Joshua Nassary ataka Kamati za Zitto na Mrema kuvunjwa pia!

Az 89

JF-Expert Member
Nov 20, 2011
1,658
691
Ni hivi punde Mh. Joshua Nassary ameomba mwongozo wa kiti kuhusu kashfa ya rushwa inayozikabiri kamati hizo za madini na ile ya mashirika ya umma..amemtaja Zitto na Mrema na ikiwezekana wafukuzwe au wabadilishiwe kamati...nawasilisha
 
Dakika tano zilizopita Joshua Nassary ameomba mwongozo toka kwa Naibu Spika kwamba isivunjwe Kamati ya Nishati tu kama ilivyoelezwa wiki jana, bali kamati zote zinazotuhumiwa kwa rushwa kama Kamati ya Augustine Mrema, Kamati ya Zitto Kabwe, na nyingine nimeisahau.

HOja yake ni kwamba utendaji wa kamati hizi unahusisha mikataba mingi na ndiyo maana wabunge wengi wanazikimbilia na wanaacha Kamati kama ya Huduma za Jamii.

Hivyo wazo lake ni kwamba wabunge wa kamati zile watawanywe kwenye Kamati zisizo na Mikataba ili waonje huko kulivyo kuvunjilia mbali tabia ya wabunge kukimbilia zile zenye Mikataba.

Imebidi Naibu Spika aite Kamati ya Uongozi wa Bunge ili ijadili suala hilo na walete majibu baadaye.
 
Umesikia vibaya, hajawataja kwa majina akimanisha walichukua rushwa, bali amesema kwa kuwa kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na madini inatuhumiwa kwa rushwa sambamba na kamati ya hesabu za mashirika ya umma-poac, na kamti nyingine iliyowahi kutuhumiwa siku za nyuma ya erikali za mitaa,akataja wanaoziongoza kuwa ni Zitto na Mrema.

Ni kweli hata mimi nahitaji tamko rasmi watu hawa watajwe, tena nahisi kama vile wanawaogopa kama si kuwabembeleza naomba watajwe rasmi badala ya kuzunguka zunguka
 
Kamati ya Mrema iliwahi kupeleka majina na USHAHIDI wa watuhumiwa wa Rushwa kwenye Ofisi ya SPIKA.

Surprising enough hadi leo Ofisa ya Spika imekalia majina na ushahidi wa watuhumiwa wa rushwa, bila kuchukua hatua yeyote.

For those of you who have short memory, Anne Makinda ameupata USPIKA kwa pesa za mafisadi. Hivyo na yeye ni party of the problem.
 
wakifanikiwa wale watu mtayumba sana na tayari mmeanza kuyumba ...hivi mnajua jana kulikuwa na hafla ya kupongezana?
 
Nassari nassari nassari polepole mguu mmoja weka kwenye mafuta ila jua mkono upo kwenye handbrake maana itakuwa kukugharimu......
 
Tuhuma hizi si ngeni masikioni mwetu, hawa wabunge wamekuwa wakichukua rushwa sana hata hizi tuhuma chache zilizotajwa ni zile tunaziozifahamu zipo nyingi sana.Hasa kamati ya POAC, LAAC na Nishati na madini.
  • POAC iliwahi kutuhumiwa kuhongwa wakati wa sakata la CHC extension tenure tuhuma alizitoa Mh.Mkulo
  • LAAC ilituhumiwa na Kafulila kuwa kuna wala rushwa wakubwa
  • Nishati na madini ilituhumiwa sana hasa January Makamba kufanya biashara na TANESCO na pia kuhusu kutokumalizika kwa mgao wa umeme, katika hili ngereja yumo sana na malima
Mama makinda alidhani watu wanachafuana kisiasa kama ambavyo zitto anaendelea kudai, lakini ukweli ndiyo huu, alivyosema NASSARI ni sahihi tunatakiwa kuwajua ili tusonge mbele
 
Nassari nassari nassari polepole mguu mmoja weka kwenye mafuta ila jua mkono upo kwenye handbrake maana itakuwa kukugharimu......

acha nidhamu ya woga. Ndio maana kila siku tunalilia vijana wajae bungeni ili wafanye mambo ambayo wazee hawayawezi.!
 
Compareno.............. Can you make a comparison between Nassari and Silinde? Is like Pure drinking water VS Maji taka!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kuna mmoja wa waliokuwa Mawaziri aliwahi kuniambia kwamba Zitto alihongwa M60 suala la CHC kuongezewa mkataba, mimi nikaona kama anampiga vijembe tu kwa sababu ni mpinzani, lakini leo naanza kupata picha!!!!
 
Back
Top Bottom