mkasa huu ninaokuhadithia, alikuja mwanamke mmoja ambaye alionekana mwenye maisha ya kifahari. Ilikuwa tofauti na wateja wengi kuja mchana, yeye alikuja saa moja na nusu usiku.
Baada ya kumkaribisha bila kumjua ni nani alinieleza matatizo ya mume wake.
ENDELEA..."

Samahani mzee nina tatizo la muda mrefu kwa mume wangu."
"Tatizo gani?" nilimuuliza.
"Japo ni aibu lakini imenibidi nije mwenyewe baada ya kuwatuma watu ambao waliniletea nilichowatuma bado tatizo limekuwa kubwa lililokosa ufumbuzi."
"Ni tatizo gani?" Nilimuuliza.

"Mume wangu ana tatizo la nguvu za kiume."
"Unasema umeshawahi kumtuma mtu hapa kwangu?"
"Ndiyo."
"Ulipomtuma ikawaje?"
"Ulimpa dawa ya kuweka kwenye chai na kumueleza mwenye tatizo atumie vyakula vya aina gani?"
"Mmh! Ikawaje?"

"Kwa kweli ilikuwa vigumu kwa vile chakula cha mume wangu kina mtu maalumu wa kupika siyo mimi na vyakula anavyokula hupangiwa na si kupanga mimi."
"Mmh! Ipo kazi sasa unataka kufanya nini?"
"Kwa kweli ndoa yangu haina raha kabisa imekosa amani kabisa, ukimuona mume wangu mbele za watu ana heshima kubwa lakini ndani hana lolote."

"Sasa tufanye nini ikiwa unasema vitu vingi vinapangwa kufanyiwa mumeo na si amri kutoka kwako?"
"Nasikia wewe ni mtaalamu mkubwa wa matatizo ya wanawake hivyo naomba msaada wako kwani nimekuwa nikitoka nje ya ndoa yangu kuitafuta starehe ambayo sikupenda kuipata nje zaidi ya mume wangu."
"Tatizo hilo mume wako analijua?"
"Analijua lakini hataki lijulikane kwa watu zaidi ya kuwa siri yetu wawili."
"Lina muda gani?"

"Mmh! Tangu alipoukwaa uheshimiwa."
"Kwani wewe ni mke wa nani?"
"Wa kiongozi wako wa nchi."
Kauli ile ilinishtua na kujiuliza ina maana kiongozi wangu wa nchi ndiye mwenye tatizo zito kama lile. Nilijikuta nikitetemeka baada ya kujikuta nikiwa mbele ya mke wa mkuu wa nchi. Baada ya kuyagundua mabadiliko yangu alinituliza.

"Mzee wangu punguza presha upo huru kutoa msaada wowote kwangu nakuahidi kukupa chochote ukitakacho ili kutatua tatizo hili. Nisingekuwa mke wa mheshimiwa wala nisingesumbuka kuja huku ningeendelea na kidumu changu."
"Unasema wewe mke wa mheshimiwa unawezaje kutoka nje ya ndoa yako?"
"Mara nyingi hutumia mlinzi wa mume wangu ambaye naye huficha siri hii, naamini kabisa penzi halina siri wasiwasi wangu mume wangu akigundua natembea na mlinzi wake anaweza kumuua na pengine mimi kuingia katika kashfa."
"Umesema mumeo anatambua tatizo lake?"
"Ndiyo."

"Amelishughulikia vipi?"
"Kila akirudi ziara zake huja na dawa za kumeza lakini hazimsaidii lolote, nimemueleza ajaribu miti shamba amekataa kwa vile anaamini waganga wa mjini ni waongo."
"Tatizo lipo katika kumpa dawa kwa vile asilimia ya chakula chote kinatayarishwa katika umakini wa hali ya juu hivyo dawa zetu hazina nafasi."

"Huna dawa hata ya kumpaka sehemu zake za siri usiku akiwa amelala nimpake?"
"Mmh! Dawa hiyo ni nzuri kama mwenyewe anatambua kwa vile kuna dawa nyingine ya mizizi nakuambia akinywa lazima akeshe juu ya kifua."
"Sasa huko si kukomoana hata raha ya mapenzi haitakuwepo?"
"Itakuwepo kwa vile umekosa raha hizo kwa muda mrefu nawe hutataka ateremke upesi kwani kuna dawa nikikupa itakuongezea hamu ya mapenzi."

"Si unipe."
"Tatizo la dawa ile unamchua mpaka bakora inasimama hapo mnaanza mapenzi kwa wiki tatizo lote linakwisha kabisa."
"Mmh! Kwa njia hiyo haitawezekana kama nilivyokueleza bado anaamini dawa za kizungu zitamponya."
Nilitulia kwa muda na kuwaza jinsi ya kumsaidia mke wa mkuu wa nchi ambaye aliamua kujivua nguo mbele yangu ili kupata tiba ya mumewe kuishiwa nguvu za kiume. Dawa iliyokuwepo ilikuwa ya kuingiza sehemu za siri ambayo ingemsaidia pale anapokutana na mumewe bakora isiweze kupoa haraka.

Niliamini kwa vile anatoka nje ya ndoa yake na mlinzi wa mumewe basi angetumia dawa ile wakati wa kuiba basi yule mwanaume aitumie kisha aweze kwenda kukutana na mumewe.
Japokuwa ilikuwa dawa ambayo inatakiwa kutumiwa na watu wanaotaka kutatua tatizo kwa makubaliano kwa vile hakukuwa na jinsi niliamua kutumia njia ile kuokoa ndoa ya mke wa mkuu wa nchi.
"Sasa mama kuna dawa moja ambayo nina imani inaweza kukusaidia."
"Dawa gani hiyo?"

"Kuna dawa nitakupa kabla ya kukutana na mumeo inatakiwa uiingize ndani kwa kumtumia mwanaume, kama mumeo angekuwa yupo tayari wala usingepata shida ungempaka na yeye kuingiza ndani ingewasaidia, lakini kwa vile hataki kutumia dawa tunazoziamini zitamaliza tatizo itabidi ujitahidi siku ya kukutana na mumeo uanze kukutana na mlinzi wake ili kuingiza dawa ndani."
"Mmh! Si nitaonekana nimetumika?"
"Hapana, ataingia taratibu bila kufika mwisho ili kuingiza dawa tu kisha unakwenda kukutana na mumeo bila kuonesha kasoro yoyote."

"Mmh! Sasa hivi siwezi kufanya hivyo, huwa nakutana naye kwa siri sana."
"Sasa tutafanyaje?"
"Nakusikiliza wewe."
"Hakuna njia yoyote, labda awepo mtu mwingine bila hivyo dawa hiyo itashindikana."
"Kwa kweli sina, kama unavyojua mimi ni mke wa mheshimiwa natakiwa kujiheshimu sana siwezi kuutoa mwili wangu ovyo."

"Mmh! Kuna njia moja ambayo nimewasaidia wanawake wengi waliokuwa na wanaume wabishi kama mumeo...lakini kwa wewe siyo nzuri."
"Jamani mganga nisaidie na mimi nipo tayari kufanya unavyotaka ili kuishi katika ndoa ya furaha. Nitakupa hata zawadi ya nyumba na gari nisaidie mganga," Mke wa mheshimiwa alisema huku akionesha dalili za machozi kuonesha tatizo lake ni zito sana.

"Mara nyingi nimekuwa nikiwawekea mwenyewe na mwisho wa siku ndoa zao zimesimama. Lakini kwa vile wewe mke wa mtu mkubwa siwezi, nakuheshimu pia namuheshimu mkuu wa nchi."
"Mganga ukuu ni cheo lakini ubinaadamu uko palepale, raha anazozipata mke wa mheshimiwa hazipishani na mtu wa kawaida hata maumivu ya moyo ni yaleyale wote tuna moyo wa nyama. Naomba nami unisaidie."
"Naweza kukusaidia lakini naona kama utajishushia heshima."
 
JOTO LA MAPENZI-17

ILIPOISHIA

"Mganga ukuu ni cheo lakini ubinaadamu uko palepale, raha anazozipata mke wa mheshimiwa hazipishani na mtu wa kawaida hata maumivu ya moyo ni yaleyale wote tuna moyo wa nyama. Naomba nami unisaidie."
"Naweza kukusaidia lakini naona kama utajishushia heshima."
ENDELEA..."


