Mimi hapa sioni kama kuna hoja ya kujadili kwa muda wote huu. Mwenzenu Zomba analipwa kwa kuanzisha vitu visivyo na tija kwa taifa na kufanya watu wasahau kujadili yaliyo ya msingi kwa Taifa. Rushwa inagawiwa kama njugu hata Amiri jeshi mkuu analalamika bila ya kuchukua hatua, leo hii tunajadili life expectancy ambayo kwa nchi kama Tanzania ni vigumu kuijua kwani factors zinazopelekea kuongezeka au kupungua ni nyingi, mjawapo ikiwa ni huduma za afya.
Wana JF msikubali kutolewa kwenye hoja nzito kwa manufaa ya Taifa na badala yake tunawatengenezea watu ugali, tunavyojadili muda mrefu ndio tunavyomuongezea ZOMBE mshiko mana hajalala tangu jana, yeye ni kusoma na kujibu tu