Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii
kanda ya kaskazini.
MBUNGE wa Jimbo la Arumeru
Mashariki ,Mh Joshua Nassari kesho anatarajia kufunga ndoa na Bi
Anande Nko katika kanisa la Pentekoste, Kilinga lililoko wilaya ya
Meru ambako Mh Nassari alianzia masuala ya Kiimani ikifuatiwa na
Sherehe kubwa ya Harusi itakayo fanyika katika viwanja vya Usa-River
Academy jirani na Hotel ya Ngurdoto.
Kwa Mujibu wa Mh Nassari
,sherehe hizo zitakazoanza majira ya saa saba mchana watu wote
wamealikwa wakiwemo ndugu, marafiki, Jamaa na wananchi jimbo la
Arumeru Mashariki kwenye tukio hilo na kamba hakuna
kadi.
"Nichukue
tena fursa hii kuwakaribisha ndg, marafiki, Jamaa na zaidi sana
wananchi wangu wa jimbo la Arumeru Mashariki kwenye tendo hadhimu la
kusherekea harusi yangu , Jumamosi Juni 7, Usa-River academy grounds
kuanzia saa saba mchana. Kwa Pamoja Tulianza na Mungu, Tutamaliza na
Mungu Pamoja. ...No cards on entrance!"alisema
Nassari.
Na ssari amesema watu zaidi
ya 8000 wanatazamiwa kushiriki katika sherehe hiyo ya aina yake
wakiwemo viongozi mbalimbali na wabunge kutoka maeneo mbalimbali
.