Heshima gani hiyo unayonipa ni tiba na si kutoka nje ya ndoa yangu, tena ukinipatia leo itakuwa vizuri nikitoka hapa nikakutane naye kwa vile kesho asubuhi ana safari ya nje ya nchi peke yake."
"Mmh! Hakuna tatizo."


"Basi nifanyie ili niwahi kuondoka."
Sikuwa na jinsi nilimfanyia ile dawa ambayo ilikuwa ni sawa na kuzini naye, kwa kweli muda wote nilikuwa natetemeka kutokana na sifa za mwanamke yule. Lakini muda wote alinitia moyo na kuweza kumfanyia ile dawa. Ajabu wakati namfanyia ile dawa alinogewa na kung'ang'ania niendelee ili afike mwisho asingeweza kuniacha hivihivi huku anateseka.


Nami kwa uchu wa kula vya wakubwa niliendelea na kugeuka kuwa mapenzi badala ya tiba. Baada ya kuchukua muda mrefu alionesha kuchoka kiasi cha kusema hawezi tena kukutana na mheshimiwa kwa vile alikuwa amechoka. Nilijawa na wasiwasi wa ajabu wa kujiuliza akifika kwa mumewe na kutaka kuagwa itakuwaje. Kabla ya kuondoka alitoka hadi kwenye gari lake na kurudi na fedha ambazo kwa kweli zilikuwa nyingi. Alinikabidhi na kunieleza kitu:


"Mganga katika siku ambazo nimefurahi leo nimefurahi sana, nina imani utazidi kunifurahisha. Ahadi yangu ya nyumba na gari ipo palepale nakuahidi kuyabadili maisha yako kwa muda mfupi."Niliagana na mke wa mheshimiwa ambaye alirudi ikulu na kuniacha na maswali kibao kuhusu furaha yake ni kupewa dawa au alikuwa na mengine. Kingine kilichonishangaza ni king'ang'anizi cha mke wa mheshimiwa lakini ile hali hakuwa wa kwanza, kila mwanamke niliyempatia tiba ile hakutaka kuonja alitaka kula kabisa.


Niliziangalia fedha zilizokuwa nyingi sana, na kujiuliza ni dawa au penzi ndilo lililomchanganya. Wasiwasi wangu kuingia katika mapenzi na kusahau dawa. Niliamini kama itakuwa vile ningeyaweka maisha yangu rehani kifo kilikuwa usoni kwangu kwani mkuu wa nchi asingekubali fedheha ile.


"Baada ya kuondoka niliomba Mungu dawa niliyompatia ifanye kazi ili aweze kuishi na mumewe pia nipate zawadi aliyoniahidi ya gari na nyumba. Siku ya pili niliendelea na kazi zangu kama kawaida za kutibu wagonjwa. Mjukuu wangu nilikuwa na uwezo mkubwa sana wa kutibu magonjwa mbalimbali hata huu ukimwi nilikuwa naijua dawa yake japo toka nifike huku mti huo sijauona japo nimejitahidi kuutafuta sana kama ningeupata nina imani sasa hivi ningekuwa milionea kama Babu wa Samunge.


"Basi mjukuu wangu baada ya kazi yangu ya kutwa nzima usiku nikiwa nimejipumzisha kwenye mkeka nje ya nyumba yangu. Mara alikuja kijana aliyekuja na mke wa mheshimiwa jana yake usiku na kunieleza mke wa mheshimiwa ananiita. "Kibaya alisema amenifuata anipeleke ikulu, ilikuwa ajabu kwangu sikuwa na wazo hata la kuota ndotoni kuingia ikulu."


"Jamani kwani kuna tatizo gani?" Niliingiwa wasiwasi huenda siri ilikuwa imevuja.
"Hakuna tatizo lolote ila ametutuma tukufuate pia uende na dawa ya jana."
"Dawa! Dawa gani?""Hilo swali unatuuliza sisi, wewe ndiye unayejua hiyo dawa ya jana," alinijibu na kuamini kweli swali lile lilikuwa halimuhusu.


"Mtukufu Rais yupo?" niliuliza.
"Ameondoka leo asubuhi ana ziara ya nje ya nchi ya wiki mbili."
"Mbona hakuondoka na mkewe?""Sasa hayo maswali kamuulize mwenyewe," kila jibu lilionesha kuuliza maswali yasiyowahusu, yote ilitokana na wasiwasi wa tukio la jana yake la kutembea na mke wa rais.


"Lakini jamani kuna usalama?" nilikuwa na wasiwasi kwa kuamini ule ni mtego na kujikuta nikilaumu kwa kufanya mapenzi na mke wa mheshimiwa rais. Nilikumbuka taarifa za mtu mmoja alimpa mimba binti wa rais alipotea katika mazingira ya utatanishi. Habari za juujuu zilisema yule mtu aliuawa na vijana wake.


Hapo ndipo woga ulipozidi kuniingia na kuamini kama mwanaye alipopewa mimba alitoa hukumu ile kwa mimi niliyetembea na mkewe kwa nia ya kuiokoa ndoa yake ingekuwaje. Mara nyingi nilikuwa nikipenda mtu aje na mume au mke wake ili niwape dawa ambayo ingewasaidia kuokoa ndoa yako kwa kushirikiana pamoja.


Lakini wengine ambao waume zao waliokuwa wabishi niliamua kuwasaidia. Wasiwasi wangu mkubwa kuukwaa kwani dawa ile ilitakiwa iingizwe bila kuvaa mpira. Nikiwa katika lindi la mawazo nilishtuliwa.
"Sasa unakwenda au huendi?"


"Lakini jamani kwa nini hakuja huku?"
"Mzee tunaona unaleta utani hebu chukua hiyo dawa mara moja na tuondoke sasa si ombi bali amri."
Kauli ilizidi kunichanganya na kujua kabisa moto umewaka ikulu nilikuwa napelekwa kuhukumiwa kifo kibaya.


Nilichukua dawa ambazo hata sikujua ni za nini. Pia niliamuriwa kuvaa nguo zenye hadhi ya kuingia ikulu, pamoja na kazi yangu ya uganga nguo za kutokea nilikuwa nazo. Kila nilipokuwa nimevaa nguo za kiafisa wateja wangu wote walinipotea ilikuwa mpaka nijitambulishe kuwa mimi ndiye fulani.
 
JOTO LA MAPENZI-18

ILIPOISHIA

Kauli ilizidi kunichanganya na kujua kabisa moto umewaka ikulu nilikuwa napelekwa kuhukumiwa kifo kibaya. Nilichukua dawa ambazo hata sikujua ni za nini. Pia niliamuriwa kuvaa nguo zenye hadhi ya kuingia ikulu, pamoja na kazi yangu ya uganga, nguo za kutokea nilikuwa nazo. Kila nilipokuwa nimevaa nguo za kiafisa walinipotea, ilikuwa mpaka nijitambulishe kuwa mimi ndiye fulani. ENDELEA...


Baada ya kutia suti ya bei mbaya ambayo ilimshangaza aliyenifuata, nilichukua na baadhi ya tunguli na nguo za uganga ambazo niliziweka ndani ya mfuko na kuingia kwenye gari na kupelekwa moja kwa moja ikulu.
Nilipofika nilipitishiwa mlango wa uani bila mtu yeyote kujua kama nimeingia na kupelekwa kwenye chumba kimoja kilichokuwa na vitu vya thamani ambavyo sikuwahi kuviona kwa macho au kuvikalia.


"Karibu," yule aliyenipeleka alisema kwa sauti ya upole tofauti na amri aliyonipa kwenda kwa nguvu ikulu.
"Asante," nilijibu kwa sauti ya chini huku mapigo ya moyo yakiwa bado yapo juu.
"Unatumia kinywaji gani?"
"Chochote."
"Pombe unatumia?"
"Hapana."


"Okay, nakuja."
Aliondoka yule kijana na kuniacha nikiwa na mawazo huenda kamfuata mheshimiwa ili aje aniulize kisa cha kutembea na mkewe ni nini. Wakati nikijua kabisa ni mke wa rais. Lakini nilipanga kujitetea kutokana na maelezo ya mkewe huku nia yangu ikiwa kuiokoa ndoa yake wala si kufanya mapenzi na mkewe.


