Joshua Nassari adanganya "live" ITV

Joshua Nassari adanganya "live" ITV

Nadhani hoja ingekuwa nini source ya hizo data kabla ya kumhukumu kuwa ni muongo
 
Adanganye asidanganye inatusaidia nini? Ulizaliwa bila kuchagua siku, mwezi wala mwaka; utakufa hivyo hivyo; ya nini kujisumbua na mambo ambayo huwezi kuyabatilisha?
 
Mbunge Joshua Nassari amedanganya alipokuwa anahojiwa na ITV kwenye viwanja vya bunge Dodoma aliposema "life expectancy" ya Mtanzania ni miaka 47 kwa sasa.

Huo si ukweli kabisa, uwiano wa "life expectancy" ya Mtanzania si chini ya miaka 58 kwa sasa.

tanzania-life-expectancy-at-birth-female-years-wb-data.png

Source: Life expectancy at birth in Tanzania

Na hizi nyingine:

Chanzo kilichotangazwa waziwazi mbele ya waandishi wa habari, hizo takwimu za Nassari za miaka ya utawala wa Nyerere, nna uhakika hata yeye alikuwa bado hajazaliwa.

UNDP wanasema hivi na si hivyo tu wanazitoa rasmi mbele ya waandishi wa habari, unaweza kuzikataa?

expentance.jpg
Director of Economic and Social Research Foundation (ESRF), Dr Bohela Lunogelo (Left) speaks in Dar es Salaam yesterday during the launch of Human Development Report 2011. Center is UNDP's Economic Adviser, Amarakoon Bandara and UN Resident Coordinator Mr Alberic Kacou. PHOTO | VENANCE NESTORY

By Ludger Kasumuni
The Citizen Reporter
Dar es Salaam. Thursday, 03 November 2011 22:59
Tanzanians now have higher life expectancy fixed at 58.2 years at birth than the rest of the citizens of East African Community (EAC), the 2011 Human Development Report (HDR) released by the United Nations Development Programme (UNDP) shows.

According to the report released yesterday by the UN Resident Coordinator in Tanzania, Mr Alberic Kacou, taking the lead in the EAC in terms of ranking of life expectancy, Kenyans follow Tanzanians with life expectancy of 57.1 years and Rwandans with 55.4 years.

Source: Tanzania

Ndio hizi hapa data zenyewe:

attachment.php

zangu zinatoka hapa: http://hdrstats.undp.org/images/explanations/TZA.pdf

Wabunge wengine sijui wako dunia ipi, yaani hiyo "life expectancy" ni miaka ya Nyerere huko si leo wala jana.

Mpaka sasa sielewi huyu Mbunge anapata faida ipi kuwadanganya umma wa Watanzania kupitia vyombo vya habari.
Aombe radhi haraka sana.

Mimi nadhani ingekuwa ni vyema ukapata kuuliza alitumia njia ipi ya kufanya research hata akafikia hiyo 47%. Hiyo taarifa waliyoitoa unaowaita wataalamu wana vigezo vyao walivyokuwa wametumia kupimia.

Kuna aina kama 6 za research ambazo mtu anaweza kuzitumia kukusanya taarifa, hizi ni:
1.Basic research
2.Applied research
3.Theory testing research
4.Theory building research
5.Exploratory reserach

6. Explanatory research

Itategemea ametumia approach ipi na hao HDR wametumia approach ipi ndipo utaweza kuhitimisha kwamba Joshua kasema uongo!

Kwa nini unaiamini hiyo ya HDR, kwani wao ni nani na wamefanya research kwa watu gani? Kama watakuwa wamefanya research yao kwa kutumia watu wa vipato vya juu au kati, usishangae kwamba wamekuja na takwimu ambazo umeweka janvini. Huenda wameishia Nairobi na Dar es salaam na Kampala.

kama unaweza uka challenge njia aliyotumia Joshua ndipo utasema hii ni batili.

Vinginevyo, yupo sahihi kabisa, ila wewe kwasababu ni mbumbumbu wa mambo hayo ndiyo umekurupuka kusema kasema uongo.
 
Sisi tunamkubali, Tunamuamini ndio maana tumemchagua. na wewe nenda kamchague Zungu na wenzake wala Rushwa na wengine wanasinzia Bungeni
 
Kani hizo si data tu ambazo mtu yeyote mwenye dhamana anaweza kuzipika na zikawa zinatumika kama takwimu halali?

Unadhani matokeo ya sensa ndo yatakuwa ukweli halisi?
Matokeo ya kura huwa ni ukweli halisi?
.Unatetea uongo, huyo dogo arudi shule tu asione aibu.
 
Mnaolipwa na NAPE mna juhudi kweli za kutafuta data za uongo, hivi kwa akili ya kawaida tu maisha wakati wa nyerere na sasa ni yapi yalikuwa nafuu. Sasa hivi vijijini hata milo miwili ni tatizo halafu life expectancy itawezaje kwenda juu? Nchi hii imebaki kuongozwa kwa takwimu ambao hauendani na uhalisia.
Kila siku tunaambiwa uchumi wetu unakuwa huku watu wakivaa mitumba na nguo zenye viraka.
 
Umekomaa na DATA. hivi kweli Tanzania tuna takwimu za kweli? Mimi mwenyewe nilisubiri kwa siku mbili shinyanga ili nihesabiwe lakini sikuona watu leo hii tunaambiwa zoezi la kuhesabu watu lilifanikiwa sana. Je wale ambao hawakuwa tayari kuhesabiwa walihesabiwa kweli? Nchi hii imebaki kuongozwa kwa takwimu zisizo na ukweli.
 
