Joto Kali Dar

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
24,474
34,512
Usiku wa kuamkia tarehe 21/03/2016 kulikuwa na joto kali sana jijini Dar.
Ni kweli TMA walitangaza joto kali kufikia nyuzi 35 kwa Dar na 36 kwa Kilimanjaro ambapo joto la Kilimanjaro ndilo limevunja rekodi kwa Tanzania.

Naomba wataalam wa hali ya hewa waliomo humu watupe elimu. Hili joto kali chanzo chake nini hasa? Je kuna prediction ya lini litaisha? maana badala ya masika kunyesha, ni jasho linanyesha sasa
 
Jana jua lilikuwa ni la utosi, kwa mujibu wa wataalam wa hali ya hewa walisema jua lilikuwa karibu sana na Ikweta kuliko kipindi chochote cha mwaka. Hali hii itajirudia September.

Naamini wataalam wa tabianchi watatupa elimu hapa
 
K

Kwani miaka mingine jua linakuwa wapi mwezi na tarehe kama hizi? Mbona joto haliwi hivi?
Mkuu nadhani kuna kitu kinafichwa hapo.
hatujajua hadi sasa ni size gani ya OZONE imeshapotea. maana Nchi za magharibi hususani Marekani zimegomea kusaini mkataba wa Kyoto kupunguza joto duniani. Wao wanazalisha sana gesi ya ukaa ambayo inamaliza ozoni ye dunia.

Northern lights nahisi zitakuwa zimeongezeka sana
 
Mimi sikulisikia kabisa hilo joto kwa sababu nyumbani kwangu nina AC, kwenye gari kuna AC, ofisini kuna AC, kwa hiyo kwa hali kama hiyo joto mnasikia nyie walalahoi tu. Mtaisoma namba
Hahahahahaha
Kwa hiyo haukujaliwa hata mara moja kulionja jua la jana? Maana tangu alhamisi hali ilikuwa tete na seems wewe hujaenda kanisani ama msikitini this week
 
Mimi sikulisikia kabisa hilo joto kwa sababu nyumbani kwangu nina AC, kwenye gari kuna AC, ofisini kuna AC, kwa hiyo kwa hali kama hiyo joto mnasikia nyie walalahoi tu. Mtaisoma namba
Ww utakuwa mhaya ambae hajaelimika ila ana enzi mila toka lini jua ukalisikia
 
Back
Top Bottom