"Lakini nilipingana na wazo lile niliamini kama ni kukubali kidhibiti cha wizi, wazo lingine lilinieleza nikane mpaka kufa kuwa sijafanya mapenzi na mkewe zaidi ya kumpa dawa ya kutatua matatizo yake. Swali likaja hilo tatizo litakuwa tatizo gani ambalo litaonesha sikufanya ngono na mke wa rais.


"Kwa kweli nilikuwa kwenye wakati mgumu maishani kwani kila nililofikiria kwangu lilikuwa zito ambalo halikuwa na jibu na kuyafanya mapigo ya moyo kuyasikia kwa nje yakidunda na kijasho kilianza kunitoka japo kulikuwa na kiyoyozi kikali.
"Karibu," mbele yangu alisimama msichana aliyekuwa amebeba sinia lililokuwa na glasi yenye juisi ya embe.
"Asante." Niliipokea glasi kisha yule msichana alivuta stuli iliyokuwa pembeni kidogo na kuiweka mbele yangu ili nikinywa nirudishe juu yake.


"Unaweza kuendelea," yule msichana alisema huku akiondoka.
"Hakuna tatizo," nilijibu huku nikipeleka glasi ya juisi mdomoni na kupiga fundo moja ili kulainisha koo lililokuwa limekauka kwa hofu ya kuingia ikulu pia kukutana na maswali ya mheshimiwa juu ya mkewe kuja kwangu usiku wa jana yake.


Juisi ilikuwa tamu sana, lakini kwa hofu utamu ulikuwa mwanzo lakini kilichofuata sikujua ni utamu au nini zaidi ya kuendelea kuomba Mungu aniokoe kwenye kinywa cha mauti ambacho kuokoka kwake niliona sawa na ngamia kupita kwenye tundu la sindano.


Juisi sikuigeuza kama kinywaji cha mgeni bali kilainisho cha koo kutokana na hofu kuu iliyonitanda kwa kuhofia maisha yangu. Juisi ilikwisha na kuendelea kulainisha koo kwa mate ili lisikauke zaidi hata kushindwa kujibu maswali ya mheshimiwa rais.


Nikiwa katikati ya maswali yasiyo na majibu huku nikijilaani mwenyewe kwa kukubali kuwa mganga wa kienyeji na kukataa kuendelea na masomo ili niwe Injinia. Mara alitokea mke wa rais kwenye tabasamu pana na kunifanya nishtuke mara mbili na kufanya nizidi kukaukiwa na maji mwilini kutokana na kuvujwa na jasho la hofu.
"Ooh! Mganga karibu."


"A..a..sante," nilijibu kwa wasiwasi kitu alichokigundua mke wa mheshimiwa.
"Jamani Yamungu mbona kama hujiamini, hebu jiamini upo salama kufanya chochote bila kuingiliwa na mtu."
"Vipi mzee yupo?"
"Si nilikueleza anasafiri leo."


"Ooh! Nilisahau," nilijifanya nimesahau ili kupata ukweli zaidi.
"Wala hujasahau ni wasiwasi wako wa kujihami," mke wa rais alinizodoa.
"Si unajua sehemu hizi zinatisha huwezi kuingia kichwakichwa hasa sehemu tukufu kama hizi."
"Hii ni sehemu ya kawaida mtu yeyote anaweza kukaa, hata mimi sikuota kuna siku nitaishi hapa."
"Mmh! Tatizo nini tena?" nilijitahidi kuzungumza kwa kujiamini.


"Kabla sijakueleza tatizo langu nataka kukusifia kwa kupendeza kama tungekutana sehemu nyingine nisingekufahamu."
"Nashukuru kwa hilo.""Sasa kama nilivyokueleza ahadi yangu ya zawadi ya gari na nyumba ipo palepale kabla mzee hajarudi nataka niwe nimeitimiza."


"Vipi jana aliomba?"
"Aombe wapi, nilipofika nikisingizia kichwa, mara nyingi huwa hanigusi nikiumwa hata mafua."
"Mmh! Tatizo nini?"
"Naomba unifuate."


Sikuwa na jibu nilipitia mkoba wangu wenye tunguri ili nimfuate nao.
"Huo mkoba wa nini?"
"Wenye dawa."


"Achana nao, njoo mwenyewe."
Niliuacha mkoba na kumfuata, nilishangaa nikiingia hadi chumbani na kujiuliza nakwenda kufanya nini. Nilipofika nilikaa kwenye sofa lililokuwa pembeni ya kitanda cha thamani.
 
JOTO LA MAPENZI-19

ILIPOISHIA

“Mmh! Tatizo nini?”
“Naomba unifuate.”
Sikuwa na jibu nilipitia mkoba wangu wenye tunguri ili nimfuate nao.
“Huo mkoba wa nini?”
“Wenye dawa.”
“Achana nao, njoo mwenyewe.”
Niliuacha mkoba na kumfuata, nilishangaa nikiingia hadi chumbani na kujiuliza nakwenda kufanya nini? Nilipofika nilikaa kwenye sofa lililokuwa pembeni ya kitanda cha thamani.
ENDELEA...


“Hapa wapi?” niliuliza baada ya kuiona picha ya mtukufu rais juu ya meza ndogo akiwa na mwanaye mdogo.
“Wasiwasi wako nini?”
“Nauliza tu.”


“Naomba maswali hayo uniulize baada ya kufanya kazi niliyokuletea hapa.”
Sikuwa na swali zaidi ya kufuata yote atakayonielekeza.
Baada ya muda niliamuliwa kuvua nguo zote na kupewa taulo, nilizidi kuingiwa na wasiwasi kuna nini kinataka kufanyika. Baada ya kufanya vile na kujifunga taulo mke wa mheshimiwa naye alivua nguo zake mbele yangu na kujifunga upande wa kanga.


Baada ya hapo tulikwenda kuoga pamoja, pamoja na umbile lenye kila kishawishi la mke wa rais, upande wangu muda wote niliiomba miungu yote mheshimiwa rais asiahirishe ziara yake. Baada ya kutoka bafuni nilipandishwa kitandani pamoja na hofu niliyokuwa nayo, kutokana na umbile mantashau la mke wa rais nilijisahau na kufanyanaye mapenzi kwenye kitanda cha mtukufu rais kiongozi wa nchi ile.


Nilifanya anavyotaka, siku ile tulifanya mapenzi mpaka alfajiri ndipo nilirudishwa nyumbani na fedha kibao ambazo zilinipa hata uvivu kuhesabu. Huwezi kuamini, muda wote mheshimiwa rais alipokuwa nje ya nchi, nililala kitandani kwake na mkewe huku akinisifia mimi ndiye mwanaume sahihi kwake na kuapa atahakikisha anayabadili maisha yangu lakini kwa sharti la kuacha kazi ya uganga kwa kuhofia ningeendelea kugawa dozi ile kwa wanawake wengine.


Kwa ahadi aliyoniahidi niliamini kazi ya uganga ilikuwa haina faida yoyote kwangu kwani ningeishi nusu ya peponi. Mke wa rais alitimiza ahadi yake kwa muda mfupi, alininunulia eneo nje kidogo ya mji na kunijengea jumba la kifahari lililonifanya nionekane mtu mwenye uwezo mkubwa na hata hadhi yangu ilipanda mara dufu na kuonekana nilikuwa miongoni mwa matajiri.


Ili nionekane nina fedha za kutosha, mama alininunulia gari la milioni mia mbili hamsini. Wakati huo kazi ya uganga niliachana nayo na kuwa chombo cha starehe cha mke wa mheshimiwa. Ilikuwa kila mheshimiwa aliposafiri na kumuacha mkewe, mimi ndiye niliyekuwa mkuu wa nchi kwa kummiliki mkewe.


Siku zilikatika huku mwanaume nikiendelea kula matunda ya uhuru, maisha yangu yalikuwa chini ya ulinzi mkali kuliko kawaida sikuwa tofauti na mkuu wa nchi. Mke wa mheshimiwa aliniwekea walinzi ambao muda wote nilitembea nao kuhakikisha usalama wangu.


