Josephine03
JF-Expert Member
- Feb 7, 2012
- 752
- 302
Kwa kweli naanza kupata wasiwasi kuhusu kijana mzalendo mwana Demokrasia kwa kuanza anavyofanya katika uwanja wa Siasa hapa Tanzania,... ''Kuhusu kwamba Sehemu ya Kaskazini Ijitenge, Iwe Jamuhuri yake''. Inawezekana ni wazo au ni mojawapo ya sera Lakini SI WAKATI HUU kwa sasa, Kwani Chama Tawala kinaweza kutumia kama njia ya Kukiharibu Chadema kwa Wananchi ambao tayari walishaanza kuweka matumaini na Kumshukuru MUNGU kuwa wamepata Chama cha kuwakomboa na cha Chama cha kupeleka Sauti zao Bungeni na kwenye Serikali.
NAJIULIZA,..
1. Inawezekana huyu kijana Alisha kuwa SETUP (Kuwekwa Pandikizi) toka yupo Chuoni kama wengine walivyofanywa?
2. Au Ameshaongwa hela Ili aje Aharibu chadema?
Sielewi lakini naamini MUNGU Atasimama kwa Raia zake,....!
Kitu kinachoniacha hoi mimi ni kuwa kama kauli ya Mh. Nassari inaweza kugawa nchi basi tuna kila sababu ya kuamini kuwa tayari nchi ilishaanza kuelekea huko na Mh. Nassari anataka kumalizia tu. Nadhani pamoja na ukweli uliopo kuwa kauli ya Mh. Nassari ilikuwa na harufu ya uchochezi, kama ilivyonukuliwa kauli ya Dr. Slaa huko nyuma kuwa nchi haitatawalika, lakini kitu ambacho kitafanya nchi yetu kugawanyika au kutotawalika wala haitakuwa kauli za namna hiyo bali wizi na ufisadi unaoendeshwa na kuratibiwa na genge la wajanja ambao serikali inashindwa kuwachukulia hatua.
Kama waziri mkuu wa nchi hii alisema kuwa mafisadi wakichukuliwa hatua nchi itayumba, basi hiyo hali ya mafisadi kuogopwa ndiyo cha kuogopa zaidi kuliko kauli ya Nassari au ya Dr. Slaa. Watu wanao'capitalize' kauli ya Mh. Nassari wanataka kutufanya kuwa hatuna akili kiasi kuwa kinachosemwa na kila mwanasiasa kitakuwa hivyo eti tu kwa sababu wana ushawishi. Ukweli ni kuwa jambo ambalo wananchi watakubaliana nalo hasa baada ya kusemwa na mwanasiasa kitakuwa kile ambacho wao wanaliamini na wanalitaka. Wananchi siyo roboti ya kuendeshwa na wanasiasa kama watu wengine wanavyotaka kutuaminisha.
Amesema jambo ambalo kwa haraka linaonekana lina mantiki lakini linapuuzia uzito wa alichokisema. Kama ni mtu mdogo hivyo aligombea ubunge wa nini? Kama anakosa hekima ya kupima madhara ya maneno yake - watu wanaweza kuumia kwa kauli moja tu ya mtu mwenye ushawishi - kwa sababu yeye ni 'mtu mdogo' ananitisha. Yeye anaweza kuwa na umri mdogo lakini nguvu ya ushawishi wake inashinda baruti na siyo watu wote wanaomsikiiliza wanamchukulia kuwa ni mtu 'mdogo'. grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
Hapana siyo CCM, yeye ni kielelezo tosha namna viongozi wa CDM walivyokosa BUSARA hivyo huwaza namna ya kutugawa watanzania kwa misingi ya ukanda