Kwa ujumla tuna shida sana ya ukusanyaji, utafsiri na usambazaji wa takwimu zetu nchini. Yaani kwa indicator moja, utakutana na takwimu kama tatu au zaidi tofauti. Unaweza kukuta ya wizara husika ni tofauti na ya mamlaka ya takwimu, tofauti na ya uratibu na mipango, tofauti na iliyoko kwenye tovuti rasmi ya serikali ya JMT, tofauti na iliyoko katika shirika mwenza la umoja wa mataifa, tofauti na waliyo nayo CIA na itakuja kuwa tofauti na ya sensa.

Yaani hatuna QC katika takwimu zetu na kila mtu anaweza kuibuka na takwimu zake popote na hakuna wa kumuuliza. Kuthibitisha hili sote tulikia yaliyoonekana katika zoezi la kujiandikisha kwa ajili ya vitambulisho vya Taifa na yaliyoonekana Jeshini. Ingawa baadaye lilisawazishwa lakini ukweli unabakin kuwa kuwa kuna watu wamefoji vyeti hivyo ukiuliza takwimu ya wasomi katika taaluma mbalimbali TZ tunaonekana hatujambo lakini ukweli ni kuwa unaweza kukuta certificate au diploma moja imetumika kwa watu wawili hata watatu sasa hapo utapataje takwimu sahihi?

Pamoja na yote, Mh. Joshua anatakiwa kuwa makini kabla ya kutamka takwimu kadha iwe katika vikao au mazungumzo ya kawaida maana yeye ni kiongozi, vinginevyo atajishusha. Kama huna uhakika ni afadhali useme yapata (approx). ....

Pili, uongo ni mwingi sana katika nchi yetu. Hatuoni aibu hata katika mazishi au msibani kusikia msoma wa wasifu wa marehemu anasema kuwa marehemu amekufa kutokana na ugonjwa A wakati ukweli ni ugonjwa B na inajulikana hivyo hospitalini au baada ya ugonjwa wa muda mfupi wakati mtu alikuwa anaumwa kwa muda mrefu.

Zaidi ya yote nina uhakika kuna watu wengi sana waliozaliwa mika ya 70 ambao wananizidi umri lakini leo hii wameweza kujirudisha nyuma na wanaendelea kuwa umoja wa vijana CCM & CHADEMA wakati ni wazee wakongwe wa kutupwa ; sasa hao wakifariki wanaonekana wamefariki wakiwa vijana na inateremsha LE rate wakati wange register ukweli wangeinyanyua hiyo LE rate juu!
 
haja kosea ndo alivyo fundshwa darasani!!!!wewe ndo umedanganya 48 ilikuwa enz za nyerere sio kweli
 
takwimu zinaweza kupikwa muda wowote.sensa imefanyika mwezi wa nane lakini idadi ya watanzania haijulikani.sophisticated issue kama za life expectancy ni ngumu zaidi kuwa assured.Nassari is right and anyone else can be right.
 
Siamini kama kuna accurate data kuhusu life expectancy haswa kwa nchi za Afrika
 
Mbunge Joshua Nassari amedanganya alipokuwa anahojiwa na ITV kwenye viwanja vya bunge Dodoma aliposema "life expectancy" ya Mtanzania ni miaka 47 kwa sasa.

Huo si ukweli kabisa, uwiano wa "life expectancy" ya Mtanzania si chini ya miaka 58 kwa sasa.

tanzania-life-expectancy-at-birth-female-years-wb-data.png

Huitaji kuwa na data hata moja kwa kikomo cha kuishi cha watanzania hali halisi inajionesha.Htata NASSAR alitumia ualisia.Serikali yako inatoa takwimu wakati mwingine haziendani na ukweli hali au maisha yalivyo ya watanzania.Wanachukua sample moja tu then wanageneralize.Angalia mazingira tuliyo nayo watz,ukimwi unazidi kushambulia,njaa ndo usisema,kutoka milo miwili kwa siku mpaka mmoja unafikir huyu mtu ataishi vip?Kazi wanazofanya watz kwa asilimia kubwa ni za hatari na ndo maana kama ww ni mwelewa ungeangalia jinsi wafanyakazi wa migodi walivyo changanyikiwa walivyopata taarifa ya kusitishwa kwa fao la kijitoa.Hii kutokana na kwamba wanajua muda wao wa kuishi ulivyo limited.KWAHIYO LIFE EXPECTANCY YA MTAZ NI YA MTU MMOJA MMOJA KUJUA NAMNA GANI ANAVYOISHI.WANAOTOA DATA HIZO TENA KWA KKUJIFUNGIA NA KUTOA TAARIFA YA MAANDISHI NI WALEWALE WANAPOUGUA WANAKIBIZWA INDIA MTZ AKIUGUA ANASUBIRI MIUJIZA YA MUNGU.
WEWE HUJAONA HATA TAARIFA YA KUKUA KWA UCHUMI INAVYOTUTIA MASHAKA HATA KAMA SIO WATAALAM WA UCHUMI.UCHUMI UNAKUA LAKINI UCHUMI WA TANZANIA HAUNA INDICATORS SASA HUO UCHUMI NI WA VIPI?USIWE MWEPESI WA KUKURUPUKA TAFAKARI KWANZA.
 
Uhalisi wa nini wewe? unafikiri pale uzazi na vifo wanafanya kazi gani? au kwenu mkizaliana na kufa hamtoi taarifa?
 
Nasari is still an infant and He don't understand himself.He's not a true politician other than a politics rape.He always speak Nonsense.
 
Umeonae. Unajua mkuu ndiyo maana uwezo wa Wabunge wetu haukui hata kidogo, hata jambo la kizushi tunawapigia makofi kisa eti wewe ni mnazi wa chama anachotoka.

Tutaifanya Kigoma kuwa kama Dubai
 
Back
Top Bottom