Siku zote moto haufunikwi na shuka lazima shuka litaungua na moshi kusambaa na watu lazima watajua pale kuna moto. Siku moja mke wa mheshimiwa alikuja na kunieleza ana ujauzito.
“Yamungu nina ujauzito.”
“Eeh!” nilishtuka.
“Unashtuka nini?”
“Aa...aah.”


“Sikiliza Yamungu ujauzito huu japo sijajua ni wa mheshimiwa au wako lakini usikupe wasiwasi.”
“La...la...kini si...si... unakumbuka mtu uliyekutana naye ukiwa katika siku za hatari?”
“Ni wewe.”
“Kama ni mimi itakuwaje?”
“Kitanda hakizai haramu, wasiwasi wako nini?”


“Mmh! Wapambe wanaweza kuchongea wakiona ninafanana naye.”
“Hakuna wote ninaowatumia ni watiifu sana kwangu pia nawalipa vizuri sana hawawezi kunisaliti.”
“Usimuamini mwanadamu ni kiumbe mbaya kuliko kiumbe chochote kilichoumbwa na Mungu kuliko hata shetani.”
“Si kwa hawa, nawaamini sana.”
“Mmh! Tutaona.”


Baada ya taarifa ile ilipita siku kama kumi na nne au sita, siku moja nikiwa natoka mjini msafara wangu ulivamiwa na watu waliokuwa na silaha huku wamefunikia sura zao na kuanza kutushambulia. Kwa kweli ilikuwa vita kubwa ya kutupiana risasi.


Walinzi wangu wote waliuawa na mimi kukamatwa sikujua napelekwa wapi, nilifungwa kitambaa usoni na kutupiwa kwenye gari lililoondoka kwa kasi. Baada ya mwendo mrefu lilisimamishwa na kuteremshwa chini nikiwa bado nimefungwa kitambaa na kamba niliyofungwa mikono kwa nyuma.


Baada ya muda nilifunguliwa kitambaa usoni na kujikuta nimesimama mbele ya watu zaidi ya wanne wakiwa wameficha nyuso zao, sehemu yenyewe ilikuwa ni kichakani kwenye miti na majani mengi.
Sehemu ile ilionesha ni nje ya mji, nilijiuliza watu wale walinipeleka kule kufanya nini ikiwa pamoja na kuwaua walinzi wangu wote wanne. Mmoja alisema kwa sauti nzito:


“Anko umeacha uganga unakula vya wakubwa,” kauli ile ilifanya moyo upasuke na kujua nimekwisha, niliona siri imevuja.
“Mzee alisema tumpe adhabu gani?” mmoja aliuliza.
“Kwa vile ametembea na mkewe akatwe uume wake,” toba! Nilijua nitakufa kifo kibaya sana.
“Baada ya adhabu hiyo tumfanye nini?”


“Kwa vile hapa ni mpakani tumtupie upande wa pili akafie mbali.”
“Lakini kwa nini tusimuue kabisa kuliko kumtesa? nashauri tumuue kisha turudi zetu.”
“Lakini kumbuka mzee amesema turudi na uume wake auweke ndani mwake kama kumbukumbu ya mume mwenzie.”
Mazungumzo yale yalinikatisha tamaa na kuamini sikuwa na njia ya kupona zaidi ya kuhesabu sekunde kusubiri kifo changu. Mmoja alinisogelea na kunivua nguo zote na kuniacha mtupu kisha aliomba kisu ili anikate uume. Wakati akinishika sehemu za siri huku akisema kwa kejeri:


“Eeh! Hii ndiyo iliyompagawisha mke wa rais? Haya ngoja tuikate akanywe supu yake, Oyaa lete hicho kisu tumalize kazi,” alisema jamaa aliyeonekana kujaa ukatiri.
“Naona umeshikilia kama unataka kuchinja kuku?” alisema mwenye kisu aliyekuwa akimpelekea.


“Jamaa anatisha kutoka uganga wa kienyeji mpaka mume mwenza wa rais?”
Jamaa alionekana kunikejeri, niliona kwa nini nife bila kujitetea niliwaomba msamaha.
“Jamani ninyi ni wanaume wenzangu, heri mniue kisha mnikate sehemu zangu za siri, au kama waungwana mngeniachia nikatokomea zangu
 
JOTO LA MAPENZI-20

ILIPOISHIA

"Jamaa anatisha toka mganga wa kienyeji mpaka mume mwenza wa rais."
Jamaa alionekana kunikejeli, niliona kwa nini nife bila kujitetea niliwaomba msamaha.
"Jamani ninyi ni wanaume wenzangu heri mniue kisha mnikate sehemu zangu za siri, au kama waungwana mngeniachia nikatokomea zangu."
ENDELEA NAYO..."


Wazo la kwanza kwangu nimeliunga mkono, ila la pili kwa kweli itakuwa ngumu, sisi hatujui lolote ila mwenye mali katutuma. Heri mngefanyia uchafu wenu nje, lakini wewe na mpuuzi mwenzako mlivuka mipaka na kuamua kumdhalilisha mke wa rais kwa kufanya uchafu wenu ikulu tena kwenye kitanda cha mtukufu rais hii ni dharau isiyovumilika.


"Tena adhabu aliyokupa ni ndogo lakini mimi nikakuongezea nyingine kwa kukutoboa macho na kukukata ulimi huwezi kulidhalilisha taifa letu, kingine kibaya kumbe wewe si raia wa nchi hii," jamaa mmoja alisema kwa hasira kuonesha kitendo changu cha kulala na mke wa rais ikulu tena kwenye kitanda chake kilimuuma sana.


"Jamani basi tumalize kazi ili turudishe ripoti kwa mtukufu rais," mmoja aliyekuwa ameshikilia bunduki kubwa yenye risasi kama mkanda ambazo kwangu niliwahi kuiona kwenye sinema.
"Sinde lazima tumweleze ubaya wake hata akifa ajue amekufa kwa kosa gani."
"Lakini basi tu kwa vile ni mkuu ameamua lakini siamini kama jamaa huyu alimtongoza mke wa mheshimiwa. Ndiyo maana unaambiwa mwanamke si kiumbe cha kuaminiwa. Sasa alikosa nini kwa mheshimiwa mpaka atembee na mganga wa kienyeji?"


"Jamani sasa hivi si mganga bali pedeshee wa mjini nyumba anayoishi mmeiona na gari analotumia yote hela zetu walala hoi. Nasikia jamaa ni mtaalamu wa kitandani mke wa mheshimiwa alipanga kumnunulia ndege ya kutembelea."
"Mmh! Jamaa atakufa na kuacha mambo mazuri, lakini isiwe mheshimiwa mtoto wa watu?"
"Mmh! Hayo hayatuhusu hebu tutimize tulichotumwa na mkuu kisha tukaendelee na kazi nyingine."
"Mimi nina wazo," jamaa aliyekuwa na bunduki kubwa alisema na kuwafanya wenzake wamsikilize.


"Jamani nataka kuwaeleza kitu, naomba huyu jamaa tumuache salama na tukifika kwa mkuu tumwambie tumemuua na kusahau kuzikata sehemu za siri."
"Wazo gani la kijinga hilo, mtu huyu si wa kuachiwa, amemdhalilisha rais na sisi wananchi wake. Lazima afe kifo kibaya ambacho hakijawahi kuonekana tangu dunia ilipoumbwa. Tena nitaongeza nyingine nitampigilia kipande cha mti nyuma na kumwacha akifa kwa maumivu."


"Nasema hivi huyu mzee haguswi na mtu na atakayejitia kiherehere atanitaka lawama nitafunua kichwa chake, Moo kwanza mwache mzee huyu na urudi nyuma," nilishangaa jamaa mwenye bunduki kubwa kuwa mteteaji wangu mkubwa.
"Sa..sa..sa inakuwaje?" jamaa aliuliza huku akimtazama jamaa.


"Bwana eeh, usitutishe fanya lolote utakalo lakini lazima jamaa afe," jamaa aliyekuwa na roho mbaya kuliko wote bado alionyesha ubishi akitaka kunitia adabu."Moo sitanii ukinyanyua mguu tu nakulipua," mtetezi wangu alisema kwa sauti isiyotaka mzaha.


Moo aliona utani alinyanyua mguu ili anifuate lakini alirudishwa na risasi iliyotua kichwani na kumrusha nyuma. Wote tuliokuwepo pale tulishtuka, akiwa amevua soksi iliyomziba uso alisema:
"Na nyinyi wenye kiherehere sogeeni huku na mikono muweke juu."
Wenzake walifanya alivyowaamrisha, nilishangaa yule jamaa kunitetea kama ndugu yake wa tumbo moja. Baada ya jamaa zake kusogea mbele na kunyanyua mikono juu aliwageukia na kuwaeleza.
"Haya geukeni nyuma na mnipe visogo."


Walifanya alivyowaagiza, sikuamini nilipomuona akinyanyua bunduki usawa wa bega na kuwamiminia risasi za vichwa wenzake wawili na kuwaulia mbali. Kila kilichofanyika nilishindwa kuelewa yule alifanya vile kwa sababu gani, baada ya kuwamaliza wote alinigeukia na kunisemesha japo nami nilikuwa nimeanza kumuogopa.


"Sikiliza ndugu yangu wewe kwangu ni muhimu sana, umenisaidia vitu vingi sana wakati ukiwa mganga. Umemtibu mtoto wangu aliyeteseka miaka kumi, umemtibu mama yangu aliyekuwa kitandani miaka sita. Pia umenisaidia kupata cheo jeshini baada ya wabaya wangu kuifunika nyota yangu. Siyo hayo umeweza kufungua kizazi cha mke wangu kilichofungwa na ndugu zake sasa hivi tuna watoto mapacha kwa hayo uliyonitendea sipo radhi kukuona ukifa mbele yangu nipo radhi kufa mimi si wewe."


"Asante sana."
"Sasa ndugu yangu nakuomba uvuke mpaka na uende mbali sana najua baada ya vifo hivi watakutafuta."
"Na wewe je?"
"Mimi usiwe na wasiwasi nitajua nitakavyofanya."


Nilivaa viatu vya marehemu mmoja vilivyokuwa imara kwa ajili ya safari ya kutembea msituni. Alitaka kunipa silaha niliikataa kwa vile nilikuwa sijui kuitumia.
Alinipa fedha nyingi na kunitakia safari njema, mpaka tunaachana sikuamini kama kweli nimeokoka kwenye kinywa cha mauti. Basi mjukuu wangu baada ya kuokoka na kuvuka mpaka kwa njia za panya nilitembea kwa muda wa wiki nzima bila kupumzika kwa kuhofia huenda ungefanywa msako wa kunitafuta na kuingia upande wa pili na kuniona."
"Unataka kuniambia ulitembea wiki nzima bila kupumzika?" Ambe alimuuliza mzee Yamungu ambaye muda ule alionekana ni mtu aliyekuwa amekula chumvi nyingi.
 
JOTO LA MAPENZI-21

ILIPOISHIA

Alinipa fedha nyingi na kunitakia safari njema, mpaka tunaachana sikuamini kama kweli nimeokoka kwenye kinywa cha mauti. Basi mjukuu wangu baada ya kuokoka na kuvuka mpaka kwa njia za panya nilitembea kwa muda wa wiki nzima bila kupumzika kwa kuhofia huenda ungefanywa msako wa kunitafuta na kuingia upande wa pili na kuniona."
"Unataka kuniambia ulitembea wiki nzima bila kupumzika?" Ambe alimuuliza mzee Yamungu ambaye muda ule alionekana ni mtu aliyekuwa amekula chumvi nyingi.
ENDELEA NAYO...


"Kijana wangu asikuambie mtu maisha huwa matamu utakapojua kuna mtu anataka kuyakatisha, unaweza kuvuka hata mto wenye mamba bila kudhuriwa na mamba yoyote."
"Kwa hiyo ulitembea wiki nzima bila kupumzika?"
"Ndiyo."


"Mmh! Baada ya kutembea wiki nzima ulifika wapi?"
"Nilitokea sehemu hii ambayo ilikuwa na mfereji wa kupitisha maji niliamini sehemu hii inanifaa kukaa."
"Sasa babu chakula ulipata wapi?"
"Niliishi kwa matunda na majani."


"Mmh! Naona sasa hivi una shamba kubwa, mbegu ulipata wapi?"
"Nilikaa kwa muda wa mwezi mmoja kutuliza akili yangu kwani muda wote sikujiamini. Baada ya kuamini nipo salama nilianza kwenda kutafuta miji ya watu baada ya kusikia sauti za gari na kuamini makazi ya watu yapo jirani. Nilisogea hadi barabarani na kukuta kuna maduka kwa vile nilikuwa na dola sikuweza kupata huduma mpaka walipopita watu wanaojua dola ni nini. Baada ya kununua vitu muhimu nilirudi kwangu ambako niliamini ni sehemu iliyokuwa salama kwa kuhofia picha yangu kutangazwa kwenye vyombo vya habari na kukamatwa."


"Kwa hiyo kama mke wa rais alijifungua salama una mtoto huko ulipotoka?"
"Sijui, kama alizaliwa au hakuzaliwa."
"Hivi ukikutana na huyo mwanamke itakuwaje?"


"Sitaki hata kumuona yeye ndiye chanzo cha kunifanya niishi maisha ya watu wa kale."
Baada ya mazungumzo marefu mzee Yamungu alitoka na kwenda nyumba ya pili ambako alikuwa na mgonjwa. Baada ya kuondoka alimwacha Ambe amejilaza na kuanza kumuwaza mpenzi wake Koleta ambaye mpaka anaingia gerezani hakuwa na habari zake baada ya kutoroka kwao akiwa mjamzito kwa muda ule kama angekuwa hai na amejifungua salama mwanaye angekuwa mkubwa.


Alijiuliza kama mpenzi wake na mwanaye wakifariki angemfanya nini mzee Mtoe. Aliuapia moyo wake kama mpenzi wake alijitoa kwa ajili na kuwa radhi kwa lolote na yeye aliapa siku akikutana naye atahakikisha anarudi gerezani kwa kosa lingine la kuua na kuwa tayari kunyongwa na kumfuata mpenzi wake na mwanaye.


Kwa vile aliamini kutoka pale ingechukua muda, hivyo hakutaka kuchokoza mambo. Siku nazo zilikatika Ambe akiendelea kuishi maisha kama mkimbizi wa kivita aliyekuwa akitafutwa na mahakama ya makosa ya kihalifu ‘The Hegue'. Usiku aliweza kutoka nje na kuiona dunia.


Muda wote alioishi pale hakunyoa nywele na ndevu na kuonekana kama mzee sana, mtu kumfahamu mara moja ilikuwa vigumu. Hali aliyojiweka ilimwezesha kutoka nje hata kumsaidia kazi za shamba mzee Yamungu. Katika siku zote zile hakubahatika kumuona mgonjwa aliyekuwa katika nyumba ya majani.


Kila alipomuuliza kuhusu mgonjwa alielezwa asubiri apate nafuu, alijiuliza huyo ni mgonjwa gani asiyetoka nje. Siku moja hakutaka kwenda shamba kwa kuwa alikuwa hajisikii vizuri, baada ya mzee Yamungu kuondoka aliamua kuingia ndani kuangalia mgonjwa yupo katika hali gani.


Alifungua mlango taratibu na kuingia ndani, mbele yake kwenye kitanda cha kamba kulikuwa na mtu amelala bila nguo na sehemu kubwa ya mwili wake ulikuwa umewekwa majani yaliyosagwa. Mtu aliyekuwa amelala kitandani alionesha kama mfu kwani hakuwa akijitikisa hata kidogo.


Alimsogelea taratibu kumuangalia usoni, alipomtazama yule mtu usoni kidogo apige kelele ya mshtuko, lakini alijizuia kwa kuuziba mdomo kwa mkono. Mapigo ya moyo yalimwenda mbio na kujiuliza anayemuona ni kweli ni yeye na kama ni yeye yupo hai au amekufa?


Huku akitetemeka na jasho la mshtuko kumtoka alisogea karibu zaidi ili kuhakikisha ni yeye. Sura ilikuwa ni ileile alipeleka mkono wake kwenye pua ili kusikia kama anavuta pumzi. Lakini hakukuwa na pumzi, alitaka kumshika moyoni ili kupata uhakika kama moyo unadunda. Lakini ilikuwa vigumu kwani sehemu ya kifuani ndipo palipokuwa na majani ya dawa ya kusagwa aliogopa kuyatoa.


Alitaka kumtikisa lakini moyo ulisita aliinama sehemu ya masikio na kuanza kumwita kwa sauti ya chini, lakini mtu yule hakuitikia. Aliamua kumtikisa huku akimwita jina lake lakini vilevile hakupata msaada wowote wa kuitikiwa au mtu yule kujitikisa.


Alijiuliza kama mtu yule amekufa mzee yule ana ajenda gani na mwili ule, alijiuliza mbona mara nyingi mzee Yamungu huingia na dawa kwenda kumkanda pia hata kutengeneza uji mwepesi. Hakutaka kukubaliana na mawazo yake kuwa mtu yule kafa.


Bado alijaa maswali kama anaumwa mbona ni muda mrefu amekuwa pale mgonjwa hajatoka nje wala kuonesha mabadiliko. Aliamua kutoka nje na kuufunga mlango na kwenda kukaa chini ya mti na kujikuta donda lililokuwa limepona limechubuliwa upya.


Sehemu ile aliiona chungu na kuamua kwenda shamba, alimkuta mzee Yamungu akiwa bize na palizi alipomuona alimuuliza:
"Vipi unaendeleaje?"
 
JOTO LA MAPENZI-22

"MMH! Kidogo sijambo nina imani nikifanya kazi ndogondogo mwili utachangamka, siamini kama ni ugonjwa huenda ni uchovu kama ulivyonieleza."



"Hakuna kingine ni uchovu jana tumefanya sana kazi."
Ambe aliingia kwenye kazi, lakini muda mwingi alikuwa hayupo pale zaidi ya kumfikiria mtu aliyemuona ndani ya kibanda. Kwake ingekuwa furaha ya ajabu kama mtu yule angekuwa mzima na kuwa muujiza wake wa kwanza toka asikie sifa za mitume waliotangulia kufufua wafu.


Kila dakika alishtuliwa na mzee Yamungu akiwa amejisahau kufanya kazi na kuhamia katika mawazo ya mtu aliyemuona chumbani. Mzee Yamungu aliamini kabisa Ambe anamuwaza mpenzi wake na mwanaye.
"Ambe leo mbona hauko vizuri?"
"Ni kweli mzee ndoto za usiku mzima zilikuwa kwa Koleta."


"Koleta ndiye nani?"
"Si mpenzi wangu, yaani nimemuota akizurura mitaani na mtoto mgongoni akiwa pekupeku kama mwendawazimu."
"Hizo ni ndoto tukirudi nyumbani nitamcheki kwenye mtandao wangu kujua yupo katika hali gani. Huenda amesharudi kwao na kuolewa na mtu mwingine."
"Mzee Yamungu hayo maneno gani?"


"Kipi cha ajabu kama wazazi wake watamweka chini na kuwaelewa akusubiri wewe, waumini wameshindwa kumsubiri Masia atakuwa yeye. Ambe huu si muda wa kumfikiria mwanamke kuwa sawa na mwanajeshi anapokuwa vitani huwa hawazi nyumbani zaidi ya kuwaza kumshinda adui. Kumbuka mpaka sasa hivi unatafutwa unatakiwa kujipanga ili kujua utawezaje kuishi maisha salama."


"Sawa Babu, lakini kumbuka yote haya ni kwa ajili yake."
"Sawa, lakini si kila upangalo hutimia, cha muhimu kwanza yaangalie maisha yako ili uweze kuyatafuta mengine, huwezi kuyatafuta mengine wakati yako hayajakamilika."


"Lakini babu nimeapa kama yule mwanamke atanigeuka na kuolewa na mwanaume mwingine bora tukose wote."
"Una maana gani?"
"Nitamuua na mimi nijiulie mbali."
"Mama yako yupo?"
"Nina imani yupo."


"Toka uzaliwe umemlipa nini?"
"Sijamlipa kitu."
"Kwa nini huo ujinga unaotaka kufanya ungemfanya mama yako apumzike na kutumia nguvu kutafuta."
"Lakini kumbuka chanzo cha kufungwa kwangu ni yeye."


"Hata kama ni yeye, lakini kumbuka mama yako anakuhitaji kuliko huyo mwanamke."
"Nimekuelewa."


Kwa vile muda ulikuwa umekwenda waliamua kurudi nyumbani, njiani Ambe bado kichwani alisukwasukwa na mawazo juu ya mtu aliyemuona mule ndani na kutamani kumuuliza lakini alihofia kuonekana alibaki ili kuingia mule ndani.




Baada ya kurudi nyumbani bado mawazo yalikuwa kwa mtu aliyemuona ndani, kila alipotaka kuuliza kitu moyo ulisita na kuonesha si muaminifu asiyetakiwa kuaminiwa. Aliamua kuteseka na donge zito moyoni mawazo yake aliamini mzee yule ni mchawi ambaye hata yeye anaweza kumfanyia kitu chochote.


Lakini wazo lile alilipinga kwa nguvu zote, lakini moyoni alipanga kuendelea kufanya upelelezi wake wa siri ili ajue mwisho wa yote kuna nini kuhusiana na ule mwili aliouona usio na uhai.


Kama kawaida usiku alikuwa akimsaidia mzee Yamungu kuandaa chakula cha usiku, naye mzee Yamungu aliendelea na kazi yake ya kila usiku ya kuchemsha maji ya moto ambayo huingia nayo kwenye kila kibanda. Baada ya chakula cha usiku mzee Yamungu alibeba kikombe cha uji na debe la kuchemshia dawa lililokuwa na maji ya moto na kuingia kwenye kibanda.


Ambe naye alijifanya kuingia chumbani kwake, baada ya muda alitoka taratibu na kunyata hadi nyuma ya banda aliloingia mzee Yamungu. Kwa vile lilikuwa la majani hakutumia nguvu nyingi kutaka kuona kilichomo ndani. Kwa vile nje kulikuwa na giza baada ya kupenyua majani ya ubavuni aliweza kuona kila kitu ndani kwa msaada wa mwanga wa kibatari alichokuwa akitumia mzee Yamungu.


Ndani alishuhudia mzee Yamungu akiondoa majani yaliyokuwa juu ya mwili wa na kuchua majani yaliyokuwa kwenye debe, yakiwa yanafuka moshi aliyatoa na kuukanda ule mwili ambao kwake aliamini haukuwa na uhai.
Alijikuta akiwaza vitu vingi kutokana na aliyoyaona yakifanywa na mzee yule. Alijiuliza kuukanda mwili usio na uhai alikuwa akimaanisha nini.


Aliendelea kutulia ili ajue mwisho, alimuona mzee yule maji yale ya moto akiukanda mwili ule kwa nguvu huku akiukandamiza kwa nguvu. Kitu kilichokuwa kitendawili kwa mzee yule na kujiuliza kufanya vile alikuwa na maana gani.
Baada ya muda aliugeuza mwili ule ambao bado aliamini hauna uhai na kuendelea kuukanda kwa maji ya moto.


Ambe alijiuliza kama mwili ule ungekuwa na chembe ya uhai ungeweza hata kujigeuza au kujitikisa kwani maji yale aliamini ni ya moto sana.Baada ya kuukanda mgongoni aliulaza tena chali na kuanza kukanda kiungo kimojakimoja kuanzia mikono kisha miguu. Baada ya kumaliza zoezi lile
 
JOTO LA MAPENZI-23

ILIPOISHIA

Baada ya muda aliugeuza mwili ule ambao bado aliamini haukuwa na uhai na kuendelea kuukanda kwa maji ya moto. Ambe alijiuliza kama mwili ule ungekuwa na chembe ya uhai ungeweza hata kujigeuza au kujitikisa kwani maji yale aliamini ni ya moto sana.
Baada ya kuukanda mgongoni aliulaza tena chali na kuanza kukanda kiungo kimojakimoja kuanzia mikono kisha miguu.
ENDELEA NAYO...


Baada ya kumaliza zoezi lile ambalo halikuonesha kuna dalili za uhai katika ule mwili, alitoa chupa ndogo iliyokuwa na unga mweupe na kuiweka ile chupa sehemu za puani kwenye ule mwili.


Kwa maajabu makubwa mwili ule ulipiga chafya mfululizo, pamoja na kuona vile bado aliona kama kiini macho baada ya kupiga chafya uliendelea kulala vilevile. Mzee Yamungu aliyeonekana yupo bize alichukua mafuta kwenye chupa na kuupaka mwili wote kisha alichukua uji uliokuwa kwenye kikombe na kuanza kuunywesha ule mwili kwa kijiko.


Baada ya kumaliza zoezi lake alikusanya vitu vyake, Ambe aliondoka eneo lile na kuchepua hadi chumbani kwake. Haukupita muda mrefu alisikia akiitwa nje na mzee Yamungu.
"Babuuu."


"Naam babu," Ambe aliitikia.
"Vipi umeisha lala?"
"Bado."
"Vipi leo unalala mapema?"
"Niliogopa kukaa nje peke yangu."


"Acha uoga wewe mtoto wa kiume mbona mimi nimekaa zaidi ya miaka kumi peke yangu."
"Si umesema wewe ni mtaalamu wa miti shamba huenda ndiyo iliyokusaidia."
"Babu kuna umuhimu wa kukufundisha baadhi ya dawa zinaweza kukusaidia kuepukana na mambo mengi pia hata kutibu watu."


"Mmh! Nitaweza?"
"Kwa nini ushindwe, nataka kukuambia ukiwa mganga wa kweli huchelewi kuwa tajiri kwani dawa zangu hazina masharti makubwa."
"Babu umesema unaweza kupata dawa ya kuzuia kuepukana na matatizo?"
"Ndiyo."


"Basi nifanyie na mimi niweze kurudi nyumbani."
"Nitakufanyia usiwe na wasi."
"Na kuhusu kumpata mpenzi wangu?"
"Kila kitu kitafanyika, kuna mti mmoja nikiupata nikichanganya unarudi hakuna hata mmoja atakayekutilia mashaka."
"Mti huo upo wapi?"


"Nakumbuka niliuona njiani wakati nakuja, nilichukua kidogo ambao ulinisaidia kuishi sehemu hii salama pia kuzima kutafutwa kwani katika kuangalia rais yule alipanga kuomba msaada wa nchi hii kunisaka nikiwa hai au nimekufa."
"Babu una dawa ya kumfufua mtu?"
"Dawa kama hiyo duniani hakuna uwezo huo anao Mungu peke yake."
"Mgonjwa aliyepoteza fahamu kwa muda mrefu?"
"Hiyo ipo."


"Kama mtu aliyepoteza fahamu kwa siku ngapi?"
"Hata miaka kumi."
"Ha! Babu kuna mtu anaweza kupoteza fahamu miaka kumi?"
"Kweli upo nyuma ya wakati, kuna mtu ameishi maisha yake mpaka anakufa akiwa amepoteza fahamu kwa zaidi ya miaka hamsini."


"Sasa babu kwa nini mtu kama huyo asizikwe."
"Huwezi kumzika mtu aliyehai."
"Yupo hai vipi akiwa haelewi kinachoendelea duniani si sawa na mfu?"
"Wengi huwa na matumaini kuna siku mtu huyo anaweza kuamka."
"Mmh!"


Ambe aliguna kusikia vile palepale alipata jibu juu ya mwili uliokuwa ndani ya kibanda ambao yeye aliamini kabisa haukuwa na uhai. Lakini alijiuliza mzee Yamungu kuhudumia mwili zaidi ya mwaka alikuwa akitegemea kupata nini!
"Babu kuna mtu anaweza kupoteza fahamu na kurudi katika hali yake ya kawaida?"


"Wapo wengi, unajua wanadamu tumekuwa tukiwazika ndugu au jamaa zetu kwa haraka kudhani amekufa kumbe bado yupo hai na akipata huduma muhimu anapona. Kwa mfano kuna mtu mmoja alimuokota shambani kwangu kwa kumuangalia utajua amekufa lakini kutokana na utaalamu wangu nilijua hajafa."
"Ulimkuta kwenye hali gani?'


"Alikuwa amepigwa sana hasa sehemu ya kichwa na kuwafanya waliofanya kitendo kile cha kikatili kuamini walimuua."
"Baada ya kumleta ndani ikawaje?"
"Mmh! Baada ya kumchukua nilimleta ndani na kujaribu dawa zangu ambazo zilionesha matumaini makubwa."
"Kwa hiyo babu atapona?"


"Kwa hali anayokwenda nayo ni miezi mwili nina uhakika ataweza kujitambua. Tatizo kubwa ni kupoteza kumbukumbu na kufanya kila wakati alale sana lakini taratibu hali inaanza kukaa vizuri."
"Babu yaani nitafurahi kukutana naye tena niliamini amekwisha kufa, kweli Mungu mkubwa," Ambe alijisahau na kufurahia kusikia mgonjwa atapona baada ya miezi miwili.
"Unamjua?"


"Mm...aah...hapana," Ambe alipata kigugumizi.
"Hapana, ulijuaje kama amekwisha kufa?"
"Ni...nii...nimekisia tu."
"Ambe nina akili kuliko unavyonifikiria."
"Kwa vipi mzee?"


"Kila unachokifanya najua, hata siku ya kwanza ulipoingia kwenye kibanda nilijua si kwa kutumia akili nyingi. Kuna vitu ulivitoa sehemu yake bila wewe kujua pili hata muda huu ulikuwa unanifuatilia kwa vile nilijua ni rafiki yako sikutaka kukushtua niliendelea na kazi yangu."
"Ni kweli babu naomba unisamehe sana."


"Nilikusamehe muda mrefu kwa vile mpaka leo nakuchukulia kama mwanangu, kuanzia kesho kazi yote uliyoiona namfanyia rafiki yako utaifanya wewe."
"Nitaweza?"
"Kwani mimi nina mikono kumi?"
"Sawa mzee nitaifanya."
"Nina imani umeniona nikiifanya?"


"Nilichelewa kidogo."
"Basi kesho nitakuelekeza na ikiwezekana nianze kukukabidhi majukumu ya kufahamu dawa kama nitakufa utaweza kuwasaidia watu wengine."
"Babu mbona unajichulia kifo?"
"Kwani nitaishi milele?"
"Naweza kutangulia hata mimi."
"Basi atakayebakia kabla mgonjwa hajapona atachukua jukumu kuhakikisha mgonjwa ananyanyuka kitandani na kutembea."


"Sawa nimekuelewa mzee wangu."
"Mzee mgonjwa ulimpataje?"
"Kuna siku niliingia porini kutafuta dawa zangu, niliingia umbali mrefu ndipo nilipoukuta mwili wake pembeni ya mto. Wasiwasi wangu nilijua amekufa, kwa vile wanadamu tumefundishwa ubinaadamu huwezi kumpita mwanadamu mwenzako kama mzoga.


Nilimchukua ili nimzike, nilichimba shimo ili nimzike lakini roho ilikataa kumzika bila kumchunguza kiundani japo alionekana kabisa hana uhai. Pamoja kuwa ahemi lakini kuna sehemu nilitakiwa nimshike ili nijue kama kweli mzima au alifariki.
"Baada ya kumshika niligundua hajafa hivyo nisingeweza kumzika akiwa hai.
 
Hivi hapa JF hakuna sheria ya uchapishaji hadithi?
Natamani Administrators wa JF wangeanza kutoza kodi ya uchapishaji stori manake kuna authors wengine wanauza stori buuureeeeeeeeeeee....
 
Hivi hapa JF hakuna sheria ya uchapishaji hadithi?
Natamani Administrators wa JF wangeanza kutoza kodi ya uchapishaji stori manake kuna authors wengine wanauza stori buuureeeeeeeeeeee....

Inakuuma nn?acha wivu mkuu.zikisitishwa utanufaika nini kwa mfano?
 
JOTO LA MAPENZI-24

ILIPOISHIA

Nilimchukua ili nimzike, nilichimba shimo ili nimzike lakini roho ilikataa kumzika bila kumchunguza kiundani japo alionekana kabisa hana uhai. Pamoja na kuwa ahemi lakini kuna sehemu nilitakiwa nimshike ili nijue kama kweli alikuwa mzima au alifariki.
"Baada ya kumshika niligundua hajafa hivyo nisingeweza kumzika akiwa hai.
ENDELEA NAYO...


Nilimbeba hadi hapa na kumtengenezea kitanda cha kamba kisha nilianza kumshughulikia taratibu. Kila siku moja iliyosegea mbele ilionesha mabadiliko hata katika darubini ya asili ilionesha umri wake bado sana. Mpaka leo hii umemuona yupo katika hali hii."


"Babu Mungu atakulipa kwa yote uliyotufanyia, niliamini kabisa rafiki yangu amekufa kutokana na kauli za askari Magereza niliowasikia wakati wanarudi kutusaka."
"Mungu bado anapenda aendelee kuishi."


"Ataweza kurudi katika hali yake ya awali kweli?"
"Atarudi kwa uwezo wa Mungu, sehemu aliyoumia sana ilikuwa kichwani ilionekana walikuwa wanampiga kama wanaua nyoka. Lakini sehemu zingine zipo salama nina imani atapona tu japo atachelewa kutengeneza kumbukumbu."


"Yaani babu nitafurahi kama rafiki yangu atarudi katika hali yake ya awali kwani aliniahidi akifa bila kulipa kisasi angejiona amekufa kibudu. Lakini kama atalipa kisasi atakuwa radhi kujipeleka mwenyewe polisi ili akamatwe na kisha ahukumiwe kifo."


"Atapona tu, na akipona atajijua atafanya nini kwani kwa upande wangu nitakuwa nimemaliza kazi yangu."
"Babu nimekuelewa sijui nikulipe nini kwa yote uliyotutendea."
"Cha muhimu kunitunza mpaka hapo nitakapokufa, baada ya kunizika ruksa kuondoka."
"Kwani mjini kutoka hapa ni mbali?"


"Mbali kidogo, kutoka hapa mpaka mjini ni mwendo wa saa nne na nusu kwa gari."
"Kumbe siyo mbali."
"Babu naweza kwenda mara moja kumtafuta mpenzi wangu?"
"Siwezi kukukataza lakini la muhimu ni kuhakikisha tunasaidiana kuimarisha hali ya rafiki yako. Akipona ruksa kutoka kwani nina imani sasa hivi nachoka sana nikitembea umbali mrefu kutafuta dawa. Hii yote inaonesha umri nao unachukua nafasi yake."


"Hakuna tatizo babu nitakusaidia kwa nguvu zangu zote."
Kwa vile ulikuwa usiku mkubwa waliingia ndani kulala kuitafuta siku inayofuata.
* * *
Siku zilizidi kukatika huku hali ya mgonjwa ikiendelea kuimarika, wakati huo Ambe alikuwa amekwishaanza kufahamu baadhi ya dawa kutokana na kila siku kuingia maporini kutafuta dawa. Mgonjwa aliweza kukaa peke yake hata kuzungumza kwa taratibu kutokana na kupoteza kumbukumbu kwa muda mrefu.


Mzee Yamungu aliendelea kumpatia dawa za kunywa na kujifukiza ambazo zilirudisha kumbukumbu haraka. Siku moja wakiwa wamekaa pamoja, mgonjwa aliuliza:


"Jamani hapa ni wapi?" Aloys Mabina aliuliza baada ya akili yake kuanza kutambua kilichokuwa mbele yake.
"Kwani wewe ulikuwa wapi?" Ambe alimuuliza.
"Mmh! Sikumbuki."
"Unanitambua mimi?" Ambe alimuuliza rafiki yake.
Mabina alimtazama kwa muda kuvuta kumbukumbu lakini hakumfahamu kutokana na Ambe kuwa na nywele na ndevu nyingi.


"Hata sikukumbuki."
"Mara ya mwisho unakumbuka ulikuwa wapi?"
"Mmh! Hata sikumbuki."
"Hukuwa gerezani umefungwa?" Ambe alijitahidi kumkumbusha rafiki yake.
"Mmh! Kweli..kweli."


"Baada ya kutoka gerezani ulikwenda wapi?"
"Mmh...mmh! Mmh!"
Mabina aliguna kuvuta kumbukumbu, picha ya kutoroka ilijirudia akiwa na rafiki yake Ambe. Alikumbuka aliachana na Ambe baada ya kudondokea shimoni, baada ya muda aliwasikia askari wakimtafuta aliamua kuificha bunduki juu ya mti kisha aliteremka ili awatoroke lakini walimuona na kuanza kumkimbiza.


Baada ya kukimbizana kwa muda walimkatamata na kuanza kupigana kwa muda huku akitumia uwezo wake kuokoa maisha yake kwa kujisaidia kwa vipande vya miti. Baada ya ugomvi wa muda mrefu huku wakikataa kumuua kwa risasi, waliendelea kumuuliza bunduki aliyochukua lakini mwisho wa siku alipoteza mawasiliano kilichoendelea hakukijua mpaka aliposhtukia akiwa kwa mzee Yamungu.


Baada ya kuyakumbuka yote ya nyuma alijikuta akiikumbuka sauti iliyokuwa ikimuuliza maswali. Haikuwa ngeni katika chumba cha kumbukumbu katika ubongo wake. Ili kupata ukweli alirudia tena kumtazama aliyekuwa akimuuliza taratibu alianza kumkumbuka kwa sauti alimwita.
"Ambe!"


Ambe kabla ya kujibu alishtuka hata mzee Yamungu aliamini kazi imekwisha baada ya akili ya Mabina kuweza kukumbuka baada ya kupoteza kumbukumbu kwa muda mrefu.
"Naam Mabina."


Chris alinyanyuka alipokuwa amekaa na kumvamia Ambe na kuanza kulia asiamini akili na macho yake.
"Ambe siamini, kweli Mungu mkubwa."
"Ni kweli rafiki yangu hata mimi sikuamini kukukuta hapa nilijua askari wameishakuua. Lakini mzee huyu sijui tutamlipa nini?"


"Kwani huyu ni nani?" Mabina aliuliza huku akimshangaa mzee Yamungu.
"Ndiye aliyeokota mwili wako uliokuwa sawa na mfu, kama angetokea mwingine kutokana na hali yako uliyokuwa nayo ya umaiti kwa asilimia tisini na tisa angekuzika ukiwa hai."


"Mzee wangu...mzee wangu...asante sana..Hata sijui nikulipe nini mzee wangu!" Mabina alipiga magoti mbele ya mzee Yamungu kumshukuru kwa yote aliyomtendea.
"Kawaida kijana wangu, wa kumshukuru ni Mungu kuweza kunileta ulipokuwa na kuweza kunipa ufahamu wa kujua dawa zilizoweza kukuponya."


"Nina muda gani tangu nilipopoteza fahamu?"
"Mwaka unakatika," alijibu Ambe.
"Mungu mkubwa sifa ni haki yake."
Mzee Yamungu alimnyanyua Mabina alipokuwa amepiga magoti.


Baada ya kujifahamu Chris alijikuta akitaka kujua na rafiki yake ilikuwaje kuwa pale. Ambe naye alimweleza yote aliyokutana nayo na msaada wa yule mzee.
"Na kwa nini mzee huyu yupo huku peke yake?"
Ambe alimpa mkasa wa mzee Yamungu kuishi kama dume la nyani ‘gendaeka'. Baada ya kufahamu yote Mabina alimuuliza rafiki yake.


"Huyu mzee nina imani ni malaika aliyetumwa kuokoa maisha yetu kutokana na dhuluma na uonevu tuliofanyiwa."
"Hata sijui tutamlipa nini kutokana na wema aliotufanyia!"


"Binafsi namuona kama baba yangu mzazi hivyo basi kwa umri wake tunatakiwa kumtunza kama mboni ya jicho letu. Najua mimi sijawa vizuri lakini kwa mazoezi na dawa ninazotumia muda si mrefu tutakuwa pamoja."
 
Back
Top Bottom